Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,761
- 165,353
Nachukua nafasi hii kumsihi na kumuomba mh Zitto aombe radhi uongozi na wanachadema wote kama alivyofanya Dr. Kitila Mkumbo iwapo kuna makosa kweli kayafanya na yanastahili adhabu ya kufukuzwa yeye na mwenzake De. Kitila.
Halikadhalika, viongozi na wana-CHADEMA wote tunapaswa kuwasamehe kwani wao ni binadamu na isitoshe ni watu ambao wameendelea kuonyesha mapenzi yao kwa chama hata baada ya chama kuwatuhumu hadharani.Jamani huu ndio uungwana.
Vile vile mh.Mbowe, ili kukinusuru chama na propaganda chafu za wana-CCM na vibaraka wao achana na mpango(nia) ya kugombea uenyekiti na badala yake simamia kuna chama kinapata mrithi wako atakaetufikisha watanzania katika ile nchi ya "ahadi".Uamuzi huu pia utanusuru chama chetu.
Viongozi wa CHADEMA na wengine wenye ushawishi ndani ya chama mshaurini mh.Mbowe kuachia nafasi hiyo kwa wengine na hata ikibidi kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya chama kirudishwe katika katiba ya chama.
Wana-CHADEMA tunapaswa kujiuliza ni watanzania wangapi wamepoteza maisha yao,kupata vilema,kuwekwa ndani na hata kufungwa jela wakitetea harakati za kupigania ukombozi kupitia CHADEMA.
Mwisho,tutambue kuwa "vita vya panzi, furaha ya kunguru"
Watanzania tumechoka na CCM na tegemeo letu ni CHADEMA tu.