Passport zipo tele, vitambulisho vya Taifa vya nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Passport zipo tele, vitambulisho vya Taifa vya nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jay One, Dec 18, 2011.

 1. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,667
  Trophy Points: 280
  Hadi leo ukiniuliza vitambulisho vya Taifa ni vya nini? jibu ni sijui, sbb Passport ndio kitambulisho worldwide kinajulikana, nasisitiza huwezi kwenda nje ya nchi ukasema nina kitambulisho cha Taifa, hakuna atakaye kuelewa, Passport ipo kwenye system, ukienda nayo popote wanajua kuwa ni halali, it's computerized worldwide.
  Naona hapa tunapoteza fedha nyingiiiiii, kama sikosei bajeti ya 2010/11 ilitengewa Tshs 324 billions just kwa vitabulisho, hii ni unnecessary expenditure, imagine...!!!!

  TUNGEBORESHA PASSPORT KILA MWANANCHI APATE, ingekuwa rahisi, ndio system ya dunia nzima, na ingetumika kama kitambulisho halali kwa shughuli za kiataifa na kimataifa, jamani fedha hizi i feel sorry
   
 2. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nategemea wewe ukanushi ujio wa vitambulisho vya Taifa, bali thread yako ni swali la mzunguluko kwa kitu
  ambacho ukielewi na unahitaji ukielewe. Passport ni hati ya kusafilia, na kujitambulisha Kitaifa na Kimataifa.

  Na vitambulisho vya uraia ni kujitambulisha Kitaifa ambacho kinabeba dhamana ya jina lako, mahali pa kuzaliwa
  kwako, kitongoj, Kijiji, Wilaya pamoja na mkoa. Hususani cha muhimu zaidi katika kitambulisho cha Uraia ni
  (Residence) sehemu unayoishi yaani mtaa na namba ya nyumba.

  Hapo inamaanisha kwa chochote kitakachotokea, kutambulika ni rahisi na mara moja, kwa kupiga kura utatumia kitambulisho chako cha Uraia kwa sababu vitakuwa tayari vipo katika computer, na mifumo mingi ya kiofisi itakuwa rahisi kukufikia bila ya wewe kuhangaika katika
  maofisi, kama kulipa kodi, pamoja na mambo mengi ambayo yanaweza kukufikia kwa wakati.

  Na si wewe peke yako mpaka wale wa vijijini. Ikija Serikali ya CDM tutazidi kufungua zaidi akili zetu na kuweka
  urahisi wa matumizi ya mfumo mzima kwa Raia wote kupitia vimbulisho vya Uraia.
   
 3. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  mkuu, unawezaa ukawa hujamuelewa mleta mada au naye sio mtaalamu sana we ku-present mada kama tulivyo wengi wetu lakini hoja yake ni ya msingi zaidi ya unavyodhani.
  Ukiingia na kutafuta humu jamvini zipo thread nyingi na zina taarifa muhimu sana juu ya hili suala la vitambulisho vya kitaifa.
  Huu mradi unavyopambwa hauna tofauti sana na RICHMOND kama wengi wetu tulivyoshindwa kujua kilichokuwa nyuma ya pazia, watu wanaongelea 'matatizo ya umeme' lakini kumbe wana lao jambo!
  Hivi vitambulisho vya taifa havina tofauti na Birth Certificate ya RITA, Driving License, TIN Certificate, Passport ya kusafiria, Kitambulisho cha mpiga kura, nk ambavyo vyote vinatolewa na serikari.
  Hoja ya mleta mada hapa (kama naelewa) ni kuwa kwa vile sasa ni wakati wa teknologia, hizi data zote za hivyo vitambulisho nilivyogusi ninawekwa kwenye DATABASE. Sasa badala ya kuwa na 'vidatabase' kila ofisi ya serikali hiyohiyo vinavyotunza taarifa zinazofanana kwa kila kitu ni kwa nini wasijenge (develop) database moja yenye taariza zote kama nchi za wenzetu!!???
  Ninachotabiri juu ya mtadi wa Vitambulisho vya Taifa, baada ya 'wadau'kula 10% (kama sio 75%) wataurudisha huu mradi kwenye kitengo kingine!
  Kwa maana hiyo ni bora hizo billion wangepewa RITA (Vizazi na vifo) sasa na kujenga uwezo na hivyo kuwa taasisi inayostahili kuchukua hili jukumu!
  Watu na viongozi wanajua hili lakini nia na nafsi zao ndio mbaya!
   
