Kardinali Pengo: Wanasiasa waacheni Maaskofu wafanye kazi zao, msiwafundishe kazi

Nasubiri kuona magazeti kesho yataandika nini... Tatizo StarTv inaelekea wataonyesha ibada ya mazishi na si mazishi kwa ujumla. Wapo Kawekamo jijini Mwanza

nadhani redia maria inaweza kutangaza mazishi kwa ujumla na inapatikana online bila matatizo.
 
Atakuwa wa Kwanza kwenda motoni pia... Wa-katoliki hutumia neno la Ki-Latin "Sakililego" - Maana "Kutenda dhambi kubwa na kwa MAKUSUDI" - ndivyo anayofanya BWM
Mkuu, yawezekana kishaungama kwa Mwenyezi Mungu na akawa ni msafi tu.

Mbele za Mungu sote tuko sawa, naona ameshikilia "Misale ya Waumini" akijisomea.
 
Atakuwa wa Kwanza kwenda motoni pia... Wa-katoliki hutumia neno la Ki-Latin "Sakililego" - Maana "Kutenda dhambi kubwa na kwa MAKUSUDI" - ndivyo anayofanya BWM

Hapana mzee, hakuna mwenye kuthibitisha hukumu ila Mwenyezi Mungu pekee.

"Haimlazimu Mtume ila kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnacho kidhihirisha na mnacho kificha."
Al Maidah – 99
 
Duh,

Mkapa kawa wa kwanza kukomnika

Namwona Chenge naye kakomnika sasa hivi

Mkuu Invisible...umefurahisha kny hizo updates sana.....!

Biblia inasema ukitaka kumpokea bwana lazima ujitakase kwanza ndipo uijongee altare yake bwana!

Inawezekana hawa jamaa wamejitakasa mioyo yao kabla ya kuijongea altare kwa kuwa haya ni mambo ya imani kati ya Mungu na muumini mmoja mmoja. Sisi huku nje tunaweza tusione utakaso huo......ingawa nilitegemea matendo yao angalau yaonyeshe kuwa wametakasika!

Anyway point yangu ni kuonyesha kuwa siasa na dini ni vitu viwili tofauti kabisa.....philosophy za kila moja wapo ni tofauti kabisa!
 
Mkuu, yawezekana kishaungama kwa Mwenyezi Mungu na akawa ni msafi tu.

Mbele za Mungu sote tuko sawa, naona ameshikilia "Misale ya Waumini" akijisomea.
Mkuu kuungama then ulichoiba toka kwa maskini unaendelea kutumbua bila kuwarudishia wenyewe huwezi kuwa msafi mbele ya Mwenyezi Mungu.
NDIVYO ANAVYOSEMA KATIKA VITABU VYAKE
 
Raia Mwema la leo, wameandika "Kikwete ana kwa ana na Maaskofu Katoliki" na ndani wamesema wazi kwamba, kutatolewa tamko la kupinga maazimio ya NEC. Bravo Raia Mwema
 
kanisa liangalie upya, lifanye ufisadi nao iwe sababu ya mtu kuto komnika, kwa kuwa nayo ni dhambi
 
muacheni anene kwani katiba haimkatazi mwananchi kuongelea kile ambacho anaona kinafaa lakini tu kisiwe na uvunjaji amani,na vizuri awape live hao wanaohusika kwani zama a kuoneana aibu zimepitwa na wakati tunahitaji nchi yenye viongozi waaadilifu ili tupate kuwa na maendeleo adhimu.
 
Duhh Mkapa hivi anakula chakula cha bwana?? mmmhh anyway watasema kaungama.
Ninyi mnaomshikia bango Ben mkosafi kiasi gani, wewe ni nani mbele za mungu hadi uhesabu makosa ya mwenzako, ukifa leo utakuwa wapi? Safisha kwanza njia zako kabla huja point kidole kwa mwenzako!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu, yawezekana kishaungama kwa Mwenyezi Mungu na akawa ni msafi tu.

Mbele za Mungu sote tuko sawa, naona ameshikilia "Misale ya Waumini" akijisomea.

Nani kakwambia kuwa kuungama kwa Mungu inatosha? Wewe kama umemkosea jirani yako, biblia iko clear kwamba uende ukamwombe msamaha. Na papo hapo inatufindisha kuwa tukiombwa msamaha tusamehe.
Hivyo Mkapa anatakiwa kuomba taifa msamaha kwa 'wizi' wake.
 
Nani kakwambia kuwa kuungama kwa Mungu inatosha? Wewe kama umemkosea jirani yako, biblia iko clear kwamba uende ukamwombe msamaha. Na papo hapo inatufindisha kuwa tukiombwa msamaha tusamehe.
Hivyo Mkapa anatakiwa kuomba taifa msamaha kwa 'wizi' wake.

Mtoto kua utaona dunia ilivyo.
 
