PayTrade ya tradecarview

I thought i was asking from friends!

Kwahiyo wengine wanavyoulizaga kwenye majukwaa husika hua wanauliza from. . . . . .?!

Wageni hua wanapondwa sana wakichanganya majukwaa. . .alafu wakongwe hao hao nao wanajitia hawajui nini kinaenda wapi. Nwy ngoja wakushauri.
 
Nimenunua Gari Mara 2 via paytrade! Ni Huduma inayohakikisha kwamba hela yako haitaibiwa! Tradecarview ni kampuni na ndani Yake pana watu wameregister wanauza magari, when you use paytrade actually hela ukituma zaenda kwa trade car view na wakiridhika Gari limetumwa na ni Kama like la kwenye invoice Ndio Wana release funds kwenda kwake, ikitokea shida they refund you.

Thanks ndugu kwa elimu ulonipa. Ubarikiwe sana!
 
Sikumbuki kama niliwahi wauliza hili, naomba
jamani nijuzeni juu ya uhakika wa hii njia ya
kununua gari japan kwa kutumia Paytrade.

Na

ona wahusika waniongelea kama secure method je, ni kweli au ndo
mpango mzima wa kutaka kuingizana kingi?

Nijuzeni please, nataka nilisahau lile swali la
'hivi jirani kwa nini hununui gari'?.

Nawasubiria!

tumia kampuni ya 'autorec' ni ya uhakika na hawana mambo ya kihuni kama kampuni nyingine
 
Habari wanajf, nilitaka kujua kama kuna mtu anauzoefu ktk kutumia huduma hii. Je ikiwa kampuni haijakuletea gari with specifications km ulilolichagua ktk website hawatalipwa na ww kuweza kupata hela zako?
 
[h=6]What are the benefits to use "PayTrade"?[/h]
The following aspects can be benefits to use PayTrade service.
  • The Buyer can receive the item which he/she ordered (If the item is the Vehicle, VIN/Chassis number will be checked by Carview).
  • The Buyer can get refund if the Seller does not ship the item within appropriate period.
  • The Buyer can receive refund if the Seller cancels the order by their own reasons.
*Bank charge is required for refund.

[h=6]How does tradecarview protect me with PayTrade service?[/h]Carview guarantees the shipment of the item.

*Carview will not responsible or guarantee the condition, model type, or any other issue concern to the item.
 
Nina mpango wa kuagiza usafiri,please naombeni mnijuze kuh hili, kuagiza gari kutoka kwenye makampuni yaliyo kwenye tradecarview kupitia huduma yao ya paytrade iwapo ni njia sahihi,salama na ya uhakika ya uagizaji magari?
 
Mkuu hii huduma ni sahihi, salama na ya uhakika zaidi. Ingawa unailipia kidogo, ni bima ya uhakika ya pesa zako. Muuzaji analipwa na paytrade meli yenye gari lako ikishaondoka bandarini kuja Tz. Vinginevyo kama atakuwa hana uwezo wa ku-supply gari, paytrade watakurudishia pesa yako. Nazungumza kwa uzoefu maana nimeshawatumia mara 3.
 
mkuu hii huduma ni sahihi, salama na ya uhakika zaidi. Ingawa unailipia kidogo, ni bima ya uhakika ya pesa zako. Muuzaji analipwa na paytrade meli yenye gari lako ikishaondoka bandarini kuja tz. Vinginevyo kama atakuwa hana uwezo wa ku-supply gari, paytrade watakurudishia pesa yako. Nazungumza kwa uzoefu maana nimeshawatumia mara 3.

nashukuru mkuu,kwa ushauri wako mzuri,itabidi niwatumie hawa jamaa.
 
Ofcoz using Paytrade you get guarantee of your money by the car showroom so called tradecarview.
 
Ni kweli kwa kutumia Paytrade unakuwa na uhakika kuwa gari ulilochagua utalipata; na kama hutalipata utarudishiwa pesa yako. Hii ni njia iliyobuniwa na Wajanja wa Kijapan baada ya kuona Wateja wanaibiwa sana pesa yao na Phantom Companies. Tatizo la paytrade ni kwamba unailipia; hivyo gharama ya kuwa juu kidogo. Lakini ni salama 100%. Hata hivyo, unaweza kuni-PM nikakuelekeza alternative way, utapata gari ya ndoto yako kwa bei nafuu sana.
 
nashukuru mkuu,kwa ushauri wako mzuri,itabidi niwatumie hawa jamaa.

Mimi mwenyewe ndio naanza kuwatumia , wanaonekana ni watu wazuri kwa sababu mawasiliano yote yanafanywa wazi wazi for future reference - na ukituma pesa zinafikia kwenye account yao - nafikiri kwa maelezo ya "POWER" Muuzaji analipwa na paytrade meli yenye gari lako ikishaondoka bandarini kuja tz.

NItazidi kukutoa wasi wasis kwa jinsi nitakavyoenda nao kimsingi ni kama nimefikia 50% ya mlolongo wa kuuziana magari online
 
Nina mpango wa kuagiza usafiri,please naombeni mnijuze kuh hili, kuagiza gari kutoka kwenye makampuni yaliyo kwenye tradecarview kupitia huduma yao ya paytrade iwapo ni njia sahihi,salama na ya uhakika ya uagizaji magari?

Kuna malalamiko mengi na wengi kupoteza fedha zao kwa njia hii. Kwani unafanya biashara na mtu usiyemjua, huna pa kuanzia kufuatia pesa zako. Wengine wanaletewa magari tofauti na waliyoyachagua. Huna hakika na ubora wa gari unayoiona kwenye picha kwa vile mfanya biashara anataka gari litoke nawe huna wa kukuhakikishia kama gari ni salama au kanyagaboya.

Nilikuwa na mpango wa kufanya hivyo, lakini nilisita kwa vile siku hizi ziwezi kuamini sana njia ya kulipa online kiwango kikubwa cha pesa kutokana na wengi kuingizwa majaribuni na kuishia kupata presha. Wenye bahati hubahatika na asiye na bahati ndo hivyo tena. Ujeavyo wauzao magari si kampuni mmoja bali na watu binafsi na makampuni mbalimbali ya car dealers.

Ushauri:
Uzoefu wangu ni bora kumtumia mtu mwaminifu mtanzania aishiye huko Japan ambaye anafanya kazi kwenye moja ya makampuni ya dealership. Kuna mmoja ambaye namfahamu mwaminifu, mwazi na atakutafutia gari unalotaka na kwa kiwango cha kuridhisha. Utaweza kuongea naye kwa simu na kuwa na mawasiliano kwa email naye kwa nini kinatakiwa, na atakupa msaada wa kufaa. Hata wamissionari wanamtumia sana mtu huyo. Mimi mwenyewe nimeagiza gari kutumia yeye alinipa ushauri mzuri, na kunipa tahadhari kwa baadhi ya magari niliyofikiria mazuri kumbe ni bomu tupu. Alinichagulia gari zuri na nilipolichukua bandarini Dar sikuamini na walioona walifikiri ni jipya kwa jinsi alivyokuwa makini katika kufanya uchaguzi makini.

Yeye anafanya dealership kwa hiyo hiyo tradecarview, lakini mimi niliweza kulipa moja kwa moja kwenye kampuni nilikonunua gari kupitia kwake na kwa gharama nafuu. Huyu Kaka namfahamu kwa miaka mingi wakati yupo Tanzania, na sasa ndio yuko Yokohama - Japan.

Anayetaka kuagiza gari kupitia kwa huyu ndugu mtanzania halisi ambaye ni mwaminifu na mcha Mungu,
anipm nimpe contact zake. Siwezi kuanika tu hapa kwa vile hajaniruhusu kufanya hivyo. I'm serious, nawahurumia watanzania wenzangu, pesa yako umeitokea jasho unauchungu nayo. Thanks.
 
