Pendekezo: Waziri anayeshughulikia Misaada ya Kigeni

Pendekezo: Waziri anayeshughulikia Misaada ya Kigeni

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,097
Reaction score
43,309
Misaada ya Kigeni ina sehemu Kubwa Sana katika uchumi wetu. Hii ni kweli kiasi kwamba bajeti yetu huwa inaandaliwa ikipigia hesabu misaada hii ya moja kwa moja ya bajeti. Wanaotupa misaada wana vyombo vyao vinavyosimamia na hata Mawaziri au Manaibu Waziri. Sote tunajua vyombo Kama USAID, DANIDA, SIDA, CIDA (imebadilisha Jina nadhani), na JICA nikitaja machache ni taasisi za nchi mbalimbali zinazosimamia misaada kwenda nchi nyingine.

Je, umefika wakati na sisi tuwe na chombo rasmi kinachoratibu na kusimamia misaada inayoingia na kutoka (Kama tuliyopeleka Msumbiji?)? Je, kwa vile misaada ya kigeni ni sekta rasmi na yenye mchango mkubwa unaostahili Waziri kamili hata Kama ni ndani ya Ofisi ya Rais? Je, kutakuwa na faida au hasara gani tukiwa na sera rasmi ya misaada ya kigeni na Waziri mwenye kusimamia sera hiyo?

Au tuendelee tu hivihivi(maintain the status quo) yaani bila kuwa na sera au mtu (point person) anayeweza kuulizwa na kujibu? Je, wizara ya Mambo ya Nchi za Nje inatosha baadhi ya wahisani wameweka International Development Kama cabinet level ministry.Tusiwaige?
 
Huko kutakuwa ni "kujichora" bora misaada iwe inakuja kimya kimya kama ambavyo watawala wanataka.
Wanabeza midaada halafu wanaomba na kuililia! Mpango aendelee tuu kuifatibu kimya kimya ili mkuu awe huru.
Sisi tupo uchumi wa kati ,hatutaki misaada ya Mabebelu .
20201124_182411.jpg
20201122_161633.jpg
 
Mzee Mwanakijiji
Huu ni wakati wa kuchapa kazi tujenge nchi kwa pesa zetu za ndani.
Mabeberu hawatutakii mema. Mitano tena.
Ndio point yangu, tuondoe kabisa misaada ya moja kwa moja ya bajeti, misaada iwe sehemu ya mahusiano ya kibiashara, na uwekezaji katika rasilimali watu na uhamishaji wa ujuzi. Bajeti yetu ni lazima iwe inatokana na mapato ya ndani new asilimia 100 ndio kujitegemea huko.
 
Yaani pesa ya msaada utumie tena kununua GX za Ths 300,000,000 kuajiri watu na maptumizi mengine badala ya kwenda kushughulikia wananchi!!. Hao wenzio ni watoa msaada si wapokeaji!. Hivi Mwanakijiji yule wa zamani aliibiwa jina au kachuja kimawazo!
 
Yaani pesa ya msaada utumie tena kununua GX za Ths 300,000,000 kuajiri watu na maptumizi mengine badala ya kwenda kushughulikia wananchi!!. Hao wezio ni watoa msaada si wapokeaji!. Hivi Mwanakijiji yule wa zamani aliibiwa jina au kachuja kimawazo!
Labda hujanielewa..kwani Sasa hivi hiyo hela haitumiki kununua hizo GXs?
 
Kwa hiyo hili linaweza kubadilika simply kwa kulianzishia wizara yake?
Ni sekta muhimu ya uchumi.Kama sekta nyingine za uchumi zina Wizara zake na nyingine mchango wake ni mdogo kulinganisha na misaada ya kigeni. Kwanini basi tusiitendee haki sekta hii na kutambua umuhimu wake?
 
Ni sekta muhimu ya uchumi.....Kama sekta nyingine za uchumi Zina wizara zake na nyingine mchango wake ni Mdogo kulinganisha na misaada ya kigeni..kwanini basi tusiitendee haki sekta hii na kutambua umuhimu wake?
Kwa nchi yenye miaka zaidi ya nusu karne toka ipate Uhuru ni fedheha kuwa na wizara ya kushughulikia misaada tunayopokea.

Hatuwezi kuwa ombaomba milele hivyo hakuna ulazima kuanzisha wizara ambayo inakinzani na malengo yetu ya kujitegemea.

Tunawahubiria raia wetu kuhusu kujijengea uwezo wa kujitegemea kama taifa alafu tunaanzisha wizara ya kuratibu upokeaji wa misaada huko ni kuwachanganya wananchi na siasa za kihuni hizo.
 
Ni sekta muhimu ya uchumi.....Kama sekta nyingine za uchumi Zina wizara zake na nyingine mchango wake ni Mdogo kulinganisha na misaada ya kigeni..kwanini basi tusiitendee haki sekta hii na kutambua umuhimu wake?
Kama biashara za ndani zinazidi kufa, hayo mapato yatatoka wapi tuweze kujiendesha bila misaada yao?

Ningetegemea kwanza muinue hali ya kipato ya Mwananchi mmoja mmoja, msiwasumbue na wawekezaji, pesa itakapokuwa nzuri kwenye mzunguko ndio uje na mpango kama huo, lakini kuja na mpango huo wakati huu bado tunaomba misaada ya kumalizia Nyerere Dam, na SGR, kwangu naona ni ndoto.
 
Back
Top Bottom