fasiliteta
JF-Expert Member
- Jul 2, 2014
- 2,598
- 4,472
Kwa jinsi ninavyoona muelekeo wa serikali baada ya kifo Cha JPM na kumpata Rais mpya Mama Samia Suluhu, ni wazi sasa panga pangua ya safi ya uongozi unaendelea ili mama apate cream yake ya kuliendesha gurudumu hili pamoja na kujarbu kurekebisha mapungufu madogo madogo ya mtangulizi wake yasijirudie.
Ameanza na wizara mbalimbali kaja makatibu wakuu na wakuu wa Taasisi za serikali. Ni wazi sasa wanaofata ni:
Si vibaya pia kwa jicho la tatu kama wananchi tunaweza kutoa maoni yetu na pendekezo kwa nafasi hizi mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wilaya kama akipita humu aangalie sehemu ya wananchi wake Wana maoni gani kabla hajamalizia kufanyia kazi anayoendelea kuyapanga.
Binafsi namuona GODWIN GONDWE.
Apande cheo kutoka kua mkuu wa wilaya kua mkuu wa mkoa.
Jamaa ni mchapakazi sana na hana majivuno. Pamoja na umaarufu wake lakini anajishusha kwa wananchi. Ni mkuu wetu wa wilaya ya Temeke. Mimi kama raia nimemshuhudia Mara nyingi akitatua kero za watu na ukimsimamisha anasimama na kusikiliza kabisa na hata raia wengi wa Temeke ukiwauliza watakwambia hilo hilo.
Wananchi wengi tunatamani kesi zetu na shida zetu nyingi ziishie kwa wakuu wa wilaya au mikoa na si mpaka kwenda wizarani au Rais na kupata ufumbuzi na si majibu ya hovyo na nenda rudi kila siku Kama wakuu wengi wa wilaya wanavyosumbua wananchi wake.
Hakika GONDWE ni kiongozi haswaa.
Namuona pia Dada yetu JOKATE anavyopambana. Ni muda muafaka sasa akabiziwe mkoa wa Pwani ili aendelee kuutengeneza zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Kunenge aendelee huyu huyu maana hana papara kabisa. Huko mikoani pia tuangalie.
Nawasilisha

- Wakuu wa mikoa
- Wakuu wa wilaya
- maDED
- maDAS n.k.