Pepo mchafu katikati ya mtu mwema

Tutanota

Member
Aug 5, 2020
18
77
PEPO MCHAFU KATIKATI YA MTU MWEMA

Ukisoma Katika Biblia Kitabu cha Mathayo 2 Utakutana na Mtu mmoja aloyeitwa Herode. Wakati Mungu akiwa na Mipango yake Hakuna mtu yeyote anaweza Kuzuia. Herode kwa Nguvu zake, Ufalme wake na jeshi lake ila aliposikia Mtoto Yesu kazaliwa na atakuja kuwa mfalme aliagiza Auawe, Bila kujali aliyezaliwa ni mwana wa Mungu, Amezaliwa kwa ajili ya kuikomboa Dunia akiwemo yeye. Herode hakujali hilo yeye alichotaka ni kuangamiza mtu asiye na hatia kws ajili ya maslahi yake binafsi (CHEO) Herode ni sawa na Maadui wako ambao hawaangalii ni kiasi gani cha watu wanategemea uwepo wako katika hiyo jamii.

Nalitazama Sakata la Meya wa Moshi Mjini dhidi ya Herode, Vita kali inayohitaji Roho wa Mungu ili kuziponya Roho chafu za wafuasi wa Herode waliopewa kazi ya kumuangamiza huyu kijana.

Roho mtakatifu amenionesha Anguko la Herode dhidi ya Kijana huyu mwenye maono makubwa katika kutumikia wananchi. Wacha nikwambie leo Ndugu Juma Raibu, Mungu amekuchagua wewe katikati ya watu waliochaguliwa na wanaadamu. Hakuna mtu wa kushinda mkono wa Mungu.

Wakati Wafilisti waliopotaka kumkamata Yesu Kristo mwana wa Mungu ili wamiangamize walimtumia Yuda Eskarioti mmoja wa wanafunzi wa Yesu na Yuda alimsaliti. Usiumizwe na Viongozi wa Dini wanaosimama katika Madhabahu zao na kunena yale yasiyothibitika na kuyapa uhai. Katika Amri kumi za Mungu Amri ya Tisa inasema "Usimshuhudie uongo jirani yako." Hii ni amri ya Mungu. Wewe endelea kutumikia wananchi wa Moshi kwa maana yeyote apingaye Amri ya Mungu basi Mungu atashughulika naye.

Tambua kuna vita unaweza kupita katika Maisha yako si kwasabababu ya Umri wako, ila ni kwa sababu ya Ukubwa wa Maono uliyobeba. Kuna watu wanaingia katika vita si kwasababu ya vile ulivyo leo ni sababu wanataka kuzuia vile utakavyokua kesho.

Usikatishwe tamaa na Hadithi za Uongo dhidi yako ili kuzuia Jitihada zako kwa wananchi kwa maana hata Manabii wa Mungu walipingwa na Mungu alisimama Dhidi yao.

Uzuri ni kwamba yeyote anayejaribu kupigana na Maono ya Mungu aliyoweka ndani yako, Anasababisha Mungu akutetee na kuanza kupigana Vita yako. Sasa Mungu yu katika vita dhidi ya Pepo mchafu katikati ya Mtu mwema.

Bwana amenionesha ushindi dhidi ya Adui wanaodhorotesha jitihada zako kwa wananchi.

Kwa maana katika kitabu cha Yeremia 1:19 Bwana asema

"NAO WATAPIGANA NAWE LAKINI HAWATOKUSHINDA, MAANA MIMI NIPO PAMOJA NAWE ILI NIKUOKOE."

Mungu wetu ni Mkuu.

Rev, Arobogast Seleali
 
Back
Top Bottom