Kwahiyo huyo mkuu wa mkoa mpya anafanyia kazi zake nyumbani kwake?Salaam Mkuu,
Sasa Wiki mbili zimeisha baada ya aliyekuwa mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar kutenguliwa Cheo chake hicho baada ya yeye kuamua kugombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni ambapo kura zake hazikutosha.
Lakini tangu kipindi hicho hajakabidhi Funguo za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Mteule mpya.
Kabla ya Jumatatu anatakiwa awe amekabidhi ofisi kwa Mhe. Aboubakar Kunenge Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar.
Kesho hakuna kazi. Je, leo atakabidhi Ofisi?
Kuna tetesi zinadai anataka ajiunge ACT-Wazalendo ili akagombee Kigamboni kama CCM hawatampitisha. Kuna Nzi amesema atamuuliza swali hilo siku ya kukabidhi Ofisi. Yajayo yanafurahisha.
Thread
=====
UPDATES; 1324HRS
Zoezi la kukabidhi Ofisi leo limeahirishwa kutokana na sababu zilizo njena uwezo wa Mkuu wa Mkoa Kunenge. Ratiba imebana sana hivyo itapangwa siku nyingine ikiwezezekana Jumatatu.
Kama T bag alivyomeza funguo
Namuonea huruma sana katambi. Tamaa imemponza. Pamoja na usomi wake lakini alishindwa kufanya utafiti mdogo kama mazingira yana mruhusu kushinda au kushindwa.
Ndio mkuu. Ni msomi mzuri tu wa sheria.Katambi ni msomi?!
Alijua hawezi tumbuliwa.Inawezekana Makonda, alijua siku zake za kuwa RC zinahesabika.
Ndio maana akaamua kukimbilia kwenye Ubunge.?
Kilaza yule kasoma pale St Augustine Mwanza kwa mbinde. Hata law school hajasoma.Ndio mkuu. Ni msomi mzuri tu wa sheria.
Kuna mtu amenitonya kua kutokana na umahiri wake kwenye sheria, Diallo alishawishika kumuajiri kama mwanasheria wa Sahara media.Kilaza yule kasoma pale St Augustine Mwanza kwa mbinde. Hata law school hajasoma.
Kuna mawili either hajakabidhi nyaraka za offisi ama jengoSasa kama hajakabidhi huyu mkuu mpya anatekelezea wapi majukumu yake...!?
Una maana haendi ofisini!?
Na mimi ndiyo nimeshanga, nikauliza hajakabidhi nyaraka au funguo za offisi, hapa kunamkanganyiko, ika naona ni nyaraka za offisiJamani wewe, mbona umeongea uwongo hivi?
Hivi kweli funguo za ofisi ya umma hutembea nao watumishi?
Ofisi yake hufunguliwa na watumishi wa chini ufunguo haondoki nao mtu yoyote hubaki ofisni.
Useme hajakabidhi ofisi ikiwa na maana taarifa, watumishi nk...ila si funguo.
Mwacheni jamani apumzike!!!
Na ni formality tu, nyaraka huwa zinabaki ofisini. Ni kueleza tu kuna hili na hili, tumefanya lile na lile, bado hili na lile.Na mimi ndiyo nimeshanga, nikauliza hajakabidhi nyaraka au funguo za offisi, hapa kunamkanganyiko, ika naona ni nyaraka za offisi
daaah jamaa alijua atabaki mule mileleNakumbuka alivyoteuliwa ukuu wa mkoa inasemekana gsm waliikarabati kwa takribani milioni 400
Akifikiria hilo anatamani ameze funguo.