Patrobas Katambi: Kima cha chini mishahara ya Madereva chaboreshwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Serikali imepanga kima cha chini cha mshahara kilichoboreshwa katika sekta ya usafirishaji kilichoboreshwa ambacho kimeanza kutumika Januari Mosi mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Juni 12, 2023 na Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda.
Mwakagenda alihoji ni lini Serikali itashughulikia kuboresha ujira wa madereva wa magari ya IT.

Akijibu swali hilo Katambi amesema Serikali kwa kutambua mchango wa sekta mbalimbali katika uchumi ikiwemo sekta ya usafirishaji, tayari imepanga kima cha chini cha mshahara kilichoboreshwa ambacho kimeanza kutumika Januari Mosi mwaka 2023.

“Mshahara na maslahi kwa madereva imeboreshwa kupitia amri ya kima cha chini cha mshahara kipya,” amesema Katambi.

Amesema utaratibu wa kazi kwa madereva wanaoendesha magari ya IT unafanyika kwa kuingia makubaliano ya kazi kati ya mmiliki wa gari na dereva husika ambapo malipo hufanyika baada ya mhusika kufikisha gari linapokwenda.

Amesema mahusiano yaliyopo si ya ajira bali ni makubaliano/mikataba binafsi ya kibiashara.

Katambi ametoa wito kwa madereva wa magari ya IT kuingia mikataba ya kazi ya kibiashara na pale ambapo atatokea mwajiri au kampuni ambayo itaajiri madereva kwa ajili ya kuendesha magari ya IT atapaswa kuzingatia Sheria ya Ajira na mahusiano kazini ambayo inaelekeza ulipaji wa ujira kulingana na Sekta hiyo.

Mwananchi
 
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 46 leo Juni 12, 2023.


Msimamo wao ni kama wa huyu hapa...
👇
1686550417396.png
 
Back
Top Bottom