PCCB Iliharibu Yenyewe Kesi ya Idd Mohamed Simba

PCCB Iliharibu Yenyewe Kesi ya Idd Mohamed Simba

masanjagama

New Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
1
Reaction score
3
Nilisikitika sana kusikia Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Dr Edward hosea akilamimika hasa kuhusu serikali kumfunga mikono, na kuisingizia ofisi yetu tukufu ya DPP kuwa inakalia majalada ya kesi ya ofisi yake hivyo kumkwamisha. mimi nikiwa mtumishi wa ofisi ya DPP ambaye nimefanya kazi hapa kwa muda wa miaka kumi (nimeanza kabla Hosea hajawa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU) watu wa nje ya mfumo wanamuona Dr Hoseah ni muadilifu sana lakini watu tuliyefanya naye kazi tunamjua kivingine, naomba nitoe mfano wa kesi ya Idd Simba na kama watu wengine wanabisha nitaweka mifano mingine halisi hapa janvini, natoa ukweli ambao mtu yeyyote anayetaka anaweza kuuchunguza, sisi tumechoka kushambuliwa kwenye vyombo vya habari wakati yeye mweyewe ndiye anayeharibu kesi zake.

Mashitaka waliyoyaleta PCCB ni pamoja na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kuuza hisa za UDA bila kufuata utaratibu wa ushindani na bila kuihusisha serikali na halmashauri ya jiji. Shitaka la kwanza la kusababisha hasara lilihusu TSH 320,000,000/= zilizolipwa katika account ya ndugu Idd Mohamed Simba na ndugu ROBERT KISENA na kosa la pili ni kusababisha hasara ya TSH 8,422,000,000/= kama hisa hizo zingeuzwa kwa ushindani. Msingi wa shitaka la kusababisha hasara ya TSH 320,000,000/= lilitokana na maelezo ya ROBERT KISENA kuwa alilipa fedha hizo katika account ya ndg Idd Simba namba 0210001002 iliyopo BENK M kama sehemu ya malipo ya hisa.

Makosa waliyofanya PCCB chini ya Hosea kwa kukusudia
katika hati mojawapo ya malipo ya tsh 250,000,000/= kutoka katika kampuni ya robasika Agro Product Ltd kwenda kwenye account ya Idd Simba iliyoko benk m, NDG ROBERT KISENA aliandika uongo kuwa kilikuwa kinalipwa kwa gharama ya usafiri. Hii ilikuwa inamfanya Robert kisena ambaye TAKUKURU walitaka awe shahidi wao na yeye kuwa mtuhumiwa kwani kama alikuwa hausiki na wala hajui kuwa anafanya wizi kwa nini aandike sababu za uongo kwenye hati ya malipo?, lakini hata hivyo TAKUKURU waliiondoa hati hiyo na walipotakiwa wailete imbatanishwe katika jadala la kesi walikataa, hata walipotakiwa kuleta jalada halisi (original) la kesi ili ofisi ya DPP ikague yenyewe walikataa.

Ofisi yetu ya DPP ilikuja kugundua baadae kuwa Robert kisena hakuishia kuhusika tu katika malipo hayo ya rushwa kwa ndg Iddi Simba lakini baadaye ilibainika kuwa alishiriki kumpa rushwa mkaguzi Neema Kiule ambaye ukaguzi wake ulizipatia thamani ndogo hisa za UDA ili Robert Kisena atakapokuja kununua ainunue kwa bei ndogo.

Ofisi ya DPP ilipogundua hivyo iliiagiza TAKUKURU imuongeze ndg Robert katika orodha ya watuhumiwa ili na yeye ashitakiwe pamoja na wengine kwani katika issue hii yeye ndiye aliyekuwa king maker (mtoa rushwa na mnunuzi katika bei ya chini) na bila kumuunganisha yeye serikali ingeshindwa kesi kirahisi. Pamoja na maagizo hayo TAKUKURU ilikataa kata kata kumuongeza na wala kumuita mahakamani, mtuhumiwa huyu hakufikishwa mahakamani tarehe 04/06/2013 kesi ilipohairishwa na hata tarehe 19/06/2013 kesi ilipoondolewa mahakamani. PCCB imeelekezwa imuchukue maelezo mtuhumiwa huyo na ichunguze kuhusika kwake kikamilifu na maelezo yake yaambatanishwe katika hati za mashitaka katika kesi hii, ikulu, mwanasheria mkuu, waziri wa sharia, dci pamoja na usalama wa taifa viimeelezwa sababu za kutoa kesi hii mahakamani.