Watu wanataka kukutapeli kijana, hao wanaokuambia eti ni-PM kuwa nao makini. Watu tumeagiza magari, tumeyapata, mazuri kama tulivyotegemea. Usifikiri eti mtanzania mwenzio ndio mwaminifu sana kuliko wajapan!!, Paytrade haina shida, kama unahofu na ubora wa gari, tumia makampuni yenye uhakika kama vile AUTOREC japo garama zao huwa ni kubwa kidogo kuliko wengine
 
Nakubaliana nawe si wote waaminifu, mimi sina mpango wa kumwahidia mtu kumwagizia gari la hasha. Ila mtu ninayemfahamu ambaye ni mwaminifu anawasaidia wengi kuchagua magari mazuri kwa kukushirikisha kujadiliana. Atakutumia picha ya gari unaliangalia na atakupa sifa na kasoro za gari hilo kwa vile huwa analiangalia kiufundi kama limekamilika au la. Mwenyewe amenifanyia hivyo na wengi hata mashirika ya dini wanamtumia sana na wamenufaika.

Ila kuwa makini na watu wanaotaka wao kukuagizia, hatari unaweza kuingizwa mjini, ujue hapa kuna watafutaji na kuna wasio na dhamiri na hawamwogopi Mungu ili mradi wapate wanachotaka. Hii hatari. Napenda kuwasaidia Watanzania wenzangu maana pesa yao wameitokea jasho, na hawa wanaouliza hapa ni wenzangu wa kiwango chetu, wenye nacho hawahitaji njia ya kujihakikishia uagizaji kwa vile nafasi zao ni kubwa.
 
Naomba kuuliza jaman nilisikia paytrade wana branch hapa Tanzania - Dar es Salaam ni kweli na kamakweli ofisi zao zipo sehemu gani
 
Kuna malalamiko mengi na wengi kupoteza fedha zao kwa njia hii. Kwani unafanya biashara na mtu usiyemjua, huna pa kuanzia kufuatia pesa zako. Wengine wanaletewa magari tofauti na waliyoyachagua. Huna hakika na ubora wa gari unayoiona kwenye picha kwa vile mfanya biashara anataka gari litoke nawe huna wa kukuhakikishia kama gari ni salama au kanyagaboya.

Nilikuwa na mpango wa kufanya hivyo, lakini nilisita kwa vile siku hizi ziwezi kuamini sana njia ya kulipa online kiwango kikubwa cha pesa kutokana na wengi kuingizwa majaribuni na kuishia kupata presha. Wenye bahati hubahatika na asiye na bahati ndo hivyo tena. Ujeavyo wauzao magari si kampuni mmoja bali na watu binafsi na makampuni mbalimbali ya car dealers.

Ushauri:
Uzoefu wangu ni bora kumtumia mtu mwaminifu mtanzania aishiye huko Japan ambaye anafanya kazi kwenye moja ya makampuni ya dealership. Kuna mmoja ambaye namfahamu mwaminifu, mwazi na atakutafutia gari unalotaka na kwa kiwango cha kuridhisha. Utaweza kuongea naye kwa simu na kuwa na mawasiliano kwa email naye kwa nini kinatakiwa, na atakupa msaada wa kufaa. Hata wamissionari wanamtumia sana mtu huyo. Mimi mwenyewe nimeagiza gari kutumia yeye alinipa ushauri mzuri, na kunipa tahadhari kwa baadhi ya magari niliyofikiria mazuri kumbe ni bomu tupu. Alinichagulia gari zuri na nilipolichukua bandarini Dar sikuamini na walioona walifikiri ni jipya kwa jinsi alivyokuwa makini katika kufanya uchaguzi makini.

Yeye anafanya dealership kwa hiyo hiyo tradecarview, lakini mimi niliweza kulipa moja kwa moja kwenye kampuni nilikonunua gari kupitia kwake na kwa gharama nafuu. Huyu Kaka namfahamu kwa miaka mingi wakati yupo Tanzania, na sasa ndio yuko Yokohama - Japan.

Anayetaka kuagiza gari kupitia kwa huyu ndugu mtanzania halisi ambaye ni mwaminifu na mcha Mungu,
anipm nimpe contact zake. Siwezi kuanika tu hapa kwa vile hajaniruhusu kufanya hivyo. I'm serious, nawahurumia watanzania wenzangu, pesa yako umeitokea jasho unauchungu nayo. Thanks.

