Pengo aongelea Posho za wabunge, ushoga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pengo aongelea Posho za wabunge, ushoga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 16, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,
  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo

  Pengo: Posho za wabunge ubinafsi

  AONYA BILA KATIBA MPYA UCHAGUZI MKUU 2015 UTAKUMBWA NA GHASIA,
  AITA USHOGA NI WENDAWAZIMU
  ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amezungumzia mambo kadhaa ya kitaifa akisema, ongezeko la posho kwa viongozi wa umma ni ubinafsi na kuonya kama Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 utafanyika bila ya kuwako kwa Katiba Mpya, utagubikwa na ghasia.Pengo alitoa angalizo hilo jijini Dares Salaam jana alipokuwa akitoa ujumbe kwa taifa kuhusu Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.

  Posho

  Kuhusu posho, Kadinali Pengo alisema viongozi wa Serikali na umma wakiwamo wabunge, wanapaswa kuacha ubinafsi na badala yake wafanye kazi kwa kuwafikiria zaidi wananchi kuliko maslahi binafsi.

  “Sisi Wakristu tunaamani kuwa, Kristu licha ya kuwa alitumwa na Mungu Baba kuja kutukomboa wanadamu alifanyika mwili na kuzaliwa katika hali ya umaskini na ufukara ili atukomboe. Viongozi wa Serikali, dini na watumishi wa umma, inatupaswa kuiga mfano huo,”alisema Pengo.

  Aliongeza, “Nasisitiza hili kwa viongozi sababu hivi karibuni kumezuka mzozo kati ya wabunge na wananchi ambao wamejiongeza posho kwa madai maisha kuwa magumu. Viongozi hatupaswi kufikiria marupurupu yetu na maslahi yetu kwanza kabla ya kuwafikiria wananchi tunaowaongoza.”

  Hivi karibuni Spika wa Bunge alitangaza kwamba wabunge wameongezewa posho ya vikao kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku kutokana na ugumu wa maisha wakiwa Dodoma. Mbali na posho ya vikao, wabunge hupewa fedha ya kujikimu Sh80,000 na Sh50,000 ya usafiri kwa siku hivyo kuwafanya kupata Sh330,000 kwa siku.

  Pengo aliwataka viongozi wa Serikali na umma kuiga mfano wa mwokozi wao, Yesu Kristu aliyesema kuwa, licha ya kuwa na nguvu za Kimungu, alipotumwa na Mungu Baba kwenda duniani kuwakomboa wanadamu, alijishusha na kuzaliwa katika mazingira ya kimasikini na ufukara ili aweze kufanikisha kazi hiyo.


  Katiba na siasa

  Akizungumzia Katiba Mpya, Kardinali Pengo alisema ni chombo muhimu kinachotakiwa kufanya kazi kwa umakini na kuhakikisha inapatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Pengo alionya kuwa bila Katiba Mpya, taifa linaweza kuingia matatizoni kwa kuwa katiba ndio inayoelekeza wananchi kuchagua viongozi. “Tukicheza na Katiba, taifa litaingia matatani. Hivi sasa watu wameshailalamikia Katiba iliyopo kuwa ni mbovu na wakati huo huo Rais anachaguliwa kwa mpangilio ulio kwenye Katiba na anaapa kulinda Katiba na kuitetea,”alisema Pengo na kuongeza: “Tumeshasema Katiba iliyopo kwa sasa ni mbovu, tuchukulie suala hili “very serious (kwa uzito), tukamilishe kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, vinginevyo tutaingia matatizoni”.

  Akizungumzia hali ya kisiasa, alisema hadi sasa Watanzania bado wanajifunza namna ya kuishi ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa baada ya kutoka ndani ya mfumo wa chama kimoja.
  Alisema jibu la kufikia kwenye siasa bora ni, kulifanyia kazi suala la Katiba, ambayo ndio itakayoamua wananchi wanataka kutawaliwa na watu wa namna gani. “Kwa sasa bado tunaishi ndani ya mawazo na mtazamo wa chama kimoja cha siasa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Ndio sababu, mawazo ya chama ndio yanayochukuliwa kama mwongozo wa Serikali. Lakini tukiweka mkazo katika Katiba, tunapaswa kutambua tunatengeneza katiba ya nchi na si ya chama kimoja,”alisema Kardinali Pengo.


  Sherehe za miaka 50 ya uhuru

  Kuhusu sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Kardinali Pengo alipongeza hatua tuliyofikia akisema ni nzuri na kutaka furaha hiyo iendelee kubaki miongoni mwa Watanzania. “Desemba 9 mwaka huu tulikuwa na Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Ujumbe wangu, tuendelee na furaha hiyo, lakini suali la kujiuliza sijui ni wangapi tulifurahia sherehe hiyo? Swali hili pia hata viongozi wanapaswa kujiuliza,”alisema.

