Pendekezo: Mahakama ya mafisadi ianze na kashfa hizi

Pendekezo: Mahakama ya mafisadi ianze na kashfa hizi

Usiwe mwoga, umeamua kuyavulia nguo yaoge. Kuna moja ya hujamtaja mhusika! Kufa kwa unaloliamini, mtaje tu; na ukimtaja hulali nyumbani leo! Uwe Aboud Jumbe, amekufa bila kuteteleke kama akina bakari mwapachu, alivuliwa vyeo vyote na amefia kwa anachokiamini
Naomba unisaidie kutaja kaka
 
Yani Mkulu anaendelea na mambo yake mengine kama vile kavaa miwani ya mbao! kutwa kufukuzana na vijipu uchungu tu
 
Hapo kuna kesi hazitafika mahakamani kwani nchi itayumba....hizo za Lugumi ,escrow nk nk....wale wanaopaswa kutolewa kafara tu ndy kesi zao zitatangulia kwy mahakama hii mpya ya mafisadi
 
Kutokana na kuwa na mtaji wa kianzio cha kesi tusihangaike na kutafta nyingine tuanze na hizi hapa

1.Richmond hasara ya 350 billions
Kashfa hii inamuhusisha waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa, ambaye kustaafu kwake kumelazimishwa kutokana na kashfa hii. Hii ndo kashfa iliyoshika nafasi ya juu kwa kuwa imeangusha mpaka serikali husika.

2.ESCROW hii ni kashfa iliyoshirikisha watu viongozi mbali mbali na mapadree, 300 billions, hii kashfa ina kutokueleweka ndani mwake maana kila taasisi ilitoa Maelezo tofauti
IKULU: Pesa za ESCROW si za serikali.

BUNGE: CCM wanasema si za serikali, CHADEMA wanasema kuna ambazo ni za wananchi/serikali.

MKAGUZI MKUU: Hajui jibu sahihi alimalizia kwakusema zinaweza kuwa au zisiwe za wananchi

3. Lugumi : hii imetikisa sana na bado hatujajua itaisha vipi na wahusika wakuu ni LUGUMI na washirika wake,

4. EPA, hii imeshika nafasi ya nne , wahusika walirejesha hela kimya kimya bila hata kujua ni kina nan,

5. Upotevu wa makontena bandarini ,

6.KAGODA, hii kashfa imetokea wakati wa uongozi wa mzee MKAPA lakin inadhaniwa kuwa imeisha kimya kimya,

7. NHC, uuzwaji wa nyumba za serikali miaka ya 1996 ambaye alihusika ni waziri mkuu ambaye alishirikiana na wahusika kukamilisha suala ilo,

8. SUKARI sakata ili lilinuhusisha bwana IDDI SIMBA ,Sukari kutoka nje tani za kutosha zilikwapuliwa kipindi hicho

9. UCHOMAJI WA BENKI KUU NA KUPORA , suala Ili wahusika wanajulikana na huwa hawatajwi sana sana,

10. ATCL, sakata la ATCL na ununuzi wa vifaa hewa , ukarabati hewa wa ndege na wafanyakazi hewa ,

11. MEREMETA,

12. AICC ARUSHA

13. UUZWAJI WA VIWANJA VYA SERIKALI KINYUME

14. UKWAPUAJI WA RANCHI ZA SERIKALI

15. UKWAPUAJI WA HELA ZA MRADI WA MAJI,

16. MAJENGO PACHA YA B.O.T BY LIYUMBA

17. MAJENGO YA UVCCM Mizengwe katika ujenzi

18. UNUNUZI WA MVUA YA THAILAND

19. UNUNUZI WA MAGARI MABOVU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

20. UTOROSHAJI WA TWIGA KWENYE NDEGE,

21. UNUNUZI WA RADA,

22. NDEGE MBOVU YA RAIS,

23. MELI MBOVU YA B/MOYO

24. UKARABATI WA NYUMBA YA UBALOZI KWA MABILION YA HELA , KWA UDANGANYIFU,

25. WIZI WA B.O.T. 1998

26. UUZWAJI WA MAGARI YA SERIKALI KINYEMELA

27. LOAN BOARD ,

28. UDA , ushahidi wa kutosha upo na Simon group wamehusika sana

Tanzania ina kesi nyingi sana zinazohusiana na uchafu wa ufisadi, hebu nawe ongezea nyingine
Asante Mkuu wana JF tuongeze maswahiba mengine pasipo kujali itkadi tuwe na double standard kama mleta Thread hapa juu ndiyo tuta heshimiane siyo nita walinda haitoshi .
Kesi zingine hizi hapa;
29. Ubinafisishaji pasipo kuwa na sheria za ubinafsishaji, kama kubinafsisha Benki ya NBC,General Tyre,Mount Meru Hotel,Sabasaba,Embassy Hotel,Migodi MKataba miaka 100,..n.k.
30.Meno ya Tembo
Tukiweka orodha vizuri hata Mkuu wa kaya haponi hata mmoja haki ya Mungu ninaapa...haya twende..
 
Kuongezea na hizi
1. NGOs za kitapeli zilizovuna mabilioni ya fedha kutoka nchi wahisani kwa kisingizio cha
kuwajali yatima na wajane
2.Dawa feki za ukimwi zilizopewa wagonjwa na huku wahusika wakijua ni batili.
3.Kashfa ya Diploma za form four Dodoma University
4.Bima za Afya zisizotoa matibabu
5.Nyumba za ibada zilizogeuzwa miradi ya wajanja
 
Uda

Nyumba za serekali

Escrow

Utoroshwaji wa twiga

Meli ya Bagamoyo

Samaki/....

Richmond

Lugumu


Magu awez kugusa kitu hapo
 
Back
Top Bottom