Kwa hiyo mtindo huu ndo utaisaidia CUF kuingia madarakani?
Ulitaka wafanyeje ili ujue hawapendi kinachofanyika?Kwa hiyo mtindo huu ndo utaisaidia CUF kuingia madarakani?
View attachment 334432
#Pemba.
Wanachama wa CUF Wilaya ya, Majimbo yote matano (Wete, Kojani, Mgogoni, Mtambwe na Gando) leo wameafikiana ktk kikao chao kuendelea na mgomo rasmi juu ya CCM kwa mambo yote ya kijamii ikiwemo Arusi,Misiba,Biashara, Ugonjwa na hata magari na meli na kuazimana vitu/vfaa vya majumbani nk. (CUF kwa CUF na CCM kwa CCM tu mpaka kieleweke)
"Mikutano ya Matawi kwa sheiha zote za Wilaya ya Wete itafanyika kwa uhamasishaji zaidi, katika hatua hio bila kujali uzawa/udugu, din...i, kabila au tunapo toka.
Tumekubaliana kama aliefiliwa ni CUF mmoja au wawili au idadi yeyote basi kuungana nae ni kutokwenda kwenye msiba huo uliowakuta wana CCM waliomo ndani ya familia yake.
HAYO TUME KUBALIANA"
Alisema mmoja wa wafuasi hao wa CUF.
Umenena ukweli mkuu. Politicians wakitanzania wengi wao ni wanafiki sana. Hata wabunge wakiwa bungeni na hasa wakiwa live mapovu huwatoka lakini ukiwakuta usiku wanakula kuku choma mitaa ya DOM wakifurahia na dada Poa.mambo ya kijamii yasiharibiwe na uamuzi wa wachache ambao family zao zimehamishiwa ughaibuni. Wapemba wawe na subira usuluhishi wa sintofahamu hii utapatikana soon.Sasa nyie wananchi wa Pemba mkifanyiana hivi mnamkomesha nani?
Wanasiasa wanaendelea na maisha yao Maalim akiumwa Shein anamjulia hali wewe babu yako akifariki auendi kumzika kisa ni mwana ccm.
Huko Mungu yuko chini siasa iko juu, eti nimtelekeze mzazi wangu mtoto wangu ama Dada yangu kisa siasa, hiyo siasa nilizaliwa nayo ama nimeikuta tu. Kilichofanywa na CCM huko Zanzibar ikishurikiana na tume ya uchaguzi si cha kuungwa mkono, ila hunigombanishi na ndugu zangu sababu tu mapenzi yao kisiasa ni tofauti na mimi. Alafu pembeni nadai haki nada Demokrasia nini sasa maana ya haki nini maana Demokrasia, eti alafu uneanda msikitini mara tano, huku kifua kimejaa chuki, wanaojifanya wanaijua dini ndiyo watenda dhambi wakubwa.Siasa za chuki zimerudi tena kama awali hii miaka 10 ilopita ndivyo waliviyokuwa wakiishi, imam akiwa CCM , wa C.U.F. haingii kuswali, Sijajua hawa watu wanamuabudu mungu yupi kwakweli alieagiza kuwatendea majirani mambo hayo, naomba hizi habari zisiwe za kweli.