Paul Makonda alitakiwa akabidhi Ofisi leo, zoezi limeahirishwa hadi Jumatatu. Je, Makonda atakanusha kugombea Kigamboni kupitia ACT-Wazalendo?

wagotheleopardskiller

Senior Member
Jan 9, 2020
105
225
Salaam Mkuu,

Sasa Wiki mbili zimeisha baada ya aliyekuwa mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar kutenguliwa Cheo chake hicho baada ya yeye kuamua kugombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni ambapo kura zake hazikutosha.

Lakini tangu kipindi hicho hajakabidhi Funguo za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Mteule mpya.

Kabla ya Jumatatu anatakiwa awe amekabidhi ofisi kwa Mhe. Aboubakar Kunenge Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar.

Kesho hakuna kazi. Je, leo atakabidhi Ofisi?

Kuna tetesi zinadai anataka ajiunge ACT-Wazalendo ili akagombee Kigamboni kama CCM hawatampitisha. Kuna Nzi amesema atamuuliza swali hilo siku ya kukabidhi Ofisi. Yajayo yanafurahisha.

Thread

=====

UPDATES; 1324HRS

Zoezi la kukabidhi Ofisi leo limeahirishwa kutokana na sababu zilizo njena uwezo wa Mkuu wa Mkoa Kunenge. Ratiba imebana sana hivyo itapangwa siku nyingine ikiwezezekana Jumatatu.
Kwahiyo huyo mkuu wa mkoa mpya anafanyia kazi zake nyumbani kwake?

Sent from my SM-N910W8 using JamiiForums mobile app
 

Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,204
2,000
Mkuu wa Mkoa Mpya hataki upumbavu
Bashite alipanga kufanya sherehe kukabidhi Office Naona Mkuu wa Mkoa amelisambaratisha zoezi mpaka Jumatatu (siku ya kazi) hakuna tarumbeta wala vinanda kabidhi funguo mafile sepa.
 

Nakukunda

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
582
1,000
Napata picha jamaa kafika na mbwembwe zake secretary anamwambia suburi nimpigie mkuu kaenda kwenye ziara...Mkuu anapigiwa simu anakata anaambiwa atume sms niko kwa ziara...secretaty na makonda wanatuma sms mkuu anawajibu wasubiri anatarajia kurejea soon..makonda anazunguka zunguka kwenye corridor na kaambiwa asubiri...baadae mkuu anatoka nje ya ziara anamwambia ratiba imebana wafanye j3...makonda anatoka nje huku anazungusha funguo zake anapanda gari yake hasira ya kupotezewa muda...

Akiwa njiani anakumbuka anahitaji mtoto wa pili atampataje na US wamempiga ban sio yeye tu ila na familia yake....

Anawaza Lissu karudi kapokelewa na nyomi...usiyempenda kaja....


Anamalizia wajumbe wa kigamboni

Anamalizia kwa sonyo la Mange Kimambi
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
14,498
2,000
Mwenye picha ya offisi ya mkuu wa mkoa dar atuonyeshe ina hadhi gani, mpaka ndugu yetu akimbize funguo
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
14,498
2,000
Jamani wewe, mbona umeongea uwongo hivi?

Hivi kweli funguo za ofisi ya umma hutembea nao watumishi?

Ofisi yake hufunguliwa na watumishi wa chini ufunguo haondoki nao mtu yoyote hubaki ofisni.

Useme hajakabidhi ofisi ikiwa na maana taarifa, watumishi nk...ila si funguo.

Mwacheni jamani apumzike!!!
Na mimi ndiyo nimeshanga, nikauliza hajakabidhi nyaraka au funguo za offisi, hapa kunamkanganyiko, ika naona ni nyaraka za offisi
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
14,498
2,000
Ila pia ni kwa mujibu gani acheleweshe ufunguo? Kitu nachokiona ameacha mambo yapite yaliyo trend then siku anakabidhi ufunguo watu wote jicho kwake na baba atamuonea na huruma
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom