PCCB Iliharibu Yenyewe Kesi ya Idd Mohamed Simba

Nilisikitika sana kusikia Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Dr Edward hosea akilamimika hasa kuhusu serikali kumfunga mikono, na kuisingizia ofisi yetu tukufu ya DPP kuwa inakalia majalada ya kesi ya ofisi yake hivyo kumkwamisha. mimi nikiwa mtumishi wa ofisi ya DPP ambaye nimefanya kazi hapa kwa muda wa miaka kumi (nimeanza kabla Hosea hajawa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU) watu wa nje ya mfumo wanamuona Dr Hoseah ni muadilifu sana lakini watu tuliyefanya naye kazi tunamjua kivingine, naomba nitoe mfano wa kesi ya Idd Simba na kama watu wengine wanabisha nitaweka mifano mingine halisi hapa janvini, natoa ukweli ambao mtu yeyyote anayetaka anaweza kuuchunguza, sisi tumechoka kushambuliwa kwenye vyombo vya habari wakati yeye mweyewe ndiye anayeharibu kesi zake.

Mashitaka waliyoyaleta PCCB ni pamoja na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kuuza hisa za UDA bila kufuata utaratibu wa ushindani na bila kuihusisha serikali na halmashauri ya jiji. Shitaka la kwanza la kusababisha hasara lilihusu TSH 320,000,000/= zilizolipwa katika account ya ndugu Idd Mohamed Simba na ndugu ROBERT KISENA na kosa la pili ni kusababisha hasara ya TSH 8,422,000,000/= kama hisa hizo zingeuzwa kwa ushindani. Msingi wa shitaka la kusababisha hasara ya TSH 320,000,000/= lilitokana na maelezo ya ROBERT KISENA kuwa alilipa fedha hizo katika account ya ndg Idd Simba namba 0210001002 iliyopo BENK M kama sehemu ya malipo ya hisa.

Makosa waliyofanya PCCB chini ya Hosea kwa kukusudia
katika hati mojawapo ya malipo ya tsh 250,000,000/= kutoka katika kampuni ya robasika Agro Product Ltd kwenda kwenye account ya Idd Simba iliyoko benk m, NDG ROBERT KISENA aliandika uongo kuwa kilikuwa kinalipwa kwa gharama ya usafiri. Hii ilikuwa inamfanya Robert kisena ambaye TAKUKURU walitaka awe shahidi wao na yeye kuwa mtuhumiwa kwani kama alikuwa hausiki na wala hajui kuwa anafanya wizi kwa nini aandike sababu za uongo kwenye hati ya malipo?, lakini hata hivyo TAKUKURU waliiondoa hati hiyo na walipotakiwa wailete imbatanishwe katika jadala la kesi walikataa, hata walipotakiwa kuleta jalada halisi (original) la kesi ili ofisi ya DPP ikague yenyewe walikataa.

Ofisi yetu ya DPP ilikuja kugundua baadae kuwa Robert kisena hakuishia kuhusika tu katika malipo hayo ya rushwa kwa ndg Iddi Simba lakini baadaye ilibainika kuwa alishiriki kumpa rushwa mkaguzi Neema Kiule ambaye ukaguzi wake ulizipatia thamani ndogo hisa za UDA ili Robert Kisena atakapokuja kununua ainunue kwa bei ndogo.

Ofisi ya DPP ilipogundua hivyo iliiagiza TAKUKURU imuongeze ndg Robert katika orodha ya watuhumiwa ili na yeye ashitakiwe pamoja na wengine kwani katika issue hii yeye ndiye aliyekuwa king maker (mtoa rushwa na mnunuzi katika bei ya chini) na bila kumuunganisha yeye serikali ingeshindwa kesi kirahisi. Pamoja na maagizo hayo TAKUKURU ilikataa kata kata kumuongeza na wala kumuita mahakamani, mtuhumiwa huyu hakufikishwa mahakamani tarehe 04/06/2013 kesi ilipohairishwa na hata tarehe 19/06/2013 kesi ilipoondolewa mahakamani. PCCB imeelekezwa imuchukue maelezo mtuhumiwa huyo na ichunguze kuhusika kwake kikamilifu na maelezo yake yaambatanishwe katika hati za mashitaka katika kesi hii, ikulu, mwanasheria mkuu, waziri wa sharia, dci pamoja na usalama wa taifa viimeelezwa sababu za kutoa kesi hii mahakamani.

Nyuma ya pazia.
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Dr Edward Hosea alishapewa tsh 300,000,000/= na ndugu Robert Kisena, na kumuhakikishia kwamba hatamujumuisha kwenye watuhumia na atamtumia kama shahidi, ndiyo maana anasita kufanya kitu amabacho kinaonekana dhahiri.

Kwa nini TAKUKURU inamlinda kingmaker wa deal hili ndg Robert Kisena kiasi cha kukataa kumjumuisha katika orodha ya watuhumiwa wa sakata hili? Hosea alijibu kwanza swali hili kabla hajaanza kulalamika hovyo na kusingizia taasisi nyingine kuwa ndio zinamzuia kufanya kazi vizuri.

Inanishangaza sana utumishi wa Umma wa namna yako MASANJAGAMA...suala lililotokea ndani ya ofisi yenu ya DPP unakuja kuianika humu kwenye Jamii Forum, hivi kuna siri tena za Serikali hapa...mambo haya ndio yamekuwa yakilalamikiwa sana na Mama Selina Kombani kwamba watumishi wa Serikali siku hizi mnatumiwa na vyama vya Siasa kuchomoa taarifa za kwenye mafaili na kuzitoa nje. Uadilifu wako kwa Serikali yako upo wapi hapa hadi uamue kutoa siri nzito za ofisi ya DPP kwenye JF??? Inanishangaza sana...
 
wezi hulindana.

Asakuta Same unaloambiwa ni busara tu wala sio "wezi hulindana"...unaweza kuona mwenyewe aina ya utumishi wa umma alionao mtoa hii post...mambo ya ofisini na kwenye mafaili kuletwa kwenye jamii forum. Ukiichambua hii post yake ni dhahiri mtoa post ameamua kumshambulia Hosea kwa chuki zake binafsi...kesi zote za rushwa mahakamani zinaendeshwa na DPP sasa Hosea amehusikaje kuondolewa kwa kesi ya Simba mahakamani??? DPP ndiye anapaswa kubebeshwa hili ziogo kwani ndiye anahusika kwa asilimia 100 kuendesha kesi zote za jinai nchini...
 
kaka usimlaumu, Watanzania wanataka kujua ukweli, kwa nini kesi ya Idd simba Ifutwe?, Huyo mtoa maada Hana kosa. Wewe ndiyo mwenye kosa ,kwa kutaka kuficha ukweli
 
Hapana Bintiwangara simlaumu wala kujaribu kuficha ukweli...lakini ni busara watanzania wakaujua ukweli wa mambo kama ulivyo lakini hoja hii inaonesha chuki binafsi za mtoa post...unapokuwa kwenye utumishi wa umma ni vyema maadili ya utumishi yakazingatiwa kwa mambo muhimu ya nchi.
 
mambo ya umma yanahitaji siri? au ndiyo mnafanya siri kuficha uozo wenu?
 
Watanzania kutaka kujua ukweli wa kwanini kesi ya idd simba imefutwa ilihali tunafahamu kuna madudu yamefanyika UDA ,haina maslahi kwa umma? au ndiyo kuficha maovu kwa mgongo wa utumishi wa umma uliotukuka?
 
Mzee iddi simba hakuwa na kesi waliomtengenezea kesi ni akna rdhwan na robert kisena kwa sababu iddi simba alkuwa anakataa simon group kupewa ubia uda na simon group ni ya rdhwan hivyo wakamtengenezea idd simba kesi mzee idd simba na wenzake wakiwa kwenye kesi rdhwan akajimilikisha uda baada ya hapo dpp na takukuru wakaagzwa wafute kesi...ata lawrence mafuru mkurugenzi mtendaji
wa nbc aliyeacha kazi alkataa kuipa kampun ya rdhwan grk law chambers tenda ya kuendesha na kusmamia kesi za nbc tanzania kwa maelezo ya mafuru ni kwamba kampun ya rdhwan bado ni changa na haina uzoefu na wataalam rdhwan akamtumia mwenyekiti wa bodi ya udhamini ya nbc kumsmamisha kazi mafuru kwa muda kupsha uchunguzi baada ya kampun ya rdhwan grk law chambers kupewa tenda bila ushndani nbc bodi ikamrudisha mafuru kazini kwa kulinda hadhi yake lawrence mafuru ambaye ni moja wa vijana smart kwenye utendaji akakataa kurudi nbc akaresgn/akaacha kazi nbc kulinda heshima yake huyu kijana rdhwan anavuruga nchi tuwe naye makini ila mwsho wake umekarbia 2015 si mbali
 
Kuumbe...sasa ndio najua kwanini Mafuru aliacha kazi ghafla kivile, huyo Riz1 ni hatari kama ukoma
 
mambo ya umma yanahitaji siri? au ndiyo mnafanya siri kuficha uozo wenu?

Ofisi yetu ya DPP haina maadili ya kusoma majalada ya watuhumiwa na kuja kuanika siri za ofisi kwenye jamii forum, muda wote sisi ni watunza siri za nchi kwani tunayaona mengi...lakini alilolifanya MASANJAGAMA ni kuidhalilisha ofisi yetu tena kakosa hata aibu kusema amefanya kazi hapa ofisini kwa zaidi ya miaka 10...kwa uozo huu basi hajajifunza kitu na hafai kuwa ofisi ya DPP, nashauri akafanye kazi ofisi nyingine.
 
Wewe Oswald mbona unatia aibu. Miaka yote hiyo ya utumishi hujakomaa tu?
Ama kweli uroho wa umaarufu unakumaliza ndugu yangu. Umejishushia credibility yako binafsi kwa tunaokufahamu kwa muds mrefu na hasa ofisi ya DPP kwa ujumla. Nimeamua kukuandikia openly baada ya kutojibu PM zangu zaidi ya tano.

Menosugu
 
Menosugu unamaanisha aliyeweka hii post ya aibu humu JF ni ndugu yetu Oswald Tibabyekomya wa ofisi yetu ya DPP...duuuh, asitake kutugombanisha na ofisi ya TAKUKURU jamani. Bora umemuumbua aubebe mzigo wa unafiki peke yake na sio kuichafua ofisi yote ya DPP. Aliyoyaandika Oswald humu JF sio maadili ya Ofisi ya DPP napenda kuwahakikishia watanzania...ni tamaa yake ya kutaka kujipatia umaarufu na vyeo...!!!
 
Ndugu yangu Masanjagama umeandika taarifa inayovutia na kuonekana kuna kaukweli ndani yake maana hata ukamataji wa wakosaji kwa upande wa PCCB una walakini. Lakini hata ofisi yenu ya DPP inaonekana inafanya mambo kisiasa zaidi maana kuna tetesi kwamba wakati mahakama kuu ilipofuta mashitaka ya ugaidi kwa Ndugu Lwakatare, Fereshi alitamka kwamba majaji wana ajenda ya siri/wana lao jambo na CHADEMA wakati mshitaki/mshitakiwa wenu alikuwa ni Lwakatare kwa maana kwenye hati ya mashtaka na haikuwa CHADEMA. lakini mtu anakuja kufanya siasa utafikiri pilisi wakati kwa uelewa wangu ninyi ndo wataalam wa sheria katika nchi hii. Kama kweli ndo fikra alizokuwa nazo huyo kiongozi wenu basi hata maandishi haya uliyoyaandika hayana maana yawezekana analake jambo.
 
kaka usimlaumu, Watanzania wanataka kujua ukweli, kwa nini kesi ya Idd simba Ifutwe?, Huyo mtoa maada Hana kosa. Wewe ndiyo mwenye kosa ,kwa kutaka kuficha ukweli

Kawaida ukimshitaki mtu bila ushahidi wa kutosha atakushinda, na akishashinda kesi anaanza kudai gharama za kundesha kesi. Madai ya DPP kua R.Kisena aitakiwa aunganishwe kwenye kesi nayo yana msingi, labda PCCb wangetueleza sababu za kisena kua shahidi wakati nae ni mhusika namba moja.
 
