Pesa kidogo tuu unaanza kuepulia sufuria kwa 10k
Pesa kidogo tuu unanipa 10m ili niachane na binti'ako
Pesa kidogo tuu hutaki kuoga kwenye beseni
Pesa kidogo tuu utaki kutazama TBC
Pesa kidogo tuu unafungua akaunt ya twitter
Pesa kidogo tuu unamiliki smartphone na kitochi
Pesa kidogo tuu unamuita boss wa simba mudy
Pesa kidogo tuu unakarabati nyumba ya kupanga
Pesa kidogo tuu unatumbua chunusi hospital
Pesa kidogo tuu kwenye daladala unasoma gazeti la the citizen
Pesa kidogo tuu msibani unaenda wakati wa mazishi
Pesa kidogo tuu kwenye harusi unaahidi zawadi badala ya kuileta hapo hapo
Pesa kidogo tuu unatafuta mhasibu
Pesa kidogo tuu elfu kumi unaniita pesa ya maji
Pesa kidogo tuu ume-download my DStv kwenye simu yako
Pesa kidogo tuu unaogea maji ya kilimanjaro