Karibu ndugu. Swali zuri hiyo tunaondoa majani yasiote kwenye maungio ya paving
Nafikiri sio sahihi kabisa kuweka nylon chini ya paving blocks.
Moja kati ya faida kubwa ya paving blocks ni kusaidia kupunguza changamoto za fall water (maji ya mvua), uwekaji wa paving blocks unasaidia kuruhusu kufyonza maji ya mvua (seepage/penetration of fall water) ili kuondokana na changamoto ya maji mengi (urban waste water) hasa katika miji mikubwa.
Zamani watu walikuwa wanapenda kuweka floor za zege ambazo zilikua zinatiririsha maji na kutoyaruhusu kwenda Ardhini, mbadala wa paving blocks ni kiruhusu maji kufyonzwa ardhini na kuacha floor kavu bila maji.
Sasa unapoweka nylon chini ya paving blocks, maana yake unazuia maji yasipenye kwenda ardhini, hivyo kusababisha maji kujaa juu ya paving wakati wa mvua na kusababisha tatizo la maji taka hasa katika miji mikubwa wakati mwingine kusababisha mafuriko.
Je nini kifanyike kuzuia majani yasiote?
Kwanza kabisa kama unaona majani yanaota maana yake chini ulishindilia (compact) mchanga wenye uchafu na mizizi (organic matter) kwahiyo mchanga unapopata maji unasababisha hiyo mizizi kuchanua
Lakini pia kama ujapanga paving blocks zako vizuri, maana yake unaacha nafasi kati ya paving block moja na nyingine, hivyo kuruhusu mzizi kuchanua katikati ya paving blocks
Nini kifanyike.
1. Hakikisha unaweka layer ya kutosha ya mchanga safi na kushindilia kabla ya kulaza paving blocks, hakikisha unaondoa uchafu wote kwenye mchanga kabla ya kuanza kuushindilia.
Lakini pia hakikisha unatumia mchanga unaoshauriwa ambao hau-support kirahisi kuota kwa nyasi.
2. Unaweza pia kuweka dawa (hii ni option) kwa ajili ya kuzuia ukuaji wa mimea (lakini kama utafanya kwa ufahasa pendekezo hapo juu basi hii sio muhimu sana)
3. Unapolaza paving blocks, hakikisha unazipanga vizuri ili kupunguza nafasi kati ya paving block moja na nyingine.
Naomba kuwasilisha.