  Katika ujumbe wake huo, Pengo alisema Uhuru wa kweli hauji kwa kubahatisha bali kwa kufanyakazi.
  “Mwalimu Nyerere alisema Uhuru ni Kazi. Sisi tukasema Uhuru na Kazi. Lakini ujumbe unabaki kama ulivyo, nami leo ujumbe wangu kwa Watanzania ni kutambua bila kazi hakuna maendeleo,”alisema Kardinali Pengo.


  Suala la ushoga

  Alipoulizwa kuhusu suala la mataifa makubwa ya Uingereza na Marekeni kutaka mataifa yanayowapa misaada kuwatambua watu wanaojihusisha na ushoga, Kadinali Pengo alijibu kwa kifupi “Ushoga ni wendawazimu”.

  Alisema Mungu alipoumba watu; mwanamke na mwanaume na kuwapa hisia, alitaka watu wazaliane na kuujaza ulimwengu. Akahoji “Huyo mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke wanakutana ili iwe nini?”

  Pengo alisema wanaoshiriki ushoga wanamkosea Mungu na kusisitiza, kamwe hakutakuwa na furaha kwa mtu anayekwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.


  Elimu

  Kuhusu matatizo yanayiokabili mfumo wa elimu hapa nchini, Pengo alisema suala hilo linapaswa kuangaliwa pande zote mbili za wananchi na Serikali. Alipinga njia inayotumiwa na wanafunzi kudai haki kwa maandamano na kulazimisha mambo wanayoyataka kufuatwa na watu wengine.

  “Maandamano katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliibuka kwa mara kwanza lilipoanzishwa JKT, wanafunzi katika chuo hicho waliandamana na kumpinga Mwalimu Nyerere kuwa hata kama utatulazimisha hilo tunapinga na tutakwenda huku mioyo yetu ikiwa nje ya hilo,”alisema Pengo.

  Alisema siyo jambo jema kwa mtu yeyote anayedai haki kuhamaki kwa viongozi wa nchi na kusisitiza, zipo njia sahihi za kudai haki hizo. “Iko namna ya kudai haki, miaka iliyopita kulikuwa na mgomo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,vijana walikuja kwangu kuomba msaada, nikawaambia hakuna anayepingana nanyi kudai haki zenu, lakini ninachoogopa ni tendo la baadhi yenu kutumia hata nguvu kulazimisha watu wengine kufuata mnachotaka,”alisema Pengo na Kuongeza: “Kesho mkiwa viongozi wananchi wakikataa mnayotaka kufanyika mtalazimisha”.

  Hata hivyo, alisema ni vema Serikali ikakaa chini na kuangalia madai ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kuyafanyia kazi.Alisema kama kuna upendeleo miongoni mwa makundi yanayosoma katika vyuo hivyo, harakati za kudai haki haziwezi kunyamazishwa kwa nguvu.
  Pengo alifafanua kwamba mambo yanayoweza kuchochea vurugu katika vyuo ni kitendo cha upendeleo wa utoaji haki, ikiwamo mikopo kwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo hivyo.

  “Ikiwa utamnyima mikopo mtoto masikini wa mkulima na kumpatioa mkopo mtoto wa mbunge mwenye mshahara unaoridhisha kuwa ndio anayesitahili kamwe harakati hazitazuilika hata kwa kutumia silaha,”alisema.

   
 2. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hapa ndo amesema jamba la tafakuri...........

   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hapa naona katumia falsafa ya hali ya juu kuhusu mfumo wa uongozi wa sasa na mizengwe ya uandaaji wa katiba mpya.
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CARDINAL PENGO-The strongest religion leader I admire in this country.God bless you today and forever...
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,356
  Trophy Points: 280
  catholic church has been consistent on their stands,never waivered once(atleast for my memory),and this one is a piece of wisdom..shalom cardinal
   
 6. King2

  King2 JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Lazima bakwata wajibu.
   
 7. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Labda wajibu kuhusiana na mahakama ya KADHI. kwao ni muhimu kuliko zaidi kuliko Hospitali na shule.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  BAKWATA walishatolea kauli kupinga ushoga na kuridhia matakwa ya CCM kuhodhi uandaaji wa Katiba mpya, vinginevyo watakuwa wanarudia walichokwisha kisema.
   
