Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

Habari zenu wakuu,

Mimi nina swali kuhusu ardhi, mimi ni diaspora lakini kwa sasa nipo kwenye mchakato wa kutafta kiwanja ili nijenge kibanda changu, lkn swali langu ni diaspora wanaruhusiwa kumiliki ardhi ama ndo maujanja maujanja 2.

Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Scino,
Kua diaspora sio ishu ishu ni uraia, unaweza kua diaspora na ukawa still ni raia wa Tanzania, ila kama uliukana uraia wa Tanzania kwa mujibu wa sheria ya Ardhi hauwezi.

Ila watu ambao sio waTanzania hua wanajenga tu under trustee ya mtu mwingine, tafta ndugu muaminifu au mwanasheria muaminifu au rafiki muaminifu, basi una nunua kiwanja ukitakacho kwa jina lake then utaendelea na ujenzi wako ila documents za umiliki wa icho kitu utakua unakaa nazo wewe.
 
Wakili,hivi kisheria Tanzania ni kosa gani na kifungo kipi humzuia mtu kugombea uongozi kama urais,ubunge na udiwani? Nilishswahi sikia eti ukifungwa miezi sita hurusiwi kugombea ukweli upoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakili,hivi kisheria Tanzania ni kosa gani na kifungo kipi humzuia mtu kugombea uongozi kama urais,ubunge na udiwani? Nilishswahi sikia eti ukifungwa miezi sita hurusiwi kugombea ukweli upoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kosa lolote la jinai ambapo utakutwa hatiani mahakama na kufungwa kwa muda unaozidi miezi sita.
 
Habarini wakili najua unaweza nisaidie mawazo kwnye huu utata unaonizunguka Mimi na majirani zangu kuhusu urasimishaji wa ardhi.mimi na majirani zangu tulinunua viwanja vikiwa Bado havijapimwa na tuka Jenga wote ikatokea mmoja wetu kajenga ukuta.

imekuja kampuni ya upimaji wanasema Yule mwenye ukuta hawezi kupimiwa barabara hivyo viwanja vyetu sisi wa upande wa pili ambao hatujajenga ukuta vimekatwa barabara hatua sita na kuwekwa bikon.

Sasa swali langu hv Hapo nafanyeje ili kupata haki yangu maana nimekatwa ubavuni Kuna barabara na mbele ya nyumba kunabarabara eti kukusaidia Yule aliyejenga ukuta kupata barabara ndo kiwanja changu kimekatwa barabara msaada wa kimawazo ndugu zangu mliosomea haya Mambo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kadada wa pili,
Ilo kampuni la upimaji ni wametoka manispaa au ni binafsi?

Basi chakufanya mapema, nenda mipango miji kaangalie hali ya ilo eneo kwa miaka ijayo na michoro yake ipoje, je eneo ambalo tayari limekwisha pangiwa shughuli zingine kwa miaka ijayo au vp? Kajua hali ya eneo husika, na kikawaida kila eneo hapa nchini hua limekwisha pangiwa miaka mingi mbele na mfanano wake utakavyo kua.

Usiwe na hofu upimwaji wa kitu chochote hausiani na maswala ya haki ya mtu ktk ardhi husika, yaan wapimaji ni watu tu ambao wamekuja kutekeleza walichoambiwa au kuagizwa na waliowatuma au waita, ila kulazimishiana haki ktk ardhi ni jambo lisilo kuwepo, mtu hawezi kuja tu kutoka alikotoka akasema kuanzia leo barabara itakua inapita hapa, hapana huo ni uchizi, kama haki ya njia ambayo kitaalam tunaita easement ina taratibu zake na hatua zake sahii, na swala la barabara kwa bahati nzuri hua tunatumia sheria inayoanzia miaka ya 1930 na ambayo target yake hua imekua ktk main roads.

So usiogope, kajua status kwanza ya ilo eneo huko mipango miji au halmashauri, then uta tafuta wapimaji binafsi wakupimie alaf utaenda kurasimisha ilo eneo wizarani na utapata hati yako na utajiwekea mipaka yako. Kwa msaada zaidi mtafute wakili yoyote alie eneo karibu yako atakusaidia hizi process kama utaona zinakuchanganya.
 
Habari zenu wakuu, me nna swali kuhusu ardhi, mimi ni diaspora lkn kwa sasa nipo kwenye mchakato wa kutafta kiwanja ili nijenge kibanda changu, lkn swali langu ni diaspora wanaruhusiwa kumiliki ardhi ama ndo maujanja maujanja 2
Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata kama sio raia Kampuni yangu inakuwezesha kujenga na kumiliki kwa mkataba mrefu say 98,65,32 years with selling rights whenever you want.
 
Mkuu naomba kujua!

Mfano mnahamishwa na wawekezaji wa madini ni sheria zipi zinachukuliwa ili waamishwa wapate haki zao ikiwa ni pamoja na stahiki na thamani ya ardhi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gormahia,
Sheria zinazotumika ni za madini, na labda kidogo sana ardhi, kwakua sheria za ardhi hazitambuibkama madini ni sehemu ya ardhi.

Na tangu ardhini inapohusishwa na madini basi sheria ya ardhi ina koma kufanya kazi na hapo hapo sheria za madini zina angaliwa zinasema nini?.

Ulipwaji wa fidia upo na ni lazima.
 
Naombeni kuuliza wakuu, hivi hakimu wa mahakama ya mwanzao ambaye alisaini katika wosia flani kama shahidi, je anaweza kuja kusikiliza shauri lolote linalohusu wosia ule hapo baadae? kama kuna sheria inatamka hilo au kesi yoyote ile mnisaidie wakuu
 
naombeni kuuliza wakuu,,, hivi hakimu wa mahakama ya mwanzao ambaye alisaini katika wosia flani kama shahidi, je anaweza kuja kusikiliza shauri lolote linalohusu wosia ule hapo baadae? kama kuna sheria inatamka hilo au kesi yoyote ile mnisaidie wakuu
Hawezi na haruhusiwi.
 
666 chata,
Naomba kufahamu haki ambazo na stahiri kupata pale ninapo taka kuacha KAZI ambayo nime ajiliwa
Unapo acha kazi unakua ni kama umevunja mkataba mwenyewe na hasa pale mkataba wako bado haujaisha, kwaio mpaka unaacha kazi kwa hiari ni lazima kusiwe na makandokando ya nyuma yaani likizo umeenda zote, umelipiwa huduma za afya na maswala ya kodi TRA.

kila kitu kama mkataba ulivyokua unajionesha, kila kitu kiwe vile sawa na mkataba ulivyosema na sheria za kazi na ajira zilivyoelekeza, kama itakua ni tofauti ni una ruhusiwa kuvidai ivyo vyote mpaka siku unayo acha kazi, yale ya mbele yako hautoweza kuyadai kwakua kazi umeacha mwenyewe kwa hiari yako, mfano unaacha mwenyewe kazi leo ila una dai mshaara wa mpaka 2028, hii haiwezekani.
 
Back
Top Bottom