Hi coverage ya Clouds FM haikuwa balanced kutoa picha halisi
Air time kubwa kapewa Makonda ili ajisafishe na Mpanju akimsadia
Hili liko wazi hata kwa mtu asie na elimu ya msingi (darasa la saba) kama ilivo ainishwa kwenye katiba inayopendekezwa
Kwanini Clouds hawakufanya initiative za kutafuta watu wengine waliokuwa kwenye mdahalo..ambao wako neutral..sio Wahariri wa habari tu ambao for some reasons watatoa maelezo kwa mlengo wa vyombo vyao vya habari?
Clouds FM nadhani ni chombo cha habari kisicho na credential za misingi ya habari za kumkomboa mwananchi
.nadhani ni busara kwao kuendelea na habari za mambo rahisi rahisi tu kama kuandaa matamasha, Fiesta, habari za michezo na interviews za wasanii wa bongo flavor na Bongo movies...
kwenye issues sensitive zinazo husu nchi yetu waache watu wenye ueledi wa tasnia ya habari wafanye hiyo kazi ya kumkomboa Mtanzania..wao tutawasikiliza baada ya kazi kwenye sports extra tukiwa Bar na Tusker lite ya baridi!
Mimi nimemsikiliza Huyo Amon Mpanju..kwa maneno yake mwenyewe amesema hakuna mtu aliye mpiga tofauti na Makonda anavyodai alikuwa ana mlinda kwamba kuna watu walikuwa wana mpiga...
Mpanju mwenyewe kasema kuna vijana walimfuata kumwambia aachane na Makonda wao wamlinde yeye ndo akakataa..!
Makonda anamtumia Mpanju kudistract main agenda kwamba yeye na UVCCM wenzie ndo waliorganize hayo mabango na fujo zote zilizo tokea..hata kama yeye ukumbini hakupiga mtu lakin amehusika directly kuandaa huu uhuni wote.
Amoni Mpanju anaonekana ana akili lakini anataka kujitoa akili kutumika kutetea upuuzi wa CCM, amepoteza mantiki na kuanza kubishana na Warioba kuwa katiba pendekezwa haijasema elimu ya msingi ni darasa la saba..wakati hata kipengele cha elimu kama kigezo cha Mbunge kimetaja awe na darasa la saba (ambayo ndo elimu ya msingi)