Peniela (Story ya kijasusi)

SEASON 2

SEHEMU YA 37

“ Ahsante sana kijana wangu lakini kuna jambonataka nikuweke wazi.Nimekueleza jambo hili lakini tafadhali sana naomba usimweleze Peniela kwani ndiyo yalikuwa makubaliano yangu na John na sikuwahi hata mara moja kuyavunja kwa kumueleza Peniela kwa hiyo naomba na wewe usithubutu kumweleza chochote.Iko siku John mwenyewe atamueleza “ akasema Bi Bernadetha

“ Nimekuelewa bibi na sintafanya hivyo.Nitakachofanya nitamueleza tu kwamba nimekuja kukutembelea na kukuta unaumwa na nitamsisitiza kwamba aje akutembelee.” akasema Mathew kisha akamuaga Bi Bernadetha na kuondoka

“ John Mwaulaya ni baba yake Peniela??..akajiuliza Mathew akiwa garini
“ Hapana hainiingii kabisa akilini eti John Mwaulaya awe ni baba yake Peniela halafuakatae mwanae kumfahamu.Hili ni jambolisilowezekana.Kama kweli ni baba yakena hakutaka peniela afhamu na badala yake akatambulishwa kwake kama mfadhili basi kuna kitu alikuwa anakificha na ambacho lazima nikifahamu.Amakweli dunia imekuwa ndogo sana.Hatimaye mimi na John mwaulaya tunakwenda kukutana tena uso kwa uso.This time I’ll be the one making him talk.” Akawaza Mathew



ENDELEA…………………

Abiria waliokuja na ndege ya shirika la ndege la Emirates walianza kutoka nje ya uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere.Peniela akiwa ameongozana na Jacob na Francis tayari walikuwapo hapo uwanjani wakiwasubiri wageni wao waliofika na ndege hii.Mikononi mwao kila mmoja alikuwa na picha mbili za wageni wanaowasubiri kwani hawakuwahi kukutana nao hata mara moja.Ni Peniela aliyekuwa wa kwanza kumtambua mmoja wa wageni wale waliokuwa wakiwasubiri.Nickson Strawberry alitambulika kwa urahisi kutokana na mtindo wake wa nywele .Alikuwa na nywele ndefu alizozikusanya kwa nyuma na kuzifunga.

“ That’s Nickson “ akasema Peniela na kumuita Nickson akasimama akageuka na kutmazama Peniela, akamfuata.

“ hallow Nickson.karibu sana Tanzania” akasema Peniela

“ Ahsante sana.” Akajibu Nickson

“ Naitwa Peniela na hawa ni wenzagu Jacob na Francis” Peniela akafanya utambulisho mfupi
“ Peniela !.akashangaa Nickson
“ wewe ndiye Peniela?! Akasema Nickson na kumkumbatia Peniela kwa furaha
“ Nimefurahi sana kuonana nawe Peniela” akasema Nickson kisha akawaita wenzake akawatambulisha.Alikuwepo Joe Levernsky mmarekani mweusi ,alikuwepo pia Bill beherds,Stanley Phoenix,Alexander Piscat na Edwin Washington.Kisha salimiana wakaelekea katika maegesho wakaingia katika magari mawili waliyokuja nayo akina Peniela na kuondoka
“ Nilitegemea kumuona Osmund hapa uwanjani.Yuko wapi?akauliza Nickson aliyekuwa amekaa kiti cha mbele pembeni ya Peniela

“ Osmund? Peniela akashangaa

“ Ndiyo” akajibu Nickson

“ Ina manaa hamna taarifa? Peniela naye akashangaa

“ taarifa gani penela?

“ Kuhusiana na Osmund”
“ Hatuna taarifa zozote kuhusiana na osmund.Tulipopanga safari hii yeye ndiye tuliyekuwa tukiwasiliana naye kwani ndiye aliyekuwa akiongoza team SC41 badala ya John lakini kwa siku kama tatu hivi hapatikani simuni hivyo ikatulazimu kwenda nje ya taratibu za team Sc41 na kuwataarifu vijana ofisi kuu dare s salaam kuhusu ujio wetu.Mara nyingi safari kama hizi hufanyika kwa siri.Yuko wapi Osmund? akauliza Nickson

“ Nini kinaendelea katika Team SC41? Kama tukio linaweza likatokea huku Tanzania na ninyi makao makuu msilifahamu basi ni hatari sana.Inaonekana wazi kwamba hakuna mawasiliano kati ya ofisi ya Dar es salaam na ofisi kuu Marekani.Ninaamini Team SC41 Tanzania ina watu wengi ambao wangeweza kuwapa taarifa.Kwa nini washindwe kutuma taarifa za matukio yanayotokea huku ? akauliza Peniela
“ Unayosema Penielani ya kweli kabisa.Toka John mwaulaya alipoanza kuumwa kumekuwa na tatizo katika ofisi ya Dar es salaam.Alimteua Osmund lakini bado hali ilikuwa ile ile.lakini usijali tumekuja kuweka mambo sawa na kila kitu kitakwenda vizuri sana.Kuna taarifa gani ya kuhusiana naOsmund? Akauliza Nckson.Peniela aliyekuwa akiendesha akapunguza mwendo na kusimama katika foleni kisha akasema
“ Osmund amefariki dunia”

“ Osmund amefariki dunia? Lini ?Akashangaa Nickson

“ Ndiyo tena si Osmund pekee bali na Dr Burke ambaye alitumwa kuja kufuatilia hali ya ugonjwa wa John .” akawema Peniela na kumstua sana Nickson ,aliyebaki anamtazama Peniela hadi pale gari zilipoanza kusogea

“ Peniela taarifa hizi ni ngeni kabisa kwetu.Hatukuwa tukifahamu chochote kilichotokea.Hapa ndipo unapokuja ukweli kwamba John mwaulaya alikuwa na nafasi kubwa sana katika team SC41.Kabla hajaumwa mambo kama haya hayakuwepo kabisa.Hakuna mtu yeyote aliyekamatwa hadi hivi sasa kuhusiana na mauaji hayo? Akauliza Nickson

“ Hapana.hakuna aliyekamtwa hadi hivi sasa “ akajibu Peniela.Nickson akainama akafikiri halafu akainua kichwa na kusema

“ Peniela kuna tatizo kubwa Team Sc41 Tanzania.Kuna kitu kinachoendelea hapa kwa sababu haiwezekani watu wawili wote team SC41 wauawe kwa wakati mmoja.Lazima tulifanyie uchunguzi suala hili ili tufahamu ukweli.Ninahisi kuna kitu hakiko sawa ndani ya team SC41 na hii ni hatari sana” akasema Nickson

“ Unahisi Dr Burke na Osmund waliuawa na mtu toka ndani ya team SC41? Akauliza Peniela

“ Sina hakika bado kama ni mtu toka ndani ya team SC41 lakini mazingira ya vifo hivyo yanatia shaka sana kwani inaonekana wazi waliuawa na mtu aliyekuwa na sababu Fulani.Lakini tutafahamu kila kitu baada ya kufanya uchunguzi wa kina.” Akasema Nickson
“ Ninajiuliza endapo tusingekuja,tusingetaarifiwa kuhusu kifo cha Osmund na Dr Burke? Huu ni udhaifu mkubwa sana umeonekana katika Team Sc41.Kuna kazi kubwa inatakiwa kufanyika kuisuka upya team SC41. Ahsante sana Peniela kwa taarifa hizi.kazi yetu itakuwa kubwa sana tofauti na nilivyokuwa nikitazamia.Team SC41 tanzania inatakiwa isukwe upya ili iwe imara kama ilivyokuwa mwanzo.Tukiachana na hayo vipi hali ya John mwaulaya? Akauliza Nickson

“ hali ya John si nzuri hata kidogo.kwa siku kadhaa hapo kati kati hali yake ilikuwa nzuri na wote tukawa na matumaini kwamba muda si mrefu atapona lakini ghafla hali yake ilibadilika na mpaka leo bado si nzuri.Anahitaji matibabu makubwa,kuna rafiki zake madaktari wanaweza wakaingia muda wowote kwa ajili ya kuja kumfanyia upasuaji” akasema Peniela
“ hakuna haja tena ya hao madaktari.Tumekuja na madaktari bingwa wawili kwa ajili tu ya kuja kuangalia ukubwa wa tatizo la John na kumpatia tiba.John anatakiwa kupatiwa tiba toka kwa madaktari wanaotambuliwa na Team SC41 .Usijali atapona tu” akasema Nickson na safari ikaendelea kimya kimya
“watuhawa wanataka kuisuka upya Team SC41 ili iwe na nguvu kama zamani Wakati nikiwa katika mikakati ya kuisambaratisha.Nimekwisha azimia kulifanya hilo na lazima nihakikishe linafanikiwa.Halafu kuna kitu nimekikumbuka kuhusiana na mauaji ya Dr Burke na Osmund.Nina hakika kabisa John alihusika katika vifo vya Dr Burke na osmund.Hawa jamaa wakifanya uchunguzi wao na kugundua kwamba John alishiriki sijui watafanya nini,nahisi wanaweza hata wakamuua.” Akawaza peniela huku safari ikiendelea.
Josh alimtaarifu kwamba kila kitu kuhusiana na mahala pakufikia wageni wale kilikuwa kimekamilika,Peniela akawapeleka kwanza hotelini kila mmoja akapata chumba chake halafu wakaondoka tena kuelekea nyumbani kwa John Mwaulaya ambako walipokelewa na Josh na moja kwa moja wakapelekwa chumbani kwa John mwaulaya ambaye alifurahi kuonana tena na watu wale baada ya muda mrefu.Kisha salimiana wote wakatoka na kuelekea katika sebule ya John Mwaulaya kwa ajili ya maongezi.Nickson ndiye aliyeongoza kikao kile kifupi

“ Peniela ,Josh,Jacob na Francis,kwa niaba ya wenzangu wote napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana kwa mapokezi yenu mazuri.Sina haja ya kurudia kujitambulisha tena kwani tayari sote mnatufahamu kwa hiyo basi nitakwenda moja kwa moja katika mambo makuu yaliyotuleta hapa.’ Akasema Nickson
“ jambo kubwa la kwanza lililotuleta hapa ni kuhusiana na operesheni 26B.Hii ni operesheni muhimu sana kwetu kwa hiyo tmelazimika kuja na kuifuatilia kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kwamba inakwenda kama inavyotakiwa na inakamilika.Tulimpa maelekezo Osmund kwamba ndani ya mwezi huu tunatakiwa tuwe tumeikamilisha operesheni hii na kuipata package hiyo muhimu sana kwa marekani na dunia kwa ujumla.Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari ni kwamba mawasiliano kati ya Dr joshua na wanunuzi wa package hiyo yamekwisha anza na muda wowote wanaweza wakafikia makubaliano.Tayari akaunti za benki zimekwisha funguliwa ambako wanunuzi hao wanatakiwa kuweka kiasi kikubwa sana cha fedha na kisha watakabidhiwa mzigo wao.Kwa gharama zozote zile hatutaki jambo hili litokee kwa hiyo lazima tuhakikishe tunaipata hiyo package.kwa hiyo nahitaji kusikia toka kwenu mmefikia wapi hadi hivi sasa? Akauliza Nickson

“ Nadhani peniela anaweza akajibu vizuri zaidi swali lako kwani yeye ndiye kiongozi mkuu katika operesheni 26B” akasema Josh
“ Ni kweli kama alivyosema Josh.Mimi ndiye niliyekabidhiwa jukumu la kuhakikisha kwamba tunaipata pachage hiyo_Operesheni hii ilisimama kwa muda wa kama mwaka mmoja hivi baada ya mimi kuingia matatizoni lakini baada ya matatizo kumalizika operesheni imeendelea tena na ninapenda kukuthibitishia kwamba tumepiga hatua kubwa tayari.Ili kujiweka katika hatua nzuri ya kuipata package hiyo tayari nimejenga uhusiano wa kimapenzi na rais Dr Joshua pamoja na katibu wake .Vilevile tunaye captain Amos.Huyu ni mshirika mkubwa wa rais katika bashara hii na yeye ndiye ambaye ananipa taarifa za kila kinachoendelea kwa hiyo ushirikiano baina yetu ni mkubwa na tunachoshubiri kwa sasa ni siku ambayo package hiyo itatolewa ikulu kisha tuichukue.” Akasema peniela
“ Hongera sana peniela.Umefanya kazi kubwa na nzuri.Sisi tutakuwa nyuma yako kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda vizuri.Tutapata wasaa mzuri wa kujadili kwa upana kuhusiana na namna bora tunavyoweza kulikamilisha jambo hili hapo baadae.”akasema Nickson.

“ Nickson kuna jambo nataka kuuliza .Hiyo package ina nini ndani yake? Nimeyatoa mhanga maisha yangu kwa ajili ya kitu ambacho sikifahamu.Nadhani ni wakati mzuri sasa wa mimi kufahamu kitu ambacho nimekuwa nikihangaikia kwa muda huu mrefu ni kitu gani hasa.” Akauliza peniela
“ peniela wewe ni teamSC41 na ukiwa ndani ya kikundi hiki unakuwa ni kama askari mpambanaji,ukiambiwa fanya kitu Fulani basi unakifanya bila kuhoji.Sintaweza kukueleza kwa sasa kwani ni nje ya taratibu za team SC41.Una swali lingine?”akasema Nickson.Peniela akatingisha kichwa ishara kwamba hana tena swakli lingine lakini moyoni alikuwa amekasirika sana

“ Tuendelee.Jambo la pili lililotuleta hapa ni kuhusiana na afya ya John Mwaula.Kama mnavyofahamu ni kwamba John Mwaulaya hawezi kutibiwa katika hospitali za serikali wala haruhusiwi kuonekana nchini marekani kwa hiyo anatakiwa kutibiwa na madaktari walio ndani ya team SC41 pekee na ndiyo maana katika ujio huu tumeambatana na madaktari bingwa wawili wa mambo ya mishipa ya fahamu na kazi iliyowaleta hapa ni kumuhudumia John.”akasema Nickson

“ jambo la tatu ambalo tutalifanya tukiwa hapa ni kuhakikisha Team SC41 inasukwa upya na inarejea kuwa na nguvu kama zamani kabla John hajaanza kuumwa na jambo la mwisho kabisa tutahakikisha mwili wa Dr Burke unarejeshwa nyumbani kwa mazishi.Hayo ndiyo mambo ambayo tuyafanya katika kipindi ambacho tutakuwa hapa Dar es salaam.” Akasema Nickson.Sebule yote ilikuwa kimya.Nickson akaendelea

“ Nadhani mpaka hapo tumeelewana kwa hiyo kinachofuata sasa hivi sote tutaelekea kupata chakula cha mchana na baada ya hapo madaktari watarejea hapa kwa ajili ya kuanza kumfanyia John uchunguzi na wengine tutaelekea katika ofisi kuu ya team SC41 Tanzania tutasalimiana na watu wote pale na shughuli itaanzia hapo.Tukisha pata chakula cha mchana madaktari watarejea hapa ili waendelee kumfanyia uchunguzi John wakati sisi tukiendelea na kazi nyingine.Ninachoomba toka kwenu ni ushirikiano wenu mkubwa kwani bila ninyi hakuna tutakachoweza kukifanikisha.Kipindi hiki kifupi tutafanya kazi usiku na mchana hadi tuhakikishe kwamba tumefanikisha mambo yote.” Akasema Nickson

“ Nickson ninashukuru sana kwa ujio wenu huu ambao utakuwa na faida sana kwetu sote na team SC41.Ninashukuru sana kwa kuwaleta madaktari kwa ajili ya kuangalia afya ya John.Kwa kuwa jioni ya leo tutakuwa pia na kikao kikubwa kujadili kwa upana kuhusu mambo haya yote hususan operesheni 26B basi kwa mchana huu sintaweza kupambatana nanyi kuna jambo la muhimu na kwenda kulishughulikia ambalo linahusiana pia na operesheni yetu.Jacob na Francis watawapeleka katika ofisi kuu na mtakutana na watu wengine wote huko” akasema Peniela.
“ sawa peniela hakuna tatizo.Tutaonana jioni ya leo” akasema Nickson kisha wakaagana na kuondoka na kuwaacha Josh na peniela
“ Kazi imeanza.Wiki hii itakuwa ni wiki ngumu sana kwa Team SC41.Mambo mengi yatafanyika ndani ya wiki hii” akasema Josh,Peniela akamtazama kwa makini na kusema
“ Josh kuna kitu nataka kukuuliza na tafadhali naomba unipe jibu la kweli” akasema Peniela

“ Uliza chochote Peniela nakuahidi nitakueleza ukweli” akasema Josh.Peniela akamtazama na kuuliza
“ nani alimuua Dr Burke na Osmund?
Swali lile likamstua sana Josh.Alibabaika akasindwa ajibu nini

“ Naomba unijibu Josh.Nani alimuua Osmund na Dr Burke? Uko karibu sana na John muda wote na John hakuwa akimtaka kabisa Dr Burke aje na nina hakika ni yeye ndiye aliyetoa amri Dr Burke auawe .Kwa kuwa yeye hawezi kuifanya kazi hiyo lazima alimtuma mtu toka ndani ya team SC41.Niambie nani alifanya mauaji yale? Nina hakika unafahamu.” akasema Peniela.
“ Kwani kuna nini Peniela? Dr Burke na Osmund wamekwisha fariki na suala hili liko mikononi mwa polisi wakilifanyia uchunguzi”

“ Unawaona watu hawa waliokuja? Tayari wamehisi kwamba kuna mtu ndani ya Team SC41 ndiye aliyefanya mauaji yale na wanaanza uchunguzi wao mara moja na nina hakika lazima watampata na wakimjua nadhani unafahamu kitu watakachomfanyia.Josh kama unamfahamu mtu aliyefanya mauaji yale tafadhali nieleze” akasema Peniela.Sura ya Josh ilibadilika na alionekana kuogopa sana..
“ Peniela its me” akasema Josh.Peniela akamuangalia kwa mshangao mkubwa.

