Pengo: Msiwachague wanaogawa khanga na fulana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pengo: Msiwachague wanaogawa khanga na fulana

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Sep 27, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Na Peter Mwenda

  ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo amewataka wakristo kufuata dhamira ya Mungu ya kuchagua viongozi ambao hawawarubuni kwa khanga, bia na fulana.

  Akihutubia waumini katika ibada ya kuombea amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi mkuu iliyofanyika katika Kijiji cha Hija, Parokia ya Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema wakristo wakatoliki wajue kwamba kura zao zina thamani kubwa kwa jamii na mbele ya Mungu.

  "Kama mngejua thamani ya kura yako kwa jamii na mbele ya Mungu huwezi kupokea zawadi za khanga na bia kwa ajili ya kumpigia mtu asiyefaa kupewa kazi ya kuongoza," alisema Kadinali Pengo.

  Alisema Mwenyezi Mungu anafanya kazi kupitia dhamira ya kila mwanadamu, hategemei ushabiki wa vyama wala kumchagua kiongozi asiye na utashi ambaye anatoa rushwa ili apate uongozi.

  "Si kuambiwa na mwenyekiti wa jumuiya, kasekista (Mwalimu wa dini), kadinali au padre kuwa mchague fulani, hakuna atakayesimama kwa dhamira yako, anayefaa ni yule anayejiepusha na matendo ya rushwa," alisema Kadinali.

  Alisema kumetokea minong'ono hivi karibuni kuwa Kanisa Katoliki limeteua viongozi wa kupigiwa kura katika ngazi ya juu. "Huo si msimamo wa Kanisa Katoloki."

  Alisema akiwa kiongozi wa kanisa hilo anaweka bayana msimamo wa Wakatoliki kuwa hawafungamani na itikadi za kichama, kisiasa au kabila.

  "Kanisa Katoliki lingefanya hivyo likawa na watu wake au kusema fulani ni chaguo la Mungu ni balaa linaloweza kuleta machafuko na uvunjifu wa amani," alisema Kardinali Pengo.

  Alisema uchaguzi wa kibinadamu ni chanzo cha mfarakano lakini wakristo ambao wana utashi wa Mungu wasimchague kiongozi wanayemjua kuwa ni mwizi na mla rushwa ambaye anatumia kushawishi ili achaguliwe.

  "Tuchukue na kuamini hilo kuwa ni ukweli wa Kanisa Katoliki halina mtu kuwa huyu awe rais, mbunge au diwani. Haliwezi likasimama likasema fulani awe hivi," alisema Kadinali Pengo.

  Alisema Wakristo nchini kote wapige kura kwa dhamira ya kumuogopa Mungu kuwa siku ya mwisho watasimama mbele yake na kusema madhambi yao.

  Katika ibada hiyo ambayo Kadinali Pengo alisaidiwa na mapadri 15 kutoka parokia mbalimbali za Jimbo Kuu la Dar es Salaam alisema kutafuta madaraka kwa kutumia nguvu au ushawishi ili kuhalalisha madaraka si njia ya kuleta amani bali kuashiria machafuko ambayo kanisa inapinga vikali.

  Mkurugenzi wa Haki na Amani wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Alister Makubi aliwaasa waumini wa kanisa hilo nchini wasichoke kusali kuombea amani wakati wote wa uchaguzi.
   
 2. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,807
  Trophy Points: 280
  Sasa Huyu Ndio ASKOFU Maneno yake yamekaa kibusara zaidi!! huwezi ukamfananisha na KAKOBE ambaye ameweka kisasi mbele sababu TANESCO!
   
 3. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Njiwa, CCM wamekupa nini hata utake kuwachagua tena? Hivi Kikwete anaposimama jukwaani kusema Lowasa ni msafi alisingiziwa, Mramba ana kesi ndogo tu atashinda unaona kweli ni kiongozi wa kuendelea kumchagua huyu? Mtu anayeteua wakuu wa Wilaya wakiwa na kesi za rushwa mahakamani, mtu anayechaguliwa watendaji wa serikali na Rostam Azizi mwizi na jangili wa uchumi wa nchi yetu, bado unaona anafaa kweli huyu? Kumbuka hata kama wewe ni mwana CCM taabu kwa ndugu zako na kwako mwenyewe haichagui uko chama gani vinginevyo na wewe ni mnufaika wa huu wizi wa mali za nchi yetu na umeamua kuwasaliti ndugu zako wanaotaabika katika lindi la umaskini katika nchi iliyojaa vyanzo vya mapato lukuki.
   
 4. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,807
  Trophy Points: 280
  chadema iko sawa .. ila mgombea wao si mkubali...! chadema namkubali Mgombea mmoja Tu!... MNYIKA! BASI!?
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Kwani chama gani kinagawa khanga pilua na pombe kila baada ya miaka mitano?............sio chama hiki cha mafisadi kweli?.....hakika ni ccm inasemwa hapa.....lakini pengo kuna wazee wengi tu kule vijijini hawana uwezo wa kuvaa khanga na fulana isipokuwa wanafaidi keki ya taifa kila baada ya miaka mitano.......bora ungewashauri wachukue hizo zawadi za ccm ila wasiipigie kura kwani watatembea uchi wazee wetu
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwani TANESKO wanaingilia vipi?somo ni moja tu usichagua chama kinachogawa khanga na fulana na hiyo ni direct kuwa usimchague Kikwete na CCM..Simple!!!
   