 9. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Wabunge wamekuwa wezi badala ya wawakilishi wa wananchi. Posho ya mafuta wanayolipwa kwa siku inatosha kusafiri umbali wa km 150. Wanasafiri umbali huo kila siku kwenda wapi kama sio wizi. Hili halina CCM wala mpinzani, wote tuseme hapana.
   
 10. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Mkapa amefanya maovu mengi, have they condemned him? Are they persecuting Kikwete simply because he is not one of their own?
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wizi wa hali ya juu unaofanywa na wabunge dhidi ya wananchi. Safari wanayopaswa kulipwa gharama ya usafiri ni ile ya kutoka kwenye jimbo lake la uchaguzi na kuttua Dodoma na siku atakaporudi jimboni kwake baada ya kumalizika vikao vya bunge.

  Watumishi mbalimbali ambao mshahara wao pengine ni pungufu ya 200,000 ni hizo hizo anazotumia katima kujiikimu kimaisha na usafiri na hana la ziada.
   
 12. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hata mtoto mdogo anjua udhaifu wa JK wa sasa umepitiliza. Mkapa huwezi kulinganisha na mkwer#. Hata angekuwa mkatoliki tungesema tu kwa maslai ya Taifa.
   
 13. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,077
  Likes Received: 10,437
  Trophy Points: 280
  huyu ndo kiongozi wa dini!! jembe langu Pengo!! god bless you sanaaaaaaa
   
 14. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,077
  Likes Received: 10,437
  Trophy Points: 280
  watajibu upupu! wale ni vilaza wa kujichanganya(bakwata)
   
 15. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #15
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Scop Candid tunashukuru kwa taarifa muhimu;
  1, Ni kudanganya watu kusema kuwa kauli kama hii ni kuchanganya siasa na dini. Hivi vitu vyote viwili havigawanyiki kwa kuwa wapiga kura wa wanasiasa ndio waumini wa mashekh na maaskofu. Wote wanahitaji haki, maji, afya na elimu sawia. Wanasiasa wakiharibu hakuna atakayekwenda msikitini wala kanisani.
  Kauli yake imezungumzia mambo muhimu ya kitaifa.

  2, Wadau hapo kwenye red ya kwanza na ya pili sijaelewa. Anaposema
  zipo njia sahihi za kudai haki hizo. “Iko namna ya kudai haki,
  Hapa alikuwa anapinga matumizi ya nguvu kama migomo vyuoni;
  Katika aya nyingine mwishoni mwa tamko lake kuna sentensi nyingine inayosema;
  Ikiwa utamnyima mikopo mtoto masikini wa mkulima na kumpatioa mkopo mtoto wa mbunge mwenye mshahara unaoridhisha kuwa ndio anayesitahili kamwe harakati hazitazuilika hata kwa kutumia silaha
  Hapa sijaelewa kwa kuwa hajataja hizo njia nzuri za kudai haki. Ni zipi? Lakini pia hapa chini anasema harakati hazitazuilika hata kwa silaha.

   
 16. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwemye hili hauko sahihi hata kidogo,wakristu si wanafiki na wakati mwingi hatupelekwi na upepo. Kadinali kaongelea maswala yanayohusu taifa letu wala hajaongaea hayo kwa wakristu peke yao.
   
 17. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #17
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Nafuatilia nijue kama Spika naye anachukua pesa ya mafuta, maana huyu anatumia gari la serkali, na mafuta anapewa na serikali. Ipo haja ya wabunge wote kutumia magari ya serikali kama watumishi wa mihimili mingine ili tuondokane na wizi kupitia ile mikopo ya magari ya m 90.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Inaweza kuonekana kukinzana katika matamshi hayo kama ulivyoainisha, lakini tukumbuke kuwa aina na hadhi ya kiongozi wa kiroho hawezi kushabikia utaratibu ambao unahatarisha amani, kukosa maadili na mengineyo, ndio maana pengine utaratibu wa kimaadili unaposhindikana hapo watu hujichukulia sheria mkononi ni kwa sababu ya viongozi wa serikali kufumbia macho madai yao. Kiongozi wa kiroho hawezi kuhamasisha maandamano ila atasisitiza siku zote haki itendeke kwa raia. Hata hivyo matamshi yanayotolewa na viongozi hawa tuangalie aina ya viongozi na mfumo wao wa maadili ya maisha yao.
   
 19. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Anna Mkapa alijimilikisha nyumba za NBC, mume wake alijimilikisha Kiwira mine. Kamuulize Pengo analisemeaje hilo maana nalo linahusu taifa.
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tunachotofautiana sikielewi kwa vile tunaotaabika ni sote, hivi mwenzetu unaishi Tanzania ipi usiyejua hali ya maisha na tatizo la serikali yetu?
   
Loading...