PayPal Tanzania

PayPal Tanzania

Sajili laini ya Voda yenye tarakimu za zamani kama 075... au 076. Laini mpya za 072... zinakataa. PayPal bado haizitambui. Hakikisha namba hiyo ya voda unaiweka kwenye account yako ya PayPal. Kama PayPal account yako ulikuwa unaitumia kufanya malipo, basi hawatakudai verification documents. PayPal yangu nimeitumia tangu 2018 kufanya malipo online, so nilipoilink na M-Pesa App nilianza kupokea pesa papo hapo bila ku-verify chochote.
 
Attachments

  • Screenshot 2026-09-24 120052.png
    Screenshot 2026-09-24 120052.png
    39 KB · Views: 3
  • Screenshot 2026-09-24 120111.png
    Screenshot 2026-09-24 120111.png
    14.9 KB · Views: 3
Sajili laini ya Voda yenye tarakimu za zamani kama 075... au 076. Laini mpya za 072... zinakataa. PayPal bado haizitambui. Hakikisha namba hiyo ya voda unaiweka kwenye account yako ya PayPal. Kama PayPal account yako ulikuwa unaitumia kufanya malipo, basi hawatakudai verification documents. PayPal yangu nimeitumia tangu 2018 kufanya malipo online, so nilipoilink na M-Pesa App nilianza kupokea pesa papo hapo bila ku-verify chochote.
Chief, naomba nielekeze namna ya kujiunga PayPal,, Kuna kitu nataka kununua eBay
 
Kununua kwa PayPal ni rahisi na salama. Fungua akaunti ya PayPal hapa Send Money, Shop, Manage Payments & More | PayPal TZ jaza taarifa zako sahihi. Cheki hapa:
View: https://youtu.be/a3b6jGzcCoQ

Unganisha PayPal akaunti yako na Benki akaunti yako. Link kwa kutumia zile namba 16 zinakuwa kwenye mafungu ya nne nne, siyo namba yako ya akaunti.

Ukishaunganisha wakati wa malipo chagua option ya PayPal badala ya MasterCad au Visa. PayPal itakata kile kiasi kutoka kwenye benki yako. Na mtu aliyepokea malipo ataona umemlipa kwa PayPal, hawezi ona taarifa yoyote kuhusu akaunti yako ya benki. Manunuzi yangu ya kwanza kwa PayPal yalikuwa eBay pia.

Tumia laini ya Voda unaposajili ili uwe na advantage ya kupokea pesa kwa PayPal ikiwa utaiunganisha na M-Pesa App. Hakuna namna utapokea pesa kwa PayPal bila kufanya hivi.
 
Back
Top Bottom