meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,464
- 4,832
Mkuu kwani MSD inafanya biashara na serikali pekee? Mbona hospitali au halmashauri zina uwezo wa kununua dawa kupitia vyanzo vyake wakati wanasubiri fedha kutoka serikalini, lakini kinachotokea ni kukosekana kwa dawa hapo MSD dawa ambazo ukienda maduka binafsi unazipata.Nitawatetea MSD kwa hili:
Kwa miaka zaidi ya 6 kiwango kinachotengwa na serikali MSD kwa kila kituo kimekuwa kilekile. Hiyo haizingatii mfumko wa bei za dawa uliopo na ongezeko la watu.
Km toka 2006 kila zahanati hupelekewa msd 1.2m kwa kila robo mwaka. Hiyo 2006 angalau kiasi zilitosha,lakini sio sasa. Mfano 2006 tabs Quinine 1000T ilikuwa 30,000/= hivi sasa ni zaidi ya 80,000/= (ongezeko la 267% ! ).
Mwisho wa siku utakuta kituo kinadaiwa zaidi ya 10m msd. Hapo kitaendelewa kuletewa dawa kwa "huruma" ya MSD tu.
All in all kwa hali hii hata akija mbadala wa MSD tatizo litabaki palepale endapo serikali haitalipa madeni na kuongeza fungu.
Meningitis,Mkuu kwani MSD inafanya biashara na serikali pekee? Mbona hospitali au halmashauri zina uwezo wa kununua dawa kupitia vyanzo vyake wakati wanasubiri fedha kutoka serikalini, lakini kinachotokea ni kukosekana kwa dawa hapo MSD dawa ambazo ukienda maduka binafsi unazipata.
Mkuu ni kweli, ila bado nailaumu serikali, hivi hizo bilioni ngapi inazodaiwa ingezitupia pale MSD, kusingekuwa na mabadiliko ya hizo OS Items zinazozidi IN items kwa sasa?Mkuu kwani MSD inafanya biashara na serikali pekee? Mbona hospitali au halmashauri zina uwezo wa kununua dawa kupitia vyanzo vyake wakati wanasubiri fedha kutoka serikalini, lakini kinachotokea ni kukosekana kwa dawa hapo MSD dawa ambazo ukienda maduka binafsi unazipata.
MSD inafanya biashara na wala haitoi huduma tuache ujanjaujanja wa maneno.Meningitis,
Maoni yako ya kutaka MSD ipate mshindani ni dhahiri kwamba yamejikita katika mtazamo wa kibiashara ambapo msingi mkubwa ni Faida. Usichoelewa ni kwamba msingi wa MSD ni kutoa huduma na kujiendesha. Huyo mshindani unayemtaka unategemea atapata faida kwa kupeleka dawa na vifaa Tiba Nambendo au kwa kupiga panga pesa za dawa zinazotengwa na hazina Kwa mtindo Wa EPA? Fikiria hakuna aliyekatazwa kupeleka dawa na kuziuza Kokote nchini mbona sioni famasi Buhemba au Kiterere?
Mkuu usiimbe wimbo wa wafanyabiashara ya dawa utaua watanzania walio maskini ambao huwaoni kwa kukaa mjini.
"MSD might not be efficient but your visibility of a solution from your suggestion is Myopic big time" ipecacuanha
Nitawatetea MSD kwa hili:
Kwa miaka zaidi ya 6 kiwango kinachotengwa na serikali MSD kwa kila kituo kimekuwa kilekile. Hiyo haizingatii mfumko wa bei za dawa uliopo na ongezeko la watu.
Km toka 2006 kila zahanati hupelekewa msd 1.2m kwa kila robo mwaka. Hiyo 2006 angalau kiasi zilitosha,lakini sio sasa. Mfano 2006 tabs Quinine 1000T ilikuwa 30,000/= hivi sasa ni zaidi ya 80,000/= (ongezeko la 267% ! ).
Mwisho wa siku utakuta kituo kinadaiwa zaidi ya 10m msd. Hapo kitaendelewa kuletewa dawa kwa "huruma" ya MSD tu.
All in all kwa hali hii hata akija mbadala wa MSD tatizo litabaki palepale endapo serikali haitalipa madeni na kuongeza fungu.
Mkuu,meningitis,
Inaonekana hujafanya utafiti kwani ulipaswa kujua kuwa 'NHIF' ina enjoy monopoly market kwani wateja wake ambao wote wapo katika ajira za taasisi za serikali hawana option ya kuhamia katika bima zingine kama AAR n.k
NHIF nayo katika huduma ina mapungufu yake kama vile doctors kulazimika ku prescribe dawa zile tu ambazo zipo kwenye list ya NHIF, hata kama siyo preference ya daktari husika.
MSD haifanyi retail business hivyo haiwezi kufungua viduka vidogo vijijini.
Ni kweli MSD inatoa huduma make mwaka jana katika baadhi ya mikoa ilianza kupeleka dawa moja kwa moja (direct delivery) vijijini badala ya kuishia wilayani kwa DMO's ambako kulikuwa na ucheleweshaji. Hata hivyo, inasemekana kuwa hiyo direct delivery siyo economically justifiable kutokana na uduni wa miundombinu vijijini na huenda serikali isifidie gharama hizo ipasavyo lakini MSD inalazimika kupeleka vijijini ili kutoa huduma.
Je, ni wafanyabiashara wangapi wako tayari kufanya kazi ya hasara?
Tatizo ni serikali kwa kiasi kikubwa ila nadhani MSD nao wana some share of spoilTatizo si MSD bali ni serikali yenyewe. Ni kweli kuwa hospitali zetu na zahanati pamoja na vituo vya afya havina dawa muda mwingi na vifaa tiba, au havipati kwa wakati, lakini tatizo ni serikali kutokulipa madeni kwa wakati.
Serikali kuu ina tatizo katika kupeleka hela kwa wakati katika maeneo yote. Hata halmashauri hazipati ruzuku kwa wakati lakini kwa kutumia ubunifu zinaweza kutekeleza miradi mbalimbali. Sasa kwanini MSD ilalamikie jambo hilo kama ndio tatizo la wao kutoa huduma mbovu?tatizo ni serikali kwa kiasi kikubwa ila nadhani MSD nao wana some share of spoil