Pendekezo: Wapangaji wa vyumba wapitie Serikali za mtaa ili kupunguza bei ya kodi

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,563
22,123
Kutokana na bei holela ilivyo sasa Kwa wamiliki wengi Wa Nyumba za kupanga; pamoja na kujiamulia kupandisha bei kila wanapojisikia wakishilikiana na madalali;

Ni wakati sasa serikali kupitia ofisi za serikali za mitaa kote nchini kufanya yafuatayo:

1. Itoe tamko Kwa wamiliki wote Wa Nyumba za kupanga wapeleke taarifa za kupangisha Nyumba zao serikali za mitaa.

2. Serikali za mtaa itoe bei elekezi Kwa wamiliki kulingana na ubora/hadhi ya eneo.

3. Orodha ya Nyumba zitapatikana Kwa urahisi kuliko kutumia madalali matapeli wanaozungusha watu siku nzima.

4. Serikali ya mtaa itawatambua Kwa urahisi wageni na wenyeji kupitia utaratibu huu Kwa kuweka kibali maalum cha kuhama na kuhamia.

5. Nyumba zote zipate kibari cha kupangisha kupitia serikali za mitaa Kwa gharama nafuu. (Hiki kitaongeza mapato mfuko Wa serikali za mtaa na kijiji)

6. Kila mtu anayepanga Nyumba au chumba kuwepo na asilimia kidogo ibaki ofisini Kwa ili kutunisha mfuko!

7. Maelekezo ya matumizi ya fedha hizo yaamuliwe na baraza maalum la mtaa/kijiji Kwa kushilikiana na diwani na watendaji ili kutatua changamoto za eneo husika. Kwa mfano! (Kulipa walinzi shirikishi, wakusanya taka n.k)

*****************************
Mbali na hapo madalali wataendelea kupandisha kodi kila siku pasipo utaratibu pamoja na kukaribisha wezi pasipo kuwatambua.
 
Wewe unataka kuleta balaa, ni muda wa wakulima kutajirika- mtukufu. Na huu ni muda wa wenyenyumba kutajirika. Na madalali pandisheni bei za vyumba mara 3 zaidi ili nanyi mtajirike
 
Jenga yako ndio uanze kujipangia yote hayo. Hujui gharama za ujenzi zilitokea wap na yap yalimkuta mwenye nyumba. Uchumu huu wacha wenye nyumba nao wafaidi na kujivunia kujenga mapema.

Ushauri wako umejaa chenga chenga za uvunjaji wa amani yaani kweli ofis ya mtaa zinakabana mashati kwa kipato kidogo walicho nacho halafu wewe unapendekeza pia wapate hela za wanaopangisha si watu watauana kisa pesa.(ya kagera hayajafunza wengi aiseee)
 
WELL SAID. NA PIA HAWA WA KUTAKA MIEZI SITA AU MWAKA NAO WABANWE.
 
Duuh unalinganisha daladala na nyumba!? Tuanzie kwanza Bei elekezi ya sukari ni sh ngapi,je ndio bei inayotumika madukani?
Soko huria ? Kwenye nauli Kwa wamiliki Wa madaladala mbona kuna bei elekezi? Basi na wenye mabasi wapandishe ili iwe soko huria! Ujinga ujinga tu unaweza kupinga hilo
 
Jenga yako ndio uanze kujipangia yote hayo. Hujui gharama za ujenzi zilitokea wap na yap yalimkuta mwenye nyumba. Uchumu huu wacha wenye nyumba nao wafaidi na kujivunia kujenga mapema.

Ushauri wako umejaa chenga chenga za uvunjaji wa amani yaani kweli ofis ya mtaa zinakabana mashati kwa kipato kidogo walicho nacho halafu wewe unapendekeza pia wapate hela za wanaopangisha si watu watauana kisa pesa.(ya kagera hayajafunza wengi aiseee)
Kuna Mdau hapo juu kauliza swali la msingi!!!KAMA NI GHARAMA ZA UJENZI JE; KWANI HAYO MABASI YANAYOPANGIWA BEI ELEKEZI WAMILIKI WANAYAPATA BURE?
 
