Pendekeza jina jipya la timu yetu ta taifa..."taifa stars"

Pendekeza jina jipya la timu yetu ta taifa..."taifa stars"

only83

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
5,342
Reaction score
2,528
Katika siku za karibuni kuwekuwepo hoja kuwa jina la timu yetu ya Taifa libadilishwe, hii inatokana na wadau wengi wa michezo kuhoji kwanini tusiwe na jina linaloakisi baadhi ya rasilimali zetu au chochote ambacho ni tamaduni yetu mfano Rwanda wao wanaitwa AMAVUBI( Manyuki), Kenye wao wanaitwa HARAMBEE STARS( Hii inatokana na umaarufu wa harambee kule Kenya hasa kwenye kuchangia maendeleao), Cameroon wao wanitwa INDOMITABLE LION( Simba wasioshindika) nk....na hoja hii haikuanza leo, ilianza tangu Maximo akiwa kocha wa timu hii...mfano Maximo alipendekeza Taifa Stars iitwe "The Blues of Africa".

Hoja hii pia iliungwa mkono na TFF siku za karibuni kupitia kwa katibu mkuu na hapa namnukuu alisema...." ............Sioni tatizo kama wadau wanapenda jina la timu yetu libadilike, sisi tuko tayari kuanzisha huo mchakato..."

Je, wewe kama mdau wa michezo na hasa soka ungependa Taifa Stars iitwe jina gani badala ya hili lasasa? PENDEKEZA JINA LAKO.
 
Jk 11 kama ilivyozoeleka. Siongezi kitu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Timu hii iitwe: 'Itwe Lya Nsaji' maana yake 'Li Kichwa La Mwenda Wazimu' kwa vile ni utamaduni wetu kufungwa kila tukicheza na timu nyingine, hata Mwinyi alidai timu yetu ni sawa na kichwa cha mwenda wazimu ambapo kila kinyozi hujifunzia kunyoa. Nadhani hili ni jina stahili, tukibadilika, tutabadilisha jina pia.

ONYO:
Wenye pressure jichungeni msije mkafa bure! Haya ni maoni yangu na hapa ni JF where we dare to talk and write openly!
 
Iitwe Rift valley (Bonde la ufa) stars, maana tumezidi ukibonde.
 
Ata ikkiitwa MKUYATI STARS si mbaya wachezaji wetu wanaweza uzinzi kuliko kipiga kandanda la uhakika.
 
Haaahaaa duh si mchezo, watu mmepinda! Majina ni mengi mno, Simba wa Serengeti,Kilimanjaro Squad, Mashujaa wa Tanganyika, Mashujaa wa Serengeti, kama bado kuna ule muungano feki tunaweza kuwaita Kunguru wa Zanzibar!
 
Back
Top Bottom