Muju4
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 5,489
- 7,445
Kwanza nianze na pongezi nzito kwakuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam..hii inaonesha ni namna gani bidii katika kazi huzaa matunda,sikuwa na shaka kuwa utapata uteuzi huu kwasababu Mh. Rais alishakuahidi siku alipokuwa akiongea na wazee wa Dar es salaam na kwakuwa Mh. Rais ni mtu makini ni lazima awajue watu makini kama yeye.Rai yangu kwako sasa uendeleze kasi yako ile ile maana mjuhudikaji hulipwa kutokana na juhudi zake,wahudumie watu wa Dar es salaam kwa umakini Mkubwa na Mungu atakulipa KIKUBWA zaidi ya HICHI......narudia tena Hongera sana na kua nafasi kubwa mbele yako hapo baadae wale wote wanaokuangalia kwa jicho la HUSUDA Mungu ataendelea kuwaonesha kuwa wewe ni mtu makini na kwa mabaya watakayo kuombea Mungu atakubariki ili waendelee kushangaa