Nyuma ya pazia.
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Dr Edward Hosea alishapewa tsh 300,000,000/= na ndugu Robert Kisena, na kumuhakikishia kwamba hatamujumuisha kwenye watuhumia na atamtumia kama shahidi, ndiyo maana anasita kufanya kitu amabacho kinaonekana dhahiri.

Kwa nini TAKUKURU inamlinda kingmaker wa deal hili ndg Robert Kisena kiasi cha kukataa kumjumuisha katika orodha ya watuhumiwa wa sakata hili? Hosea alijibu kwanza swali hili kabla hajaanza kulalamika hovyo na kusingizia taasisi nyingine kuwa ndio zinamzuia kufanya kazi vizuri.
 
Nyuma ya pazia.
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Dr Edward Hosea alishapewa tsh 300,000,000/= na ndugu Robert Kisena, na kumuhakikishia kwamba hatamujumuisha kwenye watuhumia na atamtumia kama shahidi, ndiyo maana anasita kufanya kitu amabacho kinaonekana dhahiri.

Hapo ndo paanze kuchunguzwa. Hivi hakuna chombo kingine cha kumchunguza huyu Hosea. Maana kama yeye ndo mkurugenzi wa PCCB basi tusitegemee kujichunguza mwenyewe. Kama DPP anayomamlaka ya kufanya uchunguzi na kumshtaki mtu kwanini tusianze naye na kisha kukailisha utaratibu wa kuwashitaki tena hawa wazee wa UDA.
 
Bwana Masanjagama hapo unatudanganya kama upo ushahidi wa Hosea kuchukua fedha tunaomba taarifa hizo uzitolee ushahidi kwa Katibu Mkuu kiongozi Ikulu kwani ndiye mwajiri wa Hosea
 
Wezi kama hawa wanaachiwa kiurahisi sana, lakini kesi za kijinga ndo wanazishikilia, hii CCM itoke tu, tuwape hata TLP bana!
 
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Dr Edward Hosea alishapewa tsh 300,000,000/= na ndugu Robert Kisena, na kumuhakikishia kwamba hatamujumuisha kwenye watuhumia na atamtumia kama shahidi, ndiyo maana anasita kufanya kitu amabacho kinaonekana dhahiri.
Kwa nini TAKUKURU inamlinda kingmaker wa deal hili ndg Robert Kisena kiasi cha kukataa kumjumuisha katika orodha ya watuhumiwa wa sakata hili? Hosea alijibu kwanza swali hili kabla hajaanza kulalamika hovyo na kusingizia taasisi nyingine kuwa ndio zinam
 
UHUSIANO WA KIBIASHARA KATI YA ROBERT KISENA na RIDHIWANI KIKWETE
1. uhusiano wa kibiashara kati ya Ridhiwani Kikwete na Robert Kisena ..yamekuwa yakiongelewa kwa muda sasa....kuanzia kwenye ununuzi wa pamba [kisena akilaumiwa kuwapusha mzani wakulima]...hadi biashara ya kupeleka mafuta migodini...na uchakachuaji wa mafuta.....katika hali inayoendelea ni wazi kila mtu atajiuliza Robert Kisena ni nani hadi aweze kumilikishwa UDA ...Kwa kiasi cha shilingi milioni 250 tu.....

Ukizingatia mali zinazohamishika na zisizohamishika...za mabilioni ya shilingi ..ikiwemo yard kubwa sana jirani na bandarini.........imeshangaza sana kuwa uda inauzwa asilimia 52% kwa bilioni 1.4 ,Robert anatoa 250 million na anapewa ..haki zote....tena bila kufuata taratibu za Public Procurement...nani hapa ameona tangazo la UDA kutafuta mbia ..na taratibu zimefuatwa???

