Pesa ina nafasi ndogo katika mapenzi ya kweli

Kinyonyoke

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
3,392
2,000
Msichana kama anakupenda kweli hawezi kukuomba omba pesa.

Ukimuona binti anakupenda wewe kwa sababu unampa sana pesa, hapo hupendwi wewe bali zinapendwa pesa zako. Usijidanganye kwamba unapendwa kweli.

Binti anapokupenda kweli atakuomba pesa pale anapokuwa na shida ya kueleweka.

Siku ukiishiwa/ukiwa huna pesa mapenzi hufikia ukomo

Na kwakua pesa imetawala sana mahusiano ya siku hizi, ndiyo maana mapenzi ya kweli ni ngumu kupatikana

Pesa ni muhimu,lakini msiiendekeze, hata kama mtu alikuwa anakupenda sana, unamfanya aanze kufikiria mara mbili mbili.
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
4,618
2,000
ukitafuta pesa hutokaa kulalama kiasi hichi kwa lengo la kujipa faraja hewa, panapokosekana pesa hata upendo wa kweli huuketi pahala hapo.
 

Gluk

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,785
2,000
Dunia ya leo huwezi kupata mapenzi ya dhati bila pesa, kwanza mwanaume unawezaje kujiamini na kumiliki mtoto bila pesa?
PESA, PESA, PESA bila pesa hakuna upendo
vijana tafuteni pesa muache kujipa matumaini hewa.
 

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,066
2,000
Pesa ndo kila kitu kwenye mapenzi. Si leo, tangu bustani Aden. Shetani alimhonga Eva, akamsaliti Adam.
 

legend Babushka

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
498
1,000
Tatizo siyo kuwa na pesa na kumpa mpenzi. Ishu ni ile ya kupata hizo pesa.
Wengi wa vijana uwezo ni mdogo na hata wanaopewa hicho kidogo hawaridhiki.
Ila ni matamanio ya kila mwanaume kuwa na pesa za kutosha kwa ajili ya mwanamke wake.
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
32,574
2,000
Tatizo siyo kuwa na pesa na kumpa mpenzi. Ishu ni ile ya kupata hizo pesa.
Wengi wa vijana uwezo ni mdogo na hata wanaopewa hicho kidogo hawaridhiki.
Ila ni matamanio ya kila mwanaume kuwa na pesa za kutosha kwa ajili ya mwanamke wake.
Hahahah umeongea point ambayo haisemwagi. Big up sana!
Mapenzi pesa, lakini ili upate pesa lazma ufanye kazi kweli, hio kazi huna na haipatikani kirahisi.

Equation haiwezi kubalance😂😂😂
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom