Pesa ni Kila kitu? Hapana Hichi Ndio Kitu Chenye Thamani Zaidi ya Pesa!

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,305
8,655
Ni ukweli usiopingika kwamba katika hii dunia ya kitandawazi watu wameweka pesa Mbele sana huku wakiamini Pesa ni Kila kitu!

Lakini wanasahau kwamba mwishowe kila mtu duniani anatafuta furahaa...asikwambie mtu furaha ni kila kitu hata mimi kila siku naiomba furaha na naipenda Japo Haidumu!

Lakini Furaha ya kweli inaanzia wapi? Furaha ya kweli Huanzia Pale unapokuwa na Afya Njema kabisa....ukiwa na afya njema maisha yako yatatawaliwa kiasi kikubwa na furaha hata kama pesa ni changamoto!

wapo watu wana hela nyingi ila wana afya dhaifu kiasi kwamba pesa zao haziwasaidii!

Kwa maana hiyo ningefurahi watu wangeukubali huu ukweli wa kutafta furaha ya kweli kabla ya Pesa!

NB: TAFUTENI HELA...MONEY TALKS!

TheMason
 
1 Pesa ndio kila kitu bila ya kuwa na pesa utasikia tu watu wanavyokula bata.
2 Ukiwa na mpenzi na mkapendana kikweli hapa furaha itakuja tu.
3 Ukiwa mgonjwa hela inaweza kukupeleka India, UK au US. Lakini ukiwa pangu pakavu mchuzi nuksi hata muhimbili hupati kitanda utaishia chini tu.




Ndukiiiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo yote tunayofanya ni njia tu za kuifikia hiyo furaha. Furaha ndio lengo letu sote.
 
Ni kweli.utajiri wa kwanza ni afya njema.ukiwa namaradhi makubwa mwilini ata uwe na maela yote duniani kamwe huwezi kua na furaha.
 
Furaha ni nyoko sana aisee!

Utafanya kila namna uwe na afya njema but still utatamani pesa then utahangaika wee ukizipata utatamani mwenza wa kuendana nawe na ukimpata huyo mara oooh amepungukiwa hiki mara kile na utaishia kutokuwa na furaha in the end. Furaha ina moments zake ambazo unfortunately ni very brief!
 
Furaha ni nyoko sana aisee!

Utafanya kila namna uwe na afya njema but still utatamani pesa then utahangaika wee ukizipata utatamani mwenza wa kuendana nawe na ukimpata huyo mara oooh amepungukiwa hiki mara kile na utaishia kutokuwa na furaha in the end. Furaha ina moments zake ambazo unfortunately ni very brief!



Yaani, [HASHTAG]#nasssen[/HASHTAG], ulivyoanza comment yako na avatar yako imebidi tu nicheke kwa huzuni.
 
Back
Top Bottom