 7. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  alimaaanisha msimchague mtu kwa sababu ya vitu anavyokupa, inaweza kuwa ni pesa pia na hata chadema inaweza kutoa
   
 9. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Msianza kutugawa hapa katika jukwaa hili kwa hoja za huyu ndiye askofu wa kweli kuliko yule. Unachotakiwa ni kupokea ujumbe na kuuelewa!!! Ukiwa na hoja ilete jamvini lakini utaratibu wa kupokea ujumbe ni kuwa CCM basi...... wasipate kura!!!! UJUMBE UMEFIKA toka kwa Askofu Pengo na Kakobe.
   
 10. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,807
  Trophy Points: 280
  unajuwa kwanini huwa si replay post zako... "hazitoi nafasi kwa mtu wa pili kutoa maoni" mara nyingi unatoa conclusion mwenyewe!
  acha nikujibu hii kwa mara ya kwanza PENGO hajataja chama flani... na hizo ndio busara za kiongozi!.. amewaachia waumini wachague kama ni CCM haya Kama ni CUF haya kama Chadema sawa! Pengo hatoi kauli za Jazba kama kakobe! ambaye ana command waumini wafanye hivi..!
   
 11. M

  Masauni JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njiwa mbona akili yako finyu kweli kweli, ni Rais gani anayetoa rushwa na kutafuta urais kwa nguvu kama si kikwete? Kakobe hakumtaja mtu, anachosema uwezi ukasema rais hafai kwa sababu anaoa na kuacha! Tu wanadamu tumepungukiwa na utukufu wa Mungu, tunahitahi toba.
   
 12. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,807
  Trophy Points: 280
  Asante wewe umemuelewa Pengo alimaanisha NINI!.. HEBU NISADIE KUWAELIMISHA ambao hawajaelewa
   
 13. s

  small Member

  #13
  Sep 27, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jAMNI TUICHAGUE SISIEMU IMETUTOA MBALI SANA PLEASE
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kakobe alichofanya ni kuwaruhusu waumini wa kanisa lake kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi badala ya kwenda kusali; wala hajawambia waumini wake wampigie nani kura!! Sasa haya mambo ya Tanesco yanaingiaje mahala askofu anapowaasa waumini wake watumie haki yao ya kikatiba kwenda kuchagua viongozi wao.Ukumbuke kua CCM imetumia mbinu nyingi sana kuhakikisha kuwa watu wengi hawapati nafasi ya kupiga kura mojawapo ni hii ya kupanga uchaguzi siku ya jumapili wanayojua wakisto wengi wanakwenda kusali; pia wamehakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanakuwa likizo contrary to academic timetables ambapo vyuo vikuu hufunguliwa mwezi September safari hii wanafungua November kitu kinachowanyima haki yao ya kupiga kura kwani walipojiandikisha walikuwa vyuoni!! Hopefully Nec itarekebisha kasoro hii.CCM inawasiwasi watu wengi wakijitokeza kupiga kura watadomdoka!!
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wapi Kakobe ametaja Chama au Mtu?
   
 16. M

  Masauni JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona wewe kichwa chako kigumu kuelewa!! anayesemwa ni kikwete
   
 17. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,807
  Trophy Points: 280
  Ongea ya mtu na kauli zake utajuwa yupo upande gani... ?! Pengo hakusema CCM Straght.. Mtu wa chadema utasema ameongea kuhusu CCM, Na wale wafuasi wa CUF watasema hii kauli na CCM & CHADEMA!.. waumini wa Nashangaa hamjaona busara ya Pengo hapo! kwani hakuna wagombea wa chadema wanaotoa kanga! isitoshe kanisa lake lina waumini wengi saana na ni wafuasi wa vyama mbalimbali ..

  kama hajanielewa basi bana .. nabaki msomaji sasa wa hii thread!
   
 18. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,807
  Trophy Points: 280
  ni wewe ulivyotafsiri anamsema kikwete!! .. sio waumini wake wote wametafsiri hivo
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  niko conclusive yes kwa post na hoja za ajabu ajabu zinazojaza tu nafasi hapa..kwani nani hajui kuwa CCM wanagawa Khanga na T shirt??Nani hajua CCM inabeba watu kwenye malori kwenda kusikiliza mikutano ya huyo anayejiita mgombea wao wa urais na mgombea mwenza wake?sasa kuuma uma maneno ni kupoteza muda...Askofu Pengo anamaanisha kikwete asichaguliwe yeye na chama chake kwa kuwa ndio wanaogawa khanga na tshirts
   
 20. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,807
  Trophy Points: 280
  Tanga Kuna usemi "Ashidwae pia ni mume"!! umeshinda broda! haina haja ya kupandisha munkari!!...
   
Loading...