Elections 2010 Pengo: Msiwachague wanaogawa khanga na fulana

Na Peter Mwenda

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo amewataka wakristo kufuata dhamira ya Mungu ya kuchagua viongozi ambao hawawarubuni kwa khanga, bia na fulana.

Akihutubia waumini katika ibada ya kuombea amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi mkuu iliyofanyika katika Kijiji cha Hija, Parokia ya Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema wakristo wakatoliki wajue kwamba kura zao zina thamani kubwa kwa jamii na mbele ya Mungu.

"Kama mngejua thamani ya kura yako kwa jamii na mbele ya Mungu huwezi kupokea zawadi za khanga na bia kwa ajili ya kumpigia mtu asiyefaa kupewa kazi ya kuongoza," alisema Kadinali Pengo.

Alisema Mwenyezi Mungu anafanya kazi kupitia dhamira ya kila mwanadamu, hategemei ushabiki wa vyama wala kumchagua kiongozi asiye na utashi ambaye anatoa rushwa ili apate uongozi.

"Si kuambiwa na mwenyekiti wa jumuiya, kasekista (Mwalimu wa dini), kadinali au padre kuwa mchague fulani, hakuna atakayesimama kwa dhamira yako, anayefaa ni yule anayejiepusha na matendo ya rushwa," alisema Kadinali.

Alisema kumetokea minong'ono hivi karibuni kuwa Kanisa Katoliki limeteua viongozi wa kupigiwa kura katika ngazi ya juu. "Huo si msimamo wa Kanisa Katoloki."

Alisema akiwa kiongozi wa kanisa hilo anaweka bayana msimamo wa Wakatoliki kuwa hawafungamani na itikadi za kichama, kisiasa au kabila.

"Kanisa Katoliki lingefanya hivyo likawa na watu wake au kusema fulani ni chaguo la Mungu ni balaa linaloweza kuleta machafuko na uvunjifu wa amani," alisema Kardinali Pengo.

Alisema uchaguzi wa kibinadamu ni chanzo cha mfarakano lakini wakristo ambao wana utashi wa Mungu wasimchague kiongozi wanayemjua kuwa ni mwizi na mla rushwa ambaye anatumia kushawishi ili achaguliwe.

"Tuchukue na kuamini hilo kuwa ni ukweli wa Kanisa Katoliki halina mtu kuwa huyu awe rais, mbunge au diwani. Haliwezi likasimama likasema fulani awe hivi," alisema Kadinali Pengo.

Alisema Wakristo nchini kote wapige kura kwa dhamira ya kumuogopa Mungu kuwa siku ya mwisho watasimama mbele yake na kusema madhambi yao.

Katika ibada hiyo ambayo Kadinali Pengo alisaidiwa na mapadri 15 kutoka parokia mbalimbali za Jimbo Kuu la Dar es Salaam alisema kutafuta madaraka kwa kutumia nguvu au ushawishi ili kuhalalisha madaraka si njia ya kuleta amani bali kuashiria machafuko ambayo kanisa inapinga vikali.

Mkurugenzi wa Haki na Amani wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Alister Makubi aliwaasa waumini wa kanisa hilo nchini wasichoke kusali kuombea amani wakati wote wa uchaguzi.

Nimependa haya maneno kwa kuwa yana maana kubwa sana ndani yake maana siku ya mwisho ukiwa umesimama mbele ya haki utaulizwa yote uliyoyafanya
 
Sasa Huyu Ndio ASKOFU Maneno yake yamekaa kibusara zaidi!! huwezi ukamfananisha na KAKOBE ambaye ameweka kisasi mbele sababu TANESCO!

Njiwa umepigwa falsafa baba.

Askofu hapo anamaanisha Kikwete na genge lake ni watu hatari, wezi, walafi, wanafiki, waongo wasichaguliwe tena.
 