“ katika watu wote sikutegemea kama ni wewe ambaye unaweza ukafanya kitendo hiki” akasema peniela

“ Peniela nilifanya kwa kuwa John aliniomba nifanye.Siku zote nimekuwa mtiifu kwa John na hata aliponituma nikaifanye kazi hii sikusita kufanya hivyo.John alidai kwamba Dr Burke alikuwa na lengo la kumuua na tulitakiwa kumuwahi.Kama tusingemuwahi Burke basi angemuua John.Tafadhali Peniela kama kuna lolote unaloweza kunisaidia katika hili naomba unisaidie” akasema Josh.Peniela akainama akafikiri kidogo na kusema
“ Kwa kuwa ni John ndiye aliyekutuma nitakusaidia,tutatafuta namna ya kuweza kulitatua jambo hili.” Akasema Peniela.


*****


“Lazima leo nionane uso kwa uso na John mwaulaya.Lazima ukweli kuhusiana na Peniela ujulikane leo.Jason anapafahamu nyumbani kwa John kwani ndiko alipelekwa siku aliyotekwa”akawaza Mathew baaad ya kutoka katika kituo cha kulele watoto yatima alikolelewa Peniela.Akachukua simu akampigia Jason.
“ habari za asubuhi Jason” akasema Mathew baada ya Jason kupokea simu
“ habari nzuri sana Mathew.Habari za toka jana? Akauliza Jason

“ habari nzuri Jason.Uko wapi mida hii?
“ kwa sasa niko ofisini kwangu.”

“ Jason nahitaji kuonana nawe.Nielekeze mahala ofisi yako ilipo ili nikufuate hapo” akasema Mathew na Jason akamuelekeza mahala iliko ofisi yake .

“Kwa mara ya kwanza bada ya miaka mingi hatimaye nakwenda kukutana ana kwa ana na John Mwaulaya mtu ambaye aliiteketeza familia yangu.Kwa leo sintamfanya lolote kwani ninakwenda kwa ajili ya suala la Peniela lakini safari nyingine nitamfuata rasmi kwa ajili yangu na ninahisi huo utakuwa ndio mwisho wake.Kwa kumpa salamu tu,leo lazima aeleze ukweli wote kuhusiana na Peniela.Wakati ule John ndiye aliyekuwa na nguvu na kunifanya hadi nikaikimbia nchi yangu lakini safari hii mambo yamebadilika na mimi ndiye mwenye nguvu kuliko yeye.He will talk “ akawaza Mathew na mara simu yake ikaita.Alikuwa ni rafiki yake wa kutoka nchini Israel ambaye alimtumia zile karatasi zilizoibwa ikulu zilizokuwa zimeandikwa fomula za kisayansi
“ hallow Yash “ akasema Mathew

“ Mathew habari za Dar es salaam?
“ habari za huku nzuri sana .habari za huko?
“ Hata huku kwema tu” akajibu yash
“ Mathew tayari nimeikamilisha ile kazi uliyoniomba nikusaidie.Samahani imechukua muda kidogo lakini ilinilazimu kukutana na wanasayansi wakubwa ili kuweza kutambua kilichoandikwa katika zile karatasi.Nimekutumia kila kitu katika anuani yako ya barua pepe utasoma na kuelewa kila kitu”akasema Yash
“ Ahsante sana yash kwa msaada wako mkubwa.” Akajibu Mathew

“ Mathew karatasi zile umezitoa wapi? Akauliza Yash

“ Kuna jambo nalichunguza kwa sasa na ndani ya uchunguzi huo nikazipata karatasi hizo.Kwa nini umeuliza hivyo Yash?
“ nimeuliza hivyo kwa sababu ya ukubwa wa kitu kilichoandikwa ndani ya zile karatasi.Kama ni kitu hicho kipo kweli basi ni kitu cha hatari kubwa sana lakini kama hakipo basi karatasi hizo ni za kutunza sana kwani ni hatari mno na sijui zimefikaje huko.”
“ unaweza ukanipa japo kwa ufupi ni kitu gani hicho ? Akauliza Mathew

“ Nimekufafanulia kila kitu katika barua pepe niliyokutumia.” Akasema Yash
“ Ahsante sana Yash”

“ Mathew ,nitakupigia tena simu jioni ili tuongee vizuri zaidi” akasema Yash na kukata simu

“ Nini kimeandikwa katika zile karatasi kiasi hata cha kumstua Yash ? Lazima kitakuwa ni kitu kikubwa na kizito na ndiyo maana akina Edson walitaka kuziuza kwa mabilioni ya pesa” Akawaza Mathew akiwa njiani kuelekea ofisini kwa Jason
Aliwasili katika ofisi za Jason wakasalimiana na bila kupoteza wakati Mathew akauliza

“ Jason unaweza kupakumbuka nyumbani kwa John Mwaulaya ulikopelekwa siku ile”

“ Ndiyo ninapakumbuka.” Akajibu Jason

“ Ninaomba unipeleke” akasema Mathew
“unataka kwenda nyumbani kwa John mwaulaya? Jason akashangaa
“ Ndiyo nataka kwenda kuonana na John Mwaulaya.Kuna mambo ambayo anatakiwa kuyaweka wazi kuhusiana na Peniela”
“ mambo gani hayo Mathew? John ni mgonjwa unadhani anaweza akakueleza chochote kwa hali aliyonayo ? akauliza Jason
“ He will talk.Take me there” akasema Mathew.Jason huku akiwa na wasi wasi akavaa koti lake na kutoka wakaingia katika gari la Mathew na kuondoka kuelekea nyumbani kwa John Mwaulaya.Safari ilitawaliwa na maongezi machache sana hadi walipofika katika jumba la John mwaulaya.

“ Hapa ndipo nyumbani kwa John mwaulaya” akasema Jason
“ Wow ! jumba kubwa na la kifahari.Hawa watu ni kweli wanalipwa pesa nyingi sana kama alivyosema peniela.” Akasema Mathew na kisha akasimamisha gari katika geti .

“ Shuka kabonyeze kengele “ akasema Mathew.Jason akashuka na kwenda getini akabonyeza kengele mara tatu halafu akasuburi.Baada ya dakika tano mlango wa geti ukafunguliwa .Aliyeufungua alikuwa ni Josh ambaye alipatwa na mstuko mkubwa alipoonana uso kwa uso na Jason.Kwa sekunde kadhaa walibaki wanatazamana.
“ Jason !!..akasema Josh
“ What brings you here? Akauliza Josh.Jason akafumbua mdomo kutaka kusema kitu lakini akasita baada ya kusikia mlango wa gari unafunguliwa hakujibu kitu akageuka baada ya kusikia mlango wa gari ukifunguliwa,akashuka Mathew.Josh alimtazama vizuri sana na kuikumbuka ile sura.Ni yule mtu aliyeonekana katika kamera za nyumbani kwa Peniela.Akaingiwa na woga

“ hallow “ akasema Mathew
“ Josh .Naitwa Josh “ akasema Josh na kumpa mkono Mathew

“ Josh naitwa Mathew” akasema Mathew
“ Karibuni sana.Niwasidie nini? akauliza Josh
“ Nahitaji kuonana na John Mwaulaya.”
“ John Mwaulaya? Nani kawaambia John anaishi hapa? Akauliza Josh
“ Josh naomba usinipotezee muda wangu.Utatupeleka kwa John mwaulaya au nitumie nguvu? Akasema Mathew huku akipeleka mkono mahala iliko bastora yake.Josh akaogopa akafungua geti Mathew akamwambia Jason aingize gari ndani .Jason akalitambua gari la Peniela lililokuwamo mle ndani.
“ Peniela yuko hapa? Akauliza Jason
“ Ndiyo yupo”akajibu Josh

“ Ok vizuri sana.Tupeleke aliko John” akasema Mathew na Josh akaanza kuwapandisha ghorofani kilipo chumba cha John mwaulaya.Ndani ya chumba cha John alikuwemo Peniela na Dr martin ambaye amekuwa akimuhudumia John mwaulaya kwa muda mrefu.Mlango ukafunguliwa akaingia Josh akiwa amefuatana na Mathew na Jason.Wote mle chumbani wakastuka sana.

“ Mathew ! Jason !..akasema peniela kwa mshangao na kumfanya John Mwaulaya ageuze shingo yake na kutazama mlangoni.
“ mungu wangu ! akasema John mwaulaya kwa sauti ndogo .Naye pia alikuwa ameogopa sana.Mathew akasogea hadi karibu na kitanda cha John Mwaulaya akamtazama kwa macho makali sana.Peniela akaogopa
“ John mwaulaya,hatimaye tumeonana tena uso kwa uso .” akasema Mathew
“ Mathew what are you doing here? Akauliza Peniela

“ peniela nimekuja kuonana na John Mwaulaya.Nimefurahi sana kukukuta na wewe hapa ili usikie kile ambacho ninataka John akieleze mbele yako”

“ Mathew ,John is sick and he cant talk” akasema Peniela kwa wasi wasi.

“ he will talk” akasema Mathew.

“ Mathew !!..what are you doing? Akasema peniela huku akipiga hatua kumuendea Mathew.Jason akamzuia.
“ John mwaulaya,japokuwa imepita mika ming lakini nina hakika sura hii bado unaikumbuka vizuri sana.kama umeisahau nitakuja siku nyingine kukukumbusha lakini kwa leo nimekuja kwa ajili ya jambo moja tu, Peniela.” Akasema Mathew na kumstua kidogo Peniela.John mwaulaya alikuwa anatetemeka.
“ Ulimpeleka Peniela usiku katika kituo cha kulelea watoto yatima na ukadai kwamba umemchukua toka kwa mama yake na ukataka alelewe pale.Ulimwambia mama mwenye kile kituo kwamba peniela ni mwanao lakini hukutaka afahamu kama wewe ni baba yake na badala yake ukajiita mfadhili wake.Umemfanyia Peniela mambo mengi mabaya na kuyaharibu kabisa maisha yake,umemuingiza katika Team SC41 na umezifuta kabisa ndoto za maisha yake na mmekuwa mkimtumia kwa kazi zenu kwa manufaa ya serikali ya marekani.Ninataka mbele ya Peniela uungame ukweli wewe ni baba yake mzazi? Akauliza Mathew kwa ukali.Peniela alipigwa na butwaa asiamini kile alichokisikia .Akamkazia macho John mwaulaya kusikia atatoa jibu gani.

“ John answer me!!..akafoka Mathew

“ Sifahamu chochote juu ya hayo unayoyasema” akasema John kwa sauti ndogo.

“ John nitazame vizuri machoni.Nina uhakika na ninachokisema na sina utani hata kidogo.” Akasema Mathew na kumuinamia John
“ John nitazame vizuri machoni.I’m a monster kwa hiyo naomba usiniudhi.Nataka useme ukweli kwamba wewe ni baba yake mzazi Peniela? Akasema kwa ukali Mathew

“ I don’t know anything” akajibu John kwa sauti ndogo .

“ John this is the last chance ..are you Peniela’s father? Akauliza Mathew kwa ukali.John akajibu kwa kumfanyia ishara kwamba haelewi chochote.Mathew akakasirika na kuchomoa bastora yake.Peniela akaogopa sana
“ Mathew what are yo doing? Akauliza lakini Mathew hakumjali

“ Mathew unataka kufanya nini? Akauliza Peniela kwa wasi wasi
“ I’ll count to three and if you cant answer me I’m going to kill you John ! akasema kwa ukali Mathew

“ Mathew No ! Don’t do that !! akasema Peniela huku akilia
“ Jason hold her” Mathew akamuamuru Jason amshike Peniela ili asimsogelee.

“ Three…..!!!akaanza kuhesabu Mathew huku amemuelekezea John bastora
“ Two ….!!!!
“ Mathew noo!!!!..dont do that !!..akapiga kelele peniela.
“ On………..” Kabla Mathew hajamaliza kutamka John Mwaulaya akasema
“ Ok ok..I’ll tell you..put your gun down” akasema John mwaulaya aliyekuwa akitetemeka
“ ok tell her the truth! akasema kwa ukali Mathew huku akimtazma John kwa macho ya hasira
John akamfanyia ishara peniela asogee karibu na kuanza kumsimulia kilichotokea kuhusiana na wazazi wake.Alisimulia mkasa mzima uliotokea na kupelekea kuwaua wazazi wote wa peniela.Peniela alibubujkwa na machozi mengi.John akamgeukia Mathew
“ Hiyo ndiyo historia ya Peniela.Nilishindwa kabisa namna ya kumueleza nikiogopa kumuumiza na ndiyo maana nilitaka afahamu kuhusu yeye baada ya mimi kufariki dunia.Nilijua lazima atanichukia sana akifahamu kwamba mimi ndiye niliyewaua wazazi wake.Nilimuwekea kila kitu kuhusiana na historia yake katika makasha matatu ikiwamo na picha za wazazi wake.” Akasema John.Peniela alimuangalia kwa hasira huu machozi yakimtoka.

“Leo nilikuja kwa ajili ya Peniela.Safari ijayo nitakuja rasmi kwa ajili yangu.Jiandae “ akasema Mathew na kutoka Peniela akamfuata

“ Mathew thank you so much.Umenisaidia nimefahamu jambo kubwa sana.Sikuwa nikifahamu chochote kuhusiana na wazazi wangu.John amenificha siri hii kwa miaka mingi.I hate that bastard so much.”akasema Peniela

“ Elibariki aliniomba nikusaidie kuufahamu ukweli kuhusiana na asili yako na ninashukuru ukweli umedhihiri.Naomba ukweli huu usivuruge mipango yetu.”

“hakuna kitakachovurugika Mathew.I’m a very strong woman.Kila kitu kitakwenda kama tulivyokipanga.hata hivyo nina swali nataka kukuuliza.”

“ Uliza Peniela”

“ Ulipomuelekezea John bastora na kuanza kuhesabu,ulidhamiria kumpiga risasi kama asingesema chochote ?
Mathew akatabamu kidogo na kusema

“ No ! I just wanted him to talk”

“ ahsante Mathew.Ahsante sana.Tutaonana jioni .Mwambie Elibariki nashukuru sana kwa kunijali.Bila yeye kuwa na mawazo haya nisingeufahamu ukweli kuhusu wazazi wangu“ akasema peniela na kurejea tena ndani akakuta hali ya John mwaulaya imebadilika ghafla.Ikawalazimu wawaite haraka wale madaktari wawili waliokuja toka marekani kwa lengo la kuja kuangalia afya yake.


MCHAKATO WA KUIPATA PACKAGE MUHIMU UMESHIKA KASI NA KILA UPANDE UNAJIANDAA KUIPATA NINI KITATOKEA ? FLAVIANA MKE WA JAJI ELIBARIKI BADO YUKO MAHUTUTI HOSPITALI NINI HATIMA YAKE? NINI HATIMA YA JOHN MWAULAYA? KIKUNDI KIDOGO CHA WATU WENYE NGUVU NA USHAWISHI KIKIONGOZWA NA RAIS MSTAAFU KINAPANGA KUMUONDOA MADARAKANI DR JOSHUA NA WANAFIKIRIA KUMPENDEKEZA JAJI ELIBARIKI KUWANIA NAFASI HIYO JE WATAFANIKIWA LENGO LAO ? MWISHO WA SIMULIZI YA PENIELA SEASON 2..TUKUTANE TENA KATIA SEASON 3 HIVI KARIBUNI
 
PENIELA SEASON 3


EPISODE 2


MTUNZI : PATRICK.CK


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Stop the car !!!..akasema Jason kwa ukali
“ Unataka kushuka? Akauliza Mathew

“ Mathew simamisha gari nishuke !!!..akasema Jason .Mathew hakujibu kitu akaendesha gari hadi katika kituo cha daladala kilichokuwa karibu akasimamisha gari na Jason akashuka kwa hasira na kuubamiza mlango na kutamka neno ambalo Mathew hakulisikia vizuri.Mathew hakumjali akaingiza gari barabarani na kuendelea na safari yake
“ stupid !!..akasema Mathew
“ Katika maisha yangu yote ndani ya kazi hii nimekutana na watu wengi makatili lakini si kama John Mwaulaya.Mtu huyu aliiteketeza familia yangu bila huruma na ametoa roho za watu wengi.Hata hivyo siku zake zinahesabika .Nitarudi tena kwake kwa mara nyingine na hii itakuwa ni zamu yangu.Picha za moto ule mkubwa ulioiteketeza familia yangu bado haijafutika kichwani kwangu.Nitamuua John taratibu sana na kwa mateso makali ” akawaza Mathew huku akiuma meno kwa hasira


ENDELEA……………………..



Hatimaye baada ya jitihada kubwa Dr Edwin na Dr Alex wakisaidiana na Dr Martini walifanikiwa kuirejesha hali ya John Mwaulaya katika hali yake ya kawaida.Mapigo ya moyo yalirejea katika hali ya kawaida japokuwa bado John bado hakuwa na fahamu.
“ Ouh ahsante Mungu ! akasema Dr Edwin baada ya mashine inayoonyesha mwenendo wa mapigo ya moyo kuanza kuonyesha kwamba sasa yalianza kwenda kawaida.Kwa takribani dakika mbili wote walibaki kimya wakimtazama John.Dr alex akamuita Edwin pembeni wakaongea kwa zaidi ya dakika kumi huku wakielekezana jambo fulani halafu wakamfuata Martin
“ Martin tunahitaji kuonana na Peniela” akasema Dr Alex.Martin akatoka na baada ya dakika tatu akarejea akiwa ameongozana na Peniela na Josh

“ Dr Alex vipi hali ya John? Akauliza Peniela kwa wasi wasi.Dr Alex akamshika mkono na kumketisha sofani

“ Peniela hali ya John mwaulaya siwezi kusema ni nzuri kwa sasa japokuwa mapigo ya moyo yamerejea katika hali yake ya kawaida.Inaonekana alipatwa na mstuko mkubwa na ndiyo maana hali yake ilibadilika ghafla.Tumejitahidi kwa kila tulivyoweza na tumefanikiwa kuyarejesha mapigo ya moyo katika hali yake ya kawaida.Pamoja na hayo ninaomba niwe muwazi kwako kwamba tatizo la John linaonekana ni kubwa tofauti na tulivyokuwa tunafikiria.” Akasema Dr Alex na kuzidi kumuogopesha peniela
“ Dr Alex mmegundua nini kinamsumbua John? Akauliza Peniela
“ Ni mapema sana kutamka chochote kwa sasa hadi hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika.Kwa sasa kuna kitu tunahitaji “

“ Kitu gani Alex? Sema chochote “

“ Kutokana na hali ya John ilivyo kwa sasa anatakiwa afanyiwe uchunguzi mkubwa sana katika mfumo wake wote wa fahamu.Kwa vifaa tulivyo navyo hapa zoezi hilo haliwezi kufanikiwa kwa hiyo tunahitaji kupata hospitali yenye vifaa ambavyo tunaweza tukafanya uchunguzi wa kina na kubaini kile kinachomsumbua John hospitali yenye usalama mkubwa kwani matibabu ya John yanatakiwa yawe ni siri kubwa” akasema Dr Alex

“ Hospitali itapatikana bila wasi wasi .Naomba dakika mbili nifanye mawasiliano ” akasema Peniela na kutoka mle chumbani akachukua simu yake na kumpigia daktari mkuu wa hospitali ile kubwa yenye aliyosaidiwa na Dr Joshua na kumtaarifu kwamba angempeleka John muda si mrefu kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya.Baada ya kuwasiliana akarejea tena chumbani
“ Gari la wagonjwa litafika hapa muda si mrefu kwa hiyo tuanze kumuandaa mgonjwa.Tunampeleka katika hospitali kubwa ambayo huwatibu viongozi wakuu wa serikali na hata rais mwenyewe hutibiwa hapo.Kuna vifaa vyote mnavyovihitaji na hata usalama wake ni mkubwa sana” akasema Peniela

“ Josh gari la wagonjwa litafika hapa muda si mrefu nenda kawasubiri nje uwapokee.Dr Alex,Edwin na Martini tuanze kumuandaa mgonjwa” akaamuru Peniela
Gari la wagonjwa lilifika kwa haraka na John Mwaulaya akachukuliwa na kuwahishwa hospitali.Ndani ya gari hilo walipanda Dr Alex ,Dr Edwin na Martin.Peniela na Josh wao walifuata nyuma kwa gari la Peniela.Mara tu alipofikishwa hospitali John akapokelewa na bila kupoteza muda madaktari wa hospitali ile wakisaidiana na akina Dr Edwin wakaanza taratibu za kumfanyia uchunguzi wa kina .Madaktari katika hospitali ile walijitahidi kwa kila wawezavyo kutoa huduma za kiwango cha juu kwa John wakijua ni ndugu wa rais.
Kwa kuwa hakufahamu uchunguzi ule ungechukua muda gani , Peniela akaamua aondoke akaendelee na majukumu mengine kwani alikuwa na miadi na Anitha .Walipanga waonane ili aweze kumkabidhi vifaa maalum ambavyo vitawasaidia katika kumfuatilia Dr Kigomba.

“ Josh utaendelea kukaa hapa na kufuatilia kila kinachoendelea.mimi ninatoka kidogo nina miadi ya muhimu na mtu.Utanifahamisha kila kinachoendelea hapa” akasema Peniela na kuondoka zake



********

Mathew aliwasili nyumbani kwake akashuka garini na kumkuta jaji Elibariki peke yake sebuleni wakasalimiana

“ Anitha yuko wapi? Akauliza Mathew

“ Aliondoka hapa muda si mrefu na kusema kwamba anakwenda kuonana na Peniela kwa ajili ya kumpatia vifaa vile vya kusaidia kumfuatilia Dr Kigomba.”

“ Ok good.Kuna habari yoyote mpya? Akauliza Mathew

“ Hakuna habari yoyote mpya Mathew.Mimi niko humu ndani na sijui ni kitu gani kinachoendelea huko nje kwa hiyo nategemea sana kupata habari na taarifa toka kwako.Kwema huko utokako? Akauliza jaji Elibariki.Mathew akachukua glasi ya maji akanywa halafu akaketi sofani akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Ulikuwa sahihi jaji Elibariki,kuna mambo mengi ambayo Peniela hakuwa akiyafahamu kuhusiana na wazazi wake.John lied to her.Lakini nashukuru leo tumeufahamu ukweli wote.Peniela amefahamu kila kitu kuhusiana na historia ya maisha yake na kuhusu wazazi wake.” Akasema Mathew na kumsimulia jaji Elibariki kila kitu kilichotokea.Hii ilikuwa ni habari iliyomstua sana jaji Elibariki
“ Masikini Peniela.Sipati picha maumivu aliyonayo sasa baada ya kuufahamu ukweli kuhusiana na wazazi wake.Hata mimi nimeumizwa sana na jambo hili. Peniela needs someone to comfort her right now.Huyu John mwaulaya ni shetani mkubwa.Amemuumiza sana mwanamke ninayempenda kwa moyo wangu wote.Hana hata chembe ya ubinadamu huyu mtu na laiti kama ningekuwa karibu yake ningeweza kumfanya jambo lolote baya” akasema jaji Elibariki kwa hasira
“ Ni kweli inauma sana jaji Elibariki.John Mwaulaya ni mtu katili na ameumiza watu wengi sana .Picha ya moto ule mkubwa ukiiteketeza nyumba yangu ambayo ndani yake ilikuwamo familia yangu bado haijafutika kichwani kwangu” akasema Mathew halafu akainuka na kwenda ukutani kulikokuwa na picha kubwa iliyowaonyesha watu wawili mwanamke na mwanaume wakiwa katika tabasamu kubwa.Picha hii ikamkumbusha mbali sana Mathew ,hizi zilikuwa ni siku za furaha alipokuwa na mke wake aliyempenda sana

“ Get ready John.Your days are numbered.Kipimo kile kile ulichokitumia kuiteketeza familia yangu ndicho hicho nitakachokitumia kuhakikisha kwamba unakufa kwa mateso makali sana” akasema Mathew kwa sauti ndogo
“ Kwa hiyo nini kinaendelea hivi sasa Mathew? Huyu John tunamfanya nini? akauliza jaji Elibariki

“ Just relax judge.I’ll handle this ,don’t worry” akajibu Mathew halafu akaelekea katika ofisi yake
“ Sasa ni wakati wa kuufahamu ukweli wa kile kilichomo katika zile nyaraka zilizopoteza uhai wa Edson na wenzake nyaraka ambazo zina thamani ya mabilioni ya fedha.” Akawaza Mathew huku akiiwasha kompyuta yake na kuitafuta barua pepe kutoka kwa Yash.Barua pepe hiyo iliandikwa hivi


“ Mathew,nimechelewa kidogo kurudisha majibu ya kile ulichoniomba nikusaidie kukifanyia uchunguzi.Hii ni kutokana na jambo lenyewe kuwa kubwa tofauti na nilivyokuwa nikilifikiria.Ilinilazimu kuwashirikisha jopo la mabingwa wa sayansi ili kwa pamoja waweze kutambua kilichoandikwa katika zile karatasi.Baada ya uchunguzi wa kina imebainika kwamba kilichoandikwa katika karatasi zile ni kanuni ya kutengeneza kirusi hatari sana ambacho kinaweza kufanya maangamizi makubwa endapo kitatumika kama silaha.Hiki kitu kimetustua sana sote.Wamenihoji sana wakitaka kujua mahala nilikozipata karatasi zile hatari na ni mwanasayansi gani aliyeandika kanuni zile lakini sikuwaeleza chochote kwa kuhofia kuingilia uchunguzi wako lakini Mathew ukae ukijua kwamba yeyote uliyemkuta na karatasi hizi ni mtu hatari sana na lengo lake si zuri hata kidogo.Yeyote uliyemkuta na karatasi hizi anatakiwa ashikiliwe kwa nguvu zote ili aweze kutoa maelezo ya kina kuhusiana na karatasi zile.Nimekuwekea pia viambatanisho kadhaa ili uweze kupata picha halisi ya nini kinaweza kutokea endapo kirusi hicho kikiweza kutengenezwa kwa kutumia kanuni hizo.Mathew jambo hili ni hatari sana kwa usalama wa nchi yako na dunia kwa ujumla kwani sifahamu mtu aliyekuwa na karatasi hizi alikuwa na malengo gani ila ninachokuomba jitahidi kufanya kila kinachowezekana kuzuia kirusi hiki kisitengezwe na kama tayari kimetengenezwa fanya kila uwezavyo kuhakikisha kwamba kinapatikana mahala kilipo kabla ya kuleta maangamizi makubwa.Binafsi niko tayari kukupa msaada wa namna yoyote ile utakaouhitaji muda wowote .Najua kwa sasa uko katika uchunguzi wako na mimi sihitaji kuingilia jambo unalolichunguza ila narudia tena kukuomba kwamba jambo hili ni hatari kwa nchi yako na dunia kwa ujumla kwa hiyo jitahidi kwa kila utakavyoweza kuhakikisha kwamba wale wote wenye lengo ovu hawafanikiwi lengo lao.Ninategemea kupewa tena taarifa nyingine kutoka kwa wanasayansi ambao bado wanaendelea kufanyia uchunguzi kanuni zile kwa kina zaidi na mara tu nikiipokea taarifa hiyo nitakutaarifu mara moja.”


Hivyo ndivyo ilivyosomeka barua pepe ile kutoka kwa Yash kijana anayefanya kazi katika shirika la kijasusi la Israel Mossad .Mathew akairudia tena kwa mara ya pili kuisoma barua pepe ile pamoja na viambatanisho vyake vyote kwa lengo la kuwa na uelewa mpana sana kuhusiana na kile alichokisema Yash .Alipomaliza kusoma akavua shati na kubakiwa na fulana ya ndani,alihisi joto kali

“ Anything wrong Mathew?
Sauti ya jaji Elibariki ikamstua Mathew.Kwa muda wa dakika kadhaa Elibariki alikuwa amesimama mlangoni akimtazama Mathew bila ya yeye kuwa na habari.

“ Ouh ! Elibariki.Karibu” akasema Mathew

“ Nimesimama mlangoni kwa dakika zaidi ya kumi .Akili yako yote umeihamisha katika hicho unachokisoma katika kompyuta yako. Is Eeverything ok Mathew? Akauliza jaji Elibariki.Mathew akamfanyia ishara avute kiti aketi,akamtazama kwa sekunde kadhaa na kusema
“ Eli,kila uchao jambo hili linazidi kuwa kubwa na kuchukua sura mpya.” Akasema Mathew
“ Kazi ya kwanza uliyoniomba nikufanyie ilikuwa ni kuchunguza kuhusiana na kifo cha Edson .Tumekwisha fahamu ni kwa nini Edson aliuawa lakini yameibuka mambo mengine makubwa.Katika uchunguzi huo tumefanikiwa kugundua mambo kadhaa makubwa kiasi cha kutulazimu tuendelee kuyachimba hadi mzizi wake.Tumefanikiwa kuzipata karatasi ambazo zilisababisha kifo cha Edson na wenzake na kama utakumbuka karatasi zile ziliandikwa lugha ya kisayansi kiasi kwamba sote tulishindwa kuelewa nini kilichokuwa kimeandikwa.Ilinilazimu kuomba msaada toka kwa washirika wangu .Ninaye rafiki yangu mmoja anaitwa Yash yeye anafanya kazi katika shirika la ujasusi la Isrel Mossad na ni mtaalamu sana wa masuala ya silaha za kibaolojia.Pamoja na utaalamu wake katika sayansi lakini alishindwa kutambua kilichoandikwa ikamlazimu kuwashirikisha wanasayansi wakubwa.Kwa kushirikiana na jopo la wanasayansi wakubwa wamezifanyia utafiti karatasi zile na kugundua kilichoandikwa na leo hii Yash amenitumia majibu ndiyo maana nilikuwa nimeelekeza akili yangu yote huko nikiisoma taarifa yake.” Akasema Mathew
“ Wow ! That’s good news.Amegundua nini? Akauliza jaji Elibariki.Mathew akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Katika uchunguzi wao wamegundua kwamba kilichoandikwa katika karatasi zile ni kanuni za kutengeneza kirusi hatari ambacho kinaweza kusababisha maangamizi makubwa endapo kitatumika kama silaha iwapo kitatua katika mikono isiyo salama.Kwa mujibu wa Yash,kirusi hicho ni hatari mno iwapo tayari kimetengenezwa au kikitengenezwa.” Akasema Mathew
“ Ouh Mungu wangu !!!...” jaji Elibariki akastuka sana.Kikapita kimya kifupi .

“ Kwa taarifa hii ya Yash,tayari tumeanza kupata picha ni kwanini karatasi hizi zilitaka kuuzwa kwa thamani kubwa sana.Kumbuka mtu ambaye anatajwa kutaka kununua karatasi hizi alitaka kuzinunua kwa mabilioni ya fedha.Ilitia shaka kidogo kwa mtu kutaka kununua karatasi kwa fedha nyingi kiasi kile kumbe alifahamu kilichoandikwa katika karatasi hizo.” Akasema Mathew

“ mambo yanazidi kuwa makubwa.Sikutegemea kabisa kama suala hili lingekuwa kubwa kiasi hiki.Ni nani aliyetaka kununua karatasi hizo kwa fedha nyingi kiasi hicho na alitaka kuzipeleka wapi? Do you know him? Akauliza jaji Elibariki

“ Tayari tunamfahamu mtu aliyetaka kuzinunua karatasi hizo.Anaita Habib Soud ni tajiri toka nchini Saudi Arabia.Bado hatujui ni kwa nini alizihitaji karatasi zile na kwa sasa inabidi tumfanyie uchunguzi mkubwa sana huyu mtu ili tufahamu nini hasa lilikuwa lengo lake la kutaka karatasi zile .Yawezekana akawa na mafungamano na makundi ya kigaidi na yawezekana akawa alihitaji karatasi zile kwa ajili ya kutengeneza kirusi ambacho wangekitumia katika mashambulio ya kigaidi.Tutafahamu haya yote baada ya kufanya uchunguzi wa kina.Pamoja na hayo bado kuna maswali ya kujiuliza mfano Ni nani aliyeandika kanuni zile? Ni wazi hazikujiandika zenyewe lazima kuna mtu ambaye aliziandika,kama ni hivyo ni nani basi aliyeandika? Tutanatakiwa tulitafutie majibu swali hili.Pili karatasi zile zilifikaje katika ikulu yetu na kuhifadhiwa pale? Tatu ,kama nyaraka zile zilihifadhiwa ikulu basi ni lazima kuna mtu au watu waliokuwa wakifahamu mahala zilipo na katika hao wachache lazima kuna mmoja wao aliyevujisha siri na kupelekea kuibiwa. Kwa unyeti wake karatasi hizi lazima zilikuwa zikihifadhiwa sehemu ya siri sana ambako si rahisi kwa mtu kama Edson kufahamu kwa hiyo ninapata picha kwamba Edson lazima alielekezwa mahala zilipo na akaziiba.Kama ni hivyo mtu huyo ni nani? Tunatakiwa kumfahamu pia.Kingine kikubwa ambacho tunatakiwa tukifahamu ni je kirusi hicho tayari kimekwisha tengenezwa au bado? Kama tayari kimekwisha tengenezwa kiko wapi? Kama bado lazima tufute kabisa mipango yote ya kukitengeneza kwa kuwatia nguvuni wale wote wanaohusika katika suala hili.Lazima tulichimbe jambo hili hadi mzizi wake na hakuna hata mmoja ambaye anahusika na suala hilo atabaki salama.” Akasema Mathew

“ Mathew nimekosa neno la kusema lakini ni wazi nimestushwa mno na taarifa hii” akasema jaji Elibariki

“ Hii ni taarifa ambayo hata mimi imenistua mno .Wakati ninaisoma taarifa hii mwili ulikuwa unanitetemeka.Sikuamini kama jambo hili linaweza kuwa kubwa kiasi hiki.Hapa nilipo ninahis joto kali sana na ndiyo maana unaniona nimevua hadi shati.Si kwamba nimeogopa ila nimestuka tu kwani ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kupatikana hapa nchini kwetu.Pamoja na ukubwa wa jambo lenyewe lakini lazima tutalichimba hadi mzizi wake na kuhakikisha tunazizuia njama zote ovu .Tutafahamu karatasi hizi zimetoka wapi, nani kaandika na zilifikaje ikulu na nini lilikuwa lengo la Yule aliyetaka kuzinunua.” Akasema Mathew halafu akasita kidogo na kusema

“ Kuna wazo limenijia.Suala hili haliwezi kuwa na mahusiano na lile suala tunaloendelea kulichunguza kuhusiana na package ambayo Dr Joshua anataka kuiuza? Mpaka sasa hakuna yeyote ambaye anafahamu chochote kuhusiana na kilichomo ndani ya package hiyo .Dr Joshua yuko tayari kufanya chochote kile kuhakikisha kwamba mpango wake unafanikiwa na hii inaonyesha uthamani mkubwa wa package hiyo. Lakini hata hivyo ni mapema sana kusema chochote.Kila kitu kitajulikana baada ya uchunguzi.” Akasema Mathew na kuinama chini akafikiri kwa sekunde kadhaa halafu akasema

