PayPal Transaction

leh

JF-Expert Member
May 30, 2012
827
369
natafuta mdau ambaye ana dollars kwenye PayPal yake tufanye biashara maana nimechoshwa ni CRDB. sijaweka post kwenye matangazo maana watumiaji wengi wa PayPal wapo humu ndani
 
natafuta mdau ambaye ana dollars kwenye PayPal yake tufanye biashara maana nimechoshwa ni CRDB. sijaweka post kwenye matangazo maana watumiaji wengi wa PayPal wapo humu ndani
Mimi ninayo card ya bancABC ni mwisho wa matatizo. Account yangu kwa sasa ina dolar kama 12 hivi. Nikitaka kufanya manunuzi kama vile template za web huwa ndio naweka pesa.
 
Sasa huyu anataka akutanishwe na watu wenye PayPal si bora akazane na hii. Au akafungue Standard Chartered ila hawa Bank ABC wako vizuri sana
 
  • Thanks
Reactions: leh
Natumia hiyo card safi sana ndani ya dk 15 ushapata kard ya visa. Ujue watu wanang'ang'ania vibovu tu
kweli tunag'ang'ania vibovu. CRDB wamekataa kunibadilishia namba ya simu na niliyokuwa natumia zamani napata shida sana kujua kama hela imekatwa nikiwa porini porini
 
Ni Banc ABC wanaitwa sijui hiyo Bank ABC au ABC Bank inaweza mislead mtu

Wanapatikana Arusha na DSM

DSM wana branch mbili nazozijua,Ukienda pale na National ID yoyote inayotambulika unapata card hapo hapo wanaziita Cash Cards yaweza kuwa ya USD au TZS

Ninayo card yao ya mda kwa mda mrefu unfortunately siku hizi ukifanya transaction haupati SMS notification kwamba hela imekatwa, sijui kama wote wana experience hili,wakati naanza SMS zilikua zinakuja kawaida kila nkifanya transaction.

Kama hauna hela kwenye account au hela haitoshi e.g unataka nunua 5$ service/material wakati wewe account ina 3$ watakulima 1,200/= kama adhabu.

Faida yao hamna mambo ya Bloking transactions,hhamna delays za refund na ziko automatic in 48hrs

Conversion rate yao sina hakika nayo ukilinganisha na competitors wengine
 
Back
Top Bottom