Paul Makonda: Meya Isaya Mwita ni mwanasiasa bora tofauti na viongozi wengine wa CHADEMA

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,695
1,470
RC wa Dar es Salaam Mh. Makonda amempongeza Meya wa jiji lake mstahiki Isaya Mwita kwa namna anavyosimamia miradi ya maendeleo jijini tofauti na viongozi wengine wa CHADEMA ambao kazi yao ni kuwasakizia watoto wa wenzao waingie barabarani wakavunjwe miguu.

Meya Mwita amekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na viongozi wa serikali bila kujali itikadi ya vyama. Makonda ameyasema hayo katika sherehe ya wiki ya maji katika ukumbi wa JNICC.

========

makonda+pic.jpg

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesifia utendaji kazi wa meya wa jiji Isaya Mwita kwa kile alichodai hayumbishwi na misimamo ya vyama.

Akizungumza leo Machi 16, Makonda alisema Mwita ambaye ni diwani wa CHADEMA hana tabia kama za wenzake na muda mwingi anafikiria maendeleo.

Akiwa katika uzinduzi wa wiki ya maji baada ya Mwita kumkaribisha kuzungumza, Makonda alianza kwa kumtania,

"Meya nilijua utazungumzia maandamano ila niseme wazi namkubali sana Isaya, ni miongoni mwa watu ambao unaweza kukaa nao mkazungumzia maendeleo."

"Hii ndiyo aina ya maandamano inayotakiwa. Tunataka kuandamana kwa kujadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto kwa wananchi tunaowaongoza.

"Wangekuwa wale wengine wangejiweka huko lakini huyu anapenda maendeleo.

"Wengine wanasubiri wawaingize watoto wa watu barabarani waandamane wavunjwe miguu halafu wawatafute watu wa Ulaya wawape hela," amesema Makonda.

Chanzo: Mwananchi
 
Rc wa Dsm mh Makonda amempongeza Meya wa jiji lake mstahiki Mwita kwa namna anavyosimamia miradi ya maendeleo jijini tofauti na viongozi wengine wa Chadema ambao kazi yao ni kuwasakizia watoto wa wenzao waingie barabarani wakavunjwe miguu. Meya Mwita amekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na viongozi wa serikali bila kujali itikadi ya vyama. Makonda ameyasema hayo katika sherehe ya wiki ya maji katika ukumbi wa JNICC. Source TBC
Ukiona Adui yako anakushauri au anakusifia basi kuna mahali kakukamata
Sitashangaa akijivua uMEYA nakuunga Mkono viwanda
 
RC wa Dar es Salaam Mh. Makonda amempongeza Meya wa jiji lake mstahiki Isaya Mwita kwa namna anavyosimamia miradi ya maendeleo jijini tofauti na viongozi wengine wa CHADEMA ambao kazi yao ni kuwasakizia watoto wa wenzao waingie barabarani wakavunjwe miguu.

Meya Mwita amekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na viongozi wa serikali bila kujali itikadi ya vyama. Makonda ameyasema hayo katika sherehe ya wiki ya maji katika ukumbi wa JNICC.

Chanzo: TBC
Nakumbuka Magomeni Kota tulimbagua kisa sio mwanaccm siasa haziendi hivyo
 
Bashite sterling wa utekaji anashauri kitu gani Chadema, amshauri babake sizonje namna ya kuongoza nchi kwa kuheshimu misingi ya katiba ya nchi na siyo kuhubiri amani huku mkononi ameshika pyu pyu na kwa upande wa kiunoni ameficha jambia na panga
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom