Pengo aonya mafundisho ya upotoshaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pengo aonya mafundisho ya upotoshaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by minda, Jul 8, 2010.

 1. minda

  minda JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  [​IMG]Wednesday, 07 July 2010 21:07
  Gazeti la mwananchi.
  Geofrey Nyang'oro
  ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo , amewaasa viongozi wa kanisa hilo kuepuka mafundisho ya upotoshwaji yenye lengo la kujitafutia sifa akidai mafundisho ya aina hiyo ni hatari kwa ustawi wa kanisa la Mungu.

  Askofu huyo alitoa kauli hiyo kwenye ibada ya misa takatifu ya upadirisho wa mapadri watatu wa kanisa hilo iliyofanyika jana katika Parokia ya Kristu Mfalme ya Tabata jijini Dar es Salaam.

  Alisema katika karne hii, wapo watu wanaoweza kufikiria kutumia nafasi walizonazo kufundisha neno la Mungu kwa lengo la kutafuta umaarufu miongoni mwa jamii na kwamba vitendo hivyo ni hatari kwa ustawi wa kanisa.
  Kauli hiyo aliitoa wakati Watanzania wa sasa wanashuhudia kuibuka kwa madhehebu na wahubiri wa aina mbalimbali ambapo baadhi yao wanajitangaza kuwa wana uwezo wa kufanya miujiza ya kutisha ikiwemo ya kufufua wafu, upako katika biashara, kuondoa mikosi, kurudisha ndoa, kufaulu mitihani , na hata kufanikiwa katika masuala ya kutafuta kazi.

  Baadhi ya viongozi wa madhehebu hayo wanaomba kwa kupayukapayuka kinyume cha maagizo ya Mungu kupitia kwenye Biblia Takatifu ambamo ameagiza sala zote zifanywe kwa unyenyekevu na hata kwa siri kwa kuwa yeye anaona yote ya siri...

  Pengo alisema viongozi wa kanisa wawe tayari kuteketea kama chumvi inayoyeyuka kwa ajili ya kunogesha radha ya chakula.

  “Maaskofu, Mapadiri na Mashemasi, ninyi mnapaswa kuwa chumvi na si mawe, chumvi ni kiungo kinachotumiwa katika kunogesha radha ya chakula, kiungo hiki hukubali kuteketea na kupoteza hata uhalisia wake ingawa uwepo wake huonekana kwenye ladha ya chakula,”alisema Pengo.

  KWA HIYO?: suala langu wana jf ni hapo pekundu, je hawa viongozi wa dini za kisasa sio sawa na waganga wa kienyeji tunaowasikia kila siku uswazini? hivi ni kweli wana uwezo wa kutenda mambo hayo?
   
 2. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako ni kuwa umezoea mafundisho manyonge na ukiona yale ambayo Biblia imeagiza watumishi wa Mungu watende unadhani ni nguvu za giza. Hauna tofauti na mafarisayo ambao walipoona Yesu anaponya wagonjwa, anatoa pepo na kufufua wafu wakasema anatumia nguvu za giza (Belzebubu).

  Maandiko yako wazi kuwa mtu akimwamini Yesu kazi alizofanya Yesu na zaidi ya hizo atafanya. Yesu alitoa pepo, alifufua wafu na kuponya wagongwa. Kwa hiyo wanaomwamini Yesu nao wamepewa mamlaka ya kutenda miujiza ikiwemo kufufua wafu, kuponya magonjwa na kutoa pepo (Mathayo 10:2-8).

  Pengo hana mamlaka yeyote kuwaonya wale wanaotenda miujiza kwa jina la Yesu. Yeye ni kiongozi wa dini ya Katoliki na nadhani alikuwa anawaonya washirika wake. Tusidanganyike kwa kufuata maneno matupu ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu wakati hawatendi yale Mungu anayoagiza watumishi wake watende. Na kama sisi tumeshindwa kutenda miujiza tusianze kuwabwatukia wale wanaoitenda kwa Jina la Yesu. Kwa taarifa yako Mungu bado anatenda miujiza (ikiwemo kufufua wafu) na anawatumia watu wa kawaida.
   
 3. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sio kila wamuitae bwana, bwana watauonja ufalme wa mbinguni. Yeye amesema watakuja na kumuambia tulikuwa tukiokoa watu na kuponya kwa jina lako lakini atawaambia ondokeni siwatambui.
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  kufufua wafu wa kiroho, lakini sio wafu wa mwili!!!
  Lakini kama Mungu kasema anaweza kuponya watu, kwa nini iwe muujiza? Muujiza ni nini hasa???
   