 4. K

  Kamura JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acha ushamba pasipoti haiwezi kuwa mbadala wa Kitambulisho cha Taifa. Hujaona vipindi vya NIDA kwenye vyombo vya habari?
   
 5. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu hata wewe ni kama sijakuelewa. Kwani logic yako hapa nini sasa; ubora wa vitambulisho au mradi wa watu(Richmundi)?
  Mimi pia ni miongoni wa wale wanaopenda kwamba ikiwezekana kila Mtanzania awe na passport, lakini siamini kama passport pekee ndiyo suluhu utambulisho wetu.Lakini pia siamini kwamba passport ndiyo mbadala wa vitambulisho vingine. Kwa mfano umesema nchi za wengine passport ndiyo kila kitu, siamini kama passport inaweza kuwa mbadala driving lecense-hii ni profesional certificate kama nyingine.

  Kwani nini maana ya hati ya kusafiria(passport)? Hiki ni kitambulisho kama vingine, utofauti wake ni kwamba yeyewe inatambulika worldwide. Issue ya kwamba imeunganishwa na mtandao sio hoja, kwa sababu inatumika kimataifa ni lazima iwe katika mfumo unaowezesha kutambulika popote duniani. Kwa mantiki hiyo, mimi sioni kama hiki ndicho hasa watanzania kwa ujumla wake wanahitaji sana. Kama ni database hata hivyo vitabulisho vya uraia vinaweza kuwekwa na kila mwenye nacho akwa anatambulika kitaifa.

  Kwa mtazamo wangu, hitaji la kwanza la raia sio hati ya kusafiria bali kitambulisho cha uraia. Afahamike kwanza nyumbani kisha uwekwe utaratibu mzuri sasa wa kupata passport kwa yule anayeihitaji- usiwepo urasimu kama ilivyo sasa. Mimi sioni kama kutakuwa na hivyo 'vidatabase' ulivyosema, kwanza vya kazi gani. Kwenye databse kutakuwa na jina la 'XX' taarifa zote zinazohitajika zitapatikana chini yake, hata hiyo passport na vitu vingine kama anavyo vitawekwa pale. Ugumu uko wapi?

  Je, tumeishajiuliza gharama ya kuteneza hizo passport zinazotambulika kimataifa? Tumelinganisha na gharama ya hivyo vitambulisho vitakavyotengenezwa? Prioritize kwanza. Hii ni hisabati rahisi tu jamani. Sina maana kwamba hakuna uwezekano wa kutengeneza passport kwa kila mtanzania, la hasha. Ila sioni mantiki ya kuanza na passport badala ya vitambulisho vya hapa nyumbani kwanza.

  Kimsingi hapa tujadili iwapo mahitaji ya watanzania kwa sasa kama ni pasport au vitambulisho vya uraia. Habari ya ufisadi ni nyingine, maana hata kama tukiamua kutengeneza passport kama ufisadi upo ni upo tu. Sidhani kama passport zinashindikana kufisadiwa.
   
 6. m

  mahangu Senior Member

  #6
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45


  Kiukweli mwanajamii forum mwenzangu achilia mbali passport, hebu fikiria maamuzi ya kuanzisha mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) wakati tuna RITA ( Registration, Insolvency and Trusteeship Agency), RITA inajua taarifa nyingi za kuzaliwa kwa mtu, ilikuwa ni busara kabisa na kuokoa fedha za walipa kodi kuanzisha kurugenzi ya vitambulisho vya Taifa ndani ya RITA. sioni kama mtu anaweza kuja na hoja ya kunipinga kuwa hatukuwa na sababu ya kuanzisha mamlaka/wakala mpya.
  Nchi hii zama hizi maamuzi yanafanywa kiholela tu bila kufikiria, saizi Tanzania tuna wakala na mamlaka nyingi lakini maendeleo bado tuko nyuma. utategemea wakala au mamlaka inapoanzishwa in kuja kuboresha ufanisi eneo husika kumbe ni kuleta urasimu zaidi. we subiri vitambulisho vya taifa uone urasimu wake, hizo form ukisoma utaona mtu wa RITA anatakiwa, Uhamiaji anatakiwa. Je NIDA itawezaje kuthibitisha uraia wa mtu bila kupta taarifa RITA? kama ndivyo si tungewaachia RITA tu kufanya kazi hiyo. Matokeo ya NIDA itakuwa kama Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB), kushindwa kujua hali ya uchumi wa wazazi wa mwombaji.

  Jamani Tanzania tujikomboe kifikra, sio kila tunachoshauriwa na wafadhili au wabia wa maendeleo ( wakoloni wa kisasa) tukubali.

  Lets change our thinking
   
Loading...