kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,876
Kwanza niseme wazi kabisa kwamba nakubaliana na meneno ya wahenga kwamba mwenzako akinyolewa zako tia maji. Juzi hapa CHADEMA walimvuna ndg Nyalandu kutoka CCM na leo CCM wamemvuna Patrobas , hiyo ndiyo siasa na kila siku mwenyekiti wa CHADEMA anasisitiza kwamba kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu. Kwahiyo waliiondoka ama ccm , cdm au ACT wametimiza usemi huo.
Ila nimemsikia ndg Patrobas Katambi akisema CCM inatoa fursa kwa vijana tofauti na huko upinzani na kwamba juzi aliona aliyekuwa mwenyekiti wake akiwa chuo amepewa mjumbe wa kamati Tanzanite. Kwa sentensi ile kaonesha wazi kwamba fursa anayoizungunza ni cheo au ulaji ambayo hata hivyo chadema hawawezi kuitoa kwasababu hawana serikali. Hivi kuna fursa zaidi ya kuwa mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA? AU MIMI NDIYO SIJUI MAANA YA FURSA KISIASA?. Kwa nafasi aliyokuwa nayo katambi ndani ya CHADEMA mimi naona chama kilimpa fursa tena fursa ya kuonesha uwezo wake , kipaji chake na huenda kwa hiyo nafasi yake angefika mbali. Ndg John Heche alianzia huko na leo ni mbunge au yeye alitaka fursa gani, kuwa mwenyekiti au?
Nimalizie kwa kusema haya, katiba imetoa nafasi na uhuru wa watu kuhama vyama wapendavyo kwahiyo hawa wametekeleza haki yao ya kikatiba wala watu wasitumie muda mwingi kuwalaumu. Ila nalaani sana siasa za fursa, siasa za vyeo, siasa zinazofanya vijana kudhalilisha utu wao ili tu wapate vyeo. Lazima vijana tufanye kazi zingine kujipatia maisha tusitegemee siasa. Tutakuwa wakosoaji wazuri sana, wateteaji wazuri sana kama tuna kazi zetu za kufanya. fanya siasa bila mategemeo ya zawadi na fursa za kupewa bali tutafute fursa wenyewe kwa kuthubutu kugombea nafasi na tuwe wavumilivu ndani ya vyama vyetu. Unaweza kuhamia chadema leo kumbe 2020 ungegombea kwa ccm ungeshinda au unahamia ccm leo kumbe 2020 ilikuwa bahati yako kwa CHADEMA.
Niwatakie watafuta fursa (vyeo ) kazi njema ila at least waje na sababu strong basi.
Kindikwili -Ndanda