Habari za saa hizi,
Jamani Jamiiforums siku hizi imejaa maigizo....sielewi watoto ambao hawajapevuka ni wengi au ndo penye wengi pana mengi??
- Kuna wanaopendana,wakaachana hadharani(LOVE IS IN THE AIR):A S wink:
Tujifunze kuweka mambo yetu personal private jama...haumnufaishi yoyote kuanika mambo yako hadharani bali unajiexpose na unawapa vizabizabina maneno ya kusema...na uhusiano huo unakuwa na nafasi kubwa ya kutokudumu!!Hakuna mtu anayetaka kujua upo na nani na kwaajili gani au umeachana nae lini.Sisemi kwa ubaya na sikatai kupenda na kupendwa raha lakini kumbuka hio raha yako si ya wote,tunafurahi tukiona watu mnapendana na mapenzi shamsham lakini keep it low people,cause thats how matured people do it...YOUR LOVE LIFE IS YOUR PERSONAL BUSINESS!!
- Kuna wanaokuja na mada za ajabu ambazo hazina misingi yoyote sielewi watu hawa wanafikiri nini??
Tuwe na heshima,fikiri kabla hujaandika kitu,hii ni sehemu yenye watu tofauti wa rika tofauti.Kuna wengine wanakuzaa,kuna mpaka babu zetu,jiheshimu nawe utaheshimiwa.Tutoe mada ambazo zitakuwa na manufaa kwetu ambazo zitachangamsha ubongo wetu na kujenga jamii yetu.
- Kuna ambao wanajiona wapo huru kuandika/kuquote utumbo wowote ule,LADY/GENTLEMAN PLEASE....
Ndio hatujuani lakini tunatambuana utu wetu kutokana na fikra zetu kutokana na michango yetu.na michango hiohio inatutambulisha sisi ni watu wa aina gani.
- Kuna drama queens na kings ambao kila kukicha ni full dramas.
Sijui kama kuna kitu ambacho hakiwatokei,misukosuko yote huwapata wao,NAJUA LIFE IS UNFAIR...Lakini kila mtu na shida zake.Watu wakiamua kuzianika hapa tutatafutana....
- Kuna wale ambao wana ID tatu tatu,whom are you fooling?
Ni hayo tu kwa sasa kama una ya ziada ongezea....