Pendekezo: MSD wapate mshindani

Shiii Kaa kimya Hivi wewe hujui nyumba zetu ndo kwanza zipo kwenye kozi ya nne- hayo mambo yako ya ushindani yakija tuta fanya vipi finishing-Watu bwana
 
Shiii Kaa kimya Hivi wewe hujui nyumba zetu ndo kwanza zipo kwenye kozi ya nne- hayo mambo yako ya ushindani yakija tuta fanya vipi finishing-Watu bwana

najitahidi sana kufuatilia ufisadi wa msd nikipata ushahidi nitauanika hapa jamvini
 
Asilimia kubwa ya wagonjwa wanakwenda kwenye hospitali za serikali (umma) kupata matibabu aghalab huishia kuwaona madaktari na kisha kuandikiwa dawa, lakini wakifika kwenye dirisha la dawa lugha wanayokutana nayo ni kwamba hakuna dawa. Wenye fedha hununua dawa walizoandikiwa kwenye maduka ya dawa ya watu binafsi, tena yakiwapo ya hao madaktari wenyewe.

Hali hii ya kukosekana kwa dawa katika hospitali za serikali imekuwa ni kawaida, wananchi wamezoe na wengine hawalalamiki tena, hata hivyo, hali hiyo inaendelea wakati dawa za mabilioni ya fedha kila mwaka zinateketezwa baada ya muda wake wa matumizi kumalizika zikiwa zimehifadhiwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

Juzi Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilibaini kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imepata hasara Sh. bilioni 4.7 kutokana na dawa zilizonunuliwa na MDS kukaa bila kutumiwa na mwishowe zikaharibiwa, pia vifaa vyenye thamani ya Sh. bilioni 1.6 vilivyonunuliwa havikupokelewa, kwa maneno mengine ni vifaa hivyo ni hewa na vilivyonunuliwa kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011.

Ni vigumu kupata maneno ya kuelezea hali hii, kwamba kodi za wananchi zinatumika kununua dawa, kutoka kokote ndani au nje ya nchi, halafu zinarundikwa stoo wakati hospitali za umma zikizihitaji kwa ajili ya wagonjwa, lakini hazifiki na matokeo yake zinakaa hadi muda wake wa matumizi unafika ukomo hivyo kuharibiwa.

Hakika hali hii haina tofauti yoyote na mtu aliyechukua fedha zake na kuzichoma moto. Ni uharibifu mkubwa wa rasilimali muhimu zinazohitajika kwa ajili ya stawi wa watu wa taifa hili. Lakini pia ni haki na halali kabisa kueleza hali hii kama madudu mengine ya taasisi za serikali katika uendeshaji wa shughuli zake.

Kama alivyosema Mwenyekiti wa PAC, John Cheyo, kuwa wameshtushwa na madudu hayo kwa kuwa zipo hospitali zilizo hoi kutokana na kukosa dawa, lakini vitabu vya wizara vinaonyesha kuwa dawa za mabilioni ya fedha zimeharibiwa kutokana na kwisha muda wake wa matumizi. Wahusika wametakiwa kutoa maelezo ya kina.

Wakati madudu haya yakitokea, MSD wanalalamika kuwa wanakabiliwa na hali ngumu kwani wakati mahitaji ya dawa nchini kwa sasa yanafikia thamani ya Sh. bilioni 150 zikiwa ndizo fedha walizoomba serikalini kwa mwaka wa fedha wa 2011/12, ni kiasi cha Sh. bilioni 78 tu kiliidhinishwa, lakini hata hicho kidogo matumizi yake yamezingirwa na uzembe wa hali ya juu.

Habari zinasema kuwa kwa mwaka wa fedha unaokuja MDS wanatarajia kuwa mahitaji ya dawa na vifaa yatafikia kiasi cha Sh. bilioni 198, hali inayoonyesha kuwa bado suala la upatikanaji wa dawa katika hispitali za umma si wa uhakika kwani mahitaji ni makubwa kuliko kiasi cha fedha kinachotengwa. Ni miujiza tu itawezesha kupatikana kwa Sh. bilioni 198 kama bilioni 150 ilikuwa vigumu kuidhinishwa.

Pamoja na changamoto hii ya ufinyu wa bajeti, kila tunapotafakari hali hii ya kuharibika kwa dawa kwa sababu tu hazikusambazwa kwenye hispitali mbalimbali za umma nchini, tunashindwa kupata majibu ni kwa nini tatizo hili mwaka baada ya mwaka halimaliziki kwani hata mwaka jana kulikuwa na tatizo la kuharibika kwa dawa zenye thamani ya mabilioni kwa kuwa tu hazikusambazwa.

Kumekuwa na kurushiana lawama baina ya watendaji wa MSD na hospitali za umma juu ya hali hii. Wakati hospitali zikilalamika kuwa maombi yao yanapopelekewa MSD kumekuwa na urasimu wa kuyashughulikia, MDS nao wamekuwa wakilalamika kuwa maombi kutoka hospitali hizo yamekuwa yakichelewa mno, kiasi cha kuathiri utoaji na usambazaji wa dawa hizo.

