Zakumi,
Hapo umenena mkuu.
Kwenye Biblia kua sentenso inayosema "mwanadamu siku zake ni miaka 70"!
Sasa unajiuliza, je ukishajipatia kila kitu kama Johnson Lukaza alivyojichumia kabla hata ya kuwa na miaka 35, je ile mingine 35 iliyobakia atafanya nini?
Zaidi Uchotaji huu laiti ungekuw ani mara moja na utumike kama mtaji au msingi, bali huendelea milele.
Sasa kwenye uchotaji, kunakuja rushwa na kuvunja sheria nyingine ambako hufikisha kupotea au kutoweka kwa ushahidi muhimu.
Nikirudi kwenye nia halisi ya kusema kuwa hili ni changa la macho, kwa kina Jeetu Patel na Lukaza, sijui ni vipi tunaweza kuwashikisha adabu. Je hatuwezi kuwashitaki kwa kutumia ile sheria ya uhujumu uchumi na hata kuwafilisi?
Inapokuja kwa Yona na Mramba, hata ukiwaingiza kina Chenge, Lowassa, Karamagi, Meghji, Msabaha, Mgonja, Mboma na wengine, inakuwa kama ni tosha kuwamaliza kisiasa kwa kuwashitaki kwa uzembe, matumizi mabaya ya madaraka na kupotea kwa mali za umma kutokana na maamuzi mabovu na uongozi mbaya.
Nafikiri doa hili litanata kama gundi kuliko kutafuta wapi walificha hela!