Paul Chizzi amuumbua Mwakyembe


Kuna mambo mengine hayaitaji hata kujua mambo ya anga kama kukodisha ndege pasipokujulikana na wausika wa serikali, ndege moja kuwa na wafanyakazi zaidi ya 200, huyu atakuwa alikuwa akinufaika kwa njia flani ndo maana inamuuma na pia hizo uniform si zitakuwa na rekord ktk matumizi? Basi hesabu likaguliwe then mwongo atajulikana
 
Kama aliyekanusha ana ushahidi basi Mwakyembe shule haijamsaidia au nitaamini kuwa hata ukiwa msomi na intergrity yako ukiingia CCM unakuwa juha .

hilo ndilo tatizo kubwa!
 
Mwakyembe ni mpenda misifa, msiomjua nawapa pole.

Namjua Dr Mwakyembe;ni Mbunge wangu!Watz tujiandae kumlipa Chizi mamilion ya pesa akienda mahakamani;Dr Mwakyembe ni mtu wa kupenda sifa zisizo na msingi!Yeye na Magufuli hamna aliyemzidi mwenzake!

Kusitishwa kwa ajira ya mtu kuna utaratibu wake inabidi ufuatwe na sio kuwaita waandishi wa habari na kutangaza fulani nimemfukuza kazi!Kwa ufupi Dr Mwakyembe ni abuser mkubwa wa haki za binadam!

Kyela 2015 tumekwisha mkataa na analijua hilo!
 
Kama kulikuwa na option ya kushona kwa bei ya chini ambayo ni $ 200 kwa uniform kwa nini hawakuitumia ilhali shirika halina na uwezo mkubwa kwa sasa, mimi haja ni convice hata kidogo $ 18000 still is too much lets be realistic.
 
Kama kutumia dolla 18000 kununua uniform tu bado watu wanamtetea Chizzi basi kuna tatizo somewhere kwenye vichwa vyetu. watanzania tuamke kama mtu habani matumizi katika kampuni anayoiongoza basi hafai.kulikuwa na sababu gani kununua sare hizo ulaya?Mwakyembe kaonesha njia na mawaziri wengine wafuate.kila anaye hujumu Nchi lazima akutane na adhabu.MKIENDEKEZA CHUKI BINAFSI KWA SABABU ZOZOTE ZILE NCHI HAITA PIGA HATUA. VIVA MWAKYEMBE.
 
Mkuu kama una nafasi nakuomba ukanunue gazeti la leo la Guardian ndio utaamini kuwa kumbe hata wale wenye Phd za ukweli wana matatizo.

Hakuna binadamu ambaye ni perfect, hata kama una PhD. Kumi.
 
Sidhani kama shirika linao wafanyakazi hao unasema. Chizi siye aliwaajiri. ATCL ilikufa sababu ya hao maafisa wa serikali na wanasiasa kama Mwakyembe kuingilia utendaji.
 
Tafuta mashirika mengine kiasi gani kununua sare za wafanyakazi wake. Kwa umasikini wetu unaweza ona hiyo pesa ni nyingi wakati ktk hali halisi ni pesa ndogo.
 
Kama mtu anaona USD 200 - 600 kwa unifirm ni kubwa hakuna namna waweza mweleza gharama za uendeshaji wa shirika la ndege akakuelewa. Akijua za mafuta Dar-Mwanza ni millioni 15 atashauri waweke maji.
Jamani uniform za wafanyakazi wa ndege sio mabatiki kama ya dancers. Suti tu ya rubani sio kama za MC. Kuna viwango vinavyotakiwa kimataifa, otherwise chini ya kiwango hata abiria hupati kama sio kunyang'anywa leseni ya aviation kabisa. . Ndege sio kama wa daladala jamani. Mi ningemheshimu Mwakyembe (PhD) akija na utafiti kutoka mashirika mengine kama Emirates, 540, Precision, KLM, etc. WAO GHARAMA ZAO ZIKOJE? Data Si zipo? Kwa nini tuongee tetesi? If you think education is expensive try ignorance' likewise, If we think Airline Business is expensive let's try daladala"
 
Kama ni hivi Chizi anachemka kwa kujitetea kwenye magazeti. Naanza kuwa na wasiwasi naye coz naona waandishi wengi wanakimbilia kumtetea badala ya kusubiria akajitetee pale Kisutu mahakamani..
 

Precision nasikia ilikuwa around 300Mils Tsh.. Lakini wao wana ndege 11 sasa nyie mnangapi?
 
Precision nasikia ilikuwa around 300Mils Tsh.. Lakini wao wana ndege 11 sasa nyie mnangapi?

Kama ni kweli Precision walitumia TZS 300 mil na wana ndege 11 umesema vema. Ila ujue kuwa kuna fixed costs ambazo haziendani na wingi wa ndege. Variable costs ndo zingetegemea idadi ya ndege. Hapa nategemea Mwakyembe angetoa amri kupunguza wafanyakazi ili nguo zinunuliwe chache. Nguo hizo zimenunuliwa kulingana na idadi ya wafanyakazi waliopo. Tunataka kujua ni nani amewaajiri na kama wote wanahitajika. Pia kujua pea ngapi zimenunuliwa na kama kuna ziada, kwa nini? Pia aseme kuna options zingine za kushona mabatiki kama sheria za usafiri wa anga zinaruhusu. This is what we want to hear from a PhD holder.
 
Hakuna hapa anayemtetea Chizi bali nina pinga njia zilizotumika kumfukuza!Sheria za kazi zinasema wazi kabisa njia zinazopaswa kufuatwa ili kumfukuza mfanyakazi!Dr Mwakyembe hajasema kama bodi ya udhamini ya ATC ilimuita Chizi kumsomea makosa yake then kumpa nafasi ya kujitetea kabla ya kumtimua!

Dr Mwakyembe anaingiza siasa kwenye ajira za serikali!
 

Sasa Wikolo u ve missed everything! Hata hesabu zimekushinda kupiga? nyie ndio mnaoeneza taarifa zisizo rasmi, umeambiwa uniforms ziligharimu U$ 18,000 including za ma-airhostess na pilots, kwamba uniform moja iligharimu kati ya U$ 200-600. Wewe hesabu hizo umezitoa wapi jamani?
 

Mdau, unajichanganya sasa, unajadili na kufanya reference kwenye gazeti la Tanzania daima lililomnukuu Waziri wakati mada hii inanukuu gazeti la the Gurdian linalokanusha taarifa za waziri kwa kumkariri Bw. Chizi kwamba mambo yamepotoshwa ikiwa ni pamoja na taarifa unazonukuu wewe kwenye gazeti hilo. Rejea mada husika.
 
But Mwakyembe should be very sceptical na huyu katibu wa wizara (Chambo) amekuwa akiche kwenye wizara ya Ujenzi na uchukuzi kwa muda mrefu,asije akamuingiza mkenge.
 

Tulinganishe hiyo RED ya Chizi na BLUE ya reliable source. Mh. Chizi hiyo imetoka ikirudi ina pancha. Tujipange kwa wizi mwingine.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…