PENDEKEZO: Waalimu nao wafanye NECTA za masomo yao

maringeni

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,198
3,894
Wadau nimefuatilia kwa muda mijadala ya sababu za kushuka kwa elimu yetu na nini kifanyike. Katika mijadala hii lipo kundi la upande wa waalimu, watunga sera, wachambuzi wa sera, wazazi, waalimu nk.

Kila kundi limejaribu kuonyesha mapungufu ya upande fulani. Wengi tumepitia shule na vyuoni na waalimu wetu tunawajua na wengine hata majina tumewapa kwa ufundishaji wao ama mzuri au mbaya.

Pendekezo langu ni kuwa kila NECTA wanapotoa paper zao za kidato cha 4 au 6 mwalimu wa somo husika afanye na darasa lake na usahihishwe na NECTA.

Nia ni kuona kiwango cha waalimu husika cha waalimu wa masomo hayo kama kweli wanauelewa wa kutosha na kama kweli wanafunzi wanafaulu kwa kufundishwa au kwa juhudi zao binafsi?

Na huo uwe sehemu ya hitaji kwa mwalimu kupandishwa cheo/ daraja.

Nawasilisha.
 
Hata mwalimu akifanya mtihani akafaulu au kufeli! Bado lengo litakuwa halijafikiwa kwani lengo ni mwanafunzi kufaulu sio mwalimu!!
Halafu sijui mnasahau au hamjui mchango wa mwalimu katika kufaulu kwa mwanafunzi ni 30% tuu!! Kwa nini msihangaike na hizo 70% zitaboreshwaje mnahangaika na 30% au ndo mambo ya mbaazi ikikosa maua!!
 
Mkuu kuna walimu wanafundisha madarasa yasiyofanya mitihani ya NECTA kwa mwaka husika, mf darasa la I-VI, kuna Form I, Form III na Form 5, hawa unaqaweka kundi gani?
 
Wengi tumepitia shule na vyuoni na waalimu wetu tunawajua na wengine hata majina tumewapa kwa ufundishaji wao ama mzuri au mbaya.
Kwa mawazo haya sidhani kama umepita chuoni maana unaonekana ni mbovu kuliko mwanafunzi wa darasa la IV.Hivi anayefundisha Mathematics form IV lazima awe amefundisha wanafunzi hao kuanzia form I had III? AU hukuona hilo udhaifu katika fikra zako.
 
Kama kaweza kufaulu mtihani wa degree aliosomea atashindwa kufaulu mtihan wa form 4!!!!!
 
Kama walifeli mitihani ya Necta mwanzoni usitegemee wakafaulu tena
 
Wadau nimefuatilia kwa muda mijadala ya sababu za kushuka kwa elimu yetu na nini kifanyike. Katika mijadala hii lipo kundi la upande wa waalimu, watunga sera, wachambuzi wa sera, wazazi, waalimu nk.
Kila kundi limejaribu kuonyesha mapungufu ya upande fulani.
Wengi tumepitia shule na vyuoni na waalimu wetu tunawajua na wengine hata majina tumewapa kwa ufundishaji wao ama mzuri au mbaya.
Pendekezo langu ni kuwa kila NECTA wanapotoa paper zao za kidato cha 4 au 6 mwalimu wa somo husika afanye na darasa lake na usahihishwe na NECTA. Nia ni kuona kiwango cha waalimu husika cha waalimu wa masomo hayo kama kweli wanauelewa wa kutosha na kama kweli wanafunzi wanafaulu kwa kufundishwa au kwa juhudi zao binafsi?
Na huo uwe sehemu ya hitaji kwa mwalimu kupandishwa cheo/ daraja.
Nawasilisha.

Hao NECTA wa kusahihisha hiyo mitihani iliyofanywa na walimu zitakuwa mashine za NECTA au walimu haohao? Au unakusudia NECTA iteue walimu wa shule za msingi ndio wasahihishe hiyo mitihani ya walimu wa sekondari? Au walimu wa sayansi wasahihishe mitihani ya walimu wa sanaa na lugha na kinyume chake? Kitaaluma mwalimu akishafuzu na kuthibitishwa hupaswa kuendelea kunolewa kupitia semina na paneli za masomo ambazo hukutanisha walimu wenye uwezo na ujuzi tofauti kwa somo husika. Mambo haya hayafanyiki kikamilifu na ndipo tatizo lilipo. Hivi prof anayevurunda kwenye utendaji wake naye arudi akafanye utafiti upya? Serikali iliporuhusu walimu wa mazingaombwe kusomeshwa mwezi mmoja na kukabidhiwa darasa unategemea upate matokeo gani hapo?