 5. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Kwa mujibu wa Biblia Yesu alifufua wafu wa kimwili (eg Lazaro, binti Yairo na kijana kwenye lango la Naini). Jamani naomba tusimweke Mungu mipaka, hakuna gumu la kumshinda Mungu. Tunapoona mambo yametushinda tusi-conclude kuwa hayawezekani. Dont put God in the box...

  Muujiza ni jambo ambalo kwa kibinadamu haliwezekani. Kwa mfano kutembea juu ya maji, kugawa bahari, kiwete kutembea, bubu kusema na mambo yanayofanana na hayo. Mungu hutenda miujiza
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Hivi hapo pekundu ni maneno ya Pengo au mwandishi ametaka kukoleza habari!!??
   
 7. M

  MJM JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Avuae nguo huna haja ya kumpima akili achana naye! Sidhani kama ufufuo huo na miujiza inahitaji tujikite Kinigeria zaidi. Lakini!!! anyway!!tusije kuitwa kina Sauli bure!
   
 8. minda

  minda JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  kukoleza habari!
   
 9. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Imani ni jinsi mtu anavyopokea kitu na inatofautiana baina ya mtu na mtu, nawashauri tusiishindanie IMANI.
   
 10. minda

  minda JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Ni kweli, "Mungu bado anatenda miujiza (ikiwemo kufufua wafu) na anawatumia watu wa kawaida lakini wengi wao sasa hutangaza kwamba miujiza hiyo (ila sio kufufua wafu kimwili) hufanya wao kwa nguvu zao na hujitangazia utukufu wao kupitia vyombo vya habari; tena baadhi yao hutumia vitu halisi mfano maji kutoka nchi za nje kufanya miujiza hiyo (isipokuwa ufufuo wa mwili).

  kwa upande wa ufufuo binafsi sijawahi kumwona mtu/msukule aliyekufa na kuthibitishwa na daktari akafufuliwa zaidi ya hadithi za hao watumishi ambao hujigamba kwa lugha za wakati uliopita,"nilifufua mtu" na sio Mungu! tatizo langu ni hapo tu.

  Katika kituo kimoja cha tv jumapili iliyopita, suala hili lilizungumzwa kwa kuhusisha mganga wa kienyeji mtaalamu wa masuala ya msukule na mtumishi wa mungu mfufua misukule. amini usiamini, maelezo yao yanafanana na inaonesha kwamba "wataalamu" hao huufanyia kazi ufalme unaofanana! tatizo langu ni hapo tu!
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Jul 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  :A S 112::decision::hand:
   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  Jul 8, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hapa Pengo alikuwa anazungumzia juu ya watu wa kanisa lake (RC)!
  Lakini aliyeripoti habari hii ameongezea chumvi zaidi na kuzungumzia madhehebu mengine;
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Minda,

  Kujibu swali lako, viongozi wa dini ni wabaya kuliko waganga wa kienyeji, kwa sababu waganga wa kienyeji afadhali watakudanganya kwa jina la "waungwana" na mizimu na upuuzi mwingine kama huo. Viongozi wa kidini wanakudanganya kwa kukuambia wao ni wawakilishi wa mungu muweza yote aliyeumba mbingu na nchi.

  Pengo anashangaza sana.

  Ukisoma doctrine ya ukristo utakuta yote anayoyashambulia yameandikwa katika biblia, kuanzia hiyo miujiza mpaka kunena kwa lugha.Kwa hiyo hamna kitu kigeni wanachofanya hawa wahubiri. Actually biblia (Mark 11:22-24 and the parallel Scripture to that in Matthew 21:21-22.) inakwambia imani itahamisha hata milima, sasa Pengo anataka kutuambia watumishi wa mungu wasioweza kuhamisha milima leo hawana imani au vipi?

  Tatizo kubwa ninaloliona hapa ni kwamba, huwezi kuwa unahubiri uongo mkubwa, kwamba kuna mungu anayetupenda aliyeumba mbingu na nchi na kutushushia biblia, halafu ukalaumu watu wanaofuata maneno ya uongo huu mkubwa yaliyo ndani ya biblia.

  Au anataka tumnukulie vifungu baada ya vifungu hapa? Tunaweza.

  Ukigundua kwamba huyu mungu "personal" wa JudeoChristian ni fraud, hivi vi skirmish kati ya waongo hawa na waongo wale wala haviwezi kukupa shida.

