Mkodoleaji
JF-Expert Member
- Apr 27, 2008
- 458
- 138
Fredy Azzah na Ibrahim Yamola
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema Watanzania wanasherehekea miaka 50 ya uhuru huku kukiwa na makundi ya viongozi na vigogo nchini wanaojineemesha kupitia migongo ya wananchi bila kujali wanawasaliti, wanawaongezea umaskini na kuwaua.
Kardinali Pendo alilaani akisema: "hayo yamekuwa yakitendeka kinyume na misingi iliyoainishwa na waasisi wa taifa wakati wakidai uhuru kutoka kwa wakoloni ambapo walitamani kujenga Tanzania yenye utukufu.
Kardnali Pengo alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akiongoza ibada ya maadhimisho ya miaka 50 ya Tanzania, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme Parokia ya Tabata.
"Waasisi wetu walipokuwa wanapigania uhuru wa taifa hili, lengo na maono yao yalikuwa kutengeneza taifa lenye utukufu, lenye kutawala mataifa mengine …," alisema Kardinali Pengo na kuongeza:
"Katika miaka 50 tunayoikamilisha, kumekuwa na mafanikio na changamoto nyingi tu, inabidi tujipange ili watakao kuja kuadhimisha miaka 100, au hata miaka 25 ijayo wasije wakasema afadhali wakati wa mkoloni."
Katika ibada hiyo ambayo pia ilitumika kuliombea taifa, Pengo alisema wakati wa kupigania uhuru lengo ilikuwa ni kulifanya sehemu salama na bora ya kuishi watu wake.
Kardnali Pengo alitahadharisha akisema: "Lakini sasa Taifa lina makundi ya watu wasaliti, wenye ubinafsi na ambao wako tayari kujitafutia utukufu hata ikibidi kuwakandamiza na kuwaua wenzao".
Kwa sababu hiyo akawataka Watanzania kutafakari katika kipindi hiki cha kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, wajiulize wamekuwa wakijitafutia utukufu binafsi au ule ulioasisiwa na taifa wa wananchi wote kufaidi matunda yake.
Kwamba, tumepata utukufu wa aina gani?" Alisema Kardinali Pengo na kuonya; "Baadhi ya watu wanapata utukufu bila hata kujali kama watu wengine wanakufa, jambo ambalo ni hatari kwa taifa."
Kardinali Pengo aliwaonya waliopewa dhamana ya uongozi na kutumia nafasi hiyo kujitajirisha, kuwa ni usaliti kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla.
Tuhuma za dawa za kulevya
Katika hatua nyingine, Kadinali Pengo, alilaumu mtindo wa viongozi wa Serikali na dola kutotaja hadharani majina ya watu wanaowatuhumu kuhusika na biashara ya dawa za kulevya huku wakiendelea kulalamika kuwa wapo na wamewakamata.
Alisema hali hiyo haionyeshi nia yao ya dhati katika kupambana na biashara hiyo haramu.
Akikumbushia kauli aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete wakati wa Sikukuu ya kumwekwa wakfu na kumsimika Mhashamu Askofu John Ndimbo kuwa Askofu wa Jimbo la Mbinga kuwa baadhi ya viongozi wa dini huuza dawa za kulevya, alisema alitakiwa kuwataja.
Kardinali Pengo alisema kitendo cha Rais Kikwete pamoja na baadhi ya viongozi waliojitokeza kuzungumzia suala hilo huku wakisema hawawezi kuwataja kwa majina, huo ni usaliti mkubwa kwa taifa.
"Haiwezekani mtu mkubwa tu, wala siyo mdogo kuja katika eneo la Kanisa la Katoliki, kukiwa kumejaa Maaskofu kutoka karibu nchi nzima, unasema maneno haya halafu unasema, siyo nyie ni viongozi wa makanisa madogomadogo," alilalamika Kardinali Pengo.
Aliongeza kwamba: "Kama ndivyo hivyo kwa nini sasa uje kuyasema maneno hayo katika eneo la Kanisa Katoliki."
Akasisitiza: "Mapadri, watawa; naomba tujiangalie kama sisi tunaguswa na hii kauli, kama haitugusi tumshukuru Mungu, lakini ni vyema hawa watu wakatajwa.
Hata kama ni mimi njoo uniambie, ukisema hunitaji kwa sababu ni kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, huo ni usaliti mkubwa kwa taifa."
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, William Lukuvi, aliwahi kuliambia Bunge hivi karibuni kuwa Serikali ina safari ndefu katika kufanikisha mkakati wa kukomesha biashara hiyo haramu.
Alisema Serikali inaamini kuwa vita ya kuwakamata wanaojihusisha na dawa za kulevya ni ngumu lakini akasisitiza kuwa anaamini mwishowe watashinda uhalifu huo.
Lukuvi alisema mbali na kuwataja hadharani baadhi ya viongozi wa dini, imebainika kuwa wana mtandao mkubwa.
"Hapa sio kuwataja tu maana kama ni kuwataja tayari Serikali ilikwisha wataja na watu wanajua kuwa kiongozi wao ni yule Askofu wa Nigeria, lakini hapa suala ni namna ya kupambana na kuwajua wengine,'' alisema Lukuvi.
Hata hivyo, mara baada ya Rais Kikwete kutoa kauli hiyo, Jumuia ya Kikristo Tanzania (CCT), ilikuja juu na kumpa saa 48 za kuwataja hadharani viongozi wa madhehebu ya dini wanaohusika na biashara hiyo haramu.
"Rais ataje majina ni kina nani wanahusika na ndani ya saa 48 awe ameyataja la sivyo itakuwa ni aibu zaidi kwake na Serikali," alisema Makamu Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dk Valentino Mokiwa.
Rais Kikwete alijibu wito huo kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwamba, viongozi wa dini siyo malaika kwa hivyo wasijivune kuwa hakuna miongoni mwao ambao ni wahalifu.
Source: Gazeti la Mwananchi
My take:
Kweli Pengp amesummarise vizuri behaviour za Kikwete kuwa ni msaliti maana kuna matukio mengi yametokea na hajatoa kauli wala kuchukua hatua zozote sasa kama huu si usaliti kwa wananchi ni nini?