Tunapenda kuwa na wawekezaji wazawa lakini ..kitendo kinachodhaniwa kufanywa na mtoto wa rais kupenyeza rafiki zake kama kivuli cha kujimilikisha UDA hakikubaliki kabisa ...kwani kila mtu anajuwa uhusiano wa kibiashara kati ya Robert na Ridhiwani ...hii ilipelekea hadi kwa ushawishi wake Roberty akapitishwa kugombea Ubunge Maswa ..hata baada ya kushika nafasi ya tatu nyuma ya Shibuda,na Joseph......hii ilipelekea CCM ...Kupoteza jimbo...serikali ya kishkaji
!


UDA yauzwa kwa bei chee, Ofisi zake Zavamiwa - Page 4


MGOMBEA WA CCM AMPIGA OCD,RIDHIWANI AMDHAMINI......


"Mgombea huyo (Kisena) ametiwa nguvuni kutokana na mzozo wake na OCD wa Maswa juzi kituoni hapo na kumpiga OCD," alisema Kamanda Siasi, ambaye mwishoni mwa wiki alikaririwa akisema kuwa suala la shambulizi hilo ni la OCD Ndunguru na si Jeshi la Polisi na kufafanua kuwa ofisa wake ndiye aliyetakiwa kuamua au kutoamua kumshtaki mgombea huyo kwa tuhuma hizo za kufanya jinai.

Akizungumza kwa njia ya simu siku ya tukio, OCD Ndunguru alisema mgombea huyo wa CCM aliyeambatana na viongozi wa chama hicho walifikika polisi na kuuliza mahali alipo Shibuda, lakini kabla ya kujibiwa Kisena alimrukia OCD na kuanza kumshambulia kwa mateke kiasi cha kumuangusha chini.

"Alinirukia na kunipiga," alieleza OCD, lakini 'bosi' wake, ambaye ni Kamanda Siasi, akasema kuwa "Suala la Kisena na OCD ni jambo la kawaida kiutendaji na wala siwezi kulizungumzia... kwa sasa hapa ninashughulika na suala zito la mauaji



THE driver of the Chama Cha Mapinduzi (CCM) parliamentary aspirant for Maswa West Constituency, Mr Steven Kuilasa (16), was attacked and killed on Friday by Chadema supporters. The deceased was the driver of Maswa aspirant Mr Robert Kisena.
Mwekezaji mpya UDA lawamani

Meneja Uda aliyesimamishwa kazi amjibu Meya Masaburi

Meneja wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), Victor Milanzi, aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma za ubadhirifu , amekanusha kuhusika na ubadhilifu wa Sh.millioni 200 zilizopotea na badala yake amemtaka Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, alisema Masaburi anaficha ukweli kwa sababu anashirikiana na mmiliki wa Kampuni ya Simon Group Robert Kisena kumchafua ili malengo yao yatimie."Meya Masaburi akishirikiana na wamiliki wa Simion Group ambao ni vigogo mbalimbali akiwemo Waziri wa muda mrefu wameapa kuichukua Uda kwa nguvu ili waigeuze Container Terminal ili kukidhi matakwa yao binafsi," alisema Milanzi.Milanzi alisema Meya Masaburi aliitisha kikao Juni 10 mwaka huu na kubariki maamuzi ya bodi ya Uda kwa kufanya kikao na mmiliki wa kampuni ya Simon Group huku akijua kuwa bodi ilikosea kwa kuwa ilikuwa haikuwahusisha wanahisa wakubwa.Aidha, Milanzi alisema Meya katika kikao hicho alipitisha maamuzi hayo akijifanya yeye ni Mwenyekiti na Robert Kisena mmiliki wa Simion Group kuwa katibu na kufanya maamuzi batili bila ridhaa ya baraza la madiwani na wanahisa wakubwa.Hata hivyo, uchafu huo ulikamilika pale alipomkabidhi kampuni ya Uda siku hiyo hiyo Simion Kisena kwa vile alilipa milioni 285 sawa na asilimia 12.5 ya hisa zote za Uda na kumtangaza mbele ya wafanyakazi.Alidai kuwa mmiliki wa kampuni hiyo Juni 22, saa 2:00 ya usiku alivunja ofisi za umma za Meneja Mkuu wa Uda na kuiba nyaraka muhimu zikiwemo hati miliki ya majengo na kuitaka serikali isikae kimya wakiangalia mali za Uda zikiporwa kwani wao ndio mmiliki.Awali Meya alitangaza kuunda tume mbili kwa ajili ya kuchunguza fedha zilizopotea Uda na mkataba uliopo pia kuchunguza matatizo yanayopatikana katika kituo cha Ubungo na kwamba zitagharimu milioni tisa hadi watakapo maliza uchunguzi.Meya alisema Sh. milioni 200 zilikuwa zimepotea na hazikuonyesha matumizi yake yoyote na ameipa tume mwezi mmoja ili kuweza kujua ukweli wa jambo hilo.
 