  Dini zote by nature ni uongo, sasa itakuwaje muongo mmoja apate moral authority ya kumshambulia muongo mwingine?

  Au anaona sadaka zinapungua na hawa wenzake wamemzidi kwa mbinu za uongo na michojo mingi (prosperity gospel, giving false hopes to the sick and desperate etc) na hivyo anajihami asijikute kanisa katoliki halina mfuasi na maganga-ongo wenzake wamemchukulia waamini wote ?

  Maana ukiangalia sana haya mambo wanajifanya ku front mungu, mambo ya kiroho, mbinguni etc kumbe wanapigania sadaka na influence tu.
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huwa natatizika sana na baadhi ya vitendo na maombi yanayofanywa na baadhi ya wahubiri kwa sababu zifuatazo na Mungu anisamehe kama nakosea:

  1.Binadamu kupitia wakati mgumu - iwe ni magonjwa, kifo, kukosa kazi, matatizo ya ndoa nk ni kitu cha kawaida kisichokwepeka. Iweje basi binadamu atake kubadilisha hali ya ubinadamu na kufanya kama vile dunia ni paradiso? Utawezaje kumlazimisha Mungu kujibu ombi lako au kutenda kama mganga wa kienyeji?
  ( ati watu wananunua vitambaa "vyenye upako", wanapakwa mafuta sehemu mbalimbali za miili yao ili kupata majibu kwa yanayowatatiza).Nakubali kabisa kwamba inawezekana kuondoa mapepo kwa maombi hilo sibishi maana hayo ni mambo ya ulimwengu wa kiroho.Lakini hainiingii akilini ati kwenda kuombewa wakati naumwa jino kwa sababu limeoza, au naumwa malaria shauri ya kuumwa na mbu waletao malaria, au kuumwa tumbo shauri ya uvimbe wa fibroids kwa akina mama - haya yote ni magonjwa yenye tiba na Mungu kaweka kipaji cha uponyaji kupitia waliosomea udaktari. Sasa kama kila mtu ataombewa, madaktari wakikosa kazi nao wataombewa wapate kazi gani ilhali walisomea taalamu ya utabibu?
  ( Naombeni mnieleweshe vizuri kwenye hili)

  2. Kwanini kumezuka madhehebu mengi sana ya kutatua matatizo ya kimwili zaidi ya yale ya kiroho? siyo kweli kwamba binadamu asiyekuwa na imani madhubuti anataka short cut au majibu ya papo kwa hapo kwa kila kitu kama kwenda kwa wapiga ramli? Na hiki kimekuwa chambo au kivutio kikubwa cha kuwatoa watu kwenye imani zao na kujiunga huko - in the process michango, sadaka etc vinaongezeka na kuneemesha baadhi ya watu?( NASEMA TENA SINA NIA YA KUKOSOA KWA UBAYA... nisamehewe kama nakosea tafadhalini!)

  3. Mwisho wa siku nadhani tunatafuta kumwabudu MUNGU wa kweli... haijalishi kama nasali kwenye dhehebu langu
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Wos,

  Ukichunguza sana maswali yako utaona majibu yote yanaelekea kwenye ukweli kwamba majibu ya maisha ambayo watu wanayatafuta katika dini, dini haiwapi, hivyo wanaibadilisha dini na kuifanya iwe ya kimwili zaidi ya kiroho.

  Ndiyo maana unakuta kuna "prosperity gospel" which is nothing but "feel good therapy to the poor and desperate"

  Ndiyo maana mambo ya kuombea watu wenye magonjwa yasiyotibika kirahisi au wasio na access na health services.

  Watu deep inside (perhaps subconsciously) wanaona kwamba habari za kiroho nyingi ni uzushi tu, wewe kama unaweza kunihubiria jinsi gani ninaweza ku build confidence nipate kazi kesho (kwa kuniambia mimi ni mtoto wa mungu wa mapato ninayestahili vitu vizuri) na kunipa psychological relief / placebo effect kwa kuniombea wakati kansa yangu hospitali imeniambia haiponi, nitakuona wa maana kuliko yule anayenihubiria ufalme wa mbinguni wa mungu asiyejionyesha.

  Matokeo yake hata hizo Evangelical churches / gospels nazo watakapo zi examine (kama wakiweza kujitoa katika sentimentalism) wataziona ni uzushi ule ule tu.
   
Loading...