Penzi la kweli halichuji, kwanini wapenzi wanabadilika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Penzi la kweli halichuji, kwanini wapenzi wanabadilika?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Nov 4, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mapenzi yamekuwa yakichukuliwa na baadhi ya watu kama fasheni hali inayowasababishia washindwe kudumu kwa muda mrefu na wapenzi wao.Kimsingi ipo hali ya kujisahau baada ya wapenzi na wanandoa na ndiyo hasa huibua mabadiliko mazuri au mabaya, haieleweki kama ni mzuka lakini imekuwa kama fasheni kwa wanandoa kutokukumbuka enzi hajaitwa mume au mke.

  Mtu anaweza kubadilika kitabia, muonekano, kujali na kama ulikuwa unasikia fununu tu juu ya mwandani wako utaanza kushuhudia 'live' na kuthibitisha ukweli wa ulichokuwa ukiambiwa.Huenda mlikuwa na desturi ya kununuliana zawadi kama maua, kadi, chokoleti tabia hiyo itapotea, hakuna kati yenu atakayekumbuka kitu hicho, ni wachache sana ambao wanakwenda na wakati ndiyo huendelea kuzingatia hilo.Kuna wale ambao walikuwa na tabia ya kukutana kila mara kimapenzi kabla ya kuoana, enzi hizo kila mmoja alitaka kumuonesha mwenzie namna gani alivyo fundi wa 'kuyarudi' ndani ya uwanja wa mapenzi lakini yale manjonjo huadimika kabisa.Kawaida yenu ilikuwa kubadilisha hoteli kwa ajili ya chakula cha jioni lakini tabia hiyo hutoweka, labda kila wiki ilikuwa lazima muende 'out' mara tatu katika kumbi tofauti za starehe na kusherekea uwapo wa mapenzi yenu, hali hiyo itabaki historia tu.

  Hujawahi kusikia mtu anasema "Enzi zangu kila wiki nilikuwa naenda beach na honey wangu we acha tu, siku hizi nimezeeka."Halafu ukimtazama anayetoa kauli hiyo pengine ana miaka 25 tu, lakini majukumu ya ndoa yanamdanganya na kudhani umri umemtupa mkono kumbe tafsiri yake ndiyo inampotosha, elimu zaidi inahitajika kubadili fikra hizi lemavu!Kama mlikuwa na kawaida ya kupitiana wakati wa 'lunch na kwenda kujumuika pamoja nyakati za mchana, taratibu kila mmoja ataanza kuiacha tabia hiyo na kusingizia kazi nyingi, hii ni hatari sana!Wengine hupunguza hata umaridadi, alikuwa smati kila alipoonekana lakini hali hiyo itakuwa kinyume chake baada ya ndoa, hii ni kasumba mbaya jichunguze kama unayo iache mara moja, kwa sababu unajiaibisha mbele za watu na kumchefua hata sweetie wako.Hatari kubwa lakini ya kitaalamu ni kwamba baada ya miezi kadhaa ya ndoa kila mmoja hujihisi kwamba mume/mke wake hana mvuto kama wale ambao hukutana nao barabarani, na wakati huu tamaa ya kuzisaliti ndoa zao huwa juu sana.

  Umakini zaidi huhitajika!Hata hivyo, sababu ya kuanza kumuona wa nje ni bora kuliko uliye naye ndani ni hadaa za macho tu, lakini huchangiwa zaidi na kupungua kwa umaridadi na mpenzi wako kushindwa 'kujiswafi' kama zamani hivyo ukimuona yule ambaye yuko sopsop atakuvutia na kumtamani.Pamoja na hali hiyo mabadiliko yote yana tiba, lazima ufahamu kuwa endapo ulikuwa na 'gerentii' ya kutoka na mwandani wako ijenge na uidumishe, ukiisitisha mtaanza kulaumiana ndani kwa ndani kabla ya watu wa nje kuwacheka na kusema "kumbe ilikuwa nguvu ya soda!"Aidha kuna mabadiliko ya kimaslahi, pengine mtu na mpenzi wake wameketi na kuona wanatumia pesa nyingi viwanja, kwahiyo wanaamua kupunguza au kuacha ili kujenga maisha bora kama familia, si unajua tena ukishaoa na utu uzima tayari umewadia.

  Kimsingi mabadiliko mengi ni yale yanayochusha, haiwezekani upunguze kumridhisha mke au mumeo, haipendezi upunguze usafi, haivutii uache yale manjonjo yaliyokuwa 'yakimkong'oli' mpenzi wako mpaka akawa anajiapiza kutokukuacha.Yapo mabadiliko mengi, lakini zaidi tujirekebishe na tuelewe kwamba mapenzi ya kweli hayajuchi na tukumbuke kwamba, baadhi ya vitu tulivyokuwa navyo ndivyo viliwavutia wenzi wetu na kukubali kufunga nasi ndoa kwa hiyo tukiacha tunakuwa tunawakatili.
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Please kabla hatujaenda mbali Mkuu, naomba weka aya....
   
 3. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sawa nashukuru kwa kunikumbusha
   
 4. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  dah, paragraphs zingesaidia kusoma hii kitu
   
 5. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Duh! ndeefuuuu, lakini imetulia. Ni kweli wanadamu tuna hulka ya kutamani kilicho kwenye milki ya mwanadamu mwenzetu bila kufikiri huyo anayekimiliki anakihudumia, kitunza vizuri ndo maana kikatuvutia. Ni vyema kutambua kuwa mapenzi ni sanaaa na ni vyema yakaboreshwa mara kwa mara ili yasizoeleke machoni pa watumiaji wa sanaa hiyo.

  Asante kwa uzi huu, umenipa sababu ya kufurahia weekend yangu
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Haya keshaweka tuendelee kujadili!

  Jpinduzi umenena pwent tupu hasa hapa mwishoni na ni janga kuu kwenye ndoa nyingi i tell me!
   
Loading...