MAHAKAMA YAAMURU ROBERT KISENA WA SIMON GROUP AKAMATWE


3:28 PM No comments






Na Happiness Katabazi


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imetoa amri ya kutaka mshitakiwa wa nne katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la UDA,Idd Simba, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group Limited,Robert Simon Kisena akamatwe na kufikishwa mahakamani kwaajili ya kuja kukabiliana na kesi inayomkabili.


Amri hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo Elvin Mugeta baada ya kuridhia ombi la wakili wa serikali Awamu Mbagwa na mawakili wa utetezi Alex Mgongolwa na Romani Lamwai ambao walitaka Kisena ambaye ni mshitakiwa wa nne katika kesi hiyo akamatwe na akifikishwe mahakamani hapo ili kesi iweze kuendelea.


Wakili wa Serikali Mbagwa alianza kwa kuikumbusha mahakama hiyo kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya upande wa jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa lakini upande wa jamhuri hautaweza kuwasomea maelezo hayo kwasababu mshitakiwa wanne(Kisena),bado hajakamatwa na kwamba hawezi kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa watatu wakati mshitakiwa wanne hayupo kwani kufanya hivyo ni kusumbua muda wa mahakama .


"Sisi upande wa jamhuri tulikuwa tayari kwaajili ya kuwasomea maelezo ya awali wa washitakiwa lakini kwasababu mshitakiwa wa wanne hayupo mahakamani na taarifa tulizonazo bado hajakamatwa tunashindwa leo (jana)kuwasomea maelezo hayo…hivyo tunaomba mahakama hii itoe amri ya Kisena akamatwe na haweze kufikishwa mahakamani ili aje kukabiliana na kesi inayomkabili"alidai wakili Mbagwa.


Kwa upande wao mawakili wa utetezi Mgongolwa na Masumbuko nao walidai wanaunga mkono hoja hiyo ya wakili wa jamhuri ya kutaka Kisena akamatwe na kwamba kesi hiyo iarishwe kwa hairisho la muda mfupi kwani wanaamini serikali inamkono mrefu na ainayafahamu haya makazi ya Kisena na kwamba hadi kufikia jana ilikuwa ni siku 25 tangu kesi hiyo ilipofunguliwa upya mahakamani na Kisena akaunganishwa katika kesi hiyo lakini cha kushangaza hadi leo Kisena hajakamatwa na kufikishwa mahakamani.


"Kesi hii ina watesa wateja wetu kwani hadi sasa hawafahamu makosa yanayowakabili kwa kina, hawapati ajira sehemu nyingine kwasababu ya kesi hii…hivyo na sisi mawakili wa utetezi tunaunga mkono kuwa Kisena akamatwe aletwe mahakamani ili kesi hii iweze kuendelea na kwamba Kisena ni mtu anayetafutwa sana na serikali na hata Aprili 30 mwaka huu, kesi hii ilipofunguliwa rasmi Kisena pia hakuwepo mahakamani na hivyo hakuweza kusomewa mashitaka yake ambapo siku hiyo kesi hiyo iliarishwa hadi leo lakini pia leo Kisena hajafika mahakamani"alidai wakili Masumbuko.


Akitoa amri ya mahakama, hakimu Mugeta alisema amesikiliza maombi ya mawakili wa pande zote mbili na kwamba mahakama yake inatoa amri ya Kisena akamatwe na afikishwe mahakamani na akaiarisha kesi hiyo hadi Juni 4 mwaka huu ambapo Simba na wenzake wataendelea kuwa nje kwa dhamana.
Aprili 30 mwaka huu, upande wa jamhuri uliifuta kesi ya awali ya matumuzi mabaya ya madaraka iliyokuwa ikimkabili Simba na wenzake wawili na kisha kufungua kesi mpya yenye mashitaka sita yakiwemo mashitaka ya rushwa na uhujumu uchumi na kisha kumuunganisha Kisena katika kesi hiyo ambapo katika kesi ya awali iliyofutwa Kisena alikuwa ni shahidi wa upande wa jamhuri na hivyo kufanya kesi hiyo ya makosa ya rushwa, uhujumu uchumi kuwa na jumla ya washitakiwa wa nne hivi sasa.


