Password nisizozijua kwenye Simu ya Mke wangu!

Password nisizozijua kwenye Simu ya Mke wangu!

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,792
Reaction score
2,421
Jamani naomba ushauri juu ya híi cm ya mke wangu.

Tulianza urafiki tu kama miaka mitatu ivi wote tukiwa chuo. Kwa wakati huo alikuwa na cm nzuri aina ya samsung ila kila tukikaa nae alikuwa anaacha cm kwingine mara rafiki yangu anachati nayo facebook, mara haina chaji, mara nimeisahau na sababu nyingi tu na sikuweza ata kuigusa kwa takribani miaka miwili.

Kwa kuwa niko mwaminifu sana nilijaribu kuicha cm yangu wazi kwake. Zinaingia sms bila kujua ya nani namwambia nisomee, alikuwa akikataa lkn baadae alikubaliana na hayo. Siku nyingine najifanya kama nimeisahau kwake ili kuonesha uaminifu.

Baada ya ndoa alikuja bila cm. Alisema cm yake ilipotea siku ya harusi kwenye salóon aliyokuwa akipambwa na wamemfidia fedha taslim na haoni haja ya kununua cm kwani atakuwa anatumia yangu.

Mwezi wa sita mwaka jana nilipata safari ya kikazi nikalazimika kumnunulia cm ila tuwasiliane nae tukiwa mbali.

Cha kushangaza cm hiyo anaificha sana. Ikiita anaweza asipokee. Aniambii lolote kuhusiana na cm labda nani kapiga kasema nini ananisalimia au la kama ambavyo nafanya mimi.

Akiöngea kwenye cm mazungumzo ni ya mkato na yasiyoeleweka. Utasikia mara Sawa.... Aa.... Sina... Nimesahau..... Yupo. Au nimeelewa yani neno moja tu alafu anakata cm.

Kingine amejiunga na facebook nazani kwa jina jingine kwani yuko bize na facebook lakini kila nikimtafuta kwenye fb simpati.

Leo ndio alikuwa ameenda kujifungua kwa bahati nzuri nikabahatika kushika cm yake na kuifungua ni password kila sehemu, fonebook, sms, call log na kadhalika.

Nishaurini nifanye nini na cm ya mke wangu.

Nilifika hospital leo asubui sana saa moja kasoro. Nikamfata mke wangu kumsabai

alikuwa akisubiri ruhusa. Kwa upole nikamuuliza juu ya password. Nakumwomba anijibu ili roho itulie na nianze kufikiri juu ya mtoto pekee. Mke badala ya kunijibu akaangua kilio wodini. Ni machozi macho mekundu analia tu. Sikujua analilia nini.

Mida ya saa moja na nusu daktari wa zamu alipofika alipokuta kile kilio akaniuliza kunanini. Nikamjibu anasema dumbo linamuuma. Sasa imebidi asiruhusiwe mpaka mchana waone hali yake.

Sa analilia nini ata sijui. Na kwanini asinipe tu hiyo password mi moyo utulie .

Ma mkwe nae katimba hosptal imebidi tu kumdokeza kasema nisubiri kidogo nae kama kanishangaa iv

UP TO DATE 15th Jan 2013 20:00
Nilienda kwa fundi simu nikaambiwa angeweza kuondoa password kwa kuifrash CM Ila itafuta kila kumbukumbu yani sms zote, majina na itakuwa kama mpya nikaona nimekwama hapo. Nikaenda kwenye ofisi za tigo nikiwa na laini yake kitambulisho chake na cheti cha ndoa yetu.

Wakakataa kunipa ushirikiano wakidai mpaka nipewe idhini police. Wanadai wangewajibika kama ningepata habari ambazo zingepelekea mtu kudhurika na wanalinda uhuru wa mteja.

Nikaenda police wamesema hawezi kuunda shitaka la kijinai au la madai ambalo lingepelekea wao kunipa idhini kufatilia cm wala laini.

Kufika hospitali tayari mke wangu alikuwa karuhusiwa.

Nikafika nyumbani majira ya saa 10 jioni. Nikamkuta ma mkwe, Mama mzazi, shangazi mmoja na nikaambiwa mchungaji ba mkwe yupo njiani anakuja na kunamaongezi sebuleni.

Kabla ya mazungumzo mke wangu alitoa sara kali kukemea na kufukuza mapepo.

Mama mzazi akaanza kunilalamikia kuwa sijafurahia mtoto. Mbona sikuuliza kabla mpaka sku ya kujifungua. Sijatoa pole kwa mzazi mara cn zawadi.

Katikati ya mazungumzo mke akadakia "password ni mwaka wangu wa kuzaliwa"

Jamani aibu. Nikatoa laini ile nilikuwa nimeitoa kwenye CM YAKE na kuweka kwenye Cm yangu. Mama yangu mzazi akaja pembeni yangu. Kuweka mwaka wake tu laini ile ikafunguka. Masikini aibu....
Fonebook hakuna kitu. Hakuna sms wala nini.

Kwa aibu sikuona haja ya ya kufata cm yake kuifungua tena mbele yao. Nikaomba msamaha tukasameheana wote mama akatoa tsh 50,000 na mama mkwe hivo ivo shangazi akatoa ahadi tu. Kabla ya kufunga mazungumzo mchungaji na Baba wakafika. Wakaambiwa mi ni mtoto yameisha tukapiga sara tu.)

mh kuifata cm yake lengo nimrudishie wife mara ikaingia sms. Kuiangalia ilikuwa ni sms ya 17 toka nichukue cm. Na nikaona kuna misscall kibao.

Nikasema nizisome zote ndio nirizike...

Masikini password tulizopewa hazifungui cm hii. Nikamuuliza tena mbona cm haifunguki na hizo password.

Alivyonijibu sasa ni amazing. Ni kwa kuashiria kiburi ila maneno aliyosema ni aibu kwangu ata kuyaweka hapa......

Ila poa tu...

"Siri ya simu hiyo ni yangu. Wewe haikuhusu kabisa.
Ulinioa sababu uliniwin kunipa mimba tu. Sikufichi mtoto ni wako ila hutakaa ujue siri za maisha yangu.
Nilishakuwin kwa mama na wazazi wako na ukirudisha mada hiyo tena ntasema we ndio umeziweka izo password. Kwa taarifa yako ata babaangu mzazi hawezi kukubali kuifungua cm hii... "

ni ujumbe wa maneno kama hayo sema sikuweza kuurekodi ila nahisi sijaukosea sana

sasa naiogopa mpaka nyumba kanitishia hadi maisha kuendelea kuzifatilia

natamani nitoroke tu
 
duh! mkuu umejaribu kumchunguza mienendo yake mingine kama ni ya wasiwasi au vp?

ilikuwaje ukaamua kumuoa kabla hujatatua hayo makitu ili kujua tatizo ni nini?

ni house wife au anafanya kazi?

lastly but not least , je unauhakika alikaa miaka miwili bila simu kabisa?
 
Pole sana mkuu.

Lazima kuna kitu ambacho si cha kawaida na ambacho hapendi ukijue. mweleze kuwa huridhiki na hali ilivyo kuhusu namna yake ya ku handle simu, mwambie huridhiki.
 
Kaka usionyeshe wasiwasi wowote kwake endelea kumchunguza kwa umakini kuna kitu apo kinaendelea ambacho hukijui
 
mi nakushauri achana kabisa na hayo mambo utakuja kuharibu ndoa unataka kuona ili iweje..wewe cha kufanya ongeza juhudi katika kuatafuta kipato mambo ya kuchunguza simu yashaleta vurugu sana na inategemea ulimpata katika mazingira gani? anaweza akawa ni mwaminifu tena sana ila akawa anachart na marafiki zake au hata ex akawa hataki uone....ila we jaribu kumwambia vipi tena mbona password nyingi uone jibu lake..............ila acha kabisa kufuatilia simu ya mkeo kama ni mwaminifu atakua hivyo milele ila kama ni kiruka njia atafanya tuu hata ukiona ni bora uachane kabisa na hicho kitu ufikirie zaidi kutafuta pesa...stress za nini maisha yenyewe mafupi
 
daaah!!! pole sana maana umeingia kwenye ndoa bila kutatua tatizo hilo sasa huna budi kuliacha kama lilivo na uendelee na ndoa vinginevyo kama unajiwa na mawazo kuwa mkeo si mwaminifu hukutakiwa kumuoa. Inaweza kuwa anamambo yake ambayo hawezi yatolea maelezo ila ukijua itakuwa mbaya na wewe anakupenda hivyo hiyo simu wewe ipotezee. Kwani umeoa mke au simu? na kuonesha hakutaka ugomvi na wewe alikuja kwenye ndoa bila simu hivyo hatakai kujibu maswali. Unachotakiwa ni kumuamini na kumpotezea na hii ianzie moyoni laa sivyo utaanza kumchukia mkeo na kumuona hafai ilhali ndo kwanza kichanga kimeingia nyumbani kwenu, msimtendee isivyo haki kichanga kwa wivu wenu.

Nina mengi ya kuandika ila fahamu kuwa jinsi wanaume walivyo smart kwenye kudanganya ndani na nje ya ndoa ujue mwanamke ni mara nne yake, usije ukapata presha na kisukari mapema wakati hata hujafika 40s, cha muhimu heshima iwepo kwani hata ukiwa na simu yake na isiwe na password kama ni mfanyakazi anaweza akawa na simu ingine ambayo anaitumia na kuiacha kazini na ile uliyomnunulia wewe ukajistukia ni wewe tu ndo unaitumia au mwingine kila akimaliza anadelete information. Ndugu bata ukimchunguza sana humli wewe ulishavua nguo kuoga maji mkeo huyo simu isivunje ndoa yako. Jiandae kuwa baba mzuri na utoe ushirikiano kwa mkeo. Maana baada ya mawazo hayo utaanza kuwaza aaah au huyu mtoto si wangu nipime DNA sjui nini na kama huna ushahidi wa mashaka unayomtilia mkeo ujue unaitia ndoa yako doa. Wanawake wengine wako hv anaweza kuwa hana baya lolote analofanya basi tuu anataka private na wewe ukaanza msumbua mara nn na vile halafu ukaja fanya kitu cha kijinga ukajiona ----- wa wivu wa kijinga na akachukia na kukumwaga. Mafano unaweza amua fanya uchunguzi wa kufuatilia nyendo zake marafiki zake ndugu zake wa karibu na kujua nn kinajificha ndani ya sm, kisha anakuja kujua unafanya hayo na wewe majibu unayopata yanakuwa ni mazuri kuwa mkeo wala hacheat hata huko fb yuko fresh pamoja na kujua ID yake then................? Kama anahitaji private muache akijiskia kukwambia atakwambia ukilichukulia kubwa litakuwa kubwa ukilichukulia simple litakuwa simple. Eeeh hata simalizi kuandika naishia hapa kwa leo.
Nakutakia malezi mema.
 
mi nakushauri achana kabisa na hayo mambo utakuja kuharibu ndoa unataka kuona ili iweje..wewe cha kufanya ongeza juhudi katika kuatafuta kipato mambo ya kuchunguza simu yashaleta vurugu sana na inategemea ulimpata katika mazingira gani? anaweza akawa ni mwaminifu tena sana ila akawa anachart na marafiki zake au hata ex akawa hataki uone....ila we jaribu kumwambia vipi tena mbona password nyingi uone jibu lake..............ila acha kabisa kufuatilia simu ya mkeo kama ni mwaminifu atakua hivyo milele ila kama ni kiruka njia atafanya tuu hata ukiona ni bora uachane kabisa na hicho kitu ufikirie zaidi kutafuta pesa...stress za nini maisha yenyewe mafupi

ni kweli kabisaaa
 
ndugu Mushumbusi simu ya MKE unaitakia nini? GROW UP dude...hayo sio mambo ya kufatilia kabisa...kama mwanaume u have more to work and worry for sio mambo hayo yatakuletea matatizo usiyoyatarajia bure!
 
Dah tumekatazwa mambo ya simu ila huyo mkeo ana siri nzito sana ..maisha gani hayo?
 
Jamani naomba saana ushauri wa dhati. Natamani kujua mke wangu anasiri gani kwenye cm mpaka password na tulikuwa wawili nyumbani likizo nzima mwezi moja akijiandaa kujifungua.

Kaniulizia kama nimeiona cm yake nimekataa. Nataka nitumie usiku wa leo kuweza kujua kilichofichwa ndani.

La sivyo nazidi changanyikiwa mwenzenu nahisi nisipo jib mpakua asabuioi ntakua mwehu!

Kwani niliitoa laini yake ya pembeni nikaweka kwenye cm yangu ikataa kuwaka mpaka pini nimejaribu mpaka mara mbili nikienda ya tatu tu inabrok. Imebaki lain moja ya ndani kwenye cm. Kwani cm yake ni nokia double line. Na kuna meseji imeingia yani wasi wasi tupu ata raha ya mtoto sipati jamani.
 
ndugu Mushumbusi simu ya MKE unaitakia nini? GROW UP dude...hayo sio mambo ya kufatilia kabisa...kama mwanaume u have more to work and worry for sio mambo hayo yatakuletea matatizo usiyoyatarajia bure!

kumbuka sijawahi kuigusa kwa zaidi ya miezi sita toka nimnunulie. Leo tu tena kwasababu alikuwa anajifungua na mtu alipiga nilipoipokea alikaa kimya akuongea lolote.

Kwenda kuangalia kwenye call log nijue ni nani nichukue namba nimtaalifu mkewangu kajifungua kalazwa ndo nakuta pass word

kumbuka huyu ni mke we umeoa kweli?
 
ndugu Mushumbusi simu ya MKE unaitakia nini? GROW UP dude...hayo sio mambo ya kufatilia kabisa...kama mwanaume u have more to work and worry for sio mambo hayo yatakuletea matatizo usiyoyatarajia bure!

Mhhhhh!!!???...........

Nakusalimu rafiki.
 
Pole, nenda nayo kwa fundi simu kwa ajili ya ku unlock
 
Chonde chonde naomba uvute subira
Ukiona mambo bado yanakusonga mwambie unavyooumia kichwa kwa usili aliona nao
Vp dogo mkoje akikuwa kdg (DNA)kacheki ukweli maana mda mwengine baadhi ya wasichana wanazingua sana
 
Daah pole sana kaka! Najua maumivu unayoyapata. Mimi binafsi nina mchumba wa dizaini kama wife wako. Facebook sana na simu yake kua na password.
Nafikiria kuchukua maamuzi magumu yakumtosa. Lazima kuna kitu kibaya anafanya hataki wewe ujue. Kwakua wewe umeshafunganae vunja ukimya zungumzanae mwambie hupendi hiyo tabia.
 
....umeanza nae tangu chuo,umegundua mapungufu yake,bado umeng'ang'aniaa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom