Kardinali Pengo: Wanasiasa waacheni Maaskofu wafanye kazi zao, msiwafundishe kazi

Kwa hulka na silika ya mwanadamu huwa ni mtu wa kujisahau sana.
Nakumbuka kwenye msiba wa aliyekuwa askofu mkuu wa kanda ya ziwa baba askofu mayala baba asikofu pengo alitamka maneno yafuatayo.
Nanukuu
Serekali haiwezi kuingilia mambo ya dini,serekali haipaswi kuwafundisha viongozi wa dini namna ya kuubiri neno la yesu,akimanisha injili,injili ni neno la mungu halitakiwi kuongezwa kitu wala kupunguzwa,tena alienda mbali zaidi na akatolea mifano nchi za kipepari na nchi za kikonist.
Nanukuu mapepari japo wana dhambi lkn wanaamini kuwa kuna aliyeko juu yao ambaye ni mungu baba,wakomunisti hawamini dini na kutokuamini kwao hamna dini pia wanaamini kuna mungu,sasa juzi baba askofu amekubali serekali iwafundishe viongozi wa dini namna ya kuhubiri neno la mungu (injili) ndio maana nimesema binaadamu ni watu wa kujisahau sana na ndio maana huwa wanatenda dhambi kila wakati.
Baba askofu aliyasema hayo kwenye msiba wa baba askofu mkuu kanda ya ziwa,tena raia kikweke alikuwepo na viongozi wengine wengi tu,akiwemo na sita membe wasira na wengine wengi tu,baba askofu alitamka hayo akiwa anajibu kauli ya mh:rais kikweke kwenye kampeni za mwaka 2010 baada ya baraza la maskofu tanzania kutoa waraka wa kinabii unahusu uchaguzi mkuu mwaka 2010.
Kwa wali wasikumbuka waraka ule ulileta mgongano mkubwa sana kati ya mzee kingunge na kanisa kayoliki.
Sasa cha kushangaza mtu yule yule amebadilika,amewajeka wenzake,kwa kifupi amelijeuka baraza la maskofu tec kwa kisingizio cha kutoa maoni yake binafsi lkn tufanyeje ndio kiongozi wetu na ni mtu mzima hawezi kuomba msamaha hadharani,kiafika huwa baba haombi msamaha kwa na ss tunamsamehe

Md usiunganishe uzi wangu
 
Kama waumini hawapashwi kuambiwa la kufanya, yeye kwa nini huwa anawahubiria waumini la kufanya katika kutimiza matakwa ya Ukatoliki, si awaache watafakari wenyewe na waamue la kufanya! Mahubiri mbona huwa yanatuambia tufanye nini?
 
Sijui kama ntamwini tena askofu wangu
 

Attachments

  • 1428425968512.jpg
    1428425968512.jpg
    89.5 KB · Views: 447
Pengo anatumika kama bakwatwa inavyotumiwa na Ccm hao hao kuwaminya waislamu
Lakini hakuna chenye mwanzo kikosacho mwisho,Ipo siku atatubu mbele ya wananchi na viongozi wenzie wa dini kwa kukubali kutumika kama toilet pepa.
 
Pengo ni Askofu wa Pinda na siyo Askofu wa Wakatoliki, Mungu anisamehe bure, huyu Askofu nilikuwa namuheshimu sana, lakini kwa mambo ayatamkayo nowdays nimekuwa sina imani naye, ingawa mm ni Muumini wa Jimbo Kuu Katoliki la DSM pale St. Peters!
 
Mkuu unapotosha watu, Mhadhama Polycap Kardinali Pengo, hakusema viongozi wa serikali wawafundishe viongozi wa dini nini chakufanya, tusiwe tunapotosha watu kwa hisia zetu binafsi, alisema kwa maoni yake haoni kama ni sahihi kuwaambia waamini wapige kura gani, waamini waambiwe katiba inasema nini na waachwe waamuwe wao kwa utashi wao
 
Pengo ni Askofu wa Pinda na siyo Askofu wa Wakatoliki, Mungu anisamehe bure, huyu Askofu nilikuwa namuheshimu sana, lakini kwa mambo ayatamkayo nowdays nimekuwa sina imani naye, ingawa mm ni Muumini wa Jimbo Kuu Katoliki la DSM pale St. Peters!

Pengine Pengo aligundua kwamba wanawapotosha Waumini na mwisho wa yote atakuja kuhukumiwa kwa kuvuruga Mamlaka inayotoka kwa Mungu, badala yake angeisaidia. Kwanini wahukumiwe kama walivyofanywa wenzao wa Rwanda? Nitakachomlaumu Kardinali wangu ni Kwanini hakuwa MAKINI tangu mwanzo? Haya yasingemkuta, ya kudhalilishana kama watoto wadogo, hakujua ni watu wa aina gani anafuatananao MKUMBO? La msingi ni kwamba asimame kwenye WITO wake aachane na Siasa. Sasa amekasirisha wenzake waliokuwa wameweka Matumaini ya kwamba timu yao imekuwa kubwa, atajinasuaje? Kibaya zaidi walio kinyume na Pengo na ambao ndio wengi hawajali kama wananchi wameelewa FAIDA na HASARA ya walichodhamiria wawaunge mkono.
 
Ambacho huwa anazungumza Pengo ni sahihi kabisa,ila watu wengi ni vigumu sana kumuelewa
 
Hebu tuambie wale waumini wanaokula tigo, wazinzi, waasherati wezi, askofu pengoo huwa anawaambia wasome injili alafu waamue wenyewe kuenedelea na tabia zao au huwa anawaelekeza cha kufanya kulingana na maandiko ya matakatifu,

hivi huyu askofu pengo tangu mchakato unaanza mpaka unahitimishwa BMK yeye alikuwa wapi ?? alikuwa hija vatican??

hakuona uharamia wowote ule uliofanywa na mafisadi wenzie hadi atoe ushauri wa kijinga kama ule??
mbona hajatoa tamko kashfa ya escow
, katiba ya kifisadi imemuuma saana, huyu jama ana walakini tumemjua mapema
Mkuu unapotosha watu, Mhadhama Polycap Kardinali Pengo, hakusema viongozi wa serikali wawafundishe viongozi wa dini nini chakufanya, tusiwe tunapotosha watu kwa hisia zetu binafsi, alisema kwa maoni yake haoni kama ni sahihi kuwaambia waamini wapige kura gani, waamini waambiwe katiba inasema nini na waachwe waamuwe wao kwa utashi wao
 
Back
Top Bottom