Paul Makonda alitakiwa akabidhi Ofisi leo, zoezi limeahirishwa hadi Jumatatu. Je, Makonda atakanusha kugombea Kigamboni kupitia ACT-Wazalendo?

Mwamalili

JF-Expert Member
Sep 2, 2019
1,066
2,000
Salaam Mkuu,

Sasa Wiki mbili zimeisha baada ya aliyekuwa mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar kutenguliwa Cheo chake hicho baada ya yeye kuamua kugombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni ambapo kura zake hazikutosha.

Lakini tangu kipindi hicho hajakabidhi Funguo za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Mteule mpya.

Kabla ya Jumatatu anatakiwa awe amekabidhi ofisi kwa Mhe. Aboubakar Kunenge Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar.

Kesho hakuna kazi. Je, leo atakabidhi Ofisi?

Kuna tetesi zinadai anataka ajiunge ACT-Wazalendo ili akagombee Kigamboni kama CCM hawatampitisha. Kuna Nzi amesema atamuuliza swali hilo siku ya kukabidhi Ofisi. Yajayo yanafurahisha.

Thread

=====

UPDATES; 1324HRS

Zoezi la kukabidhi Ofisi leo limeahirishwa kutokana na sababu zilizo njena uwezo wa Mkuu wa Mkoa Kunenge. Ratiba imebana sana hivyo itapangwa siku nyingine ikiwezezekana Jumatatu.
ACT WAZALENDO watakuwa wamelamba dume maana huyo alikuwa naibu rais huko CCM ni zaidi ya Membe.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
142,301
2,000
UPDATES; 1324HRS

Zoezi la kukabidhi Ofisi leo limeahirishwa kutokana na sababu zilizo njena uwezo wa Mkuu wa Mkoa Kunenge. Ratiba imebana sana hivyo itapangwa siku nyingine ikiwezezekana Jumatatu.
 

Mkwala

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
1,054
2,000
Mbona na Ole Sendeka amekabidhi wiki hii hii,sasa kwa Makonda mbona inakuwa habari kubwa sana.Kwa style hii Mhe. anaweza kumteua tuu halafu ampe Cheo zaidi mpaka tushangae.
 

jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
6,871
2,000
Nakumbuka alivyoteuliwa ukuu wa mkoa inasemekana gsm waliikarabati kwa takribani milioni 400
Akifikiria hilo anatamani ameze funguo.
Aliwatesa sana wale, jamaa. Kuanzia kuwapora magari mpaka kuwakamuwa hela kimabavu, ila GSM nawo hatuwezi waonea huruma biashara zao zina maswali mengi mno..
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,328
2,000
Baada tu ya kura za maoni kule CCM taifa likapatwa na msiba wa hayati Mkapa so Kunenge alikuwa busy na shughuli za msiba.

Jumatatu panapo uzima zoezi litakamilika bwashee!
Kilichomuondoa sio kura ya maoni. Na msiba umetokea zaidi ya wiki moja toka atemwe.
Au alikuwa anapewa muda wa kuondoa hirizi zake?
 

zinj

JF-Expert Member
Jan 1, 2013
976
1,000
kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa kindugu-ndugu chini ya awamu hii, si ajabu kukuta kumbe Makonda bado ni RC while huyu wa sasa ni proxy tu.

there're all signs Bashite is still in control.

Mkuu:
Hakuna kitu cha namna hiyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom