Paul Makonda atangaza Wizara yake imetenga Bilioni 50 ili kuwawezesha vijana wanaojihusisha na sekta ya ubunifu

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetenga mfuko wenye Sh50 bilioni kwa ajili ya kuwawezesha vijana wanaojihusisha na sekta ya ubunifu nchini, hatua inayolenga kukuza uchumi wa ubunifu na kutoa fursa zaidi za kiuchumi kwa vijana.

Akizungumza jijini Arusha jana Machi 11, 2026, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda alisema mfuko huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, yenye lengo la kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia sekta ya habari, sanaa na ubunifu.

Alisema, awali Wizara ilikuwa imepangiwa Sh20 bilioni lakini baada ya mazungumzo na Benki ya CRDB, kiwango hicho kimeongezwa na kufikia jumla Sh50 bilioni ili kupanua wigo wa vijana watakaonufaika na mfuko huo.

Alieleza kuwa kwa sasa kinachosubiriwa ni tarehe rasmi ya uzinduzi wa mfuko huo, ambapo baada ya uzinduzi fedha hizo zitaanza kutolewa kwa vijana waliopo katika sekta ya habari, sanaa na ubunifu ili kuwawezesha kukuza kazi zao na kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa.

“Wizara inapanga kuzindua rasmi mfuko huo katika hafla maalum inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni, ambapo Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.”

Your browser is not able to display this video.
 
Mambo ya fedha za Wizara si ni mpaka Bajeti ijadiliwe na kupitishwa na bunge? Au sass hivi kila kitu kinaenda kwa maamuzi tu ya watu wachache? Mfano Kodi za magari na ushuru bandarini siku zote tunajua ni suala la kibajeti, bunge ndio linapitisha viwango na tozo, lakini sasa hivi kila siku kodi inabadilika, anayepanga sijui ni kamishna wa TRA, Abdul au Boss wa DP World.

Sasa na haya mambo ya wizara kuwa na fedha kabla hata ya bunge la bajeti. Hii si ni hatari?? Zinaingiaje na zinakaguliwaje?
 
Bora warudishe kidogo kwa chawa zitaingia kwenye mzunguko japo ni makombo, wanakula sana hawa jamaa yani ni kama viwavijeshi!
 
Rushwa tu kutafuta mamaduro akubalike angalau kidogo
Mana hakuna sekta hiyo, ubunifu ni njia ya kwrnda extra miles kwemye sekta yoyote ile iwe ya afya, kilimo, nk. Makomda mpaka kuwekwa pale ni mkakati ule, hizo h3la zinaenda sekta ya ubunifu mtaan huzioni! Utawqona wadudu wa arusha wanacheza na mabodaboda mi3z miwili hela zimeisha
 
BBT
 

Mbinu za kuficha tatizo yani kuwafool wananchi wasahau na kumuacha mhalifu apite salama kwa vipande hivi vya fedha
 
“Wizara inapanga kuzindua rasmi mfuko huo katika hafla maalum inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni, ambapo Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.”

Nadhani makonda ni mpenda sherehe na matamasha (kumbuka nyama choma, landrover na mengine mengi) Kwenye hizi shughuli anatuibia!
 
Ili uwemfanyalazi mzuri kwenyesekta yyte lazima ujue kwanza JD zako.akonda hajui .ilala ya kazi yake.anapuyanha tu
 
Wizara yake ina bajet kiasi gani? Asije akawa anawaingiza watu mjini.
 
Mambo ya Vijana si yana wizara yake? Mbona kuingilia mambo ya wengine??
Zile bilioni mbili za watengeneza maudhui zimeisha?
 
Huyo tapeli alipokuwa mkuu wa mkoa wa Arusha aliwadanganya kuwa atapeleka wanafunzi 1,000 kusoma India, akaitisha hadi usaili. Kumbe ilikuwa gia ya kugombea ubunge. Hadi leo hakuna mwanafunzi amepelekwa huko India. Hicho anachosema sasa ni mundelezo wa utapeli huo huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…