Kwa vyovyote itakavyochukuliwa kuna tatizo la ama kiutendaji au kimfumo katika suala zima la usambazaji wa dawa kutoka MSD kwenda hospitali za umma; Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ndiyo msimamizi mkuu wa sera za afya katika nchi hii, ni aibu na ni jambo lisilokubalika kuona kuwa mwaka baada ya mwaka dawa zenye mabilioni ya thamani zinateketezwa huku wagonjwa wanaopatiwa huduma katika hospitali za umma wakizikosa kwa sababu tu hazijasambazwa. Ni kwa maana hiyo tunasema sasa hali hii ni lazima ifike mwisho.


CHANZO: NIPASHE
 
Kuna Ufisadi Mkubwa kwenye hi Wizara ya Afya. Ingelikuwa bora Maofisa wa hii Wizara ya Afya wajiuzulu hata Waziri Afya Mwenyewe ajiuzulu hafai kuongoza hii Wizara ya Afya na pia hafai kuwa Waziri wa Afya.
 
Nchi hii itakuwa hivi hadi lini ?! Watu maskini vijijini wanakufa kwa kukosa dawa na fedha za matibabu,huku dawa zinateketezwa kutokana na mfumo mbovu wa usambazaji !
Kisha wanapotokea watu wa kuwatetea inaibuka mijitu ileile miuaji,inavuruga akili zao na kuwafanya watetezi hao waonekane ndo wauaji.
 
aTaarifa hii ni ya jumla sana, maana unaposema ni dawa, vyema kujua ni dawa za kundi lipi. Maana binfsi ni mdau, na nimezunguka sana nchi hii katika zahanati, vituo vya afya, hospitali na kanda mbalibali za MSD, na kuna dawa nyingi zinazoexpire, hasa family planning pills mfano microgynon, lofeminal,n.k. Na pia kuna dawa nyingi za msaada ambazo huletwa nchini kwa program mbalimbali kama negeleted tropical diseases ambazo mara nyingi muda wake wa matumizi unakuwa umebaki kidogo sana. Hivyo ni vyema kama tukajua ni dawa zipi na program ipi, vertical au???
Tatizo lingine ni la uwasilishaji wa fomu za maombi ya dawa. Wizara ya afya kwa sasa (MSD) wanatumia mfumo wa "agiza dawa kulingana na mahitaji yako" yaani "intergetrated logistic system" (ILS). ni mfumo mzuri tatizo ni namna ya ujazaji maana wataalamu wengi huko vituoni si wafamasia, zinajazwa na nurse attendants au nurse midwifery ambao wengine hawajapata mafunzo ya ILS, unamuuliza kwa nini hujapata dawa, anakuambia ni MSD hawajaleta dawa, ukimwambia nionyeshe form ya maombi (R&R) atakuambia sijajaza au kajaza lakini kimakosa, na ikumbukwe Mfumo wa ILS kituo kinapata dawa kila baada ya miezi mitatu, akikosa mzunguko wake atapata baada ya miezi mingine 6. Kwa sasa hasa kwa dawa za ukimwi, malaria na nyinginezo zinazofaadhiliwa na global fund, kuna wataalamu kila kanda ya msd wanaofanya kazi kuisaidia MSD kimfumo. Kwa dawa hizo zinazoeexpire ni chache na zina maelezo yanayojitosheleza.
 
Ndugu waziri dawa ya kusafisha na kuwa na mfumo mzuri kiutendaji amini usiamini ni ku OUTSOURCE wataalamu kutoka nje.
Ghana, pia Marekani inaweza tutusaidia kutupa wataalamu wa logistics. wataalamu wetu wawe wasaidizi. Tazama John Snow Inc. invyofanya kazi nzuri ya kutrack dawa zao za misaada hasa mseto.
otherwise yule mama wa quality control pale msd na wengine wanaofahamika wataendelea kuhujumu tu.
 
Umetoa dawa bila kufanya tathimini ya chanzo na asili ya tatizo...
 
Dawa zote zilizopo Tanzania haina ubora wowote. Nyingi ni chokaa, ndio maana waTanzania wanakufa sana. Madawa haya yamechakachuliwa ile mbaya. Akina mama wanasema zamani mtoto akipewa dawa kuna harufu kwenye jasho, mkojo nk, lakini siku hizi hata alishwe ampicillin 10 hamna kiti.

Ufisadi MSD ni mauti yetu
 
Du haya mkuu you have already made your conclusion. Anyway MSD IS A GOVERNMENT ORGAN OPERATING UNDER IT'S MICROSCOPE.

doesn't matter how MSD is operating,what we need is results!MSD wanatumia hela kufadhili timu za mpira kwa nini hatuna dawa?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
sasa tunahotaji mshindani wa mshitiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…