Pengo: Nchi imeoza!

Dini inaongoza na kugusa roho ya binadamu,wakati siasa inagusa mwili wa binadamu kwa hiyo kwa ujumlisho wa vitu hivi viwili tunapata binadamu kamili. Ni wapi ilipo siasa dini haiingii,na wapi ilipo dini siasa haiingii wakati binadamu ni yuleyule?

Mfumo unaotawala maisha ya binadamu mara zote ni intergration ya mifumo miwili au zaidi ili kupata mfumo mmoja kamili, ni kama ilivyo kuishi Kisoshalisti pekee kusivyowezekana bila kuchanganya na U-Capitalist and vice versa is true, dini na siasa ni vivyo hivyo.

Dini zinajenga shule ,vyuo na mahospitali kazi ambayo kwa akina akili finyu inatakiwa iwe ya wanasiasa kwa nini hili halilalamikiwi? Ni siasa au katiba ya nchi gani duniani inaruhusu wezi, walaghai, waongo, wazinifu n.k? Je, ni dini gani inaruhusu hayo? Utofauti wa dini na siasa uko wapi hapa?

Kwenye mambo ya msingi yanayogusa mustakabali wa maisha ya kila Mwananchi tuache ushabiki wa vitu visivyo na msingi.
 
Kweli kabisa wewe ni DOGMA!Kati ya hao walioandika huo waraka na huyo Mwanya(PENGO) ni nani kila kukicha anausemea huo waraka?

Nimeamini unaweza ukamaliza madarasa hata mwalimu kufa darasani bila ya kuelimika!Maskini wee,yaani unatia aibu kutetea utumbo!Huko katoliki hakuna demokrasia leo anayetetea hiyo demokrasia atokee katoliki!Maajabu,mbona askofu Malasusa tumemchagua wenyewe hapa bongo?Na ndio maana utagundua viongozi wote wa kidini wanaoteuliwa au kuchaguliwa nje ya nchi yao ni watumwa wa mabeberu hao wa nje kwa ajili ya utashi wao binafsi.Hata ufanye vipi hutaweza kujitakasa na maji ya ******.

Umetaka ndio hivyo hukutaka ndio hivyo,huko hakuna kitu toka njoo huku lutheran au nenda anglican kwani demokrasia inapatikana na si kuletewa mamluki toka roma.
 

Leo nimepata somo kubwa.
 

Mkuu! hapana mi napenda nikuite Mheshimiwa!

Yaahn nimezipenda hizo hoja zako " they are relevant arguments i dare to say that!.Kama ingekuwa wote wanatoa points kama hizi na Materials kama haya nadhani nchi yetu ingepiga Maendeleo makubwa sana!

Keep keeping on Mheshimiwa!
 
Mbona wapoapa wanashikiria biblia au quran? si wanasema Mungu nisaidie? sasa huyo kiongozi wa kiroho akiwakemea kwa kutotimiza haya waliyaoapa kuyatekeleza ana kosa gani?
Tuwe wachambuzi -comeup na kusema kipengele so and so cha waraka au mwongozo ni kibaya kwa sababu one, two nk.
 
Nakuunga mguu kwani Pengo kashindwa kuendesha ibada kama ulivyosema,kwa taarifa nyepesi nilizonazo sasa anajiandaa kugombea ubunge mwaka 2010,mambo hayo!

Hivi nyie mnafikiri Pengo siyo raia wa nchi hii??? Pengo na wanadini wote wana haki sawa ya kutoa maoni yao kama raia wengine au NGOs provided that hawavunji sheria. Dini zote zinazo-operate TZ zimesajiliwa kwa mujibu wa sheria za JMT. Sasa mtueleze Pengo kama raia au mwana dini amekiuka au amevunja kipengere kipi cha katiba ndiyo tuwaelewe.

Kila siku tunalia humu ndani na mafisadi, sasa leo Pengo akisema inakuwa nongwa. Sasa wenzetu mnataka nani aseme?? Wewe na mimi hakuna anayetusikia kazi yetu imebaki kuandika humu JF na hakuna tunayembabaisha so far zaidi ya kuongeza awareness miongoni mwetu (vita vya taratibu), akina Sitta na group yake (mnaowasifia humu) tayari NEC ya CCM ishawafunga midomo. On the other hand TZ hakuna hata NGOs za kupigania haki za wananchi. NGOs zimekuwa miradi ya watu.

Sasa, kama serikali haiendeshwi vizuri, personally sioni kwa nini Pengo au wanadini wengine wasiseme kitu. In fact huwezi kutenganisha dini na siasa. Unafikiri kwa nini Obama alipopata madaraka alikwenda Rome??
 
Hujaelewa mada. Pengo hajazungumzia kutokuwapo kwa demokrasia, anazungumzia ufisadi.
Kama utaratibu wa kuteuliwa na roma unawafanya wateuliwa wa TZ wawe waroma lakini bado wakakumbuka kutusaidia kukemea ufisadi, basi ni jambo jema kuliko hao tunaowachagua sisi wenyewe wakatugeuka na kuwa mafisadi. Mbona mara nyingi tunaomba marais wa nchi zenye nguvu watusaidie kutatua matatizo yetu? hata huu ufisadi, uzuiaji wa watu kujiandikisha kupiga kura nk tunaomba viongozi wa nchi nyingine watusaidie - kwani sisi tuliwachagua?

Jadili mada na si dhana yako, vinginevyo anzisha thread yako ya je kuna demokrasia kanisa katoliki?
 
Napata ushawishi kidogo wewe umeelimika na si kwenda shule tuu kama wenzio waliotangulia.Wewe tunaweza tukajadili mambo na kupata muafaka si kukurupuka kama hao.....
 