“ Katika nyakati hizi ninamkumbuka sana Noah.Alikuwa ni mtu mwenye msaada mkubwa sana kwangu na katika wakati huu angenisaidia sana.” Akasema Mathew
“ Mathew tafadhali usinikumbushe kuhusu Noah.Picha ya usiku ule bado haijafutika haijafutika kichwani kwangu.Kama si yeye tayari ningekwisha kuwa marehemu sasa lakini Noah aliyatoa maisha yake kwa ajili yangu.Nina deni kubwa sana kwake na namna pekee ya kuweza kulipa deni hilo ni kuwapata wale wote waliosababisha kifo chake.I don’t know how I’m going to do this but I promise you we’re in this together.” Akasema jaji Elibariki kwa hisia kali sana.
“ Samahani Elibariki kwa kukukumbusha kuhusu Noah.He was a good guy.Binafsi nimefanya naye kazi kwa muda mrefu and that’s why it’ll take a long time to forget him. Hata hivyo hakijaharibika kitu na tutaifanya kazi hii mpaka mwisho.Niko mimi ,Anitha pamoja na wewe.Tunaweza kuifanya kazi hii.Anitha ni mtu ambaye atatusaidia sana katika suala hili.Ni mtaalamu mkubwa sana wa teknolojia na ni mwepesi sana katika kufikiri na kuchambua mambo.Binafsi ninapokuwa naye katika kazi Fulani basi huwa sifikirii kushindwa hata kidogo katika jambo lolote na hata katika hili nina hakika tutafanikiwa tu” akasema Mathew halafu akachukua simu na kumpigia Anitha

“ Hallow Mathew ,uko wapi? Akauliza Anitha baada ya kupokea simu
“ Tayari nimerejea nyumbani.Wewe uko wapi? Akauliza Mathew

“ Niko njiani ninarejea nyumbani.Nimetoka kuonana na Peniela na tayari nimemkabidhi vile vifaa na jioni ya leo atakapokutana na Dr Kigomba tutaanza kupata kila taarifa toka kwa Dr Kigomba.” Akasema Anitha

“ Good job Anitha.Ninakusubiri hapa nyumbani.Kuna suala zito linalotukabili”

“ Kuna jambo jipya ? akauliza Anitha kwa wasi wasi kidogo
“ Si jipya sana lakini ni mwendelezo wa kile ambacho tumekuwa tunaendelea nacho” akasema Mathew
“ Sawa Mathew .Niko njiani ninakuja sasa hivi” akajibu Anitha na kukata simu


TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………………
 
PENIELA SEASON 3

SEHEMUYA 16

ILIPOISHA SEHEMUILIYOPITA
“ Nitakuwa nikikufahamisha kila kitu kuhusiana na kinachoendelea lakini kuna jambo nitaomba ulifanyie uchunguzi.Ninataka unisaidie kufanya utafiti Rosema Mkozumi yuko wapi ? Idara yenu ya usalama wa taifa mnazo nyenzo za kuweza kupata taarifa mapema sana kwa hiyo nisaidie kufahamu mahala aliko Rosemary .Can you do that for me? Akauliza Vincent
“ Niachie suala hilo nitalifanyia kazi .Nitafuatilia ofisini ili nione kama kuna taarifa zozote zimepatikana kuhusu mahala alipo Rose.” akasema Jesica
“ Ahsante sana Jesica.Lifanyie kazi sualahlo kwani nina wasiwasi sana na kutoweka huku kwa kutatanisha kwa Rose .Yule ni mtu anayetufahamu sana sisi na anayafahamumamboyetu mengi kamasisi tunavyoyafahamu yak wake “: akasema Vincent akaagana na Jesica.
“ Sasa kidogo ninaweza kuvuta pumzi baada ya kuwa na uhakika Amos ametoweka.Huyu alikuwa ni mtu muhimu mno kwa Deus na ndiye alikuwa anamtegemea sana katika mpango wake.Kwa sasa mipango yake haitaweza kufanikiwa tena na ni nafasi yetu kumuandaa mtu wetu ambaye atatusaidia sana endapoatashika madaraka “ akawaza Vincent.


ENDELEA……………………

Mathew akaingIa chumbani kwake akalifungua kabati ambao huhifadhi baadhiya vifaa vyake mbalimbaLi.Akachukua sanduku moja la kijani pamoja na vifaa kadhaa akatoka mle chumbani na kuelekea katika chumba alimolazwa Rosemary Mkozumi.Akakinyonga kitasa na kuingia ndani.Rosemary alipomuona akainuka na kukaa kitandani.Alikuwa na hasira kali sana “ Who are you? Kwan in umeniweka humu? Nani kakutuma ufanye hivi? Akauliza kwa ukali Rosemary.Mathew hakumjibu kitu akaviweka vifaa vyake mezani akavuta kiti na kuketi akamtazama Rosemary kwa sekudne kadhaa kisha akasema
“ Hello Rosemary! “ Sina haja ya salamu yako.Tafadhali kijana naomba usijitafutie matatizo zaidi.Mpaka sasa tayari umekwishajiingiza katika matatizo makubwa.Umemuua Henry na kama vile haitoshi umeniteka na kunifungia humu chumbani.Unadiriki kumteka nyara mke wa rais? Umelipwa shilingi ngapikijana wangu hata ukakubali kujihatarisha namna hii? Tafadhali naomba uniachie huru haraka sana na nitaangalia namna ya kukusamehe na kukusaidia kukutoa katika janga hili ulilojitumbukiza bila kujua....” akasema Rosemar y Mkozumi kwa sauti ya juu .Mathew akamtazama kwa makini na kusema
“ Rosemary Mkozumi just relax…”
“ Kijana naomba tafadhali usiendelee na upuuzi wako unaotaka kuufanya.Nani lakini kakutuma unifanyie hivi? Unashirikiana na akina nani? Hao waliokutuma wamekuingiza katika tanuru la moto na wewe kwa tamaa zako ukakubali kuingia na kuungua .Ninakuonya kwa ara nyingine kijana tafadhali naomba unifungue haraka sana miguu yangu inaumia” akasema Rosemary.
“ Rosemary tafadhali naomba uniskilize kwa makinisanana sihitaji mzaha hata kidogo” Akasema Mathew.
“ Ninaitwa Mathew,ni mchunguzi wa kujitegemea.Nimewahi kufanya kazi katika idara ya usalama wa taifa Tanzania idara ya kupambana na kuzuia ugaidi na baadae nikaacha kazi hiyo na kuanza kufaya kazi zangu binafsi za kiuchunguzi.Mwezi wa pili mwaka jana kijana mmoja aitwaye Edson aliyekuwa akifanya kazi katika idara ya mawasiliano ikulu aliuawa na watu wasiojulikana lakinikesi hiyo ya mauaji ikamuangukia mpenzi wake aliyeitwa Peniela.Mahakama ilimuachia huru Peniela baada ya kuridhika kwamba hakuw ana hatia na hakumuua Edson kama ilivyodaiwa.Nilikabidhiwa jukumu la kumtafuta muuaji halisi wa Edson .Katika uchunguzi wangu niligundua kwamba Edson alishiriki katika uibwaji wa nyaraka nyeti sana toka ikulu.Niligundua kwamba ili kulifanikisah jambo lile Edson hakuwa peke yake alikuwa akishirikiana na watu wawili Mzee Kitwana na Mzee Matiku ambao kwa sasa wote ni marehemu.Nyaraka hizo zilizoibwa zilikuw ana kanuni za kutengeneza kirusi hatari sana ambacho kinaweza kusababisha maangamizi makubwa sana kwa binadamu.Nimelichimba suala hilikwa undani zaidi na kugundua kwamba mtu aliyetaka kuzinunua karatasi hizo anaitwa Habib Soud raia wa Saudi Arabia .Habib anatajwa kuvifadhili vikundi kadhaa vya kigaidi nahivyo kunifanya niamini kwamba yawezekanaalizihitaji karatasizile kwa ajili ya kutengeneza kirusi kile ili wakitumie kwa mambo ya kigaidi.Sikuishia hapo nilimchunguza Habib na kugundua kwamba amekuwa na mawasiliano nawe ya mara kwa mara .Nimegundua pia kwamba wewe ndiye uliyeratibu na kufanikisha mpango mzima wa kuibwa kwa karatasi hizo ikulu kwa kumtumia Edson na baadaya kuzipata karatasi hizo uliwazunguka washirika wako na kuwamaliza ili ubaki na karatasihizo na pesa yote itokanayo na mauzo ya karatasi hizo uipate peke yako.Ili kuendelea kuuficha uhusika wako katika suala hili kumbu umbu za mawasilianokatiyako na washirika wako wakuu katika suala hili yaani mzee Kitwana na matiku zilifutwa kabisa .” Akasema Mathew na uso wa Rosemary ukabadilika .Mathew akaendelea.
“ Kwa bahati mbaya pamoja na kuwaua washirika wako lakinihukufanikiwa kuzipata nyarakazile kwani ziifichwa na mmoja wa washirika wako.baadaya kuona jambo lile limeshindikana hukukata tamaa ukaingia tena katika biashara nyingine namtu mmoja anaitwa samir Asaad.Umekuwa ukiwasiliana na Samir na katika mojawapo ya barua pepeuliyomtumia Samir umemuhakikishia kwamba muda si mrefu toka sasa utafanikiwa kuupata mzigo anaoutaka kwani una mawasiliano ya karibu na mtu wa karibu na rais .Baadae tukagundua kwamba mtu uliyemtaja kuwa karibu na rais ambaye umekuwa na mawasiliano naye ni Captain Amos ambaye ni daktariwa familia ya rais.Tulimpata Captain Amos na wakati tukimfanyia mahojiano ,alitokea mtu na kumpiga risasi akamuua na hili lilifanyika makusudi ili Captain Amos asiweze kutoa siri.” Mathew akanyamaza akamtazama Rose ambaye matone ya jasho yalionekana usoni pake.
“ Amos is dead?! Akauliza Rosemary kwa msahngao mkubwa
“ yes ..he’s dead” akasema Mathew.Rose akainamisha kichwa kwa masikitiko
“ Rosemary kuna mambo mengi ambayo ninyafahamu kuhusu wewe namtandaowako nasitaki kpoteza muda kuyaongelea hapa.Ninachokihitaji toka kwako nikunipatiamajibu sahihiya kila nitakachokuuliza kaini kama hutanipa ushrikiano wa kutosha na kuniletea jeuri sahau kabisa kutoka hapa ukiwa hai.” Akasema Mathew na kunyamaza kidogo halafu akasema
“Kitu cha kwanza ninachotaka toka kwako nataka kufahamu ,ukiacha wale washirika wako walikwisha fariki,nani mwingine ambaye umeshirikiana naye katika kuziiba karatasi zile ikulu? akaulizia Mathew .Rosemary Mkozumi akasonya na kubetua midomo kwa dharau akasema
“ You go to hell,wewe na huyo aliyekutuma!! .Mathew akamuangalia na kusema
“ Rose ninakukumbusha kwa mara nyingine kwamba hapa ulipo ni nusu ya jehanamu kwa hiyo nataka unijibu kiufasaha kila nitakachokuuliza na kitakachokuokoa ukaweza kutoka humu ndani ni ukweli..Tell me the truth and you’ll get out of here alive..Ninarudia tena nilichokuuliza mwanzo,nina kila ushahidi kuthibitisha kwamba ulihusika katika kuratibu mpango wa kuziiba karatasi zile ikulu.Ninataka kufahamu ni akina nani wengine ulioshirikiana nao kulifanikisha jambo hili ukiacha wale ambao wamekwisha fariki? Akauliza Mathew.
“ You go to hell you witch..nakuhurumia sana wewe kijana kwa nini unakubali kutumiwa kirahisi namna hiyo ? tafadhali achana na huu upuuzi unaoufanya.Mwambie aliyekutuma kwamba hawezi kupambana na Rosemary..” akasema Rosemary kwa dharau
“ Hakuna mtu aliyenituma bali ninafanya kazi hii kwa niabaya serikaliya jamhuri ya muungano wa Tanzania na si mtu binafsi kama unavyodhani..” akasema Mathew.Rose akacheka kwa dharau na kusema “ Serikali !! Unafahamu serikali ni nani? Poor boy hujui hata unachokiongea.Tafadhali naomba unifungue niondoke zangu na nitakusamehe,lakini ukiendelea kunishikilia hapa kwako kwa dakika kumi zijazo ninakuapia kijana sintakusamehe hata kidogo.”akasema Rosemary
“ Vitisho vyako havitaweza kukusaidia hata kidogo Rose.Nakuonya kwa mara ya mwisho kwamba utatoka humu ndani ukiwa salama endapo utanipa majibu ya kile ninachokitaka.Ukileta jeuri ninakuapia Rose hautatoka humu ndani salama.” Akasema Mathew na Rose akaukunja uso wake
“ Kijana kwa nini unakuwa mgumu kunielewa? Kwa nini unaendelea kuhatarisha maisha yako na kujiweka katika matatizo makubwa? Ninakwambiwa kwamba ndani ya muda mfupi ujao utajutia hiki unachokifanya .Sintokusamehe kabisa na wala usidhani kwamba h iyo serikali unayodai unafanya kazi kwa niabayake watakusaida kitu .Iam the government! ….Akasema kwa ukali Rose. Mathew akainuka na kumsogelea karibu. “ Rose ninafahamu kwamba unalengo la kugombea urais na kwa sasa mimi ndiye nitakayeamua kama jambo hilo litafanikiwa ama vipi.Endapo sintaridhika na majibu yako ndoto hiyo kubwa haitatimia kamwe.Nita…” Ghafla Mathew akastuka baada ya kutemewa mate usoni
“ I’ve told you go to hell you black devil !! akasema kwa ukali Rosemary.Mathew akamtazama Rosemary kwa hasira na kusema
“ umefanya kosa kubwa sana.Ni bora ungekutana na mtoa roho kuliko mimi.Sasa kwa kuwa umekataa kunijibu kwa hiari yako na umeonyesha kiburi ,nitakulazimisha kunijbu kwa nguvu” akasema Mathew na kuchukua ndoo ya maji akammwagia Rosemary na kumloanisha chapa chapa
“ Are you crazy?!!.I swear I’ll never forgive you for this ”akafoka Rose.Mathew akalifungua lile sanduku halafu akatoa vifaa kadhaa akaviweka mezani.Akachukukua vyuma Fulani viwili vyenye nyaya akavichomeka katika lile sanduku halafu akaliunganisha katika umeme kisha akavigusanisha vyuma vile vikatoa cheche.Rosemary Mkozumi akatumbua macho “ Unataka kufanya nini? Akauliza.Mathew hakumjibu kitu akarekebisha kiasi cha umeme anaouhitaji na kisha akasogea kitandani na kugusisha vyuma vile vyenye umeme katika pingu aliyofungiwa Rosemary mguuni.. "Aaaaaggggghhhhh!!!!!!!!!!!!!!!...”Rosemary akapiga kelele kubwa..Mathew akatulia kidogo halafu akarudia tena zoezi lile..Rose akaendelea kupiga kelele kubwa
“ Give me the names!!...akasema kwa ukali Mathew.Halafu akatulia
“ Give me the names!! nani u nashirikiana nao? Akauliza .
“ There is..there..iiii..there are no names..” akasema Rosemary huku akitetemeka mwili.mathew akagusisha tena vyuma vile katika pingu na kuendelea kumtesa Rosemary..
“ Stop that.!!.please stoooop !!!!!..” akalia Rose.Mathew akasimama
“ Ni akina nani ulishiriana nao katika mpango ule? Akauliza Mathew. “No one..sijashirikiana na mtu yeyote na wala siufahamu huo mpango unaousema..” akasema Rose huku akitweta.
“ This is not working…!!! Akasema Mathew kwa sauti ndogo.Akavua shati na kubakiwa na fulana ya ndani akamshika Rosemary kwa nguvu akamfunga mikono yake kwa pingu.
“ Nilikuonya toka mwanzo kwamba usiombe ukutane na mimi lakini ukapuuza.Utanieleza kila kitu leo ”akasema Mathew halafu akachukua kisu na kukata kijisehemu kidogo katika kidole cha mguu wa kulia wa Rose halafu akachukua bomba la sindano akavuta dawa fulani nyeupe toka katika kichupa kidogo na kudondoshea matone kadhaa mahala palipokuwa panatoa damu.Rose akagalagala pale kitandani huku akipiga kelele kubwa kwa maumivu aliyoyasiki..Mathew akachukua gundi na kumfunga mdomo ili asiweze kutoa ukelele halafu akadondoshea tena matone kadhaa mahala alipopakata..Rosemary akaendelea kugugumia kwa maumivu makubwa.Mathew akamfungua ile gundi aliyomfunga nayo mdomo akamuuliza
“ Uko tayari kuniambia ninachokihitaji?Akiwa ndani ya maumivu makali sana akasema
“ You go to hell you devil !! Mathew akamfunga tena mdomo na kumkata kidogo shingonihalafu akadondoshea matone kadhaa mahala alipokata..Rose akaruka ruka kana kwamba anakata roho.Mathew akamuangalia halafu akamfungua ile gundi mdomoni. “ Utanijibu nilichokuuliza? Akauliza Mathew lakini Rose hakumjibu kitu akabaki analia kwa maumivu makali.
“ C’mon Rose ..nijibu haraka nilichokuuliza !!!! akasema Mathew kwa ukali Rose akaendelea kulia kwa maumivu makali sana aliyoyasikia.
“ Dah ! sijawahi kukutana na mwanamke mwenye roho ngumu kama huyu mama.Lakini leo hii atanieleza kila kitu ninachotaka.”akawaza Mathew.Akaelekea mezani kwake na kuchukua kifaa kidogo cha kukatia akakiwasha na kukijaribu
“R ose umetaka mwenyewe tufike hapa tulipofika na nilikuonya toka mapema kwamba usiombe ukutane na mimi.I’ m a monster na ninachokwenda kukufanyia kitabaki katika kumbu kmbu za uzao wako daima.Nitakukata kidole kimoja kimoja nikianzia na vidole vya miguu na halafu nitakuja mikononi na halafu nitanyunyiza dawa hii inayouma na utajihisi kamaumetupwa katika shimo la moto kwani mwili wote utawaka moto kwa maumivu utakayoyasikia..Utasikia maumivu makali mno ambayo hujawahi kuyasikia toka umezaliwa.Ukitaka nisifanye hivyo nijibu haraka kile nilichokuuliza” akasema Mathew lakini Rosemary hakujibu kitu bado aliendelea kulia kwa maumivu makali.Mathew akachukua kile kifaa akakiwasha na kisha akakishika kidole cha mwisho cha mguu wa kulia wa Rosemary na kukikata. Rosemary akapiga ukulele mkubwa sana
“ C’mon Rose,usinilazimishe nikakufanyia hivi.Niambie kile ninachokitaka” akasema Mathew kwa ukali.Bado Rose aliendelea kugalagala huku akilia kwa maumivu makali mno.
“ Bado anaendelea kuwa na kiburi ..leo lazima nimbadilishe sura yake..Atanieleza tu .” akawaza Mathew na kukishika tena kidole kinachofuata akakata.Rose akapiga ukele mkubwa hadi sauti ikaanza kumkwama..
“ Please stop !!.stop hurting me !!!!!!!!!!..akasema Rosemary..
“ Are you ready to tell me what I want? akauliza Mathew
“ I will tell you..i will tell you everything ..stop hurting me…” akasema Rose huku bado akiendelea kulia kwa maumivu makali.Mathew akachukua bandeji na kufunga mguu ule wenye majeraha halafu akamchoma sindano ya kupunguza maumivu.
“ Now tell me everything” akasema Mathew
“ I will tell you everything you want..please don’t hurt me




ROSE ATAMUALEZA NINI MATHEW? TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………
 
PENIELA SEASON 3

SEHEMU YA 30

MTUNZI:pATRICK.CK


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Safari iliendelea hadi walipofika Jamaica nigt club.Mathew akamuelekeza Jason sehemu ya kuegesha.Jamaica night club ni mojawapo ya kumbi za burudani inayotoa burudani kwa saa ishirini na nne.Gari zilikuwa zinaingia na kutoka.Walikaa mle garini kwa takribani dakika saba mara ikaja gari moja nyeusi mbele yao na kusimama kisha taa kubwa zikazimwa na kuwashwa haraka haraka mara tatu.Mathew akamgeukia Peniela.

“ Peniela we have to go” akasema na kumshangaza Jason
“ Mathew mnakwenda wapi? Akauliza
“ Jason ahsante sana kwa msaada wako mkubwa.Siwezi kukusahau kwa msaada huu mkubwa ulioutaidia kwa usiku huu wa leo.Muda wowote nikihitaji tena msaada nitakupigia.Tafadhali kuwa muangalifu sana” akasema Mathew na kuufungua mlango wa gari akashuka ,akamfungulia Peniela mlango akashuka ,akamshika mkono akamuongoza hadi katika lile gari lililosimama mbele yao wakaingia na gari likaondoka.Jason akabaki amepigwa na butwaa.

“ wanakwenda wapi? Gari ile iliyokuj akuwachukua ni ya nani? Akajiuliza Jason bila kupata jibu



ENDELEA………………………………..



“ Karibu tena nyumbani madam.” Mmoja wa walinzi wa Rosemary Mkozumi akamwambia Rose huku akimfungulia mlango.Rose akasaidiwa na walinzi wake kushuka ndani ya gari na kuingia sebuleni akakalishwa katika sofa.

“ Ahsanteni sana vijana.Mmefanya kazi nzuri usiku waleo.” Akasema Rose

“ madam kwa niaba ya wenzangu wote ninaomba samahani sana kwa tukio lile lililotokea.Sisi hatukujua kama watu wale walioongozana na Henry ni watu wabaya namna hii.” Akasema Yule mlinzi.

“ Fernando haya mambo si wakati wake sasa,nitakuwa na maongezi na ninyi.Hebu nieleze kuna habari gani hapa nyumbani katika muda wote ambao sikuwepo?

“ Baada ya wewe kuchukuliwa katika lile gari la wagonjwa ,tulipigiwa simu na watu wakatuarifu kwamba kuna mwili wa Henry mle ofisini kwako tuliwasiliana na polisi ambao walifika hapa wakafanya uchunguzi wao wakavunja mlango na kuondoka na mwili wa Henry.Hiyo ndiyo habari kubwa iliyopo.Zaidi ya hiyo hakuna tena habari nyingine yoyote” akasema Fernando.
“ Ok safi sana.Imarisheni ulinzi na kuanzia sasa mtu yeyote asiingie humu ndani bila ruhusa yangu na yeyote atakayeingia humu hata kama ameruhusiwa lazima apekuliwe ili kujua kama hana silaha ya aina yoyote ile.Nitaongea zaidi na ninyi kesho “ akasema Rose

“ lakini madam ni nani aliyefanya ukatili huu ? Huyu aliyefanya hivi anatakiwa asakwe hadi apatikane na afundishwe adabu “Akauliza Fernando.
“ usijali Fernando.Atasakwa na atapatikana tu.kwa sasa wale wote watu tuliowachukua kule wafungieni kila mmoja katika chumba chake.Nitakuwa na maongezi nao nao mmoja mmoja asubuhi.Kwa sasa naombeni mnipeleke chumbani kwangu” akasema Rose na walinzi wake wakambeba hadi chumbani kwake.
“ Ok ahsanteni sana vijana.Naombeni mniache sasa ninahitaji kuwa mwenyewe.”akasema Rose na walinzi wake wakaondoka wakamuacha mwenyewe.Akampigia simu mfanyakazi wake wa ndani akamuomba amtengenezee supu kwani hakuwa ameweka chochote tumboni.Alihisi maumivu makali sana kila sehemu ya mwili wake.Mlango ukagongwa akaingia Dr Imelda daktari binafsi wa Rosemary .

“ madam pole sana kwa mkasa huu.Nani kakufanya hivi? Imelda akashangaa

“ Imelda nashukuru sana umefika kwa wakati.Hali yangu ni kama unavyoniona.Si nzuri hata kidopo”akasema Rose.Dr Imelda akamchunguza Rose majeraha yake halafu akasema
“ Inabidi kabla ya kuanza kutibu nikusafishe kwanza majeraha yote ili tujue ukubwa wake.Can you walk?akauliza Imelda.Rose akasimama na kuuma meno kwa maumivu aliyokuwa akiyasikia.Imelda akamsaidia akamuingiza bafuni na kumuogesha kwani hakuwa akitazamika kwa damu iliyomtapakaa kila mahala.Baada ya kuhakikisha amekuwa safi akamrudisha chumbani na kumlaza kitandani akaanza kumtibu majeraha akianzia na yale makubwa ya miguuni ya kukatwa vidole.
“ Ni katili gani ambaye alifanya hivi madam? Mtu huyu aliyefanya hivi hana roho ya ubinadamu hata chembe. Lengo lake lilikuwa ni kukuua” akasema Dr Imelda wakati akitibu majeraha ya miguuni.
“ Imelda katika hii dunia tunaishi na maadui wengi sana na waliofanya hivi ni watu wenye visasi na mimi na lengo lao ni kuniua.” Akasema Rosemary.

“ Inasikitisha sana kwa ukatili huu kufanyiwa mtu mkubwa kama wewe.Yeyote aliyefanya hivi anatakiwa kuozea gerezani.Alichokufanyia kinatisha sana” akasema Imelda na machozi yakaonekana machoni kwa Rosemary

“ They will all pay..!!..They must pay ! ..akasema Rose.
Dr Imelda akaendelea kumganga Rose majeraha yake na wakati wanaendelea simu ya Rose ikaita matibabu yakasimama kidogo ili aweze kuongea na simu ile kwani alisema ni ya muhimu sana

“ hallow Rose”ikasema sauti ya upande wa pili baada ya Rose kupokea simu

“ Hallow Vincent !!!
“Rose ninataka kuripoti ukosefu wa adabu wanaonifanyia hawa walinzi wako.Dont they know who I am? Akauliza Vincent
“I’m sorry Vincent.Ni mimi ndiye niliyewapa maagizo ya kuhakikisha kwamba kila mtu anayeingia hapa anapekuliwa ili kuhakikisha hana silaha yoyote.I don’t trust anyone right now.Nipe kiongozi wao niongee naye” akasema Rose na baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti ya Fernando
“ hallow Madam”
“ Fernando mruhusuni Vincent apite moja kwa moja”akasema Rose na kukata simu na matibabu yakaendelea.
Baada ya dakika kumi mlango ukagongwa Dr Imelda akaenda kuangalia ni nani aliyekuwa anagonga akakutana na Vincent akamueleza aketi sofani katika sebule ya Rose asubiri hadi amalize kazi aliyokuwa anaifanya.
Baada ya saa nzima Dr Imelda akamaliza kumtibu Rose majeraha yake halafu akamchoma sindano na kutoka mle chumbani ili kumpa nafasi Rose ya kuongea na mgeni wake.Vincent akastuka sana baada ya kumuona Rose akiwa na majeraha
“ Ouh my God ! who did this to you Rose? Vincent akashangaa

“ I have so many enemies Vincent” akasema Rose
“ Pole sana Rose.Whoever did this to you,must be pay.Umekwisha mfahamu ni nani aliyefanya unyama huu?akauliza Vincent
“ Tayari nimewajua walionifanya hivi na hata aliyewatuma wanifanyie hivi” akasema Rose.
“ Good.Its pay back time..”akasema Vincent kwa hasira
“ Not so fast Vincent.Wameuwasha moto wenyewe sasa watakosa maji ya kuuzimia.Nitapambana nao taratibu na kuwafyeka mmoja baada ya mwingine. Kwa bahati mbaya waliotumwa wanifanyie hivi hawakutaarifiwa kwamba Rosemary ni nani na sasa watakwenda kunifahamu mimi ni nani.Ninakuhakikishia Vincent yeyote ambaye ana mkono wakekatika jambo hili lazima atalipa.Hakuna atakayesalimika hata kama ni nani.Tuachane na hayo nimekuita hapa kwanza kukujulisha kwamba nimerejea nyumbani ingawa nimechakazwa kila sehemu ya mwili wangu.Nilivamiwa na kutekwa na watu ambao walimuua pia Henry.Watu hao wamenitesa sana kama hivi unavyoona.”
“ Dah ! pole sana Rose.” Akasema Vincent kw masikitiko

“ Ahsante Vicent.” Akasema Rose na kugugumia kwa maumivu kisha akasema

“Jambo la pili ninalotaka ulifahamu wewe kama mshirika wangu ni kwamba kuanzia sasa tuko vitani.Watu hawa walioniteka tayari wanafahamu mambo mengi sana kuhusu mimi na hata wale ambao ninashirikiana nao...”akasema Rosemary na kumfanya Vincent astuke

“ They know ?!! akauliza

“ Ndiyo Vincent.wanafahamu kila kitu kuhusu mimi,wamepekua kompyuta yangu,simu zangu,wamefahamu mambo mengi sana kwa hiyo nimekuita ili kukupa taarifa hizi ili unisaidie kupambana na watu hawa.” akasema Rose.
“ Ni nani hawa watu? Nani kawatuma? Halafu tukio hili lilitokeaje? Akauliza Vincent
“Henry alikuja na watu hao na sifahamu alitoka nao wapi .Kuna kitu nilisahau hivyo nikarejea mara moja ndipo nilipotaarifiwa kwamba Henry amekuja na wageni.Moja kwa moja nikaja mpaka ofisini ili niwafahamu wageni hao ni akina nani na mara tu nilipoingia ofisini Henry akaruka ili anipe taarifa kwamba nisingiie mle ofisini lakini watu wale wakamuwahi na kumpiga risasi akafariki pale pale.Ouh masikini Henry wamemuua mpenzi wangu jamani !!..Rose akasema kwa uchungu mkubwa na kushindwa kuyazuia machozi kumtoka.

“ Pole sana Rose.”akasema Vincent.Rose akafuta machozi na kuendelea.

“ Watu wale sifahamu walitoka wapi na Henry lakini ninachoweza kusema kwamba walimtumia Henry ili kuingia hapa ndani. Ninamfahamu Henry vizuri kwa namna yoyote ili asingeweza kuwaleta hapa kwangu watu ambao anajua ni hatari .Watu wale hadi wakamtumia Henry ni watu ambao tayari wamenifahamu kwa undani na wanajua kila kitu kuhusu mimi na yeye.Wamepekua kila mahala wamechukua kila taarifa waliyokuwa wanaitaka na huko walikonipeleka wamenitesa sana ili niwaeleze baadhi ya mambo “ akasema Rose

“ Dah pole sana Rose.” Akasema Vincent

“ Ahsante sana Vincent.Lakini nimegundua aliyewatuma watu hawa lazima atakuwa ni mmoja wa washindani wangu wa kisiasa na hili ni jaribio lao la kutaka kuizima ndoto yangu ya kugombea urais lakini nakuhakikishia kwamba hawataweza.Nitagombea urais na nitashinda tu”akasema Rose
“ Nakubaliana nawe Rose unapoingia katika siasa na hasa katika jambo kubwa kama kugombea urais lazima utapata maadui wengi na vikwazo vingi.Lakini ni nani basi ambaye unahisi ameianzisha vita hii ? akauliza Vincent

“ Ni Deus “ akasema Rose na kumstua sana Vincent
“ Deus ? akauliza Vinmcnet

“ Ndiyo ni Deus.My x husband”

“ Are you sure Rose? Akauliza Vincent
“ Ndiyo nina hakika kabisa ni yeye.Toka tulipoachana amekuwa ni adui yangu mkubwa na aliposikia kwamba nina nia ya kuwani aurais amekuwa ni mpinzani wangu mkubwa .Nina hakika kabisa kwamba ni yeye ndiye aliyewatuma vijana wale wanifanyie hivi.Lakini ninakuhakikishia Vincent kwamba simuogopi Deus na nitamuonyesha kwamba mimi ni nani.Safari hii ataifahamu nguvu yangu” akasema Rose.Vincent akamtazama Rose na kusema.
“ Rose kuna kitu ninataka kukuuliza.Una hakika gani kwamba ni Dues ndiye aliyewatuma watu hao kwako ?

“ Nina uhakika huo Vincent.Vijana wale walipokuwa wananitesa walitaka kufahamu kuhusu Hasheem Abullah.Ni Deus pekee ambaye anafahamu kuhusu mimi na Hasheem na hii ilikuwa ni sababu kubwa ya mimi na Deus kutengana. Nina hakika aliyewapa taarifa hizo zote ni Deus.Jambo hili ni la ndani sana na wasingeweza kulifahamu kama si kuambiwa na Deus.Kwa hiyo safari hii I swear nitamuonyesha mimi ni nani ” Akasema Rose.
“ Rose kabla hujafanya lolote nataka uwe na uhakika kama ni kweli Deus ndiye aliyekuwa nyuma ya hao watu,kama huna hakika na suala hilo naomba usifanye hilo tafadhali. “ akasema Vincent
“ Vincent nina uhakika mkubwa sana kwamba hakuna mtu mwingine anayeweza kunifanyia hivi zaidi yake.Deus hataki kuniona nyota yangu iking’aa kisiasa na ndiyo maana anafanya kila awezalo kuhakikisha kwamba mambo yangu hayafanikiwi na lengo la kuwatumia vijana wale ni ili kuweza kunivurugia mipango yangu wa kuwania urais kwani anajua kabisa kwamba nina watu wengi wanaoniunga mkono na kwamba lazima nitashinda tu na kuwa rais wa kwanza mwanamke Tanzania.Nimeishi na Deus na ninamfahamu vizuri sana kuliko mtu mwingine yeyote Yule.He’s a monster” Akasema Rose.Vincent akajiweka vizuri na kusema
“ Rose kuna mambo kadhaa ambayo ninataka uyafahamu kabla hujafanya hichounachotaka kukifanya.Kwanza kabisa…” akasema Vincent na simu ya Rose ikaita ikambidi asubiri hadi Rose alipomaliza kuongea akaendelea.

“ Kwanza kabisa ninataka ufahamu for years now I’ve been working with Deus.Mimi nay eye ni washirika wakubwa .”

“ What ?!..Rosemary akashangaa

“ Ina maana kwa muda huu wote umekuwa ukishirikiana na Deus bila ya kunitaarifu? You traitor !!“ akasema Rose kwa ukali
“ Rose tafadhali usihamaki.Nisikilize vizuri.Nimeamua kukueleza jambo hili kwa sababu sitaki ukurupuke katika maamuzi yako na uje kujutia baadae.NInataka kukusaidia kumfahamu muhusika halisi aliyefanya jambo hili.Mimi na Deus tumekuwa marafiki na washirika wakubwa kwa muda mrefu.Tuna kikundi cha watu wachache mabilionea wakubwa ambao tunakifadhili chama anachokiongoza Deus na nyakati ningine tunafanya hata maamuzi makubwa yanayohusu nchi.Hiki ni kikundi cha watu wenye nguvu ya kufanya jambo lolote katika nchi.It’s us who decides who is going to be the next president” akasema Vincent na kumfanya Rose azidi kumtumbulia macho
“ Nimekueleza haya yote ili kukupa picha kwamba katika vikao vyetu vya maamuzi hata siku moja hatujawahi kukuzungumzia wewe na hata siku moja sijawahi kumsikia Deus akikuzugumzia.Katika watu ambao wanazungumzwa kuwa na nguvu kubwa kisiasa na katika uchaguzi ujao wewe haumo hata kati ya tano bora kwa hiyo nina hakika kabisa kwamba Deus siye aliyewatuma hao watu wakufanyie hivyo kwa sababu hana shida na wewe . There is must be someone else behind this and not Deus. We have to find him” akasema Vincent.