Nimeutafakari ujumbe wa pengo,kwa bahati mbaya au nzuri nina tofautiana naye sana. Natofautiana naye si kwa maudhui ya kile alichokisema bali kwa dhamira ya yale aliyoyasema. Sio pengo tu, viongozi wote wa dini kwa ujumla wamekuwa wanatuchanganya. Mfano ni viongozi hao wa dini wanajua wazi kuwa katiba yetu ina utata na hakuna haki. Ni wangapi wamewahi kusema kuhusu hilo. Viongozi wetu wa dini wanajua kuwa mfumo wa uchaguzi una matatizo hasa katika haki[level field] ni wangapi wamesema kuhusu hilo. Unapowaambia waumini wachague kiongozi safi bila kuchukua khanga huku ukijua kuwa kuna wizi wa kura na hukemei, hii ni nini kama si woga au unafiki.
Viongozi wa dini wanajua wazi kuwa haki haitendeki, wakulima wanaponyan'ganywa ardhi yao na kigogo mmoja tu, wangapi wameongelea hilo!
Viongozi wa dini wanajua kuwa kuna wizi wa kodi za wananchi na kikundi kidogo cha watu, mbona hawajakemea hadharani licha ya kuongea kwa mafumbo. Viongozi hao hao wanaona jinsi akina mama na watoto wanavyoteseka huko vijijini ili hali kodi zao zina nunua mashangingi, mbona wamekaa kimya. Ni hao hao kwa kutumia dini zao wanaingiza magari bila kulipia kodi na kuyauza, je ujasiri wa kuwakemea wagawa khanga wanaupata wapi.
Kiongozi Askofu mmoja aliwahi kumwalika Rais mmoja mstaafu na kuwaambia wananchi rais huyo ni msafi amefanya mengi juu ya uchumi. Kiongozi huyo anazijua tuhuma za wizi ambazo zipo wazi dhidi ya kiongozi huyo, lakini kwa kutaka milioni 5 za mchango akamsafisha mbele ya waumini wake. Sasa kiongozi huyu ataniambia niache kuchukua khanga kwa kumumini kwa lipi. Ninakemea vikali tabia za kuchukua khanga na kofia au 20,000 kuuza kura, lakini dhamira yangu lazima iambatane na matendo. Hawa viongozi hawana hilo.
Taifa lilipogubikwa na kashfa za wizi wa hali ya juu, viongozi wa dini zote walikaa kimya na kuwaachia akina ''Kubenea'', sasa leo wanatambua umuhimu wa viongozi wasio wala rushwa, swali ni je walifanya nini kutetea haki za mamilioni ya watanzania yaliyotafunwa kwa kupitia mikataba feki kama richmond,? au labda wizi wa kalamu ni dhambi ndogo kuliko kuvunja banda la kuku!
Nina jumuisha kwa kusema, alichosema Kadinali Pengo ni sahihi kabisa, lakini yeye na viongozi wa dini zote na madhehebu yote hawajasimamaia yale wanayoyajua, ni vipi leo watufundishe kile wasichoweza kukisimamia.? Ningewaomba wakae kimya watuachie mapambano ya khanga, kofia na bahasha za 20,000 sisi wapiga mayowe kwasababu tunaamini mayowe yetu yatasikika kwa mungu na wadhalimu wanaotutia umasikini siku zao zinakarabia, inaweza isiwe leo au kesho lakini tunaona pambazuko la matumaini mema.
Nitamsiiliza Dr Slaa kwasababu yeye amethubutu kusimama si mara moja au mbili kukemea maovu kwa dhamira yake,kwahiyo akiniambia anaichukia rushwa ninamwelewa zaidi kuliko yule anayenishawishi niichukie rushwa huku akiwabeba wala rushwa kwa namna flani ilimradi tu mambo yake au yao yaende vizuri.

Naomba nikupongeze kwa maelezo yako - ambayo kwa upande wangu naona ni KWELI KABISA. Hata hivyo naomba usiwalaumu sana viongozi wa Dini kwani sio wote WANAJUA KWA UNDANI VITU VINAVYOENDELEA - MIKATABA FEKI INAYOFANYIKA; RUSHWA ZINAZOTOLEWA NYINGINE KWA SIRI ETC. NA KAMA KAWAIDA WAKIJUA NI LAZIMA WAWE NA USHAHIDI PIA; NA PIA SIO WOTE WANA UJASIRI WA KUONGEA AU WALIO NA MAHALI SAHIHI PA KUONGELEA - KUMBUKA DR. SLAA ALIONGELEA BUNGENI KWA VILE ALIKUWA NA CHANCE YA KUFANYA HIVYO . NAKUUNGA MKONO NA NAMPONGEZA DR. SLAA KWA UJASIRI WAKE WA KUWEKA MAMBO WAZI NA KAMA MUNGU ANGEMPA NAFASI YA KUWA RAIS - NAAMINI TAIFA LETU LINGEBADILIKA NA UMASKINI UKATUTOKA - MUNGU MBARIKI DR. SLAA NA KUMLINDA - AMEN!!
 
Sasa Huyu Ndio ASKOFU Maneno yake yamekaa kibusara zaidi!! huwezi ukamfananisha na KAKOBE ambaye ameweka kisasi mbele sababu TANESCO!
njiwa bwana mbona kakobe kafuta ibada tarehe 31 watu wakapige kura?nae ni askofu hakuna mtu ambaye ni PERFECT.HUMAN BY NATURE NI SELFISH alikuwa anavutia kwake.
 
ujumbe huu umewafikia watu wangapi? au ndo waliokuwa ibadani na wana jamii forum tu ambao wengi wenu mnauwezo wa kulipia huduma hii ya internet na kupata taarifa kama hizi?mh kazi ipo kwani najua wapewa kanga na tshirt walikuwa wachache ibadani hapo anapoongoza askofu huyu,pili na kama ni magazeti wapewa tshit na khanga wachache wananunua magazeti kujua ujumbe uliotolewa na askofu.

Na Peter Mwenda

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo amewataka wakristo kufuata dhamira ya Mungu ya kuchagua viongozi ambao hawawarubuni kwa khanga, bia na fulana.

Akihutubia waumini katika ibada ya kuombea amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi mkuu iliyofanyika katika Kijiji cha Hija, Parokia ya Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema wakristo wakatoliki wajue kwamba kura zao zina thamani kubwa kwa jamii na mbele ya Mungu.

"Kama mngejua thamani ya kura yako kwa jamii na mbele ya Mungu huwezi kupokea zawadi za khanga na bia kwa ajili ya kumpigia mtu asiyefaa kupewa kazi ya kuongoza," alisema Kadinali Pengo.

Alisema Mwenyezi Mungu anafanya kazi kupitia dhamira ya kila mwanadamu, hategemei ushabiki wa vyama wala kumchagua kiongozi asiye na utashi ambaye anatoa rushwa ili apate uongozi.

"Si kuambiwa na mwenyekiti wa jumuiya, kasekista (Mwalimu wa dini), kadinali au padre kuwa mchague fulani, hakuna atakayesimama kwa dhamira yako, anayefaa ni yule anayejiepusha na matendo ya rushwa," alisema Kadinali.

Alisema kumetokea minong'ono hivi karibuni kuwa Kanisa Katoliki limeteua viongozi wa kupigiwa kura katika ngazi ya juu. "Huo si msimamo wa Kanisa Katoloki."

Alisema akiwa kiongozi wa kanisa hilo anaweka bayana msimamo wa Wakatoliki kuwa hawafungamani na itikadi za kichama, kisiasa au kabila.

"Kanisa Katoliki lingefanya hivyo likawa na watu wake au kusema fulani ni chaguo la Mungu ni balaa linaloweza kuleta machafuko na uvunjifu wa amani," alisema Kardinali Pengo.

Alisema uchaguzi wa kibinadamu ni chanzo cha mfarakano lakini wakristo ambao wana utashi wa Mungu wasimchague kiongozi wanayemjua kuwa ni mwizi na mla rushwa ambaye anatumia kushawishi ili achaguliwe.

"Tuchukue na kuamini hilo kuwa ni ukweli wa Kanisa Katoliki halina mtu kuwa huyu awe rais, mbunge au diwani. Haliwezi likasimama likasema fulani awe hivi," alisema Kadinali Pengo.

Alisema Wakristo nchini kote wapige kura kwa dhamira ya kumuogopa Mungu kuwa siku ya mwisho watasimama mbele yake na kusema madhambi yao.

Katika ibada hiyo ambayo Kadinali Pengo alisaidiwa na mapadri 15 kutoka parokia mbalimbali za Jimbo Kuu la Dar es Salaam alisema kutafuta madaraka kwa kutumia nguvu au ushawishi ili kuhalalisha madaraka si njia ya kuleta amani bali kuashiria machafuko ambayo kanisa inapinga vikali.

Mkurugenzi wa Haki na Amani wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Alister Makubi aliwaasa waumini wa kanisa hilo nchini wasichoke kusali kuombea amani wakati wote wa uchaguzi.
 
Amefanya vizuri kwakumbusha wananchi nadhani wengi sasa wamepata ufahamu ni swala la wakati tuu
 
ujumbe huu umewafikia watu wangapi? au ndo waliokuwa ibadani na wana jamii forum tu ambao wengi wenu mnauwezo wa kulipia huduma hii ya internet na kupata taarifa kama hizi?mh kazi ipo kwani najua wapewa kanga na tshirt walikuwa wachache ibadani hapo anapoongoza askofu huyu,pili na kama ni magazeti wapewa tshit na khanga wachache wananunua magazeti kujua ujumbe uliotolewa na askofu.
We dada angu Joyce unamjua Pengo au unamsikia kuna prominent figures hata akisemea chumbani na mwandishi mmoja tu habari zinashambaa kama moto wa nyika sembuse yeye kasemea hadharani.
 
"Si kuambiwa na mwenyekiti wa jumuiya, kasekista (Mwalimu wa dini), kadinali au padre kuwa mchague fulani, hakuna atakayesimama kwa dhamira yako, anayefaa ni yule anayejiepusha na matendo ya rushwa," alisema Kadinali.

Ya kweli haya! :confused2:
 
alimaaanisha msimchague mtu kwa sababu ya vitu anavyokupa, inaweza kuwa ni pesa pia na hata chadema inaweza kutoa

ila Chadema haijawahi kutoa, hivyo kwa kua CCM imeashathibitika kua inatoa rushwa ya hela, Kanga na Kofia basi, inyimwe kura
 
Wewe mpiga kuar, Pengo amekupa nafasi ya kutumia utashi wako na uelewa ulijaaliwa na Mungu kutambua jema na baya.

Alichofanya ni kukupa dondoo tu, achana na kofia, fulana na khanga. CHagua mtu sahihi... halafu piga kura. Humu sisi kwa habari tunazojua wanotoa kofia, fulana nk, ni wale wale mashati ya kijani. Kubali usikubali
 
Hapa hajatajwa mtu, kwanini watu wanajihisi?...Je ni vibaya mtu akitoa darasa hilo kwa jamii?...Tusiogope vivuli vyetu!...Naona wale waliotumwa hapa JF kwa kazi maalum tayari wamekuja juu, maana wanaona wazi nafasi ya BWANA wao inahojiwa!
The truth is...TUNAHITAJI MABADILIKO ili kutoa nafasi kwa mawazo mbadala!!
 
Ushauri wa busara sana wenye akili timamu wataelewa mazuzu watalalama daima
 
Back
Top Bottom