Mzee iddi simba hakuwa na kesi waliomtengenezea kesi ni akna rdhwan na robert kisena kwa sababu iddi simba alkuwa anakataa simon group kupewa ubia uda na simon group ni ya rdhwan hivyo wakamtengenezea idd simba kesi mzee idd simba na wenzake wakiwa kwenye kesi rdhwan akajimilikisha uda baada ya hapo dpp na takukuru wakaagzwa wafute kesi...ata lawrence mafuru mkurugenzi mtendaji
wa nbc aliyeacha kazi alkataa kuipa kampun ya rdhwan grk law chambers tenda ya kuendesha na kusmamia kesi za nbc tanzania kwa maelezo ya mafuru ni kwamba kampun ya rdhwan bado ni changa na haina uzoefu na wataalam rdhwan akamtumia mwenyekiti wa bodi ya udhamini ya nbc kumsmamisha kazi mafuru kwa muda kupsha uchunguzi baada ya kampun ya rdhwan grk law chambers kupewa tenda bila ushndani nbc bodi ikamrudisha mafuru kazini kwa kulinda hadhi yake lawrence mafuru ambaye ni moja wa vijana smart kwenye utendaji akakataa kurudi nbc akaresgn/akaacha kazi nbc kulinda heshima yake huyu kijana rdhwan anavuruga nchi tuwe naye makini ila mwsho wake umekarbia 2015 si mbali

Ndugu yangu NBC ni makaburu hawafanyi kazi kibongobongo.
 
Wala hilo si siri, hao hao tunaowategemea ndio wala rushwa wakubwa.... na ushaidi upo pale walipojitokeza na kutetea mafisadi...
 
MORINYO; Ndugu yangu NBC ni makaburu hawafanyi kazi kibongobongo.

Ata hisa alizochukua rizwan Tanzanite One ambayo ni za makaburi nao wapo smart kwa taarfa yako wapenda dili/rushwa wakubwa ni wahindi na makaburu fuatilia kwenye migodi uscheze muzki usioujua au umepewa buku 7 lumumba street uktumwa tumia na akili zako
 
Kama ulikuwepo, huyu jamma anapenda kujipendekeza mno hata nakumbuka siku moja Mheshimiwa Chenge alimtolea nje baada ya kumpelekea umbea. Ni yeye na ushaidi ambao nimetumia five times privetly ili atubu lakini amekaa kimya.Naona kwa vile alijiunga kwenye forum hii siku hiyo hiyo alipomwaga siri za ofisi hata kusoma PM bado hajui. Invisible labda ampe somo.
 
Asakuta Same unaloambiwa ni busara tu wala sio "wezi hulindana"...unaweza kuona mwenyewe aina ya utumishi wa umma alionao mtoa hii post...mambo ya ofisini na kwenye mafaili kuletwa kwenye jamii forum. Ukiichambua hii post yake ni dhahiri mtoa post ameamua kumshambulia Hosea kwa chuki zake binafsi...kesi zote za rushwa mahakamani zinaendeshwa na DPP sasa Hosea amehusikaje kuondolewa kwa kesi ya Simba mahakamani??? DPP ndiye anapaswa kubebeshwa hili ziogo kwani ndiye anahusika kwa asilimia 100 kuendesha kesi zote za jinai nchini...

Unataka afiche siri, una uhakika gani kuwa ndie yeye unayemfikiria... yuko huru kusema kilicho kuwa si sawa..wewe endelea kuficha maovu iko siku aibu itakukuta...
 
Back
Top Bottom