Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,351
- 18,606
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, amewataka viongozi na waumini wa kanisa kuacha tabia ya kulaumu na kunyooshea viongozi kidole, badala yake wazidishe maombi kwa ajili ya Rais Samia Suluhu Hassan na taifa kwa ujumla.
Akizungumza na viongozi wa Dini katika Kanisa la KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati, mbele ya waumini kanisani, Makonda amesisitiza kuwa kanisa halina sifa ya kunyoosha kidole au kushindana kauli na matamko mtandaoni, bali lina kanuni na misingi yake ya kiroho ya kutatua changamoto kupitia maombi na magoti.
Makonda amebainisha kuwa vita vya kiroho haviwezi kupigwa kwa kutumia njia za kimwili au za mtaani, hivyo ni wajibu wa kanisa kuendelea kusimama katika maombi ili kuleta majibu na amani katika nchi.