Bei ya basi na nyumba ni vitu viwili tofauti. Vyumba ndani ya nyumba na siti za basi vina tofauti pia(wingi wake)

Ndio maana mtu anaweza kumiliki gari\daladala na akawa hana nyumba(mpangaji)
Kuna Mdau hapo juu kauliza swali la msingi!!!KAMA NI GHARAMA ZA UJENZI JE; KWANI HAYO MABASI YANAYOPANGIWA BEI ELEKEZI WAMILIKI WANAYAPATA BURE?
 
Soko huria ? Kwenye nauli Kwa wamiliki Wa madaladala mbona kuna bei elekezi? Basi na wenye mabasi wapandishe ili iwe soko huria! Ujinga ujinga tu unaweza kupinga hilo

Hata kwenye daladala watoe bei elekezi, mimi nikeshe nafanya kazi ninunue daladala ya halafu wewe upande kwa bei unayotaka wewe na serikali yako?
 
Acheni watu watajirike kwa kazihalali, mtuamejinyima akajenga alafu umpangiebei ya chumba?? Huompango ukianza nitapiga hesabu kati ya kupangisha ama kufugia kuku kipi kinafaida.
 
Juzi nimepanga nyumba,nataka kumlipa kodi mwenye nyumba,anasema hawezi kupokea pesa mpaka nimpe dalali cha kwake kwanza ambayo ni kodi ya mwezi mzima.Unaweza kuona ni jinsi gani dalali anaweza kuwa mpangaji wa bei ya kukodi nyumba.
 
Kutokana na bei holela ilivyo sasa Kwa wamiliki wengi Wa Nyumba za kupanga; pamoja na kujiamulia kupandisha bei kila wanapojisikia wakishilikiana na madalali;

Ni wakati sasa serikali kupitia ofisi za serikali za mitaa kote nchini kufanya yafuatayo:

1. Itoe tamko Kwa wamiliki wote Wa Nyumba za kupanga wapeleke taarifa za kupangisha Nyumba zao serikali za mitaa.

2. Serikali za mtaa itoe bei elekezi Kwa wamiliki kulingana na ubora/hadhi ya eneo.

3. Orodha ya Nyumba zitapatikana Kwa urahisi kuliko kutumia madalali matapeli wanaozungusha watu siku nzima.

4. Serikali ya mtaa itawatambua Kwa urahisi wageni na wenyeji kupitia utaratibu huu Kwa kuweka kibali maalum cha kuhama na kuhamia.

5. Nyumba zote zipate kibari cha kupangisha kupitia serikali za mitaa Kwa gharama nafuu. (Hiki kitaongeza mapato mfuko Wa serikali za mtaa na kijiji)

6. Kila mtu anayepanga Nyumba au chumba kuwepo na asilimia kidogo ibaki ofisini Kwa ili kutunisha mfuko!

7. Maelekezo ya matumizi ya fedha hizo yaamuliwe na baraza maalum la mtaa/kijiji Kwa kushilikiana na diwani na watendaji ili kutatua changamoto za eneo husika. Kwa mfano! (Kulipa walinzi shirikishi, wakusanya taka n.k)

*****************************
Mbali na hapo madalali wataendelea kupandisha kodi kila siku pasipo utaratibu pamoja na kukaribisha wezi pasipo kuwatambua.
UNAPENDEKEZA NYUMBA ZA WATU WAKATI UNAISHI NYUMBA YA KUMBANGA NA VOCKSWAGEN YA MIL 100
 
MAISHA YAMEBANA KWELII MPWAA SI MCHEZOOO HUKOO ANA UWEZO WAKUFIKA WAMILIKI WANASERIKALI YAO
 
Hawa watu wasipangiwe kodi. Mbona soko linaamua taratibu. Kuwepo na orodha ya nyumba zinazopangishwa serikali ya mtaa na wenye nyumba wakitaka kuwatumia madalali na wao wawepo.
 
Back
Top Bottom