Halisi, Invisible.....vipi mbona hatujapata updates tena hapa? shughuli ilishaisha? je, JK or BWM kaongea....kasema nini?
 
La maana saana, Pengo alionyesha wazi kutofurahia wale wanajidai kuchukia ufisadi lakini mafichoni wanawafanya marafiki zao.

Hata hivyo mazishi haya nimeona kama ni kitubio cha CCM. yaweza kuwa ni kwa sababu ya uchaguzi ujao na yamekuwa ni mashindano ya wanasiasa kujionyesha kwa Katoliki. Hata hilo komunio la Chenge na Mkapa yaweza kuwa ni kuonekana wazi ili tuamini wamejirudi. Mambo yanaweza kuwa kinyume kama NEC ya CCM ilivyo onyesha.

Hebu tuwaombe Katolic na madhehebu mengine wasimamie jambo hili kidete.
 
Na Betty Kangonga
Tanzania Daima


ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amewashukia makamanda wanaopigana vita dhidi ya ufisadi kwa kuwataka wawe na dhamira ya kweli katika kukabiliana na ufisadi nchini.

Kardinali Pengo, alisema bila dhamira ya kweli, vita hiyo haiwezi kufanikiwa kwani wanaopiga kelele bila kusukumwa na dhamira ya kweli, wataonekana kama wana wivu kwa kukosa fursa ya kuwa mafisadi.

Alitoa kauli hiyo jana wakati wa ibada ya kumuaga Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Anthony Mayala (69), aliyefariki dunia Agosti 19 na kuzikwa jana katika Kanisa la Mtakatifu Epifania, Parokia ya Bugando, jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana jana jijini Dar es Salaam, Pengo alisema Watanzania wengi wanaokemea ufisadi, wanaongeza hasira kwa jamii, kwani uovu huo bado unaendelea kufanywa na mafisadi kwa vile wapiganaji wenyewe hawana dhamira ya kweli.

"Wote tunalalamika na kulaani matendo ya ufisadi, kama kweli tungekuwa tunalaani kutoka ndani ya mioyo yetu, basi vita hivi vingepungua ama kuisha kabisa nchini kwetu.

"Kupigia kelele ufisadi, bila dhamira ya kweli kunaonyesha hisia tu na ni bora kuacha kulizungumzia suala hilo kwani linaongeza hasira kwa wananchi na hata kusababisha amani iliyokuwepo nchini kutoweka," alisema.

Pengo alisema, makamanda wa ufisadi, lazima wajiulize kwanza wao binafsi wamechangia kwa kiasi gani katika kuwaibia wananchi, ndipo waanze kupiga vita ufisadi kwa kuwa hawana makosa.

"Hakuna aliye mkamilifu, wengi wetu tumekuwa tukiwapinga mafisadi, huku sisi tukijiona wema wakati kwa upande mwingine bado wanafanya ufisadi na kuwaibia watu, ndiyo maana vita hii kamwe haiwezi kuisha,'' alifafanua Kardinali Pengo.

Bila kutaja majina ya watu, Kardinali Pengo alisema baadhi ya wapiganaji wa ufisadi, wanafanya hivyo kwa kuwa wamekosa nafasi ya kuwa mafisadi, hivyo wanawaonea wivu wenye nafasi ya kufanya ufisadi.

Aliwageukia maaskofu wenzake kwa kuwataka wawe imara na wasiwe tayari kuyumbishwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, kwani dini na siasa kamwe haviwezi kwenda pamoja.

"Mambo yanayoendelea kutokea katika nchi yetu hatuelewi yanatupeleka wapi, kwani tunashangazwa na chama kuingilia masuala ya maaskofu ambayo ni mema, kwani yana lengo la kusaidia jamii iwe na viongozi wenye maadili.

"Leo unafikia hatua ya kumwambia askofu haruhusiwi kufanya jambo lolote mpaka akutane na chama na kupewa ruhusa ya kujua namna ya kuandika waraka huo, huko ni kutaka kuingilia mamlaka ya Kimungu na kamwe haitawezekana.

"Waacheni maaskofu wafanye kazi zao na wasifundishwe kazi, kwa maana kuandika waraka huo ni mamlaka kutoka kwa Mungu na si kwa uwezo wao, vyama visilazimishe kuwa lazima vitoe ushauri, huo ni upuuzi na inaonyesha kuchanganyikiwa," alieleza Kardinali Pengo.

Ingawa Kardinali Pengo hakumtaja mtu, lakini kwa kauli hii ni dhahiri kuwa alimlenga mkongwe wa siasa nchini, Mzee Kingunge Ngombale- Mwiru ambaye siku za hivi karibuni, alijitokeza hadharani kuupinga waraka wa Kanisa Katoliki, kwamba unaweza kuhatarisha amani na utulivu nchini.
 
Back
Top Bottom