PayTrade ya tradecarview

Retreat

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
229
70
Wana jamvini hivi kuna mtu ana idea yoyote ya hii njia ya kununu magari inayoitwa PayTrade? Ni salama kweli au kuna kanyaboya hapo? Maana nataka kuzgiza mkoko lakini nasita kutuma hiyo noti yao wanayotaka kwa njia ya PayTrade. Ushauri wajameni!
 
Pay trade ni huduma salama ukilinganisha na kutuma pesa moja kwa moja kwa supplier. Hii inatumika zaidi kwa website ya tradecarview ambayo inajumuisha wauzaji magari wengi. Unapotumia paytrade una uhakika pesa yako inafika salama na utatumiwa gari lako bila longo longo. Kuna huduma nyingine inaitwa paypal ambayo hutumika zaidi kwenye mtandao wa Ebay.
 
Asante Mwalimu, kwa hiyo nisihofu, maana jamaa wamenitumia kabisa Proforma Invoice na inatakiwa kwa kesho hiyo noti itumwe.
 
Kama unaagiza gari kupitia tradecar view then paytrade ndio njia salama zaidi kutuma hela. Kukitokea tatizo lolote ni rahisi kufuatilia paytrade kuliko kufuatilia kwa muuzaji moja kwa moja na at the end of the day wanakurefund hela yako kama biashara imeshindikana.
 
Mbali na Paytrade! Je kampuni kama Imperial Solution Ltd (ISL) ni kampuni tapeli au la? Maana Japan sasa kuna makampuni mengi hewa...na watu wanalizwa kila leo sehemu mbali mbali ikiwemo Tanzania. Nataka kuagiza gari kutoka kwenye hiyo Kampuni kama kuna mtu anauzoefu nayo naomba anijuze! Sina shaka na majibu ya kutumia Paytrade kufanya malipo ya gari niipendayo!! Natanguliza shukrani zangu.......
 
Uwe makini sana ndungu yangu maana huchelewi kukukuta hilo neno limechakachuliwa kwa mfano Wajapani walikuwa na saa ya mkononi maarufu sana inaitwa Seiko.....Wachina.. wakachakachua ..wakaita yao sesko...Take care!......Wanaweza wakalichakachua hilo neno badala ya PAYTRADE wakaita PAYTRAD
 
Mbali na Paytrade! Je kampuni kama Imperial Solution Ltd (ISL) ni kampuni tapeli au la? Maana Japan sasa kuna makampuni mengi hewa...na watu wanalizwa kila leo sehemu mbali mbali ikiwemo Tanzania. Nataka kuagiza gari kutoka kwenye hiyo Kampuni kama kuna mtu anauzoefu nayo naomba anijuze! Sina shaka na majibu ya kutumia Paytrade kufanya malipo ya gari niipendayo!! Natanguliza shukrani zangu.......

Sijawahi kusikia kampuni hii....lakini jaribu kuulizia reference zaidi kutoka kwa watu wengine.
 
Kwa anayejua jinsi ya kuagiza gari kwa njia ya
paytrade anijuze tafadhali. Kuna ndugu yangu
anata atumie huo mfumo kaambiwa ni mzuri kwa
usalama wa fedha badala ya kutma
moja kwa moja kutoka kwa seller.

Nawasubiria wakuu!
 
Unalipa commision 5% ya CiF utayolipia hilo gari wao wanapokea pesa wanamuarifu dealer uliepata nae kuhusu bei na yule dealer anaituma ile gari na doc zikifika tu,wewe muagizaji una confirm kwa paytrade kuwa gari na doc zimefika...hapo ndio dealer wako analipwa pesa zake!!!ni njia salama saaanaaa!!!!
 
Sikumbuki kama niliwahi wauliza hili, naomba
jamani nijuzeni juu ya uhakika wa hii njia ya
kununua gari japan kwa kutumia Paytrade.

Naona wahusika waniongelea kama secure method je, ni kweli au ndo
mpango mzima wa kutaka kuingizana kingi?

Nijuzeni please, nataka nilisahau lile swali la
'hivi jirani kwa nini hununui gari'?.

Nawasubiria!
 
Nimenunua Gari Mara 2 via paytrade! Ni Huduma inayohakikisha kwamba hela yako haitaibiwa! Tradecarview ni kampuni na ndani Yake pana watu wameregister wanauza magari, when you use paytrade actually hela ukituma zaenda kwa trade car view na wakiridhika Gari limetumwa na ni Kama like la kwenye invoice Ndio Wana release funds kwenda kwake, ikitokea shida they refund you.
 
Back
Top Bottom