Nafikiri hujatambua uzuri nini cha kufanya ili kuboresha elimu yetu, vinginevyo una chuki na mwalimu wako fulani.
 
Wadau nimefuatilia kwa muda mijadala ya sababu za kushuka kwa elimu yetu na nini kifanyike. Katika mijadala hii lipo kundi la upande wa waalimu, watunga sera, wachambuzi wa sera, wazazi, waalimu nk.
Kila kundi limejaribu kuonyesha mapungufu ya upande fulani.
Wengi tumepitia shule na vyuoni na waalimu wetu tunawajua na wengine hata majina tumewapa kwa ufundishaji wao ama mzuri au mbaya.
Pendekezo langu ni kuwa kila NECTA wanapotoa paper zao za kidato cha 4 au 6 mwalimu wa somo husika afanye na darasa lake na usahihishwe na NECTA. Nia ni kuona kiwango cha waalimu husika cha waalimu wa masomo hayo kama kweli wanauelewa wa kutosha na kama kweli wanafunzi wanafaulu kwa kufundishwa au kwa juhudi zao binafsi?
Na huo uwe sehemu ya hitaji kwa mwalimu kupandishwa cheo/ daraja.
Nawasilisha.
U nahitaji kupimwa akili na uwezo wako wa kufikiri.
Kwa mini usingumzie in service training ingeboreshwa ktk idara ya elimu na kukimbilia Kufanya Nectar?
 
Apa umeandka pumba tuu, na mwalm akafaulu alaf wanafunz wote wakafeli mwalm atakua anao uwezo wa kufundisha? af we unafanya kaz gan?
 
kwanza unapaswa kutofautisha kufaulu na ufindishaji kwa sababu mwalimu kikawaida anatakiwa atoe mchango wa asilimia 30 tu zilizobaki ni mwanafunzi mwenyewe. kwa mfano nchi kama singapore wana policy yao ya teach less, Learn More hii ni nchi ambayo imeadvance sana kwenye swala la elimu na nchi yenye IQ kubwa maana hata mazingira yao ya kujifunza ni mazuri. sasa tujiulize tembelea shule moja wapo ya kata hapa mjini na nyingine kijijini je mazingira hayo ya kumpa mwanafunzi asilimia 30 yanaruhusu na 70 mwanafunzi atafute mwenyewe. baadhi ya watafiti wamegawanya mafanikio katika makundi yafuatayo. 30% mwalimu,50% mwanafunzi, 10% mzazi, na 10% serikali pamoja na mazingira kwa hiyo ukiangalia hapo mwanafunzi anatakiwa aweke bidii.

Mfumo wa Kumpata mwalimu USA na JAPAN Pamoja na nchi zingine zilizoendelea.

kwa hizo nchi kuwa na digrii ya education ni swala lingine na ufindishaji yaani teaching pia ni swala lingine, mfano marekani Kila jimbo linakuwa qualifications zake ili mtu afundishe na hakuna mtihani wa taifa, cha kwanza huwa wanahitaji minimum credit hours kutoka kwenye hiyo digrii yako ya education ambayo kwa baadhi ya majimbo ni 86, halafu baadae unatakiwa uwe cheti cha ufindishaji (teaching certificate) ambacho hutolewa na taasisi inayotambuliwa na jimbo husika hiki cheti cha kufundisha hupatikana kwa kufanya mtihani ambapo kuna vitu huwa wanapima hivyo pia jimbo linaweka kiwango cha chini kutoka kwenye hiko cheti, kwa mwalimu mwenye digrii au chini hapo huwa anatakiwa kurenew cheti chake kila baada ya mwaka kwa sababu wenyewe wanaamini mwalimu anapaswa aongeze maarifa kila siku, kwa mwalimu mwenye master degree na kuendelea huo mtihani wa kupata teaching certificate anafanya mara moja tu yaani anakuwa za kupata permanent teaching certificate.
hapa chini ni muundo wa mgawanyo wa maksi kwa ajili ya kupata teaching certificate kwa JAPAN
upload_2016-3-17_9-54-48.png

upload_2016-3-17_9-55-7.png

upload_2016-3-17_9-55-27.png

*Special Certificate-hiki ni cheti kwa ajili ya kuwavutia watu wa profesheno nyingine kufundisha
*Temporary certificate-hiki ni cheti kwa ajili ya wale walimu ambao bado hawajapata post kwa ajili ya kufundisha

Sasa kwa hii hoja yako ambayo umeweka hapa haisaidii kukuza hiyo elimu wala kufundisha kiujumla mfumo wa elimu tanzania ni mbovu na si rafiki kwa mtu wa kipato cha chini na pia mpaka sasa hatujui ni nini hasa tunachakitaka kutoka kwa hii elimu yetu yaani tunaangalia idadi ya watu kufaulu wa kwanza kapata ngapi au tunataka product flani itusaidie kutokana na matatizo yanayotuzunguka ndo maana mpaka leo tuna mainjinia wengi lakini toothpick tunaagiza toka nje. mfano wao marekani wana malengo yao kumi wanayoyataka toka kwenye elimu yao nitayaweka nikipata mda.
 