Mzee wa Busara sasa hapa unatusaidia kus-solve problem au unatuvunja moyo.

Mbona siye tumekuwa tukiagiza magari kupitia makapuni ya kuuza magari - Japan na tumekuwa tukiyapata bila matatizo - kimsingi wajapan ni watu waaminifu sana - japo kwenye kundi la mijusi nyoka hawezi kosekana.

Halafu badala ya kutuweka sawa kwenye tatizo la msingi unatutoa kwenye hukomun atupeleka kwingine ambako wewe binafsi unafikiri ni salama - je tutajuaje kama na wewe ni unatupeleka kwa mtu ambaye atatuingiza mjini.

Najua kuna makampuni mengi ya kitapeli lakini si yote tatizo ni kujua lipi - na hii inataokana na ushahidi wa awatu mbali mbali ambao wameisha watumia
 
Wasiliana na japanese car auction agent wapo arusha wanadili na minada moja kwa moja ni guarantee kupata gari watumie email yako utatumiwa gari unayotaka na kiwango cha pesa unachotaka .gari japan huuzwa kwa njia za minada kwa kupitia kwenye computer zilizounganishwa moja kwa moja ,minada huanza jumatatu hadi jumamosi .kumbuka huwezi ka access hapa hadi uwe member .
 
Mzee wa Busara sasa hapa unatusaidia kus-solve problem au unatuvunja moyo.

Mbona siye tumekuwa tukiagiza magari kupitia makapuni ya kuuza magari - Japan na tumekuwa tukiyapata bila matatizo - kimsingi wajapan ni watu waaminifu sana - japo kwenye kundi la mijusi nyoka hawezi kosekana.

Halafu badala ya kutuweka sawa kwenye tatizo la msingi unatutoa kwenye hukomun atupeleka kwingine ambako wewe binafsi unafikiri ni salama - je tutajuaje kama na wewe ni unatupeleka kwa mtu ambaye atatuingiza mjini.

Najua kuna makampuni mengi ya kitapeli lakini si yote tatizo ni kujua lipi - na hii inataokana na ushahidi wa awatu mbali mbali ambao wameisha watumia

Hapa nashirikisha uzoefu wangu wala sina maana wote wafate ushauri wangu, maana kipenda roho ndiyo dawa. Cha msingi stress ambayo wengi hupata baada ya kupata magari hewa, mabovu, au kuliwa pesa zao na wajanja.

Sina nia ya kuwavunja moyo, bali ni tahadhari. Kilichonishtua na kuniogopesha mmoja ambaya namfahamu aliagiza gari kwa njia hiyo ya online, gari alilichagua ni ile ile lakini ni bomu, kwani kwa picha linaonekana zuri lakini baada ya kulijaribia na kutembea nalo ndo hivyo, hawezi kulirudisha, na gharama ya matengenezo ni kubwa. Pesa nyingi amelipa afanyeje?

Kuna watu kadhaa ambao wamelalamika kuingizwa mijini na mtindo huo, sitaki kuweka hapa watu hao ambao nawafahamu ili nisijevujisha machungu waliyopata. Kuna wanaobahatika na kuna wanaopata hasara. Magari mengi wayapatayo watu huwa yameshachoka mbaya, utatumia miaka miwili hadi mitatu gari unabidi kuweka juu ya mawe. Hilo ndilo ninalowahurumia watanzania wenzangu.

Nilipopata gari nililoagiza kwa njia ya mtu ninayemfahamu wengi wambao wameagiza online walishtuka kwani gari yangu ilionekana chuma bomba kabisa ukilinganisha ya wengi ambayo yalitangazwa kwamba ni ya karibuni, lakini yanaonekana machakavu. Gari yangu to turn on ignition utafurahia. Hilo ndilo ninalowatakia. Mimi siishi huko Japan, na sitaki kuagia gari ya mtu, ila anayetaka nimwunganishe kwa huyu mtanzania atawasaidieni. Thanks.
 
Back
Top Bottom