Ilidai siku hiyo ya Aprili 30 kuwa washitakiwa wanne na wakili Mwandamizi wa Serikali Oswalid Tibabyekomya wanakabiliwa na makosa ya rushwa,uhujumu uchumi,matumizi mabaya ya madaraka na kulisababishia shirika hilo hasara ya Sh. Bilioni 8.4. Na kwamba Tibabyekomya alieleza kuwa baada ya kuyachambua makosa hayo wamebaini kuwa yanaangukia katika Sheria ya Uhujumu Uchumi


Mbali na Idd Simba ambaye ni mshtakiwa wa kwanza na Kisena ambaye ni mshtakiwa wa nne, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba 3 ya mwaka 2013, ni Salimu Mwaking'inda na Victor Alfred Milanzi.Mwaking'inda, ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo alikuwa Mkurugenzi wa UDA na Milanzi ambaye ni mshtakiwa wa tatu, alikuwa ni Meneja Mkuu wa UDA.

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka hayo mapya katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na walisomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali Awamu Mbagwa. Hata hivyo Kisena hakuwapo mahakamani wakati wenzake wakisomewa mashtaka.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka waliyosomewa jana, shtaka la kwanza la kula njama linawahusu Simba na Milanzi na Kisena.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Septemba 2009 na Januari 2010, jijini Dar es Salaam, kwa pamoja walikula njama za kutenda kosa la vitendo vya rushwa, kinyume cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Kwa mujibu wa hati hiyo ya mashtaka, shtaka la pili la vitendo vya rushwa linamhusu Kisena peke yake, hata hivyo shtaka hilo halikusomwa kutokana na mshtakiwa huyo kutokuwapo mahakamani.

Shtaka la tatu ni la vitendo vya rushwa ambalo linawahusu Simba na Milanzi. Wakili Mbagwa alidai kuwa kati ya Septemba 2009 na Januari 2010, walikubali kupokea Sh320 milinoni kutoka kwa Kisena ushawishi wa kuiuzia Simon Group hisa za UDA ambazo zilikuwa bado hazijagawiwa.Katika shtaka la nne ambalo ni la matumizi mabaya ya madaraka, linawahusu Simba , Mwaking'inda na Milanzi.


Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 21 mwaka 2013.

KASHIFA NYINGINE-KISENA AROUND LAKE ZONE
Hi, dear friends, as we were flying around Lake Zone we found another case involving the mighty Kisena - yes the same Robert Simon Kisena of Simon Group of Dar. He is accused of buying in similar manner (like the UDA purchase) New Era Oil Mill of Mwanza which was part of NCU (for the uninformed- NCU is Nyanza Co-operative Union). Well he was also one of the beneficiaries of the "Stimulus Package" money.

The way things are and as far as we can tell - UDA will ultimately end in his hands after the "government" agree for him to pay the remainder of the purchase price. He will be the new owner of UDA. Sorry he already is. Nothing is going to change that.

Till next time!
 
Mbona hatuambiani ukweli humu ndani...hivi aliyeichunguza hii kesi si PCCB, sasa iweje yeye DPP aone kwamba ndiye anayeijua zaidi kesi hii na kuamua kuiondoa mahakamani kwa mamlaka yake???Wao PCCB waliona Kisena ni shahidi sasa iweje yeye DPP amuone Kisena ni mtuhumiwa huko si kuiharibu kesi...ulisikia wapi shahidi anakuwa mtuhumiwa jamani...hapa DPP alitakiwa atujuze watanzania ukweli kwani mashaka tuliyonayo ni ofisi yake kuvamiwa na mafisadi na kufikia maamuzi haya...tuwe makini...!!!
 
Nimemaliza kusoma hizo hapo juu. Nasubiri muendelee kutiririsha habari zaidi lakini naona kama mmeingia mitini. Mmehongwa tayari?
 