“ Vincent umenisikitisha sana.Kumbe siku hizi zote umekuwa ni mtu wangu wa karibu unayeniunga mkono na kunisapoti katika mambo mengi kumbe umekuwa pia na ushirika na Deus? Umenisaliti Vincent na sitaki kabisa kukuona tena hapa kwangu.You traitor !! akasema kwa ukali Rosemary
“ Rosemary Calm down my dear.Nimeamua kukueleza ukweli ili kukusaidia kumtafuta mtu sahihi aliyekufanyia haya na si Deus. Yule ni mtu mkubwa sana na hana mpango wowote na wewe na usijaribu kabisa kucheza naye.Hata sisi pamoja na uwezo wetu mkubwa kifedha lakini tunamuogopa na tunatii kila atakachotuambia.Japokuwa amestaafu lakini bado ni mtu mwenye nguvu sana hapa nchini” Akasema Vincent.Rose alimuangalia Vincent kwa hasira kali
“ Vincent mimi na wewe tulikuwa marafiki wakubwa nilikuamini kwamba ni mtu ambaye ninaweza kukutegemea katika jambo lolote na hata kukupa siri zangu.Na hata usiku huu wewe ndiye uliyekuwa mtu wa kwanza kukupigia simu na kukufahamisha kwamba niko salama lakini sikujua kama una ushirika na Deus ambaye ni adui yangu mkubwa.Kwa kushirikiana na adui yangu ninakuweka nawe vile vile katika kundi la maadui zangu. From now on you are my enemy !!! akasema Rose.Vincent akacheka kidogo

“ Listen to me carefull woman.Dont you ever try to do anything to Deus.Atakumaliza ndani ya sekunde moja kama mbu anavyouliwa kwa kofi moja.Kwa Deus wewe bado ni mtu mdogo sana na anaweza akakufanya chochote muda wowote.There is one more thing I want to tell you.Mtu uliyemtegemea Captain Amos amefariki..!!..Taarifa ile ilimuingia Rosemary Mkozumi moyoni kama vile kitu chenye ncha kali na kwa dakika mbili hakuweza kusema chochote
“Ulimtegemea sana Amos katika mambo mengi lakini hukujua kwamba mtu ambaye ulimuamini kama mshirika wako alikuwa ni moja wa vijana wa Deus.Rose umewekwa kiganjani na Deus na kama angekuwa na shida ya kukudhuru wala asingewatumia hao vijana,angewatumia watu wako waliokuzunguka na wangekumaliza sekunde moja.Endapo utakayothubutu kujaribu kufanya chochote kwa Deus kama unavyofikiria nakuapia atakufinyanga kama udongo so don’t try him” akasema Vincent
“ Vincent please go away !! I’m surrounded by traitors !! Go away !! Akasema Rose huku akibubujikwa na machozi.

“ Rose you called me here because you need my help..Right now I’m the only friend you can count on” akasema Vincent
“ Go away Vincent .I’ll fight this war alone”
“ Rose huwezi kushinda vita hii.Let me help you to find who did this to you” akasema Vincent.Rose akamuangalia kwa jicho la chuki kisha akauliza
“ Who killed Amos and why? Akauliza Rose

“ Siwezi kukutajia ni nani aliyemuua lakini ninaweza kukwambia ni kwa nini aliuawa.Alikuwa tayari kuvujisha siri ambayo hakutakiwa kuitoa” akasema Vincent

“ Ouh Amos nitakulilia kilio gani mimi jamani..!!..akasema Rose huku akimwaga machozi
“ Rose ninadhani sintakuwa na jambo lingile la kuzungumza nawe kwa usiku huu. Endelea kupumzika na tafadhali zingatia hayo niliyokueleza.Dont start war with Deus.Nitakutembelea tena kujua hali yako” akasema Vincent

“ Vincent don’t show your face here again you monster !! akasema Rose kwa ukali .Vincent akaufungua mlango akatoka .

“ Aaaagggghhhh.!!!!! Akalia kwa uchungu Rose na mara Dr Imelda akaingia na kumchoma sindano ya usingizi ili aweze kulala





TUKUTANE SEHEMU IJAYO………
 
ENDELEA SEASON 5

SEHEM YA 1

“ Dr Joshua “ akasema Donald baada ya chumba
kutawaliwa na ukimya
“ Baada ya kukueleza suala la pili lililonileta hapa,
sasa turejee katika suala la kwanza.” Akasema Donald
“ Sawa endelea” akasema Dr Joshua
“ Awali nilikueleza kwamba tayari tumekwisha fanya
mipango yote ya kumuua Andrew Rodney na Deus Mkozumi
na kazi hiyo itafanywa na Alqaeda na litaonekana ni
shambulio la kigaidi.Serikali ya Tanzania wala Marekani
hazitahusishwa kabisa na tukio hilo badala yake nchi zote
zitaulaani kwa nguvu mtandao wa Alqaeda kwa kitendo
hicho.” Donald akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Ili kuutekekeleza mpango huo,Alqaeda wametoa
masharti mawili.Sharti la kwanza tumuachie huru mmoja wa
watu wao muhimu ambaye tunamshikilia katika mojaya
magereza yetu.Hilo tayari tumelikubali na tutamuachia huru
kiongozi wao.Sharti la pili kuna kiongozi wao muhimu sana
anashikiliwa nchini Saudi Arabia ambaye wanataka
aachiwe.Serikali ya Saudi Arabia haiku tayari kumuachia
kiongozi huyo kwa hiyo Alqaeda wanataka kuilazimisha
serikali ya Saudi Arabia kumuachia kiongozi wao na hilo
wataklifanya kutokea hapa nchini Tanzania”
“ Tanzania tena??!!...Dr Joshua akauliza
“ Ndiyo .Wanataka jambo hilo lifanyikie hapa
Tanzania” akasema Donald na kukawa kimya.Mara mlango
ukagongwa Dr Joshua akaenda kuufungua.Alikuwa ni mmoja
wa walinzi wake
“ Unasemaje Peter?
“ Mzee kuna kitu kimetokea hapa nyumbani sasa
hivi”
“ Kitu gani? akauliza Dr Joshua kwa wasi wasi
“ Kuna mwanamke mmoja amefika hapa anasema
anaitwa Peniela na anadai kwamba anaishi hapa na
anakufahamu na wewe ndiye uliyemruhusu aishi hapa”
Mwili wa Dr Joshua ukastuka kama vile umepitiwa na
chaji za umeme
“ Peniela ???..where is she? Akauliza
“ Yuko nje tunamshikilia”
“ Muachieni haraka aingie ndani ila mpitishe kwa
mlango wa nyuma aende moja kwa moja chumbani kwake
na asiruhusiwe kutoka hadi nitakapomaliza maongezi na
mgeni wangu”akaamuru Dr Joshua
“ sawa mzee” akajibu Peter na kuanza kuondoka Dr
Joshua akamuita
“ Peter sitaki jambo hili alifahamu mtu mwingine
zaidi ya ninyi mlioko hapa.Kuhusu wale polisi pale getini
tafuta namna yoyote ya kuwadanganya .Tell them she’s my
relative or anything.”
“ Sawa mzee nitafanya hivyo” akajibu Peter kwa
adabu
“ Another thing,umewasiliana na Kareem? Akauliza
Dr Joshua
“ Ndiyo mzee nimewasiliana naye ameniambia
kwamba yuko maeneo ya kule msibani”
“ Ok Good” akasema Dr Joshua na Peter akaondoka
“ Peniela !!!.Finaly I’ve got her...” akawaza Dr Joshua
huku akihisi mwili unamtetemeka kwa ndani kiasi cha
kumshangaza hata yeye mwenyewe ...
“ Sijui kwa nini kila ninapolisikia jina Peniela,mwili
wote hunitetemeka.Ngoja kwanza nimalize maongezi na
Donald halafu nitakwenda kuonana naye nifahamu kitu gani
kilichomleta hapa.Nashukuru amejileta mwenyewe ,nilikuwa
naumiza kichwa ningempata wapi.Nilikwisha sahau kabisa
kama nilimkabidhi nyumba hii aishi.” Akawaza Dr Joshua
aliyekuwa amesimama karibu na mlango mara akastuliwa na
Donald
“ Dr Joshua kuna tatizo lolote limetokea? Mbona
umebadilika ghafla?
“ Oh hapana Donald…Tuendelee na maongezi
yetu.Tuliishia wapi?
“ Nilikueleza kwamba Alqaeda wana kiongozi wao
anayeshikiliwa nchini Saudi Arabia na wanataka kuishinikiza
serikali ya Saudi Arabia imuachie huru na jambo hilo
litafanyika kutokea hapa Tanzania” akasema Donald
“ Naomba unifafanulie vizuri Donald.Wanataka
kufanya nini kuishinikiza serikali ya Saudi Arabia imuachie
kiongzo wao? Akauliza Dr Joshua ambaye macho yake
yalionyesha wazi alikuw ana wasi wasi mwingi
“ Binti mfalme wa Saudi Arabia aitwaye Salhat
Abdullah atatembelea Tanzania kwa mwaliko wa rafiki yake
ambaye ni Dr Lucia Mkozumi .Salhat na Dr Lucia wanafanya
kazi pamoja katika shirika la fedha la umoja wa mataifa kwa
hiyo ni marafiki wakubwa.Binti mfalme huyo ambaye
anapendwa mno na baba yake atakapofika hapa Tanzania
atatekwa nyara na atatumika katika kuishinikiza serikali ya
Saudi Arabia imuache kiongozi wa Alqaeda ili Salhat aachiwe
huru.Kwa jinsi Salhat anavyopendwa na baba yake lazima
atakubaliana na matakwa ya Alqaeda tu.”akasema Donald
“ Wanataka kumteka mtoto wa mfalme? Hebu
nifafanulie Donald watafanyaje hilo? Mbona mambo mengi
yanataka kutokea hapa nchini ndani ya kipindi kifupi?
“ Mpango mzima uko hivi.Lucy ambaye ndiye
aliyemualika salhat kuja hapa nchini ataongozana naye hadi
katika jengo la biashar ala Dar city shopping mall kwa lengo la
kufanya manunuzi ya vitu mbali mbali kwa ajili ya kupeleka
zawadi katika vituo vya watoto wanaoishi na virusi vya
ukimwi kwani Salhat anayo taasisi yake inayojishughulisha na
kuwahudumia watoto wa aina hiyo .Katika msafara huo Dr
Lucia anapaswa kuhakikisha kuwa baba yake Deus Mkozumi
anaambatana nao .Wakati manunuzi yakiendelea Lucia
atampeleka Salhat katika duka moja linalouza
vinyago..Atakapofika huko Alqaeda watalivamia jengo hilo
na kuwachukua mateka Dr Lucia na Salhat na hapo ndipo
Deus Mkozumi atakapouawa”
Dr Joshua akatoa kitambaa na kujifuta jasho lililoanza
kumtoka usoni.Alihisi joto kutokana na mambo mazito
aliyoelezwa na Donald
“ Nini kitafuata baada ya hapo? Akauliza Dr Joshua
kwa wasi wasi
“ Dr Lucia Mkozumi ataachiwa huru,Salhat
ataendelea kushikiliwa na magaidi na ili aachiwe huru
watashinikiza kuachiwa huru kwa kiongozi wao kwanza”
akasema Donald
“ Itakuaje endapo madai yao yasipotimizwa? Akauliza
Dr Joshua
“ Ikitokea kwamba madai yao yasipotimizwa
wataondoka na Salhat na itakulazimu kuwasaidia kuondoka
hapa nchini lakini kwa utafiti uliofanyika tunaamini lazima
madai yao yatatekelezwa kwani mfalme anampenda mno
mtoto wake.Kiongozi wao atakapoachiwa huru watamuachia
Salhat na watapotea zao”
Dr Joshua akafikiri kidogo halafu akasema
“ Nina wasiw asi katika shambulio hilo litakalofanyika
Dar city shopping mall,watu wasio na hatia watapoteza
maisha yao.”
“ Ni kweli hilo unalolisema Dr Joshua na haliwezi
kuepukika.Lazima watu wapoteze maisha .Nadhani
unafahamu namna mashambulizi ya kigaidi
yanavyokuwa,lazima idadi kadhaa ya watu wapoteze maisha”
“ Naogopa sana Donald kusema chochote kwa sasa
hasa nikivuta picha ya watu wasio na hatia wakiwa wamelala
chini hawana uhai...Inaniogiopesha sana.Damu ya watu hao
wasio na hatia itatuandama sisi tuliosaidia kufanikisha
shambulio hilo.” Akasema Dr Joshua
“ Usiogope Dr Joshua.Kazi ya urais ni ngumu na kuna
nyakati unatakiwa kufanya maamuzi magumu sana kwa
maslahi mapana ya nchi.Wakifa watu kumi au ishirini si kitu
kwani kuna mamilioni ya watu waishio vijijni watakwenda
kunufaika na huduma za maji,afya,elimu,kilimo n.k.Kwa hiyo
usiogope Dr Joshua kufanya maamuzi kwani maamuzi
utakayoyafanya leo yanaakisi maendeleo makubwa kwa
Tanzania kwa miaka mingi ijayo.Nakuhakikishia Dr Joshua
baada ya miaka kumi Tanzania hii uionayo sasa haitakuwa
kama unavyoiona leo.Itakuwa na mabadiliko makubwa mno
lakini haya yote yanategemea maamuzi utakayoyafanya
kuhusu suala hili” akasema Donald.Dr Joshua akainamisha
kichwa akiwaza na baada ya muda akasema
“ Dr Lucia Mkozumi anafahamu kuhusiana na baba
yake kutakiwa kuuawa ?
“ Anafahamu kila kitu na ameshiriki katika kuandaa
mpango huo.Dr Lucia mkozumi hafahamiki kabisa hapa nchini
na tukio hili litachangia sana katika kumtangaza.Dunia yote
watamfahamu yeye ni nani ndani ya kipindi kifupi sana na
atakapotangaza kuwania urais wa Tanzania haitakuwa kazi
ngumu kumnadi.Dr Joshua kila jambo lina sadaka yake na Dr
Lucia Mkozumi yuko tayari kwa lolote ili aweze kuupata urais
wa Tanzania” akasema Donald..Dr Joshua akakosa neno la
kusema
“ Dah ! huyu Lucia lazima atakuwa ni mwanamke
mwenye roho ngumu sana.Kama kweli amekubali baba yake
auawe na magaidi basi ni mwanamke anayefaa kabisa kuwa
rais kwani urais unahitaji mtu mwenye kuweza klufanya
maamuzi magumu kama aliyofanya Dr Lucia.She’s a monster
just like me.Lakini hata hivyo siwezi kuukataa mpango huu
kwani umekuja kwa wakati muafaka kabisa.Kwa muda mrefu
nimekuwa nkitafuta namna ya kumuondoa Deus Mkozumi
kwani amekuwa akiingilia sana mambo yangu na sasa nafasi
hiyo imejitokeza na siwezi kuiacha.Nitaitumia fursa hiyo
kumuondoa si Deus Mkozumi peke bali na mke wake
Rosemary Mkozumi.I hate that woman so much.Najua
atakuwa ni kikwazo kikubwa kwangu kufanikisha mambo
yangu .Lazima nimuondoe haraka sana Yule mwanamke ili
mpango huu usiingiliwe na kikwazo chochote”
“ Dr Joshua !!” akaita Donald na kumstua Dr Joshua
toka mawazoni
“ Donald mambo uliyonieleza ni makubwa na mazito
sana lakini ninaiona faida kubwa mbele yake.Japokuwa
uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kubwa lakini idadi
kubwa ya raia wake bado masikini na kwa ahadi hizi ambazo
serikali ya Marekani imeziahidi ninayaona mabadiliko
makubwa kwa Tanzania.Kwa upande wangu mimi sina tatizo
katika hili ilimradi tu ahadi zote zuilizoahidiwa
zitekelezwe.Najua baada ya matukio hayo kutokea mtikisiko
kidogo wa uchumi lakini nina imani ndaniya kipindi kifupi
hali tarejea kuwa ya kawaida.” Akasema Dr Joshua .Donald
kwa furaha aliyoipata akainuka na kumpa mkono Dr Joshua
“ Hongera sana Dr Joshua.Wewe ndiye rais unayeona
mbali.Una mtazamo mpana sana kwa nchi
yako.Ninakuhakikishia kuwa maamuzi yako ya leo yatakuwa
na faida kubwa sana kwa nchi yako siku za
usoni.Nakuhakikishia wananchi wa Tanzania watakukumbuka
daima kwa kuwaachia rais kama Dr Lucia ambaye wakati wa
uongozi wake serikali ya Marekani itamwaga misaada mingi
sana kwa serikali yake itakayowanufaisha mamilioni ya
watanzania.Nataka nikuondoe wasi wasi pia kwamba mambo
yote yatakayotokea si Tanzania wala Marekani
watakaolaumiwa bali ni mtandao wa Alqaeda.Wakati dunia
ikiwalaani magaidi ,mamilioni ya watanzania watakuwa
wanapata huduma za maji safi ya kunywa,huduma bora za
afya,elimu nishati ajira pamoja na mambo mengine mengi
toka kwa serikali ya Marekani.Kwa kauli yako hiyo
mheshimiwa rais unaniruhusu niwataarifu wakubwa zangu
kwamba umekubali ili tuweze kuendelea na hatua
inayofuata?
“ Bila shaka Donald,unaweza kuendelea na hatua
inayofuata.Nini kinachofuata baada ya hapa?
“ Hatua inayofuata ni kumleta nchini rais mtarajiwa
Dr Lucia Mkozumi na tutakuwa na maongezi ya pamoja
mimi,wewe,Dr Lucia pamoja na mratibu wa mashambulio
mawili toka Alqaeda .Dr Lucia yuko nchini Afrika ya kusini
akiwa ameambatana na binti mfalme Salhat nitawasiliana
naye usiku huu na kesho atakuwa hapa nchini na kesho hiyo
hiyo jioni tutakutana hapa kwa ajili ya kukaa kikao kizito cha
kupanga mikakati ya utekelezaji wa matukio yote.” Akasema
Donald.
“ Sawa Donald.Tutaonana hiyo kesho.Tutakutana
hapa hapa kwani ndiyo sehemu salama zaidi kwa sisi kuongea
na kupanga mipango yetu” akasema Dr Joshua na kuagana na
Donald akamsindikiza hadi lilipo gari lake akaondoka zake na
Dr Joshua akarejea sebuleni akaketi sofani
“ Mambo aliyotumwa Donald aje anieleze ni mambo
mazito mno lakini endapo yatafanikiwa kutekelezwa basi nchi
yetu itapata manufaa makubwa kuliko athari zitakazojitokeza
katika utekelezaji wake .Nchi itayumba kidogo lakini ndani ya
kipindi kifupi itakaa sawa na wananchi watasahau kabisa
matukio yote.Suala hili ukilitazama kwa upana wake ni kweli
Marekani wanastahili kulinda maslahi yake kutokana na
kufanya uwekezaji mkubwa sana hapa nchini kuliko nchi
nyingine yoyote afrika.Uwekezaji huu unawapa nguvu ya
kuweza kuingia hadi katika siasa zetu na kuchagua rais
wanayemtaka ambaye wanaamini atakuwa na manufaa
kwao.Hili si tatizo as long as wananchi wetu wananufaika
kwa misaada mikubwa itakayotolewa na Marekani.Kipindi
changu cha uongozi,serikali ya Marekani wamekuwa ni
wafadhili namba moja wa bajeti yetu ya serikali na miradi
mingi ya maendeleo na endapo nikifanikisha Dr Lucia awe
rais kama wanavyotaka misaada itaongezeka maradufu”
akawaza Dr Joshua na kukumbuka kitu akatabasamu
“ Dr Lucia Mkozumi,huyu mwanamamama japokuwa
sijabahatika kuonana naye lakini anaonekana anafaa sana
kuwa rais.Anaonekana ni mtu jasiri na asiyesita kufanya
maamuzi makubwa “ akawaza Dr Joshua akajimiminia whisky
katika glasi na kunywa funda kadhaa
“ Kwa upande wangu nimeahidiwa mambo mengi
makubwa .Kikubwa zaidi ni fedha nyingi.It’s a lot of
money.Maisha yangu baada ya kustaafu yatakuwa mazuri
mno.I’ll be like an angel in heaven.Laiti kama jambo hili
lingekuja mapema kabla sijaanza mchakato wa kukiuza kirusi
Aby katu nisingeuza kitu kile kilichojaa mikosi na hadi sasa
mke wangu na mwanangu Flaviana wangekuwa bado hai..”
Mara wazo likamjia Dr Joshua
“ Kwa kuwa kuna huu mpango mpya umekuja ambao
unaonekana ni bora zaidi na una maslahi mapana kwangu na
kw anchi kwa nini nisiachane na mpango ule wa kukiuza
kirusi Aby?.Kirusi kile naona kama vile kina mkosi kwani
mpaka sasa tayari nimemkwisha wapoteza watu wangu
wawili wa karibu sana halafu kitu kingine ni kwamba
sifahamu Hussein anataka kukitumiaje kirusi hicho.”
Dr Joshua akanywa tena funda la mvinyo
“ Hapana siwezi kumpa Hussein kile
kirusi.NItamrejeshea fedha zake zote .Najua itakuwa ngumu
lakini hakuna namna nyingine lazima niachane na mpango
ule na nielekeze nguvu katika mpango huu wa Marekani
ambao una maslahi manono kwangu..”
Akatulia tena akanywa funda lingine la mvinyo
“ Dah ! Imekuwa ni siku ndefu sana iliyokusanya
mambo mengi na kichwa changu kimechoka.Nahitaji
kupumzika lakini kabla ya yote lazima nikaonane na Yule
......
 
SEHEM YA 22

“ Peniela is here already”
“ Ouh tayari amekwisha fika? Amekuja na taarifa
gani? Kuna chochote amekipata huko kwa dr Joshua?
“ Ndiyo anasema kuna mambo mazito ameyapata
huko kwa hiyo nitakaporejea atatueleza kwa sasa
nimeamuacha apitie vilivyomo katika lile kasha lake
.”
“ Umemueleza kuhusiana na kupatikana kwa kirusi?
“ Tayari nimemueleza ila sijamfahamisha
kimepatikanaje.Nitakaporejea nitamjulisha kila kitu
.Kwa sasa
tumpe nafasi aweze kupitia kwa makini kila kilichom
o ndani
ya kasha lile.Keep an eye on Kigomba” akasema Mathe
w na
kuingia chumbani kwake akachukua silaha na kuondoka
Peniela alilifungua kasha lile na kuanza kupitia
bahasha moja baada ya nyingine.Alipoifikia bahasha
yeye
picha za wazazi wake aliikumbatia picha ya mama yak
e na
kumwaga machozi mengi
“ Dunia hii imejaa watu makatili sana.kwa nini bab
a
bila ya huruma akaamuru mama auawe? Look at her,she
’s so
pretty.” Akawaza huku akifuta machozi na kuitazama
picha
nyingine ya baba yake akaichana chana kwa hasira
“ Una bahati John aliwahi kukuua shetani wewe
kwani endapo asingefanya hivyo ningekuua mimi kwa m
kono
wangu.Natumai huko uliko unaungua katika shimo la m
oto
shetani wewe” akasema Peniela kwa sauti ndogo huku
uso
wake umejikunja kwa hasira.Akaziweka pembeni picha
zile na
vitu vingine alivyovikuta ndani ya lile kasha halaf
u akachukua
flash disk akaichomeka katika kompyuta na kuanza
kuitazama video aliyojirekodi John Mwaulaya
Hadi video ile inamalika mwili wote wa Peniela
ulikuwa umeloa jasho.Akavuta pumzi ndefu na kulazim
ika
kuwasha feni ili kuipooza hali ya hewa kwani alihis
i joto kali
ghafla.Akairudia tena kuitazma video ile kwa mara y
a pili na
ya tatu .Akaegemea kiti
“ Nahisi ni kama vile niko usingizini ninaota ndot
o hii
ya kusisimua lakini haiko hivyo.Siko usingizini na
wala sioti
ndoto.” Akawaza huku jasho likiendelea kumtoka
“ Sasa nimeamni ni kweli John Mwaulaya alikuwa
ananipenda kwa dhati kama mwanae.Ni yeye ndiye
aliyenikoa toka mdomoni mwa kifo.Alitumwa kuniua mi
mi na
mama yangu lakini akaamua kuniacha hai .Toka nikiwa
mdogo nimeishi maisha mazuri mno na hata siku moja
sikuwahi kupungukiwa kitu chochote na sikuliona pen
go la
kuwakosa wazazi wangu.Haya yote aliyafanya John
Mwaulaya.Pamoja na hayo yote ni kweli aliziharibu n
doto
zangu kubwa za maisha nilizokuwa nazo kwa kuniingiz
a
katika Team SC41 lakini alilitambua kosa lake na ka
tika
nyakati za mwisho za uhai wake amekuwa akitafuta ku
fanya
kila awezalo kuyarekebisha maisha yangu ili niishi
maisha
mapya.Mambo aliyonifanyia ni makubwa na sikuyategem
ea
kabisa.Amenifanya nimekuwa binadamu mwenye thamani
kubwa kuliko wote duniani.Sikutegemea kabisa kama J
ohn
angeweza kunifanyia jambo kubwa kama hili.Angeweza
kujichoma yeye kinga yote lakini kwa kuwa ananipend
a
hakufanya hivyo badala yake akaniwekea mimi kinga
hiyo.Vitu vyote alivyoniachia si kitu bali utajiri
mkubwa
ambao ameniachia ni hii kinga aliyoiweka mwilini mw
angu
dhidi ya kirusi Aby.Huu ni utajiri mkubwa mno kulik
o hata
mapesa aliyoniacia.This is what I’ve been wanted.Th
is is what
I’ve been dreaming for so long.The whole world will
kneel
down on me.Every human on earth will speak my
name.Nitaingia katika vitabu vya historia na jina l
angu
litatamkwa kwa vizazi hata vizazi.Damu yangu itakuw
a na
thamani ya matrilioni na matrilioni ya pesa.Nitakuw
a tajiri
mkubwa sana duniani.Naweza kusema kwamba hii imekuw
a
ni bahato sana kwani nimegundua thamani yangu na wa
kati
huo huo kirusi kimetua mikononi mwetu.So I have ve
everything now.Nina kinga na kirusi pia.Ouh John th
ank you
so much for this” akawaza Peniela na kusimama huku
akitabsamu
“ Huu ni mwanzo wa kitabu changu kipya cha maisha
yangu.Kutoka Peniela niliyekuwa kama chombo cha sta
rehe
hadi binadamu ghali kuliko wote lakini ili ndoto ya
ngu iweze
kutimia lazima nihakikishe ninakimiliki kirusi Aby
mwenyewe.Mipango ya Mathew baada ya kukipata kirusi
Aby ni kukihifadhi katika sehemu salama ili kisitum
ike katika
kusababisha maangamizi makubwa.Endapo akifanya hivy
o
basi kinga yangu haitakuwa na maana yoyote.Ndoto ya
ngu
haitaweza kutimia.I have to take the virus before M
athew
comes back.” Akawaza Peniela na mwili wote ukamsisi
mka.
“ Mawazo gani haya yananijia? Nikifanya hivi
nitakuwa nimewasaliti wenzangu waliopambana mno had
i
wakafanikiwa kukipata hicho kirusi.Sintakuwa na tof
auti
yoyite na jaji Elibariki.What am I going to do?? Ak
ajiuliza na
kuinamisha kichwa kwa sekunde kadhaa.Alisikia kitu
kama
sauti ikimwambia
“ Take the virus now !!
Picha za haraka haraka za namna atakavyoishimaisha
yakitajiri zikamjia
“ Sauti hii ninayoisikia ndani mwangu iko sahihi
kabisa .Kama ninataka kuitimiza ndoto yangu basi wa
kati ni
sasa .Nikishindwa kukichukua kirusi sasa sintaweza
tena
kukichukua baadae Mathew akirejea.Lazima nikichukue
halafu nifanye mpango wa kukihakiki kama kweli ni
chenyewe na baada ya hapo nikiachie kisambae hewani
na
hapo ndipo historia ya dunia itakapobadilika.Mtu pe
kee
ambaye anaweza kunihakikishia kama kirusi hiki ni h
alisi ni
Deus Mkozui .Huyu amekuwa rais kwa miaka kumi na
anakifahamu vizuri kirusi hiki.Nitamtafuta ili nipa
te uhakika
kuwa kirusi hicho ni chenyewe.Kama ni hivyo I have
to save
Deus kwani bado namuhitaji sana” akawaza halafu
akakumbuka kitu
“ Kuna mtu mmoja ambaye anaweza akawa na
msaada mkubwa kwangu.Dr Kigomba.Huyu ana tamaa ya
fedha na kwa vile sasa hivi hana mbele wa nyuma ata
fanya
kila nitakachomuelekeza akifanye”
Peniela akajishika kiuna na kuinamisha kichwa
“ Kwa hili ninalotaka kulifanya niko sahihi? Nimet
oka
mbali na akina Mathew tumehangaika katika kuhakikis
ha
tunakipata kirusi Aby.Tumepitia mambo mengi ya hata
ri na
Mathew ameniokoa ,zaidi ya yote tayari Mathew amekw
isha
anza kuniingia moyoni.Nimatokea kumpenda .Endapo
through it.We’re going to be very very rich and I’m
going to
help you get out of the country”
“ Ouh Peniela ar.....” Kigomba akataka kusema kitu
lakini Peniela akamzuia
“ Don’t say anything yet.Hatuna muda mrefu
Mathew atarejea hapa muda wowote.Nataka nikuweke w
azi
kwamba Mathew hana mpango wowote wa kukutorosha
kwenda nje ya nchi bali anataka kuitumia familia ya
ko
kukushinikiza ili uweze kumpa siri za mtandao
wenu.Amepanga kuitesa familia yako mbele yako ili u
sikie
uchungu na useme siri zenu.Kwa hiyo mimi kwa sasa n
diyo
msaada wako mkubwa.Ninakwenda kuchukua kirusi ili
tuondoke kabla Mathew hajarejea” akasema Peniela
“ Sawa Peniela,Fanya haraka haraka tondoke.Be
careful,that man is very dangerous !!! akasema Dr
Kigmba.Penela akatoka na kuelekea moja kwa moja kat
ika
chumba cha Mathew akakinyonga kitasa cha mlango
ukafunguka kwani haukuwa umefungwa kwa funguo.Moja
kwa moja akaelekea katika kasiki ambalo Mathew alih
ifadhi
sanduku lenye kirusi Aby,akafumba macho na kuzikumb
uka
namba alizotumia Mathew kufungulia kasiki lile akaz
ibonyeza
na kasiki likafunguka.Akalitoa sanduku lile lenye k
irusi
akalifungua akatazama ndani ili kuhakiki kama kirus
i
kilikuwamo ndani akatabasamu
Akiwa chumbani kwake Anitha alisikia mlango wa
chumba cha Mathew ukifunguliwa akadhani Mathew ame
rdi
“ Mbona Mathew amerejea mapema namna hii?
Halafu iweje arejee bila ya kupita hapa chumbani kw
angu na
kunijulisha kuwa amerudi? Hii si kawaida yake” akaj
iuliza
Anitha na kuufungua mlango wa chumba chake akaeleke
a
katika chumba cha Mathew.Mlango wa chumba cha Mathe
w
haukuwa umefungwa
“ Mathew ! akaita Anitha bila kujibiwa
“ Mathew !! akaita tena lakini hakujibiwa .
Sauti ya Anitha akimuita Mathew ikamstua Peniela
aliyekuwa ndani ya chumba cha Mathew.Juu ya meza ka
ribu
na kitanda kulikuwa na kisanduku kidogo chenye silah
a
walizopewa na Edmund Dawson kwa kasi ya aina yake
akakifungua na kutoa kisu kikali taratibu mlango
ukafunguliwa na Anitha akaingia ndani.Akastuka san
a
“ Penie.......!!! Akasema Anitha lakini kabla
hajamaliza kutamka kwa kasi ya umeme na nguvu Penie
la
akarusha kisu kile kikubwa kikatua katika kifua cha
Anitha
ambaye akaanguka chini huku akitoa ukelele mkubwa.K
wa
haraka Peniela akamfuata pale chini alipoanguka
akakichomoa kile kisu na kukichoma kwa nguvu kifuan
i
sehemu ulipo moyo na kama hautoshi akakikanyaga na
mguu
kikazama chote
“ I’m so sorry Anitha”akasema kisha akalinyakua li
le
sanduku lenye kirusi akatoka mbio hadi chumbani kwa
Kigomba akamuacha Anitha anatapa tapa pale chini
“ Let’s go !! akasema na kisha akaelekea katika
chumba cha ofisi akalichukua lile kasha alilopewa
na John
Mwaulaya wakaingia garini na kuondoka kwa kasi.
Ukelele aliopiga Anitha pamoja na sauti za milang
o
ya gari kufungwa kwa nguvu na kisha gari kuondoka k
wa kasi
.....
 