Attachments

  • upload_2016-3-17_9-54-12.png
    upload_2016-3-17_9-54-12.png
    18.9 KB · Views: 39
Wadau nimefuatilia kwa muda mijadala ya sababu za kushuka kwa elimu yetu na nini kifanyike. Katika mijadala hii lipo kundi la upande wa waalimu, watunga sera, wachambuzi wa sera, wazazi, waalimu nk.

Kila kundi limejaribu kuonyesha mapungufu ya upande fulani. Wengi tumepitia shule na vyuoni na waalimu wetu tunawajua na wengine hata majina tumewapa kwa ufundishaji wao ama mzuri au mbaya.

Pendekezo langu ni kuwa kila NECTA wanapotoa paper zao za kidato cha 4 au 6 mwalimu wa somo husika afanye na darasa lake na usahihishwe na NECTA.

Nia ni kuona kiwango cha waalimu husika cha waalimu wa masomo hayo kama kweli wanauelewa wa kutosha na kama kweli wanafunzi wanafaulu kwa kufundishwa au kwa juhudi zao binafsi?

Na huo uwe sehemu ya hitaji kwa mwalimu kupandishwa cheo/ daraja.

Nawasilisha.
Walishafanya mtihani wakafaulu ndo mana niwalimu..wewe unataka wafanye mitihani mingine ya nini tena
 
Bonge LA pumbaaaaaaaa!!! Shule haina maktaba.... Shule haina maabara... Shule haina vifaa vya maabara.... Shule haina vit vya wanagunzi... Madarasa mabovu..... Madarasa haryana madirisha..

Utegemee elimu bora hapo?? Wewe mtoa post ni pumba kabisaass
 
Mtoa post nasikitika kwakuwa bado hana ufahamu wa mambo mengi:
1.NECTA ni nani?
2.Lengo la mitihani ya sekondari ,msingi,na vyuo ni kumpima nani?
3.Nani anatunga mitihani ya NECTA?
4.Kama hujui kinachofundishwa utajuaje mwalimu hajui?
5.Mwalimu aliupataje ualimu bila kufaulu mitihani?
Jambo kubwa ni muhimu kwa mtoa post kuwa kama mwalimu aliyekuwa anamfundisha hakumwelewa sababu ni nyingi siyo kwamba halijui somo.(Fuatilia 1."HOW EFFECTIVE IS SUPPOSED TO BE",2.How effective learning occur?3. strategic teaching and Learning)
 
Mtoa post nasikitika kwakuwa bado hana ufahamu wa mambo mengi:
1.NECTA ni nani?
2.Lengo la mitihani ya sekondari ,msingi,na vyuo ni kumpima nani?
3.Nani anatunga mitihani ya NECTA?
4.Kama hujui kinachofundishwa utajuaje mwalimu hajui?
5.Mwalimu aliupataje ualimu bila kufaulu mitihani?
Jambo kubwa ni muhimu kwa mtoa post kuwa kama mwalimu aliyekuwa anamfundisha hakumwelewa sababu ni nyingi siyo kwamba halijui somo.(Fuatilia 1."HOW EFFECTIVE TEACHING IS SUPPOSED TO BE",2.How effective learning occur?3. strategic teaching and Learning)
 
Ni mwalimu mmoja tu amethubutu kusema mtihani uletwe ataufanya.
Kama mchango wa mwalimu ni 30% hizo kelele za umuhimu wa mwalimu ni za nini?
Walimu wachache sana ndio mahiri kwenye madomo yao. Wengi vilaza ile mbaya.
Wengi mnstakiwa kutubu sana kwa kuwaharibia vijana wetu maisha.
 
Maringeni ni miongoni mwa watu wasiyojielewa, kama mtu anamfundisha mwanafunzi na akafaulu itawezekanaje yeye mtihani huo afeli? unamaana anafundisha kitu kingine na mtihani kina tungwa kingine? Ili mtu aitwe mwalimu si ndiyo alifanya mitihani katika hatua mbalimbaii ndiyo akafaulu? ni kwanini basi kunatuhuma walimu wanawasaidia wanafunzi mitihani,sasa wanawasaidiaje wakati wenyewe hawajui? hivi ni serikali gani inaajiri watu wafundishe jambo watoto jambo wasilolijua?
 
Back
Top Bottom