[h=3]HUYU NDIYE ROBERT KISENA..AANZA KUFANYA KUFURU JIJINI DAR.[/h]




Viongozi wa Kampuni ya Simon Group na wengine Wakielekea kuzindua mabasi15 waliyowekeza UDA.




Habari na Elias Msuya via gazeti la Mwananchi --- KAMPUNI ya Usafiri jijini Dar es Salaam (UDA) imejipanga kuteka soko la usafiri nchini ifikapo mwezi Machi mwaka 2013.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group, Robert Kisena alipokuwa akipokea mabasi 15 kutoka kampuni ya Tata Africa ya India ikiwa ni sehemu ya mabasi 30 yanayotarajiwa kuingizwa nchini ifikapo Desemba mwaka huu.

Kisena alisema kampuni ya Simon Group iliyowekeza katika shirika la UDA imejipanga kuwa kampuni kubwa barani Afrika kwa mtaji wa Dola25 milioni (sawa na Sh375 bilioni) utakaowezesha kupatikana kwa mabasi 300 ifikapo mwezi Machi mwakani, "Simon Group imejipanga kuwa kampuni kubwa Afrika ifikapo Machi mwakani na tuna mpango wa kununua mabasi 300 kwa mtaji wa Dola25 milioni," alisema Kisena.

Aliongeza kuwa kati ya mabasi hayo kutakuwa na mabasi ya wanawake, mabasi ya wanafunzi, mabasi ya binafsi, mabasi ya mikoani na mabasi yatakayosafiri barani Afrika, "Mazingira mabovu ya sasa ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam mara kwa mara yamekuwa yakisababisha udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake, bila shaka wengi wenu mtakumbuka vizuri kisa cha Maumba. Tunataka kukomesha udhalilishaji huo kwa wanawake ili wasafiri kwa uhuru na raha mstarehe," alisema Kisena.

Kuhusu mabasi ya wanafunzi, alisema yatakuwa matano kila barabara kuu jijini Dar es Salaam na yatafanya kazi hiyo tu.

Kuhusu mabasi ya binafsi (Executive class), alisema yatakuwa na nauli ya juu lakini yatatoa huduma kama vile televisheni, vinywaji, magazeti na kiyoyozi, "Tunataka tuwahamasishe watu wasitumie tena magari yao binafsi. Unajua kwa mwezi mtu hutumia katiya Sh800,000 hadi Sh1milioni kununua mafuta ya gari, hela ambayo ni nyingi mno. Lakini kwa kutumia usafiri huu, inawezekana kubana matumizi," alisema.

Akizungumzia mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) alisema kuwa wanatarajia kushinda zabuni ya kuuendesha kwa kuwa kampuni hiyo haina mshindani katika usafirishaji nchini, "Kwa sasa Dart inajengwa barabara ya Morogoro na barabara itakamilika mwaka 2014. Kwa sasa tutaendesha mradi huo kabla Dart haijaanza na kwa barabara nyingine baada ya hapo. Kwa kuwa sasa UDA haina mpinzani katika sekta ya usafirishaji nchini, naamini tutashinda zabuni ya kuendesha," alisema. Aliongeza kuwa mradi huo unatarajia kutoa ajira kwa zaidi ya Watanzania 1,500.

Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group,Robert Kisena (wa pili kulia) Wawekezaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Meneja wa Biashara wa TATA Afrika Holding Tanzania Ltd,Srinivas Nemalapuri (wa pili kushoto) kulia ni Mkurugenzi wa Simon Group, Leonard Rubuye na kushoto Kaimu Meneja Biashara,Sarvan Keshri. ikiwa ishara makabidhiano ya mabasi 15 katika awamu ya kwanza, hafla hiyo ilifanyika kwenye Ofisi za UDA Dar es Salaam.


