Pendekeza jina jipya la timu yetu ta taifa..."taifa stars"

''kakakuona stars'' jina hili linaweza kuleta bahati ya timu yetu kupata ushindi; kwani kwenye technical ni sufuri hivyo hatunabudi kuviziavizia bahati.
 
kwa jina naitwa Gang Chomba napatikana JF kila siku...
Napendekeza timu ya Taifa iitwe Zigo la Nnya...
 
Jaman wana jf tujaribu kuchangia majina mengi ili lichaguliwe moja. Napendekeza mengine. Naomba kama itawezekana basi iitwe MAKABURI YA MV BUKOBA. AU MABWEPANDE.
 
Katika siku za karibuni kuwekuwepo hoja kuwa jina la timu yetu ya Taifa libadilishwe, hii inatokana na wadau wengi wa michezo kuhoji kwanini tusiwe na jina linaloakisi baadhi ya rasilimali zetu au chochote ambacho ni tamaduni yetu mfano Rwanda wao wanaitwa AMAVUBI( Manyuki), Kenye wao wanaitwa HARAMBEE STARS( Hii inatokana na umaarufu wa harambee kule Kenya hasa kwenye kuchangia maendeleao), Cameroon wao wanitwa INDOMITABLE LION( Simba wasioshindika) nk....na hoja hii haikuanza leo, ilianza tangu Maximo akiwa kocha wa timu hii...mfano Maximo alipendekeza Taifa Stars iitwe "The Blues of Africa".

Hoja hii pia iliungwa mkono na TFF siku za karibuni kupitia kwa katibu mkuu na hapa namnukuu alisema...." ............Sioni tatizo kama wadau wanapenda jina la timu yetu libadilike, sisi tuko tayari kuanzisha huo mchakato..."

Je, wewe kama mdau wa michezo na hasa soka ungependa Taifa Stars iitwe jina gani badala ya hili lasasa? PENDEKEZA JINA LAKO.
kwa nini isibakie tu kuitwa timu ya Taifa ya Tanzania, kwani si jina tosha?

Kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo mnavyozidi kuwaona waasisi wa Taifa hili walikuwa wajinga kwani mnataka kubadilisha kila kitu walichokianzisha bila hata ya kuelewa walianzisha hivyo vitu kwa lengo gani, alianza Mkapa akaanza kuuza Dhahabu kwa maana mliwaona walioasis taifa letu na kuweka hizo sera wajinga, mkaja kubadilisha sera ya ardhi kuwauzia wazungu na sasa mnataka hata kubadilisha jina la timu yetu ya Taifa!

Hivi kuna jina ambalo linaweza kuwa na maana kwetu zaidi ya hilo la Taifa? Umeshakaa na kutafakari hata kidogo waasisi waliita timu yetu hivyo walikuwa na maana gani?
Halafu katika woote unamtaja mtu kutoka Brazil Maximo, ajabu sana Maximo anajua nini kuhusu sisi na nchi yetu, anajua hata maana ya neno Taifa? na kuna uhusiano gani kati ya Timu kufanya vizuri na jina la timu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom