VITAMBULISHO VYA TAIFA NA USAJIRI WA LAINI ZA SIMU.

ohanyitz

Member
Sep 28, 2018
37
18
Habari za wakati huu wana jamvi, binafsi Mimi ni mzima wa afya. Kama mada inavyo jieleza hapo juu. Kwa muda mrefu sasa tangu kipindi Cha awamu ya nne tumeshuhudia uanzishwaji wa VITAMBULISHO VYA TAIFA ikiwa na lengo kuu Kama utambulisho halali wa uraia wa Tanzania. Swala hili walikabidhiwa NIDA Kama muhusika mkuu katika kuhakikisha Kila Mtanzania anapata kitambulisho hiki kwa wakati na bila gharama yoyote Ile. Wote tumeshuhudia jinsi swala hili lilivyo enda tangu kipindi Cha awamu ya nne mpaka awai hi ya tano ambayo inaelekea mwishoni(jumla ya miaka 7 tangu kuanzishwa). Nijambo lakusikitisha na aibu mpaka sasa zaidi ya nusu ya watanzania hawajapata vitambulisho hivyo. Swala lingnine ambalo limenipelekea kuandika uzi huu ni ajenda kuu ya vitambulisho hivyo kuwa nikusajili line za Simu na kutoka kwenye ajenda ya kumtambulisha Mtanzania, ambapo mwisho wa kusajili laini ni mwezi wa 12 Kama ilivyo elezwa na TCRA. Kutokana siku kuzidi kukimbia na idadi kubwa ya watanzia zaidi milioni 20 Bado hawajapata vitambulisho hivyo kutokana na hilo swala hili limeanza kumbizwa haraka haraka ilimpaka tarehe tajwa ya mwisho wa kusajili laini iwe Kila Mtanzania awe amepata kitambulisho hicho, Jambo ambalo haliwezekani. Kuharakishwa kwa kuwandikishwa watu vitambulisho vya utaifa kwa Sababu eti waweze kujasili laini za simu ni ugonjwa wa kifikra ambao viongozi wetu wanazo. Wakumbuke kwamba tangu swala hili limeanzishwa ni miaka mingapi imepita, kwanini wasinge harakisha tangu swala hili linaanzishwa ambapo miaka karibia Saba imepita waje kuharakisha kipindi hiki? Pia waliopewa mamlaka ya usimamizi wa Jambo hili wanatakiwa wajue madhara ya kuharakisha, Kuna uwezekano mkubwa watu wasio na vigezo vya kuwa raia wa Tanzania kupata mwanya wa kupata kitambulisho hicho na kuwa raia halali wa Tanzania. Napenda kuishauli serikali yangu pendwa swala hili tusiliharakishe eti kwa Sababu ili tusajiri laini za simu, bali tufanye kwa malengo ya Kila raia halali wa Tanzania apate kitambulisho hiki ikiwa Kama nembo ya utanzania. Tusipo liangalia hili tutashuhudia watu ambao sio wa Tanzania kupata vitambulisho hivi na mwisho wa siku kupata haki na staili zote katika nchi hii.
 
Mbona wengi tu wameshajipatia vitambulisho na sio watanzania

Ety ukiingia chumba cha yule anayeuliza swali kuhakiki utaifa wako ,moja ya maswali “taja jina la bibi yako “, au kilugha chenu mnasalimia vipi asubuhi sasa nani atashindwa kusema
 
mkuu tunaelekea kwenye uchaguz ko wanataka wazuie watu wasipate habari mtandaoni umesahau kampen za2015 kila kilichukua kinaendelea kinapostiwa mtandaon.we fikiria unambiwa kunalain milion tano tu ndo zmesajiliwa mpaka saiz sasa watanzania wapo wangap
 
Nifkirivyo mm(ni mawazo yangu binafsi) ipo hidden agenda behind the scan, na ni kubwa kuliko watu tunavyo fikiri, kwa nini nasema hvyo, haiwezekani nchi nzima yenye watz zaid ya million 45, tukawa na wazo moja t la kusajiri line za simu, ndyo tupate kitambulisho, hakuna kitu cha namna hyo,

Mfano, ikatokea watu wakagoma kusajiri line za sim baada ya kuwa na kitambulisho cha taifa nn kitatokea?

Jambo 1 tu nnaloweza kusema the world has missions and visions, na huu ni mkakati madhubuti wa kisera, si kwa ajiri ya tz or line za sim ila ni mission pana zaidi ya hapo...

Ukiona mpka presidor, anatoa agizo mwisho uwe mwezi 12, something is bitting somewhere...

B
 
Inawezekana ndugu yangu kwa Sababu kwa kipindi hiki kipaumbele Cha kuwa na kitambulisho Cha utaifa Ni kusajili line za simu. Itanakiwa tufikili kwa umakini Sana ndugu
 
Back
Top Bottom