SEHEM YA 32

na kuufunika kabisa ule mlango wa ndani.Peniela
akachanganyikiwa hakujua afanye nini
“ Mhhh hapa tumelikoroga.Sijui Chin amefanya nini
humo ndani.Inaonekana nyumba hii ina mambo makubwa
tusiyoyafahamu.Natakiwa nitafute namna ya kujiokoa
toka
humu ndani haraka sana kabla na mimi hayajanikuta k
ama
yaliyomkuta Chin sun.” akawaza peniela na kutoka mb
io
akajaribu kuufungua mlango lakini tayari ulikuwa
umejifunga.Akachukua stuli na kukipiga kioo cha dir
isha
kikapasuka akapenya na akuruka nje .Akakimbia hadi
katika
gari la Chin sun lakini lilikuwa limefungwa na fung
uo alikuwa
nazo Chin sun.Pale nje kulikuwa na gari la Edmund ,
akajaribu
kufungua mlango haukuwa umefungwa.akaingia ndani y
a
gari na kutabasamu baada ya kuzikuta funguo zikiwa
zinaning’inia garini.Akaunyonga ufunguo na gari
likawaka.Kaba hajaondoka akalifungua sanduku lile l
enye
kirusi akahakikisha kipo salama akafungua geti na
kuondoka
na gari la Edmund
Edmund na Mathew wakiwa njiani wakirejea ofisini
,huku Mathew akiwa katika usukani baada ya kuachiwa
na
Edmnd aendeshe ,mara Edmund akasema
“ Peniela ametoroka.Ameondoka na gari langu lakini
usiogope tutampata tu kwani gari langu lina kifaa m
aalum
cha kuniweza kuliona kila mahala lilipo” akasema Ed
mund
“ sawa Edmud ,kitu cha msingi kwa sasa ni kumfuata
Peniela kwani ndiye mwenye hatari kubwa kutokana na
kirusi
anachotembea nacho.” Akasema Mathew
“ Hapana Mathew,Chin sun ni muhimu sana
kwangu.Niko hapa Tnzania kwa sababu yake kwa hiyo s
iwezi
kupoteza nafasi hii.Natakiwa kumpata akiwa hai .End
apo
tutachelewa sana anaweza akapoteza maisha kwani kwa
kawaida ofisi ile ikijifunga kuna hewa Fulani ambay
o hutoka
na kumlewesha mtu aliyemo ndani .Hewa hiyo ina muda
maalum na endapo ukichelewa sana kumzindua anaweza
akapoteza maisha.Nipeleke mimi ofisini na wewe utae
ndelea
kumfuatilia Peniela” akasema Edmund
“ Hapana Edmund,siwezi kuifanya kazi hii peke
yangu.Nahitaji msaada.Lazima twende wote” akasema
Mathew na Edmund hakujibu kitu.
*************
Dr Joshua aliwasili katika nyumba yake iliyoko
ufukweni mwa bahari kwa ajili ya kumuhoji Kareem ml
inzi
wake ambaye alionekana katika nyumba ambayo uchungu
zi
unaonyesha alikuwemo Anna.Bado kareem alikuwa
hajafikishwa.Dr Joshua akaenda katika chumba alicho
kuwa
analala Peniela lakini chumba kilikuwa kitupu.
“ Peniela yuko wapi? Mbona haya mambo yanaanza
kunichanganya sana ? akawaza Dr Joshua akakaa kitan
dani
na kuzama mawazoni.
“ Katika vitu vyote siko tayari kumpoteza Peniela
.Yule mwanamke ndiye furaha yangu.Utajiri huu mkubw
a
nikiupata hautakuwa na maana kama sintakuwa na Peni
ela
.Kwa namna yoyote ile laz.......” Dr Joshua akatolewa
mawazoni na mlio wa simu.Alikuwa ni Abel Mkokasule
“ Hallo Abel” akasema Dr Joshua
“ Mzee nimekupiga simu kukutaarfu kuwa kazi tayari
imekamilika na kilichobaki ni kuisambaratisha hote
li.Nataka
kabla sijabonyeza kitufe na kuilipua hoteli unipe r
uhusa yako
kama hakuna mabadiliko ” akasema Abel
“ Abel go ahed,hakuna mabadiio yoyote.Pleae press
the button now !! akasema Dr Joshua
“ Sawa mzee.Baada ya dakika chache toka sasa
utataarifiwa kitakachokuwa kimetokea”
“ Abel,thank you for this.” Akasema Dr Joshua na
kukata simu akatoka mle chumbani baada ya mlinzi w
ake
kumfuata na kumfahamisha kuwa tayari Kareem amekwis
ha
wasili.Akaagiza akafungiwe katika mojawapo ya chumb
a.
Kareem akaingizwa katika chumba alichoagiza rais
akafungwa miguu na mikono katika kiti na baada ya d
akika
tano Dr Joshua akaingia .Macho yake yaliwaka hasira
.Kareem
akaogopa sana hakuwahi kumuona Dr Joshua akiwa
amekasirika namna ile.Akawaomba walinzi wake watoke
nje
na wamuache na Kareem pekee mle chumbani .
“ Kareem my boy !! akasema Dr Joshua
“ Naam mzee”akasema Kareem kwa woga
“ Mungu hakunijalia kupata mtoto wa kiume kwa
hiyo nilikuchukulia wewe kama mwanangu i wa kiume.I
love
you like a son so I don’t want to destroy you.Nina
chohitaji
toka kwako ni kitu kimoja tu .Niambie Anna yuko wap
i?
“ Mzee sifahamu mahala alipo anna “ akajibu Kareem
“ kareem sina maneno mengi kwa hiyo nakuuliza
tena kwa mara ya mwisho Anna yuko wapi?Nionyeshe al
iko
Anna na nitaliacha jambo hili lipite kama vile haku
na
kilichotokea.” Akasema
“ kweli mzee naomba uniamini .Sifahamu kwa sasa
Anna aliko”
Dr Joshua akasimama kwa hasira
“ kareem naomba usicheze na akili yangu.Umekutwa
katika nyumba ambayo Anna alikuwemo .Ulifuata nini
katika
hiyo nyumba? Nakupa dakika mbili za kunieleza ukwel
i ama
sivyo hutayaona machweo ya leo.Nadhani unanifahamu
nilivyo nikichukia” akasema Dr Joshua kwa ukali.Kab
la
Kareem hajajibu kitu,simu ya Dr Joshua ikaita,aliku
wa ni Abel
Mkokasule.
“ hallow abel” akasema Dr Joshua
“ Mzee kazi tayari imemalizika.Samawati beach hote
l
is down.”
“ Good job Abel and thank you.Nitakutafuta
nitakaporejea ikulu muda si mrefu.” Akasema Dr Josh
ua na
kukata simu akamgeukia Kareem
“ Haya nieleze kareem ,Anna yuko wapi?
“ Mzee ninakueleza ukweli” akasema Kareem mwili
wote ukiwa umeloa jasho
“ Wakati wa shughuli za mazishi ya Flaviana
zikikaribia kumalizka ,Peniela alinipigia simu na k
uiambia
kwamba anahitaji kuonana na Anna.Sikuwa na wasi was
i
wowote naye kwani nafahamu mahusiano yenu.Alinielek
eza
sehemu ambayo anataka kuonana na Anna nami
nikampeleka wakaonana nikamrudisha nyumbani.Leo
uliponitaka nimtafute Peniela sikujua sehemu nyingi
ne ya
kumpata nikaenda katika ile nyumba ambako aliniagiz
a
nimpeleke Anna wakaonane lakini nilipofika nikakama
twa na
watu wa usalama wa taifa .Kwa hyo mzee sifahamu kab
isa
alipo Anna kwani toka nilipomrejesha nyumbani juzi
usiku
sijawasiliana naye kabisa.Katika ile nyumba nilikwe
nda
kumtafuta Peniela.Naomba uniamini mzee” akasema
Kareem.Dr Joshua alibaki amemtumbulia macho .Alistu
shwa
kwa taarifa ile
“ I cant believe this!! Unasema Peniela alionana n
a
Anna?
“ Ndiyo mzee”
Dr Joshua akainuka na kupiga hatua mbili kama vile
anataka kutoka nje halafu akarudi akaketi
“ Huko mahala ulikompeleka Anna aonane na Peniela
kulikuwa na watu wengine zaidi ya Peniela?
“ Ndiyo walikuwepo.Nakumbuka kulikuwa na watu
wengine wawili.Mwanaume mmoja ninayemkumbuka kwa
jina moja tu la Mathew na mwanamke anaitwa Anitha”
Dr Joshua akastuka mno na kulalama
“ Oh my God !! ..oh my God ...! On my God..!!!!
akajishika kichwa
“ Anna ameonana na huyo mtu anaitwa Mathew?
Waliongea chochote?
“ Ndiyo waliongea ila sikumbuki waliongea kitu gan
i
kwani walikuwa katika chumba kingine na hawakutaka
nisikie
walichokiongea.”
Dr Kigomba akainamisha kichwa kwa kama dakika
mbili na mara mlango ukagongwa akaufungua na kukuta
na
na walinzi wake.
“ Mzee kuna tukio limetokea muda mfupi
uliopita.Milipuko inayosadikiwa kuwa ni mabomu imet
okea
samawati beach hotel .Mheshimiwa rais kwa sasa tunao
mba
tukurudishe ikulu kwa ajili ya usalama” akasema mmoj
a wa
walinzi
“ Sawa tuondokeni ila huyu Kareem atabaki hapa
,Abel Mkokasule atakuja kumchukua baade kwa mahojia
no
zaidi” akasema Dr Joshua akaongozana na walinzi wak
e hadi
garini wakaondoka kurejea ikulu.
“ Tayari nimepata jibu.Anna anashirikiiaa na akina
Peniela na wao ndio wenye kirusi hicho kwa sasa.Eli
bariki
alikuwa sahihi Peniela ni nyoka.How could I be so s
tupid and
trust her?Hili ni kosa kubwa nimewahi kufanya katik
a maisha
yangu .Nahisi Peniela ana uchawi anautumia kiasi ch
a
kunifanya nishindwe kabisa kumuamini jaji Elibariki
ambaye
alinieleza ukweli mtupu.Suala hili limekwisha nishi
nda na sijui
tena namna ya kulidhibiti.Nahisi kama vile akili ya
ngu imefika
mwisho wake wa kufikiri kwani sijui nifanye nini ku
wapata
hawa akina Mathew “ akawaza Dr Joshua akiwa garini
akirejea ikulu.
“ Nashindwa kuelewa imetokeaje hadi Anna
akajiunga na hawa mashetani akina Mathew? Nimesalit
iwa
na mwanangu mwenyewe.Hili ni jambo ambalo sikuwa
nimelitegemea kabisa.Kwa mara ya kwanza katika maish
a
yangu nathubutu kujishusha thamani na kujiita mjing
a.I’m so
stupid” akaendelea kuwaza Dr Joshua huku macho yake
yakilengwa na machozi.
“ Inaniumiza mno kumpoteza mwanangu Anna kwani
kitendo alichokichagua cha kujiunga na akina Peniel
a tayari
ameingia katika kundi la maadui zangu.Anna amechagu
a njia
mbaya,hakupaswa kuchagua kuwa adui yangu.kwa hiki
alichokifanya Anna sintakuwa na huruma kwake hata
kidogo.Nitamsaka na kumshughulikia kama
ninavyowashughulikia maadui zangu wengine na endapo
itanilazimu kumkata pumzi sintakuwa na huruma nitam
kata
pumzi .Ni bora nibaki mwnyewe kuliko kuwa na mtoto
shetani kama Anna”
Kichwa cha Dr Joshua hakikutulia,alikuwa na mawazo
mengi mno
“ Nadhani kwa sasa baada ya Hussein kufa natakiwa
nielekeze nguvu katika mpango ule wa Marekani ili n
iondoke
kabisa hapa nchini nikaanze maisha mapya peke yangu
huko
mbali Nimepata somo kubwa sintomuamini tena mwanamk
e
yeyote” akawaza Dr Joshua
****************
Tayari Lucia Mkozumi alikwisha maliza kujiandaa kw
a
ajili ya kwenda kumpokea rafiki yake Salhat ,binti
mfalme wa
Saudi Arabia.Pamoja na kuwa tayari kwa kutoka lakin
i alihsi
miguu mizito akabaki amesimama mbele ya kioo kikubw
a
akijitazama
“ Nina wasi wasi mwingi sana,mwili unanitetemeka
kwa ndani kwa hofu ya hiki kinachokwenda kutokea
leo.Moyo unaniuma sana kwa kitendo cha kuwatoa kafa
ra
wazazi wangu.Oh ! please forgive me lord for what I’
m
doing.I’ve become a monster!!” akawaza Lucia na mic
hirizi ya
machozi ikamtoka akaanza tena kurekebisha uso wake.
“ Anyway ,I have to be strong.I cant back off now
.Kila kitu tayari kimeandaliwa .Nitaumia kwa muda m
fupi
lakini nitasahau yote pale nitakapokalia kiti cha u
rais”
akawaza huku akimalizia kupaka poda usoni.Akachukua
simu
akampiga Donald akamfahamisha kuwa kila kitu kinakw
enda
vizuri .Alipomaliza kuongea na Doald akajitazama te
na katika
kioo
“ This is it.Journey to the white house begins now

akasema kwa sauti ndogo na kutoka akaelekea sebulen
i
ambako baba yake Deus Mkozumi tayari alikuwa amejia
ndaa
akimsubiri
“ wow umependeza mno utadhani nawe ni mtoto wa
mfalme” akatania Deus na wote wakacheka
“ Usisahau hata mimi ni mtoto wa rais” akasema
Lucia
“ Are you ready? Deus akauliza
“ I’m ready”akasema Lucia akiongozana na baba yake
wakaingia garini na safari ikaanza , wakitanguliwa
na gari la
walinzi na gari lingine ambalo liliandaliwa maalum
kwa ajili ya
kupanda Salhat.Deus Mkozumi akawaelekeza walinzi
waliotangulia mbele kwamba waelekee nyumbani kwa
Rosemary Mkozumi.
.....
 
Lege inaonekana wewe ni mdau mkubwa wa Riwaya kama mimi. Kwa kweli siwezi orodhesha idadi ya riwaya nilizosoma. Nimeanza kuvutiwa kusoma kipindi nipo darasa la 3. By then nilikua naona mama akisoma sana riwaya za enzi hizo. Nami nikawa nasubiri amalize ili nisome. Kwa kweli nilikuwa na vutiwa sana. Nilikuwa msomaji mzuri kwa sababu kipindi cha magazeti ya sana nilikuwa nawasomea washkaji class. Watu wamekuzunguka hivyo unasoma kwa sauti wote wasikie. Nilikuwa nina library ya hizi riwaya kibao. Nikisafiri kwa basi pale Ubungo lazima ninunue ndani ya basi naburudika bila kuchoka. Zikaja zile za Shigongo, nilikua nakesha kwa utamu. Jamani riwaya ni tamu sana kama unazikubali. Bora nisiangalie movies lakini nisome riwaya yenye msisimko. Mathalani hii riwaya imenikumbusha enzi hizo riwaya za kipelelezi na ukichukulia hakukua na technologies kama simu na computer lakini kila kitu kilikuwa kitavutia.
Dah nimevutiwa na maelezo yako ndugu, Basi nakukaribisha ukisome kitabu cha Hidden Truth nakirusha humu Jamii Forum hivyo kifatilie ndio Kwanza Msimu wa Kwanza sehemu ya 1 (A)
 
SEHEM YA 43 NA........................

bila mafanikio hadi leo hii nilipofanikiwa.Mathew n
ataka tu
nikwambie kwamba mimi na wanangu tulichukuliwa na
kuletwa Marekani na tuliambiwa kwamba umefariki dun
ia
kuna watu wamekuua na kwamba hata sisi tulikuwa
tunatafutwa tuuawe.Nililia sana na nilijilaumu sana
kwa nini
ukachagua kuifanya kazi ile ya upelelezi? Baada ya
kufika
Marekani tulianza maisha mapya na baada ya miaka mi
tatu
nikapata bwana nikaolewa nikijua kwamba umekufa.Kwa
sasa mimi na wanangu tuna uraia wa Marekani na toka
nilipoondoka Tanzania sijawahi kurejea kwani John
aliniambia kwamba sitakiwi kuonekana tena Tanzania
kwani
siku nikitia mguu wangu ndio utakuwa mwisho wangu.K
wa
sasa nina watoto wawili kwa huyo mume wangu mpya na
tunaishi kwa furaha.Nimebadili jina naitwa Martha.
Wanao
wote wazima na wanaendelea vyema na maisha yao ila
maisha yao yamebadilika ghafla baada ya kugundua kw
amba
baba yao yu hai.Jambo hili limewastua sana .Tumewat
afutia
mtaalamu wa saikolojia ambaye anaendelea kuwasaidia
wakubaliane na hiki kilichotokea.Watakapokuwa tayar
i
watakuja kuonana nawe but for now they are not read
y
yet.Mathew sitaki kuchukua muda wako mwingi ila nap
enda
kukwambia kitu kimoja kuwa kazi yako uliyochagua ku
ifanya
ndiyo iliyofanya hadi mambo haya yakatokea.Ndiyo
iliyotutenganisha.Mara nyingi nilikuwa nikikusisiti
za uachane
na kazi hiyo lakini hukutaka kunisikia hadi yalipo
tokea haya
yaliyotokea.Ninachotaka kukushauri ni kwamba umepat
a
mke mzuri sana na nina hakika ameirudisha furaha ya
ko
tena.Peniela ni mwanamke mrembo na dunia nzima
inamuheshimu nakuomba ,muheshimu ,mtunze na
usimuumize kama mimi kwa sababu ya kazi hiyo
uifanyayo.Ukitaka maisha yako yawe na furaha achana
kabisa
na hiyo kazi unayoifanya.Huwezi kuwa na maisha ya k
awaida
yenye furaha na amani ukiwa katika kazi hiyo.Nawata
kia
maisha mema yenye furaha na amani na mpatapo nafasi
mjapo hapa Marekani msiache kuja kututembelea.Ahsan
te
sana Mathew na fungate jema.” Akamaliza Zita na kuk
ata
simu.Mathew na Peniela wakaangaliana
“ Ni mipango ya Mungu mimi na wewe kuwa
pamoja.Yote yaliyotokea yametokea ili mimi na wewe
tukutane.Let’s enjoy life my angel” akasema Mathew
na
kumbusu Peniela wakainuka na kuingia majini kuogele
a.
TAMATI


UKITAKA KUJIPATIA RIWAYA/STORY YA KIJASUSI NA YAKUSISIMUA YA WIMBO WA GAIDI. KUTOKA KWA MTUNZI WAKO MAHILI NA BINGWA WA RIWAYA ZA TAHARUKI HUSSEIN ISSA TUWA .KITABU KINAACHIWA WIKI HII

0655428085 WAHI NA UPATE COPY YAKO MAPEMAA .KAMA UJUAVYO VITABU VYA TUWA HUWA VINAGOMBEWA KAMA NJUGU.
.....
 
Unajua Mobile phones ziliingia sokoni miaka gani? Na hiyo laki mbili ya kumpa mtoto kwa miaka hiyo ya 1940 unaona ipo sawa? Na hiyo form four? Maana Back then kulikua na middle schools tu,. Vipi kuhusu huyo askari wa JWTZ kwa miaka hiyo, maana haikuwepo na badala yake tulikua na King African Riffle (KAR).
Inawezekana unayejaribu kunijibisha na kunibishia hapa ni kitukuu wangu.
Yaani unaleta uhalisia kwenye hadithi ya kutunga
 
week nzima busy na hii story hatimae leo nimeimaliza, hongera kwa mtunzi na mletaji wa story hii jukwaani. Stori tangu sana sema season ya 5 haina mpangilio mzuri kama season zile za mwanzo
 
Back
Top Bottom