Unajua Malasusa alisema nini kuhusu waraka wa katoliki?
 
pengo umenena nashangaa wapo wanaokupinga lakini hawajui hatuwezi tukawa kwenye taifa la kibabaishaji na wizi nw tumebadirika lazima wafuliee
 
Pengo ana uhuru kama Mtanzania kuongelea kero anazoziona lakini siafiki kila dini kutoa waraka/mwongozo hili litatugawa.
 

Ha ha ha..kwanza inabidi ukajifunze maana ya neon DOGMA ili usizidi kutuletea mashudu humu jamvini.

Pili, kama nilivyokwambia walio keti kitako na kuandika huo waraka wa wakatoliki ni wataalamu waliobobea ktk fani mbalimbali, yaonekana hili ni geni kwako na utaendelea kuelewa taratibu mpaka ujumbe utakapoifikia medulla oblongata yako.

Tatu, mpangilio wa hoja zako wa ovyoovyo na kuendelea na ad hominem ni kuonesha kuwa wewe ni kielelezo cha mtu asiefuta ujinga, mpumbavu, au partly, both. Demokrasia ya kanisa kwa vyovyote vile iwe mbovu au nzuri, haiwazuii wana kanisa kuzungumzia mambo yanayoigusa na kuihusu jamii inayowazunguka. Unajaribu kuleta habari za Malasusa etc nadhani unashindwa kuelewa kuwa systems za makanisa zinapishania wapi. Sipendi kulijadili hili maana kwa liko very remotely related na mada iliopo humu ukumbini.
 
Pengo ana uhuru kama Mtanzania kuongelea kero anazoziona lakini siafiki kila dini kutoa waraka/mwongozo hili litatugawa.

Pengo ni Mteule wa nchi ya Vatican (ambayo ni sehemu ya Italy). Ni raia wa Tanzania na ana uchungu na nchi yake (kama mtanzania yeyote). Lakini vile vile inawezekana anatekeleza sera za waliompa uaskofu (Vatican). Hivi inawezekana kweli huo waraka/mwongozo haukupata mibaraka ya ubalozi wao/au hata mkuu wa Vatican (Pope)? Hapo ndipo kunapokuwa na utata.
 
Huyu Pengo si ndio alienda kumbariki Jambazi Fisadi Mkuu Lowassa nyumbani kwake na kuwaponda wote wanaomsulubu, leo anajifanya ametakasika. Huyu ni mpambe wa Chama Cha Majambazi tu.
 


Mimi naona alilosema Pengo si baya kihivyo, inachotakiwa kufanya serikali ni kutazama ukweli ya yaliyosemwa na kuyafanyia kazi kubwa ya marekebisho mapungufu yote. Kwa kufanya hivyo watakuwa wameiteka dhana hiyo na washindi ni wao, lakini wakidharau wakaendekeza malumbano na sera za maneno matupu anguko lao linakuja,'' mene mene tekel peres ''
 
Hamna kitu kama separation of politics and church or religious matters bali kuna separation of powers dhana ambayo kinadharia ipo lakini kimatendo haipo. Kwa kuwadokezea tu siasa na dini ni kama chanda na kidole vinakwenda sambamba no one can separete them.
 
Pengo inabidi aanze kupambana na mshikaji wake Jambazi Fisadi Edward Lowassa ndio tutajua kama kweli ana nia ya dhati katika kupambana na ufisadi.
 

Chukua tamo tafadhali na zingine baadaye . Hivyo hiyo hata kama hawataki wanajianya kujenga hoja .Baho baho
 
Huyu Pengo si ndio alienda kumbariki Jambazi Fisadi Mkuu Lowassa nyumbani kwake na kuwaponda wote wanaomsulubu, leo anajifanya ametakasika. Huyu ni mpambe wa Chama Cha Majambazi tu.
Mkuu ndio maana tunasema awataje Mafisadi kwa majina yao huo utakuwa waraka mzuri zaidi kwa wananchi.
Kifupi kinachotakiwa kanisa kufanya ni kuorodhesha majina yote ya Mafisadi na kuwaomba wananchi wasiwape kura.

Nitarudia kusema waraka ulikuwa na malengo mazuri isipokuwa uwakilishi wake ndio umejaa utata. Kwa nini kanisa na hao waislaam wanashindwa kuorodhesha majina ya mafisadi?.. Dr. Slaa kawataja wote na ajabu baadhi ya viongozi wa dini hawakukubaliana naye leo iwe hao hao viongozi waliowabariki Mafisadi watuambie nani kiongozi bora?..Hivi kweli kumtambua fisadi kunahitaji msomi aliyebobea ktk masomo ya sayansi au ulokole!..

NCHI imeoza kweli, wala Pinda hakukosea ila kuchagua viongozi sio tiba ya Ufisadi hata kidogo ikwa tutaweza kuutazama vizuri mfumo wa uchaguzi nchini. Wagombea wote husimamishwa na vyama wala sii wananchi, hivyo tunachagua kati ya watu wawili tuliopewa na sii kweli kati ya hao wawili, watatu au wanne ni mmoja tu ndiye msafi..Mara zote mafisadi ni viongozi walioteuliwa na serikali iliyopo madarakani..kina Lowassa, Rostam na kundi lao wote hawa waliteuliwa na serikali kushika nafasi ambazo walitufisadi, leo hii hawapo ktk nafasi hizo za Uongozi na wamesimamishwa ktk nyendo zao za Ufisadi, lakini bado ni Wabunge, na ajabu wanapewa support kubwa na vyombo vya dini ili wapate kurudi madarakani..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…