Mwenyekiti Mtendaji wa Simon Group,Robert Kisena (wa nne kushoto) akiwaongoza viongozi wengine ndani ya Basi la UDA


 
Mbona hatuambiani ukweli humu ndani...hivi aliyeichunguza hii kesi si PCCB, sasa iweje yeye DPP aone kwamba ndiye anayeijua zaidi kesi hii na kuamua kuiondoa mahakamani kwa mamlaka yake???Wao PCCB waliona Kisena ni shahidi sasa iweje yeye DPP amuone Kisena ni mtuhumiwa huko si kuiharibu kesi...ulisikia wapi shahidi anakuwa mtuhumiwa jamani...hapa DPP alitakiwa atujuze watanzania ukweli kwani mashaka tuliyonayo ni ofisi yake kuvamiwa na mafisadi na kufikia maamuzi haya...tuwe makini...!!!

Unajifanya hauelewi kilichondikwa na mtonyaji hapo juu.... ndiyo walewale!
 
Robert Kisena na Rubuye ni nani hapa Tanzania? Asili yao ni wapi? Kwanini wanaandamwa sana? Biashara zao ni zipi hasa? Ziliazaje, zinaendeleaje?
 
Mkuu toka ofisi ya DPP sijaona lolote la
maana zaidi ya ujanja tu.
Kuleni lakini Upinzani ukiingia Madarakani
itabidi mteme vyote bila kijari nani ni nani.
 
Ilikwisha semwa zamani, Tanzania hakuna serikali ya kuwatumikia watu bali kuna genge la majambazi wanawakamua pesa wananchi kwa manufaa yao. Hii kesi wenye akili tulijua haita fika popote kwani Mrundi Idd Lion ni noumer kwenye deal za namana hii! Anafahamu vizuri udhaifu wa serikali yetu na mihimili yake, ataendelea kutuchezea hivi hivi mpaka tukome. Kumbukeni deal la sukari akiwa waziri wa viwanda na biashara wakati ule!
 
Ofic zote 2 zimeoza tu. DPP siku hizi hana mda na kesi za rushwa, anahangaika na nole prosecue za kuwafungulia CDM kesi za ugaidi...
 
robert kisena na rubuye ni nani hapa tanzania? Asili yao ni wapi? Kwanini wanaandamwa sana? Biashara zao ni zipi hasa? Ziliazaje, zinaendeleaje?
Ishu ikishahusisha wahindi mi napata kichefuchefu...
 
Mbona hatuambiani ukweli humu ndani...hivi aliyeichunguza hii kesi si PCCB, sasa iweje yeye DPP aone kwamba ndiye anayeijua zaidi kesi hii na kuamua kuiondoa mahakamani kwa mamlaka yake???Wao PCCB waliona Kisena ni shahidi sasa iweje yeye DPP amuone Kisena ni mtuhumiwa huko si kuiharibu kesi...ulisikia wapi shahidi anakuwa mtuhumiwa jamani...hapa DPP alitakiwa atujuze watanzania ukweli kwani mashaka tuliyonayo ni ofisi yake kuvamiwa na mafisadi na kufikia maamuzi haya...tuwe makini...!!!

Hata katika Busara ya Kawaida tu kilichofanyika hapo ni utoto tu huyu kamwaga Ugali na mwenzake anajibu mapigo kwa kumwaga mboga.Nikweli kwamba kisheria Mtoaji na Mpokeaji wote ni wakosaji ila kwa maslahi ya Uma na kuokoa mali ya uma kilichotakiwa kufanyika ni kile alichokifanya Hosea na watu wakekumfanya KISENA shahidi .

Hata Ulaya ambako tumeazima sheria hizi tunazojitutumua nazo kwa ajili ya kuokoa muda wa Mahakama na gharama za walipa Kodi huwa for Public Interest wanafanya Plea Bargaining na Mhalifu ilikiri kosa.Kwa hiyo DPP ametumia madaraka yake vibaya .Nadhani wanaoneshana ubabe tu.hakuna ueledi wowote hapo. Inaudhi na kukifu hasa pale Kesi za ajabuajabu zinapong'ang'aniwa Mahakamani na marufaa yasiyo na msingi na Kesi za Msingi na zenye ushahidi mzito kama huu zinachezewa Mf.Kesi hii.
 
Tuna tatizo kubwa la kimfumo, ikiwa mtu wa kuzuia rushwa anapokea rushwa tutafika kweli?
 
Tanzania eeeeeeeeeee inchi yangu eeeeeeeeeeeeeeeee
what can i say iache iiliwe na wenye menooooooooooooooooooooo
 
Back
Top Bottom