Pato la wastani la Mtanzania mmoja mmoja lashuka. Je tutafika kwa mwendo huu?

Cicero

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
2,924
3,073
"........Mwaka 2015, Tanzania ilikadiriwa kuwa na idadi ya watu 47,351,275 na Pato la Taifa lilikuwa shilingi bilioni 90,863.68. Aidha, wastani wa Pato la kila mtu lilikuwa shilingi 1,918,928 mwaka 2015 ikilinganishwa na shilingi 1,730,405 mwaka 2014, sawa na ongezeko la asilimia 10.9.

Hata hivyo, Pato la wastani kwa kila mtu katika dola za Kimarekani lilipungua kutoka dola za Kimarekani 1,047 mwaka 2014 hadi dola za Kimarekani 966.5 mwaka 2015 kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.

Hivyo, ni dhahiri kuwa bado kunahitajika msukumo zaidi wa kuongeza ukuaji wa Pato la Taifa ili kufikia lengo aa Dira ya Maendeleo ya Taifa la kufikia wastani wa Dola za Kimarekani 3,000 kwa kila mtu na kuwa nchi ya uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025......."

Source: Speech ya mheshimiwa waziri wa fedha na mipango bungeni.
Swali, kwa spidi hii tutafikia middle income status by 2030 kweli?
 
Back
Top Bottom